Baadhi
ya waendesha vyombo vya moto Katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani
Katavi,wamesema licha ya bei ya Petrol na Dizeli kushuka,bado wanaona bei hiyo
ni kubwa zaidi ukilinganisha na hali ya maisha kwa sasa.
Katika
mahojiano na Mpanda Radio kwa nyakati tofauti miongoni mwa madereva wakiwemo
waendesha pikipiki wamesema hawanufaiki vizuri na bei ya mafuta kama
inavyotakiwa kwa kuwa wao nauli inabaki kama ilivyo hata kama bei ya mafuta iko
juu.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji EWURA imetangaza kushuka kwa bei ya petroli na dizeli kwa
asilimia 2.7 na asilimia 3.8 na ongezeko la asilimia 0.09 kwa mafuta ya taa.
Chanzo : Issack Gerald
No comments:
Post a Comment