Vyombo
vya dola Mkoani Katavi vimeombwa kuwa makini katika kipindi hiki cha sikukuu
kuhakikisha hakuna uvunjifu wa Amani utakao sababishwa na matukio ya kihalifu.
Mchungaji
wa Kanisa la Pentecoste Tanzania Nsemulwa
Gliady Eliazeri akizungumza na mpanda redio leo amesema kuna baadhi ya watu
hutumia siku za Sikukuu kama Nyanja za kufanya uhalifu.
Kwa
upande wa waumini wa dini ya kikirsto wamesema wanatarajia kuipokea sikukuu
hiyo kwa Amani na utulivu ikiwa ni pamoja na kufika katika sehemu za ibaada ili
kuadhimisha kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu.
Sikukuu
ya Pasaka inatarajiwa kuadhimishwa tarehe mosi April mwaka huu kama kumbukumbu
ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
CHANZO:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment