MPANDA
Wamebainisha hayo wakati
wakizungumza na Redio mpanda kwa nyakati tofauti ambapo wamesema vitambulisho
hivyo vitawasaidia kufanya shughuli zao
pamoja na kuirahisishia serikali katika ukusanyaji mapato
Meneja wa mamlaka ya
kukusanya mapato TRA Mkoa wa Katavi Enosi Mgimba amesema zoezi hilo limeshaanza
kwa wafanyabiashara hao kupatiwa vitambulisho hivyo kama maagizo yalivyotolewa
na ofisi ya kamishina mkuu wa TRA makao makuu
Utoaji wa vitambulisho
kwa wafanyabiashara wadogo unatokana na marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa
Kodi ya Mwaka 2015 yaliyofanywa na Bunge la Bajeti la Mwaka wa Fedha 2017/2018 ambapo
moja ya marekebisho hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho maalum
wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi
Chanzo:PAUL MATHIAS
No comments:
Post a Comment