Saturday, 24 June 2017

WAANDISHI WA HABARI WANOLEWA NAMNA YA KUANDAA VIPINDI VYENYE UHALISIA




Kulia na mwandishi na mtangazaji wa Mpanda Redio AllyNanuswe Edward akiwa na  mkufunzi wa mafunzo hayo  Pendael Omary mwandishi mkongwe wa TBC  katika ukumbi wa Edema mkoani Morogoro.


Baadhi ya kikosi kazi kilichoshiriki  mafunzo kutoka  BBC media action juu ya namna ya kuandaa  vipindi vya  haba na haba  wakitafakari jambo namna gani ya kwenda kuandika vipindi hivyo




MOROGORO


Waandishi wa habari 24 kutoka vituo vya redio mbali mbali  nchini wamehitimu mafunzo  ya kikosi kazi cha redio washirika  Cha haba na haba.

Mwandishi wa habari na mtangazaji wa kituo cha redio Mpanda radio fm Alinanuswe Edward maalufu Kama Uncle Eddo akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo yaliyofanyikia mjini Morogoro katika ukumbi wa Edema.


Baadhi ya washiriki  wa mafunzo hayo yaliyo fanyikakia ukumbi wa Edema uliopo mjini Morogoro wamesema kuwa ujuzi walio upata utasaidia kukuza kiwango cha utendaji kwa kufuata maadili ya uandishi wa habari pamoja na kuchochea uwajibikaji kwa serikali na jamii.



Kwa upande wa mkufunzi wa mafunzo hayo Pendael Omari ameeleza nia ya mafunzo hayo kuwa ni kuwa jengea uwezo waandishi wa habari washirika wa BBC media action ili walete mageuzi ya kiuandishi katika vituo vyao.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...