JUMAMOSI 24,JUNE 2017
Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir
Bin Ally amesema Baraza kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA linaendelea kufuatilia
kuandama kwa mwezi na kwamba litatoa taarifa kamili juu ya siku ya kufanyika
kwa sikukuu ya Idd el-Fitr kama ni kesho au kesho kutwa.
Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakary
Zuberi Ally
Mufti, Aboubakar Zubeir Bin Ally
ametoa kauli hiyo jana jioni kufuatia taarifa kupitia mitandao ya kijamii
zilizozagaa na kusema kuwa sikukuu ya Idd el-Fitr itakuwa siku ya Jumatatu.
Mufti amesema hilo halijatangazwa na
kufafanua kwamba Mufti ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza baada ya kushauriana
na kamati ya mwezi.
No comments:
Post a Comment