Mkuu
wa wilaya ya Mpanda Liliani Matinga amewataka wananchi kuacha tabia ya kulima
katika vyanzo vya maji ili kuepusha uharibifu wa mazingira.
Ametoa
agizo hilo wakati wa kikao cha kuwasilisha mpango kabambe wa maendeleo katika
Manispaa ya Mpanda kilichofanyika leo amesema kumekuwepo na baadhi ya wananchi
wanaolima bila kuzingatia umbali wa mita sitini kama sharia inavyoelekeza.
Aidha
amebainisha kuwa wale wote watakaokiuka agizo hilo hatua kali azitachukuliwa
dhidi yao pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria .
Halmashauri
ya manispaa ya Mpanda imezindua mpango wa mpango miji wa mwaka 2018-2038 ambapo
mradi huo utaainisha maeneo mbalimbali ya kiutawala ,kilimo,vyanzo vya uchumi
pamoja na maeneo ya utalii ndani ya manispaa na mkoa kwa ujumla.
Mpango
huo wa miji unasimamiwa na kampuni ya city plan iliyoshinda tenda ya kupanga
mji wa Mpanda kuonekana wa kisasa kwa kuzingatia mazingira na nyakati za kukua
kwa kasi maeneo mbalimbali hapa nchini
Source:Paulo
Mathius
No comments:
Post a Comment