Mpanda radio fm imedhamiria kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo
wafanyakazi wake ili wamudu ushindani ulipo katika Tasinia ya habari.
Mkurugenzi wa Mpanda Radio Amin Mitha pamoja na mjumbe wa bodi Prosper Kwigize. |
Akizungumza mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo yaliyofanyika
kwa muda wa siku saba Mkufunzi kutoka
UNA ambaye pia ni Mwenyekiti wa asasi hiyo Silesi Malli ameeleza dhana ya mafunzo hayo kuwa
ni kuchochea uwajibikaji katika vyombo
vya habari vya kijamii.
Baadhi ya wafanyakazi pamoja na wakufunzi wa mafunzo hayo. |
Katika ufafanuzi ameelezea kuwepo kwa tatizo kubwa la kiuchumi kutokana na uelewa mdogo wa waandishi wa habari katika kuandika maandiko ya miradi ili kukidhi mahitaji jambo linalopelekea vituo vingi kushindwa kujiendesha.
Katika siku hizo saba wandishi wa habari kwa pamoja wealipata
fulsa ya kufanya kazi kwa vitendo, ili kupima uelewa wa kile walicho jifunza.
Mafunzo hayo yaliasisiwa mnamo 0ctober 2014 na mwandishi wa habari mkongwe Prosper Laurenti Kwigize kutoka shirika la habari la kimataifa la DW lenye makao yake makuu mjini Borne Ujerumani ambapo katika kipindi hicho yalilenga kuleta mageuzi ya kiuandishi ili kujenga uwajibikaji baina ya jamii na serikali.
mafunzo yakiendelea kwa vitendo |
No comments:
Post a Comment