TANGANYIKA
Wananchi wa kata ya Kasekese Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi wameiomba serikali kuwapa elimu
kuhusu zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na radio mpanda
na kusema kuwa wamejitokeza katika vituo vya kujiandikisha kwa wingi kutokana
na kuona mabango ya serikali za mitaa kutaka kujitokeza ili kuweza kupata
vitambulisho hivyo japo elimu kuhusu ujazaji wa fomu wa vitambulisho vya uraia
haikutolewa.
Naye mwenyekiti wa kata ya Kasekese Bi.Chausiku
Pandisha amesema kuwa wananchi wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya
kujiandikisha na elimu imetolewa kwa asilimia kubwa na ameiomba serikali
kuwaongezea muda wa zoezi hilo ili wananchi wote waweze kujiandikisha.
Wazo la kuanzisha Vitambulisho vya Taifa kwa raia
wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania limezaliwa mwaka 1968 katika
kikao cha “Interstate Intelligence Gathering” kilichojumuisha wajumbe Kutoka
nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Zambia.
Serikali
imeazimia kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia Utawala wa
Sheria katika nchi hizo nne ni lazima nchi za Uganda na Tanzania zikatoe
Vitambulisho vya Taifa kwa raia wao.
Chanzo: Ezelina
Yuda
No comments:
Post a Comment