Tuesday, 27 June 2017

WAISILAMU CHOCHEENI AMANI NCHINI NA UPENDO

Mamia ya waumini wa dini ya Kiisilamu mkoani Katavi wamejitokeza kushiriki swala ya Idd katika uwanja wa kashaulili uliopo halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Swala ikiendelea katika uwanja wa Kashauriri uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.


Katika sherehe hizo  Shekhe Mkuu wa mkoa huo Shekhe Ally Husein ametumia fulsa hiyo kuwataka waisilamu kuwa nguzo ya kuchochea amani na upendo nchini.
Shekhe  wa Mkoa wa Katavi Ally Husein

Amefafanua kuwa yapo mambo ambayo yanafanywa na baadhi ya waisilamu wasio waaminifu katika imani, na kuuchafua uisilamu jambo ambalo halikubaliki kidini.


Nao baadhi ya waumini wa dini hiyo wametumia muda huo kutakiana heri katika sikukuu ya Idd.

Baadhi ya waumini wakifuatilia kwa umakini hotuba mbali mbali ziliyokuwa zikitolewa.
Matangazo ya moja kwa moja kutoka katika viwanja hivyo yalikuwa yakiletwa na Mpanda radio fm 97.0Mhz.
Mtangazaji kutoka Mpanda radio fm Edward Mganga maalufu kama Doctor Edward akifanya  mahojiano ya moja kwa moja. 



Sikukuu hiyo Kitaifa imefanyikia mjini Moshi mkoani Kirimanjaro ambapo mgeni alikuwa Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

0769772262

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...