Chama cha msingi cha
wakulima wa Tumbaku cha Mpanda kati kilichopo katika Halmashauri ya wilaya ya
Mpanda Mkoani Katavi kimesema msimu ujao wa kilimo wataanza kuuza Tumbaku Kwa
kiwango cha shilingi kutoka kwenye mfumo wa dola.
Hayo yamebainishwa na
kaimu meneja wa chama hicho Marietha John wakati akizungumza na Mpanda radio
ofisini kwake amesema kuwa tayari wamepokea maagizo kutoka wizara ya kilimo
kuanza kununua zao hilo kwa kiwango cha shilingi hali ambayo itapunguza
malalamiko yawakulima kudai kuwa wanaibiwa kutokana na mfumo wa dola.
Kumekuwa na malalamiko
ya wakulima wa tumbaku kwa muda mrefu kuhusu malipo na uuzwaji wa zao hilo
kwadola kwani wengi wao ha wana uelewa
na mfumo huo
Chama cha msingi cha
wakulima cha Mpandakati kina Zaidi ya
wakulima wa tumbaku 1250 kikiwa kimeundwa na vijiji mbalimbali vya halmashauri
ya wilaya ya Mpanda.
No comments:
Post a Comment