Saturday, 24 June 2017

UZINDUZI WA KIZIMBA CHA KUWEKEA TAKA NGUMU MANISPAA YA MPANDA

Mkuu wa wilaya Ya Mpanda Lilian C Matinga akikabidhi moja ya toroli watendakazi katika uzoaji wa taka hizo



 Picha Kushoto(Aliyevalia shati la draft) ni Mstahiki Meya wa manispaa Willium Mbogo na picha kati kati ni Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga na Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Maiko Nzyungu Wakishuhudia zoezi hilo la uzinduaji wa kizimba cha kuwekea Taka Ngumu eneo la Stendi Kuu Mjini Mpanda Mkoani Katavi




Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Lilian Charles Matinga Akiweka jiwe la msingi katika kizimba cha kuwekea Taka ngumu  eneo na stendi Mjini Mpanda




KATAVI

Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Lilian C. matinga amewaagiza wananchi kuwa na desturi ya utunzaji na usafi  wa mazingira wenyewe bila shuruti

Matinga ametoa kauli hiyo Juni 23,2017 wakati akizindua Kizimba,matoroli na watenda kazi watakaokusanya usafi kupitia kata mbali mbali za manispaa ya mpanda mkoani hapa huku akiwasisitiza

Samba mba na hayo pia Matinga amesisitiza kesho siku ya jumamosi wananchi kushiriki siku ya hiyo na amepiga marufuku kali kwa wale wote wenye desturi ya kuchimba mashimo na kuchoma taka taka

Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda Maiko Nzyungu ametaja kata tano zilizotajwa kupata matoroli katika awamu ya kwanza kuwa ni kata ya kashaulili, Mpanda hoteli,Majengo,kawajense, na makanyagio

Awali kabisa mwenyekiti wa kamati hiyo Bi, Mary Kayumba amewataka wanajamii  kushiriki vema kabisa kutoa ushirikiano kwa wananchi hasa katika zoezi hilo.





No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...