Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ameupokea
mwenge kutoka mkoa wa Tabora tayari kuanza uzinduzi wa miradi ya maendeleo
Katika Mapokezi yaliyofanyika uwanja wa Ndege wa Mpanda mkoani
Katavi, mwenge wa Uhuru umekabidhiwa
kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwanri ambaye awali ameshukuru mapokezi mazuri kutoka kwa mwenyeji wake.
Baadaye Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga
ameukabidhi mwenge huo kwa mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga kwa ajili ya
kuanza kuukimbiza Katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya mpanda.
Mbio za mwenge mwaka huu zinaoongozwa na
kauli mbiu ya elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya
Taifa.
Chanzo
:MPANDA RADIO
No comments:
Post a Comment