Saturday, 29 July 2017

Kim Jong-un: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani.



Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kufanyia jaribio kombora lake la masafa marefu ICBM, wakitaja kuwa onyo kali kwa Marekani.

 Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema kuwa jaribio hilo lilibaini kwamba marekani yote ipo katika radara ya Korea Kakazini na sasa inaweza kushambuliwa, vyombo vya habari vimeripoti.
Jaribio la kombora hilo linajiri wiki tatu baada ya jaribio la kombora la kwanza la masafa marefu la Korea Kaskazini. Rais wa Marekani Donald Trump amelitaja jaribio hilo kuwa la kijinga na kitendo cha hatari kilichotekelezwa na utawala wa Korea Kaskazini .

 China pia imeshutumu jaribio hilo huku ikitaka pandfe husika zilizo na waiwasi kujizuia ili kutoendeleza wasiwasi zaidi. Ikithibtisha kurushwa kwa kombora hilo, Korea Ksakzini ilisema kuwa kombora hilo la masafa marefu liliruika kwa dakika 47 na kufika urefu wa kilomita 3,724.

Imesema kuwa jaribio hilo lilifanikiwa kujaribu uwezo wa kombora hilo kuingia. Kiongozi huyo pia alisema kuwa jaribio hilo lilithibitisha kwamba Korea Kaskazini sasa ina uwezo wa kushambulia ardhi yoyote ya Marekani kulingana na chombo cha habari cha Yonhap. Taarifa hiyo ilisema kuwa kombora hilo ni Hwasong 14 kombora sawa na lile lililojaribiwa Julai 3. Image captionKombora hilo la masafa marefu lilisafiri kwenda juu ikilinganishwa na kombora lililorushwa Julai 3 hatua inayothibitisha kuwa taifa hilo linaweza kushambulia ndani ya Marekani.

 Kombora hilo la masafa marefu lilisafiri kwenda juu ikilinganishwa na kombora lililorushwa Julai 3 hatua inayothibitisha kuwa taifa hilo linaweza kushambulia ndani ya Marekani. Hatahivyo tathmini ya kikamilifu ikiwa bado haijafanikishwa mbali na muda uliochukuliwa na kombora hilo kuruka.

Muda mfupi baada ya jaribio hilo Korea Kusini, Japan na Maafisa wa Marekani waliripoti data kuhusu eneo na umbali, pamoja na muda uliochukuliwa na kombora hilo. Ijapokuwa tathmini kamili haijakamilishwa, vitu kadhaa vilibainika. Kwanza, data iliopo inaonyesha kuwa kombora hilo lina uwezo wa kuruka umbali wa kilomita 10,400.

Kombora hilo linaweza kurushwa na kufika mji wa New York. Pili Marekani iliripoti kwamba Korea Kaskazini ilirusha kombora hilo kutoka Mupyong -ni Korea Kaskazini. Eneo hilo lilikuwa tofauti ikilinganishwa na taarifa za awali ambazo zilifanikisha jaribio yaliotabiri kurushwa kwa kombora la Kusong. Image captionUmbali wa makombora ya Korea Kaskazini Kombora hilo lilirushwa usiku wa saa tano ambao sio muda wa kawaida wa Korea Kaskazini .

 Inawezekana kwamba Korea Kaskazini ilijaribu kurusha kombora hilo usiku na hivyobasi kurusha makobora kadhaa ambayo yanaweza kuwachanganya waangalizi. Ripoti siku ya Ijuma ilisema kuwa kombora hilo lilianguka katika bahari ya Japan.

Kujibu hatua hiyo, Marekani na Korea Kusini zilifanya zoezi la pamoja la kijeshi kwa kurusha makombora ardhini kulingana na afisa mmoja wa idara ya ulinzi Marekani.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira MUWASA- Mpanda mkoani Katavi imeanza ujenzi wa mradi wa maji wa kanoge.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira MUWASA- Mpanda imeanza ujenzi wa mradi wa maji wa kanoge ili kuongeza mita za ujazo 1,000,000 kwa siku ili kupunguza kero ya maji katika manispaa ya Mpanda katika mkoa wa katavi.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa mamlaka hiyo Injinia Zacharia Nyanda katika kikao cha nne cha baraza la madiwani wa halmashauri ya manispaa baada ya baadhi ya madiwani kusema kero ya maji imekuwa jambo kubwa katika maeneo yao.

 Ameongeza kuwa kuanzia mwezi wa kumi mwaka huu mamlaka itaanza ujenzi wa mradi wa maji wa ikolongo ii vilevile kutakua na ujenzi wa bomba la maji kutoka kazima hadi katikati ya mji. Aidha ameendelea kusema kuwa mamlaka itachimba visima kumi na moja kwenye maeneo ya manispaa amabyo yanashida ya maji na ambao mtandao wa mabomba haufiki.

 Maeneo mengi ndani ya manispaa ya mpanda bado yanakabiliwa na tatizo la maji ikiwemo kata ya makanyagio ambayo kwasasa wananchi wake hupata huduma ya maji kutoka katika nyumba za kulala wageni na katika visima vya watu binafsi.

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Mpanda radio Prosper Kwigize amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa TADIO mtandao wa redio za kijamii nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa TADIO taifa na Mtia saini wake katika picha ya pamoja baada ya ushindi mnono
DAR ES SAALAM:

 Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Mpanda radio Prosper Kwigize amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa TADIO mtandao wa redio za kijamii nchini Tanzania.

 Akizungumza mara baada ya ushindi huo amewaasa wajumbe wa taasisi hiyo kuungana kwa pamoja katika kutekeleza wajibu kwa weledi ili kufikia dhana ya kuwa chombo imara kinacho weza kuleta mageuzi katika vyombo vya habari vya kijamii.

 Kwigize amesema “Tunalenga kuibua mawazo, fikra ,changamoto zilizopo maeneo ya ndani kwenye jamii ikiwa tunaibua changamoto za maeneo pia tunaripoti kwanza changamoto ya maeneo yale kwa kuipa kipau mbele cha maeneo ambayo redio ilipo”

 Kwa upande wa mkurugenzi wa mtendaji wa Mpanda radio Amini Mitha ambaye amechaguliwa kuwa mtia saini wa benki katika masuala ya kifedha amewataka watumishi wa mpanda radio kulindi heshima ya kuwa chombo bora cha habari za kijamii.

 Mkurugenzi wa mpanda radio amesema “Wameona uhaminifu wangu na kuwepokwa kitengo hicho wameona nafaa naweza kutoa shukran kwanza kauli yangu ndo narudi palepale hiyo yote ni sifa yam panda radio fm tumeonesha kazi nzuri kwa habarisha ,kuburudisha na kuelimisha hasa kuibiwa mambo katika vijiji vya pembezoni mwa nchii.”

 TADIO ni taasisi mpya ambayo ni mwamvuli wa redio za kijamii nchini Tanzania iliyo anzanishwa mara baada ya kuvunjwa kwa COMNETA.

Friday, 28 July 2017

Bi Mugabe amtaka mumewe kumtangaza mrithi wake Zimbabwe.

Rais wa Zimabwe ametakiwa na mkewe kumtaja ''mrithi'' wake ili kupunguza migawanyiko kuhusu mtu atakayemrithi.

 ''Rais hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno alke litakuwa la mwisho'',alisema bi Grace Mugabe. Bwana Mugabe ndio kiongozi mzee zaidi na chama chake cha ZANUPF kimemchagua kuwania urais kwa mara nyengine mwaka ujao.

Lakini makundi pinzani yamekuwa yakiwania urais ili kuimarisha uwezo wao huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.

Iran yafanikiwa kuifanya jaribio roketi ya kubeba setilaiti.

Iran imefanikiwa kufanya jaribio roketi ambayo ina uwezo wa kupeleka setilaiti hadi mzingo wa dunia, siku moja baada ya Marekani kuiwekea vikwazo vipya kufuatia mpango wake ya kinyuklia.

 Roketi hiyo ya Phoenix ilirushwa kutoka kituo kipya cha anga za juu kilicho Semnan kaskazini mwa Iran.

 Marekani ililaani jaribio hilo na kulitaja kuwa kitendo cha uchokozi. Ndilo jaribio la tano la roketi iliyoundwa nchini Iran tangu mwaka 2009. Televisheni ya taifa nchini Iran inasema kuwa roketi hiyo itabeba setilaiti ya uzito wa kilo 250 hadi umbali wa kilomita 500 angani.

 Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani, anasema kuwa ikiwa itathibitishwa, jaribo hilo linaweza kukiuka maazimio ya baraza la Umoja wa Mataifa.

 Iran iliapa kujibu vikwazo vipya viivyotangazwa na Marekani ambavyo vililenga makampuni 18 au watu ambao wameunga mkono programu za Makombora za Iran.

Vikwazo hivyo vipya vilitangazwa siku moja baada ya utawala wa Trump kusema kuwa Iran inatekeleza makubaliano ya mwaka 2015 ya kuachana na mpango wa kinyukia.

Boko Haram wauwa zaidi ya watu 60, Nigeria

Zaidi ya watu 40 wameuawa wakati wa jaribio la kuwaokoa watu waliotekwa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram .

Takriban watu watano wa kampuni ya kuchimba mafuta waliuawa, kwa mujibu wa chuo cha Maiduguri.

 Wanajeshi pia waliuawa wakati wa uvamizi huo. Idadi hiyo kubwa ya vifo ni pigo kwa serikali ambayo inasisitiza kuwa kundi la Boko Haram limeshindwa.

Takriban watu 20,000 wameuawa na maelfu ya wengine kutekwa tangu Boko Haram ianzishe harakati zake mwaka 2009. Katika kisa kibaya zaidi Boko Haram waliteka wasichana 276 kutoka shule ya wasichana kaskazini mashariki mwa Nigeria ya Chibok mwaka 2014.

Tangu wakati huo wamewaachili zaidi ya wasichana 100 kubadilishana na wapiganaji. Taarifa za kina kuhusu kile kilichotokea siku ya Jumanne hazijulikani, huku ripoti za awali kutoka kwa jeshi, zikisema kuwa watu ambao walitekwa waliokuwa ni wakifanya kazia katika chuo cha Maiduguri waliachiliwa,.

Siku ya Jumanne jeshi lilisema kuwa miili ya wanajeshi 9 na raia mmoja ilikuwa imepatikana. Lakini sasa chuo kikuu kimesema kuwa takriban wafanyakazi watano wakiwemo wasomi wawili na dereva waliuawa wakati msafara wao uliokuwa chini ya ulinzi mkali, ulikuwa ukirejea mjini Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria Wengine kadha hawajulikani waliko.

Thursday, 27 July 2017

ISRAEL YAONDOA HATUA ZOTE ZA KIUSALAMA MJINI JERUSALEM.




Hatua zote za kiusalama zilizoweka hivi majuzi mjini Jerusalem, zilizozua maandamano kutoka kwa wapalestina zimeendolewa kwa mujibu wa polisi nchini Israel.

Viongozi wa dini katika utawala wa Palestina sasa wataacha kususia eneo hilo takatifu.



Vizuizi hivyo viliendelelea leo asubuhi, siku mbili baada ya mitambo wa kutambua chuma kuondolewa.

 Mzozo uliibuka baada ya kuliwa kwa polisi wawili wa Israel karibu wiki mbili zilizopita. Israel imesema kuwa itachukua hatua zisizokuwa na vizuizi miezi sita inayokuja.

 Kumekuwa na karibu makabiliano ya kila siku kati ya vikosi vya usalama vya Israel na waandamanaji tangu mitambo ya kutambua chuma iwekwe baada ya kuuwawa kwa polisi tare 14 mwezi huu karibu na eneo linalofahamika kama Haram al-Sharif kwa waislamu na Temple Mount kwa wayahudi.

 Wapalestina wanne waliuawa na raia watatu wa Israel kuuliwa kwa kuchomwa visu na mpaletina ambaye alidai alikuwa akilipiza hatua za Israel eneo takatifu.

MAALIM SEIF AMVAA SPIKA WA BUNGE LA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JOB NDUGAI

Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwamba hatua ya Spika kuwavua ubunge , udiwani na kuteua wengine wapya inalenga kudhoofisha kambi ya wabunge wa CUF na Ukawa.


 Amesema Watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hata kama hicho kinachoitwa ‘kuwafukuza uanachama’ wabunge halali wa CUF kingekuwa kiko sawa, hatua kama hiyo hufuata taratibu zote za kisheria na kikanuni za Bunge kujiridhisha kwanza.


 “ Spika Job Ndugai anadhani Watanzania ni vichaa wamuamini kuwa alishachukua hatua ya kujiridhisha kuwa wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefukuzwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea na Ubunge. Ndani ya siku moja?”


 amehoji Maalim. Amesema Spika amejiridhisha vipi ikiwa hata hakuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama ambaye kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za chama na pia kwa nafasi hiyo ndiye katibu wa vikao vya Mkutano Mkuu wa Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama?

 Amesema yeye kama katibu, alimuandikia Spika Ndugai barua, Jumanne, Julai 25 akimueleza kwamba hilo lililoitwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF halikuundwa na wajumbe halali wa Baraza Kuu. “Angekuwa na nia ya kweli ya kutaka kujiridhisha si hapo ndipo pangekuwa pa kuanzia kwa kuwepo kile wanasheria wanachokiita shaka inayoweza kuingia akilini yaani ‘reasonable doubt’?’’ amehoji.


 Amesema Spika Ndugai aliyapuuza yote hayo kwa sababu ni kinyume na mkakati wa Dola wa kuihujumu CUF na kuua demokrasia Tanzania. Hapo ndipo Spika Job Ndugai alipolifikisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

WILAYANI NZEGA KATIKA MKOA WA TABORA WANAWAKE WATANO WACHOMWA MOTO HADI KUFA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA.

Watu watano wameuwawa kwa kuchomwa moto katika kata ya Uchama Wilayani Nzega Mkoani Tabora na watu wanaosaidikiwa kuwa ni Sungusungu huku wakidaiwa wameuliwa kutokana na imani za kishirikina.


 Kufuatia Mauaji hayo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agreya Mwanri, amezitaka Kamati za Ulinzi na usalama ngazi ya Mkoa na ile ya Wilaya ya Nzega kusitisha shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na sungusungu katika kijiji hicho.

 Mwanri amesema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya sungusungu hao kutekeleza mauaji hayo ya watu watano ambao wote ni wanawake wakituhumiwa kuwa ni washirikina.

 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa katika kuendelea kuchunguza tukio hilo jeshi hilo linawashikilia baadhi ya viongozi wa kijiji hicho ili kuweza kubaini waliotekeleza tukio hilo.

HALI YA MAZINGIRA MAGUMU KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO CHA GETITHEMAN MKOANI KATAVI.

Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha kulelea watoto cha Getithe man kilichopo kata ya Litapunga wilaya ya Mpanda mkoani katavi wameiomba jamii kuwasaidia mahitaji mbali mbali, ili waweze kuendesha maisha yao.

 Mpanda redio imefika katika kituo hicho na kuzungumza na watoto hao ambao wamesema kua kwa muda mrefu hawana mabweni, pia wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa chakula, pamoja na huduma nyinginezo.

 Watoto walisema “mimi ningependa watusaidie watupe moyo pia tatizo tunalokabiliana nalo usafiri wa kwenda shule,utoaji wa huduma pia changamoto zetu tunaukosefua wa mabweni na vifaa vya shule na baadh ya mahitaji mengine sisi kama watoto tunaomba serekali watusaidie”.

 Kwa upande wa msemaji wa kituo hicho ambaye amejitambulisha kwa jina moja la Mozes amekili kuwepo kwa changamoto hizo na kufafanua baadhi ya hatua zilizoanza kuchukuliwa kuwa ni pamoja na kuishirikisha jamii na Serikali katika kuchangia maendeleo ya kituo hicho.

 Mozes alielezea “tumepata mtazamo mwingine kwamba tunaweza kuboresha mazingira ya kuwalea watoto hao ila ni tabu ya mabweni tunachangamoto hiyo kubwa ambayo mabweni pia tunashukuru mungu mpaka wakati huu tunaendeleza mchakato wa ambao tunatarajia kupata mabweni ambayo ni nyumba mbili za watoto wakiume na wakike”

 Kituo hicho kimeanzishwa mwaka 1993 kwa mara ya kwanza kikiwa na idadi ya watoto wapatao miamoja yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu.

Wednesday, 26 July 2017

Trump: Wanaobadili jinsia hawawezi kuhudumu katika jeshi

Rais Trump ametangaza kuwa Jeshi la Marekani halitawaruhusu watu wanaobadilisha jinsia zao kuendelea kufanya kazi ya aina yoyote jeshini.

 Katika taarifa kadhaa kwenye mtandao wa Twitter, Bwana Trump alisema kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kufanya mashauriano na maafisa wa vyeo vya juu jeshini.

 Alisema watu wanaobadilisha jinsia zao wataligharimu jeshi kimatibabu na kuvuruga maisha ya kawaida jeshini.

Mapema mwezi huu waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis, alisimamisha uajiri wa watu wanaobadilisha jinsia zao kwa miezi sita

Utafiti: Kupungua kwa viwango vya mbegu za kiume kutasababisha kutoweka kwa binadamu.

Watafiti wanaochunguza matokeo yao tafiti 200 wanasema kuwa upungufu wa kiwango cha mbegu za kiume miongoni mwa Wanaume kutoka Marekani kaskazini, Ulaya, Australia na New Zealand ufikia nusu yake.

Baadhi ya wataalam wanashaka kuhusu matokeo hayo. Lakini mtafiti bingwa anayeongoza utafiti huo Dkt Hagi Levine anasema kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kile kitakachofanyika katika siku za usoni.

 Dkt. Levine ambaye ni mtaalamu wa magonjwa alisema kwamba iwapo mwenendo huo utaendelea basi huenda binadamu wakatoweka. Utafiti huo ambao ni miongoni mwa tafiti kubwa ulileta matokeo ya tafiti 185 kati ya 1973 na 2011.

 ''Iwapo hatutabadili mienendo yetu ya kuishi mbali na kemikali na mazingira yetu ,nina wasiwasi mkubwa kuhusu kile kitakachofanyika siku za usoni''.

 Hatimaye tutakuwa na tatizo hususan na uzazi kwa jumla na huenda ikawa kutoweka kwa binaadamu. Wanasayansi ambao hawakushirikishwa katika utafiti huo wameusifu ubora wake lakini wanasema kuwa huenda ni mapema mno kutoa tangazo hilo.

Dkt. Levina kutoka chuo kikuu cha Hebrew mjini Jerusalem alibaini kupungua kwa asilimia 52.4 ya manii huku asilimia 59.3 ya mbegu za kiume kutoka kwa wanaume kutoka maeneo ya Marekani kaskazini, Ulaya, Australia na New Zealand yakishuka zaidi.

Madiwani wa halmashauri ya Mpanda watakiwa kutatua migogoro ya ardhi katika kata zao.

MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda wametakiwa kutatua migogoro ya ardhi na mipaka katika kata zao.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Hamad Mapengo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Idala ya maji iliyopo Manispaa ya Mpanda ambapo ameeleza kuwa suala hilo litasaidia kupunguza kero zisizo za lazima kwa wananchi.

  Mwenyekiti alisema “Maeneo ya uwekezaji lazima yatambuliwe vizuri ili kuweka mikataba ambayo itakuwa na tija katika jamii na kuongeza mapata katika halmashauri nzima pamoja na wananchi wote”

 Aidha ameongeza kusema kuwa Madiwani kama wawakilishi katika kata zao wanafulsa kubwa ya kuzungumza na wananchi na kufikia muafaka kuhusiana na njia mbadala za kumaliza migogoro hiyo.

 Kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku moja tu Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiwa mkoani Singida katika ziara kuwataka viongozi pamoja na watendaji kushughurikia kero za wananchi kwa wakati.

Tuesday, 25 July 2017

MIRADI YAIPAISHA MKOA WA TABORA.

Raisi John Pombe Magufuli

RAIS John Magufuli ameweka jiwe la msingi katika miradi mikubwa miwili ambayo ni mradi wa maji kutoka Ziwa Viktoria kwenda miji ya Tabora, Igunga na Nzega, na mradi wa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora, na kufungua barabara mbili za Tabora – Nyahua na Tabora – Puge – Nzega, miradi ambayo ikikamilika, itabadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wakazi wa Tabora na maeneo jirani.

 Mradi wa maji kutoka Ziwa Viktoria utatekelezwa kwa muda wa miezi 30 kwa gharama ya Sh bilioni 600 ikiwa ni mkopo kutoka Serikali ya India na utazalisha takribani lita milioni 80 za maji kwa siku kwa ajili ya wakazi wa Tabora ambao kwa sasa wanahitaji lita milioni 36 na pia utamaliza tatizo la maji katika miji ya Igunga, Nzega, Tinde, sehemu ya Wilaya ya Uyui, Shinyanga Vijijini na vijiji 89 vilivyo kando ya mabomba ya mradi huo. “Waziri Mkuu wa India ametoa Sh bilioni 601 kwa ajili ya kusadia usambazaji wa maji nchini hususani mkoani Tabora. Mradi huu ukikamilika utawanufaisha watu takriban milioni mbili,” alieleza Rais Magufuli wakati akizungumza na maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jana jioni.

 Dk Magufulia alisema usambazaji wa maji mkoani humo ni matokeo ya ahadi ya Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi aliyoitoa mwaka jana alipofanya ziara nchini. Pia alimuomba Balozi wa India nchini, Sandeep Arya kumfikishia shukrani zake na za Watanzania kwa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi kwa kutoa mkopo wa Sh bilioni 600 kwa ajili ya kufanikisha mradi huo wa maji na pia kutoa fedha nyingine Sh trilioni 1.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi mingine 17 nchini.

 Dk Magufuli amemtaka mkandarasi anayejenga mradi wa maji kutoka ziwa Viktoria kuharakisha kazi hiyo na kuikamilisha kabla ya miezi 30 ili wananchi wa Tabora na maeneo yanayosubiri maji ya mradi huo waanze kunufaika mapema. Kwa mujibu wa hotuba ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bungeni kwa mwaka 2017/18, serikali imejipanga kuwapatia huduma ya maji wakazi wa miji ya Tabora, Igunga, Uyui, Nzega, Tinde na Sikonge pamoja na vijiji 89 vilivyopo kwenye eneo la kilometa 12 kutoka bomba kuu la mradi wa Kashwasa.

 “Mradi ni wa malengo ya muda mrefu ya kuwapatia huduma ya maji ya uhakika wananchi wapatao milioni 1.1. Mradi huu ukikamilika utaongeza hali ya upatikanaji wa maji katika Mji wa Tabora kutoka asilimia 80 hadi asilimia 100; Uyui (asilimia 30 hadi asilimia 100); Igunga (asilimia 62 hadi asilimia 100).

 “Nzega kutoka asilimia 58 hadi asilimia 100 na Mji wa Tinde kutoka asilimia 45 hadi asilimia 68. Awamu ya pili ya mradi itahusu kupeleka maji katika Mji wa Sikonge kutoka Ziwa Victoria,” alisema Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge alipowasilisha hotuba yake bungeni.

 Ili kuhakikisha wananchi wa Tabora wanapata maji safi na salama kwa haraka, Rais Magufuli alisema kwamba mradi huo umekabidhiwa kwa wakandarasi watatu ili ukamilike ndani ya muda wa miaka miwili na nusu. Kukamilika kwa mradi huo wa maji, siyo tu utawapatia wakazi hao zaidi ya milioni mbili maji safi na salama, lakini pia utawaepushia wananchi na maradhi yaliyokuwa yakiwasumbua kutokana na maji yasiyo salama kama vile kichocho, homa ya matumbo na kipindupindu.

Aidha, Rais Magufuli alifanya ufunguzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora, na kuiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kujenga jengo la abiria 500 badala ya jengo lililopo sasa la abiria 50.
 Pia amegiza urefu wa uwanja uongezwe hadi kufikia kilometa 2.5 badala ya kilometa 1.9 zilizopangwa ili ndege kubwa na ndogo ziweze kuutumia uwanja huo. Mradi wa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia sasa na ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa kwa awamu tatu katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na usanifu wa viwanja vingine 11 katika mikoa mbalimbali nchini kwa gharama ya Sh bilioni 69.7.

Imeelezwa kuwa uwanja huo kwa sasa unatumiwa na ndege zenye uwezo wa kubeba abiria hadi 70, lakini kukamilika kwa upanuzi wa uwanja huo na kufungwa taa, kutawezesha ndege kubwa zenye uwezo wa kubeba hadi abiria 150 kutua, lakini pia uwanja utakuwa ukitoa huduma kwa saa 24 tofauti na sasa. Imeelezwa kuwa maboresho hayo yataongeza ufanisi katika huduma kwa kuwa usafiri wa ndege utakuwa wa uhakika na gharama zinaweza kushuka kwa kiasi kikubwa.

 Mradi mwingine ulizinduliwa na Rais Magufuli jana katika siku yake ya mwisho ya ziara yake mkoani Tabora ni Nzega – Tabora na Nyahua – Chaya. Dk Magufuli alisema kwamba serikali itakuwa imetumia zaidi ya Sh bilioni 600 kukamilisha miradi ya barabara mkoani Tabora, ambayo pia ilimshuhudia akizindua barabara ya Kaliua – Kazilambwa, Urambo – Tabora, na kuagiza barabara ya Kaliua - Urambo kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami ndani ya mwezi mmoja.

Barabara ya lami ya Tabora – Nyahua yenye urefu wa kilometa 85 imejengwa kwa gharama ya Sh bilioni 123.773 na barabara ya Tabora – Puge – Nzega yenye urefu wa kilometa 114.9 imejengwa kwa gharama ya Sh bilioni 160.515, fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania.

 Aidha, Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Tabora kuwa serikali yake imejipanga kutekeleza ahadi alizotoa ikiwemo kujenga reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) itakayoanzia Dar es Salaam – Morogoro – Dodoma – Tabora hadi Kigoma ili kurahisisha usafiri na kukuza biashara ya ndani na nje ya nchi na amewataka wote waliojenga majengo katika hifadhi ya reli kujipanga kuondoa majengo yao kwa hiari kwa kuwa serikali haitawalipa fidia yoyote.

 Upanuzi wa uwanja huo wa ndege na ujenzi wa reli ya kisasa utazidi kuufanya Mkoa wa Tabora kuimarika kiuchumi na kufungua fursa za kiuchumi za wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani pamoja na nchi jirani hasa zile za Maziwa Makuu. Leo ziara ya Rais Magufuli imeendelea mkoani Singida ambako amefungua mradi wa barabara ya Manyoni – Itigi yenye urefu wa kilometa 89.3.

MKUTANO BAINA YA TANZANIA NA CHINA KUHUSU MFUMO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI.


MKUTANO wa majadiliano ya pamoja baina ya Tanzania na China kuhusu mfumo mpya wa vyombo vya habari unafanyika asubuhi hii jijini Dar es Salaam.

 Mjadala huo unawahusisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari vikiwepo Magazeti, Televisheni, Redio na wale wanaoendesha mfumo mpya wa habari kupitia mitandao ya kijamii hasa Bloggs.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani ndiye mgeni rasmi katika mkutano huo ulioandaliwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na serikali ya China.

 Balozi wa China, Lu Youqing na Naibu Waziri wa China mwenye dhamana ya usimamizi wa mawasiliano ninmiongoni mwa viongozi waliohudhuria.

JARIBIO LA KIFAA KINACHOWALINDA WANAWAKE DHIDI YA HIV LAFAULU.








Watafiti nchini Marekani wanasema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani walitumia mpira wa mviringo kujilinda na virusi vya HIV limefanikiwa. Utafiti zaidi sasa utafanyiwa vijana barani Afrika.

Wasichana walitumia mviringo wa plastiki uliowekwa dawa za kujilinda na ukimwi , ambao hulibadilishwa kila mwezi baada ya kipindi cha miezi sita.


Ni mojawapo ya mipango ya kutengeza kifaa ambacho wanawake watatumia kujilinda dhidi ya maambukizi ya HIV ili wasiweze kuwategemea wanaume kuvaa mipira ya kondomu.
 Wakiripoti ugunduzi huo mpya kuhusu virusi vya HIV mjini Paris, watafiti walisema kuwa wanafurahi kwamba wasichana hao walitumia mvirongo huo na kusema kuwa wameupenda.

 Wanawake na wasichana walio na kati ya umri wa miaka 15-24 wanadaiwa kuwa moja kwa tano ya visa vyote vya maambukizi ya HIV duniani. Takriban wanawake 1000 huambukizwa virusi kila siku katika Afrika ya jangwa la sahara.

Monday, 24 July 2017

MAOMBI YA LISSU KUFIKISHWA MAHAKAMANI YAPANGIWA JAJI


Wakati Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiendelea kushikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi, maombi yaliyofunguliwa na mawakili wanaomwakilisha, wakiongozwa na Fatma Karume, yamepangiwa jaji wa kuyasikiliza.

 Maombi hayo yaliyofunguliwa Mahakama Kuu Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita ya kuomba mahakama iiamuru Serikali, imfikishe mahakamani Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa Chadema.
 Maombi hayo yaliyofunguliwa chini ya hati ya dharura yamepangwa kusikilizwa na Jaji Ama-Isario Munisi.
Hata hivyo habari kutoka masjala ya jinai ya Mahakama Kuu zinasema kuwa bado maombi hayo hayajapangiwa tarehe ya kusikilizwa kwa kuwa hadi sasa jalada hilo liko kwa Jaji Munisi.
 Hadi sasa haijajulikana kama maombi hayo yatasikilizwa leo au lini.

 Mawakili hao wa Lissu walifikia uamuzi wa kufungua maombi hayo baada ya polisi kumshikilia kwa muda mrefu bila kumfikisha mahakamani.

 Lissu alikamatwa na polisi tangu Alhamisi ya juma lililopita, wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kusafiri kuelekea Rwanda kuhudhuria mkutano wa vyama vya wanasheria Afrika.

RAIS WA POLAND APINGA MISWADA TATA ILIYOPITISHWA BUNGENI

Rais wa Poland Andrzej Duda ametumia kura yake ya turufu kupinga miswada miwili kati ya mitatu inayoufanyia mageuzi mfumo wa idara ya mahakama nchini humo.

 Hatua hiyo inatuliza hofu kuwa chama tawala cha Sheria na Haki kitahujumu mgawanyo wa madaraka.

 Duda amesema ataurudisha bungeni mswada kuhusu Mahakama ya Juu pamoja na ule unaohusu Baraza la Kitaifa la Mahakama.

Kumekuwa na maandamano nchini Poland tangu miswada hiyo ilipopitishwa na mabunge yote mawili. Wakosoaji walisema sheria hizo zingeathiri uhuru wa mahakama kwa kuwapa wanasiasa nguvu za kuwaajiri na kuwafuta maafisa wa mahakama.

 Aidha, wachambuzi wanasema uamuzi wa Duda unamweka katika mgongano na kiongozi halisia wa nchi hiyo ambaye ni kiongozi wa chama tawala cha PiS lakini hana wadhifa rasmi serikalini.

Vitisho vya China vyasababisha Vietnam kusitisha uchimbaji wa gesi baharini



Vietnam imesitisha shughuli ya uchimbaji gesi katika eneo linalozozaniwa kusini mwa bahari ya China, kufuatia vitisho vikali kutoka China.

Taarifa zinaiambia kuwa kampuni iliyokuwa ikiendesha uchimbaji huo iliamrishwa kuondoka eneo hilo. Inajiri siku chache baada ya kampuni ya Respol kusema kuwa imegundua gesi nyingi.

 Ripoti zinasema kuwa wakurugenzi wa Respol waliambiwa wiki iliyopita na serikali wa Viertman kuwa China ilikuwa imetisha kushambulia vituo vyake katika visiwa vya Spratly ikiwa uchimbaji huo haungesitishwa.

 China inadai kuwa karibu eneo lote la kusini mwa bahari ya China ni lake, visiwa ambavyo pia vinavyodaiwa na mataifa mengine.

Graca Machel kumushtaki daktari wa Nelson Mandela


Mjane wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela Graca Machel, amesema atamshtaki daktari wake bwana Mandela, kutokana na taarifa alizochapisha kwenye kitabu kuhusu siku za mwisho za Mandela.
Daktari huyo Vejay Ramlakan aliongoza kikosi kilichomhudumia Mandela hadi kifo chake Disemba mwaka 2013.
 Radio ya taifa nchini Musumbiji ilitangaza taarifa iliyotolewa na wakfu wa Bi Machel ikilaani kitabu hicho vikali.
Bi Machel alisema kuwa kitabu hicho kinakiuka heshima ya bwana Mandela. Kitabu hicho kimeandika taarifa kuhusu siku za mwisho kabla ya kifo cha Mandela.

 Kimetaja kutokuwepo kwa maelewano kati ya madaktari na familia ya Mandela. Bi Mandela anasema kuwa kitabu hicho kilikiuka siri iliyo kati ya daktai na mgonjwa.

Mlinzi wa Israel amuua mshambuliaji aliyemvamia nchini Jordan


Mlinzi muIsrael amempiga risasi na kumuua mshambuliaji raia wa Jordan ambaye alimvamia karibu na ubalozi wa Israel nchini Jordan. Mtu mwingine raia wa Jordan naye aliuwawa wakati wa ufyatuaji risasi kwa mujibu wa Israel.
 Mlinzi huyo aliripotiwa kujeruhiwa. Mshambuliaji alikuwa ni seremala aliyekuwa akifanya kazi katika jengo uliko ubalozi wa Israel. Hiki ni moja ya visa vibaya zaidi kati ya nchi hizo tangu zisaini mkataba wa mani mwaka 1994.
Mamlaka za Israel hazijazungumzia kisa hicho. Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman.

Siku ya Ijumaa maelfu ya watu waliandamaa mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem. 

Saturday, 22 July 2017

KATA YA MPANDA HOTEL ILIYOPO MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI KUTUMIA SHILINGI MILIONI 21.1 KUMALIZA TATIZO LA MAJI KATIKA MITAA YAKE.

KATA ya Mpanda Hotel iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,imepata shilingi milioni 21.1 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la maji ambalo limeikumba kata hiyo kwa muda mrefu.

 Akizungumza katika Mkutano wa Hadhara ambao umefanyika kata ya Mpanda Hotel,Diwani wa Kata hiyo Mh.Willium Liwali,amesema kiasi hicho kimetengwa na serikali ili kusaidia kumaliza tatizo la maji katika kata hiyo.

 ‘’Kwa kweli Mkuu wa Wilaya hali ni mbaya katika kata ya Mpanda Hotel ambapo tatizo kubwa lililopo kuliko yote katika Mitaa ya Mpanda Hotel,msasani na Tambukareli ni maji ambapo tari tuna milioni 21.1 kwa ajili ya kujenga magati uli kupata maji ya kutosha kuhudumia wakazi zaidi ya 11,000 waliopo kata ya Mpanda Hotel’’

. Aidha Mh.Liwali amesema kata ya Mpanda Hoteli imekuwa na tatizo la utengenezaji wa barabara ambayo imesababishwa na maeneo hayo kuwa bado hayajapimwa ambapo pia amesema ukosefu wa kituo cha huduma za afya kwa wakazi wa kata ya Mpanda Hotel limekuwa tatizo.

 Kata ya Mpanda Hotel inaundwa na mitaa mitatu ambayo ni Mpanda Hotel,Msasani na Tambukareli ambayo kwa ujumla ina wakazi zaidi ya elfu kumi na moja.

Friday, 21 July 2017

FATMA :LISSU KANYIMWA DHAMANA KWA AMRI TOKA JUU.

DAR ES SALAAM.

 Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema polisi walikataa kumpa dhamana mteja wake jana jioni mara baada ya kukamatwa akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.

 Karume alisema baada ya kufikishwa polisi, Lissu alitakiwa kuandika maelezo na kupewa onyo kwa kosa la uchochezi.

“Lakini cha ajabu mpaka sasa hivi hatujaambiwa Lissu kamchochea nani, kosa la uchochezi lazima lilete madhara au uhalifu kwa wengine na ni lazima liwe la uhalifu.”

 Amesema  hata walipouliza nani anayeweza kuruhusu mteja wake apate dhamana hiyo waliambiwa imezuiwa kwa amri kutoka juu.

 Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) alikuwa akielekea Kigali, Rwanda, katika mkutano wa wanasheria wa Afrika. Karume amesema uchochezi lazima liwe ni jambo la uhalifu na mpaka sasa polisi hawajamwambia Lissu aina hiyo ya uchochezi.

 “Hili ni jambo la kisiasa, Lissu amezuiwa kwenda kwenye mkutano wa wanasheria wa Afrika, jambo hilo linawafanya hata wanasheria wote wa Afrika kujua mwenzao kakamatwa na Serikali,” amesema.

 Kwa mujibu wa Karume, Lissu amewapa ujumbe Watanzania akisema Aluta Continua, na kuwa yupo sawa.

Taifa la Tanzania latajwa kuwa eneo bora la Safari za watalii Afrika.

Taifa la Tanzania limetajwa kuwa kivutio kizuri cha safari za watalii barani Afrika kulingana na mtandao wa SafaricBookings.com ambao ndio mtandao mkubwa wa ukuzaji wa safari za Afrika.

 Mtandao huo ulifanya tathmini ya zaidi ya wataalam 2500 na wale walioshiriki katika safari hizo kabla ya kutangaza kuwa Tanzania ndio eneo bora la safari mwaka 2017.

 Tathmini hizo ziliandikwa na watalii walioenda safari pamoja na wataalam bingwa wa Afrika. Mtandao huo unasema kuwa uchanganuzi huo pia ulibaini kwamba Tanzania ilipata umaarufu wake kutokana na idadi ya wanyama mbali mbali.

 Watu maarufu katika miezi ya hivi karibuni wamekuwa wakizuru taifa hilo wakitembelea maeneo tofauti ya vivutio vya utalii nchini Tanzania.

 Watu hao ni mwanamuziki maarufu Usher Raymond, aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United na Real Madrid David Beckham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho , mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin na nyota wa filamu kutoka Marekani Will Smith na Harrison Ford. Walitembelea mbuga za Serengeti na mlima kilimanjaro.

 Mtandao huo uliitaja Zambia kuwa taifa lenye kivutio kizuri cha misitu huku wataalam wote wakikubaliana kwamba mazingira ya misitu nchini humo mi mazuri zaidi. Vilevile Zambia pia ilitajwa kuwa taifa lenye maisha bora ya ndege.
Namibia na Kenya zilitajwa kuwa bora katika mandhari mazuri pamoja na ndege waliopo mtawalia. tathimini kutoka Bbc swahili

Thursday, 20 July 2017

MSICHANA AUAWA, AFUNIKWA MFUKO WA SANDARUSI KISHA KUZIKWA KISA KAGOMA KUOLEWA MKOANI RUKWA.

MSICHANA asiyefahamika jina wala umri wake ameuawa kwa kipigo na kisha mwili wake kufukiwa kwenye shimo huku ukiwa umewekwa kwenye mfuko wa sandarusi.

Tukio la mauaji ya msichana huyo lilitokea Julai 18 majira ya saa mbili asubuhi katika kijiji cha Kate kata ya Kate wilayani Nkasi mkoani Rukwa ambapo uvumi ulienea kijijini hapo kuwepo kwa mauaji na baada ya uchunguzi ndipo lilipogundulika shimo na kufukiwa porini umbali wa kilomita moja kutoka kijijini.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando alisema baada ya kulifukua shimo hilo walikuta mwili wa mwanamke huyo na baada ya uchunguzi wa kidaktari mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha matatu kichwani ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni panga.

 Kamanda Kyando alidai kuwa marehemu alifika kijijini hapo akitokea jijini Dar es salaam ambapo inadaiwa ni mwanafunzi na kufika kwa mwenyeji wake aliyejulikana kwa jina la Samwel Selemani na kumtambulisha kwa jirani zake kuwa ni mpenzi wake.

 "Waliendelea kuishi pamoja baada ya muda kijana huyo alitoweka nyumbani na kuelekea kusikojulikana na mwanamke mwenyewe hakuonekana na kuwa siku chache za nyuma kulitokea ugomvi kati mwanaume na marehemu ambapo mwanamke alikuwa akiomba nauli ya kurudi jijini Dar es salaam kwa madai kuwa anataka arudi shule lakini mwanaume ambaye ni mtuhumiwa alikataa kuitoa nauli hiyo akidai kuwa hataki mpenzi wake huyo aondoke",alieleza Kamanda huyo.

 "Baada ya mvutano wa muda mrefu ndipo mtuhumiwa alidai kumuua mapenzi wake huyo na kuufukia mwili wake kwani hakuwa tayari mwanamke huyo aondoke kwani yeye alitaka waanze kuishi pamoja wakati mwanamke huyo alikuwa hayupo tayari kwa madai kuwa ni mwanafunzi.

 Marehemu hakuweza kutambulika na kuzikwa eneo la tukio,huku mtuhumiwa aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake hajapatikana mpaka hivi sasa na jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta na iwapo atakamatwa afikishwe mbele ya sheria.

MKUU WA USALAMA BARABARANI PWANI ATUMBULIWA.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.

Masauni alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo jana, kwa ajili ya kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana.

 “RTO ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutaki uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania,” alisema Masauni.

 “Mwaka jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria.”

 Aidha Masauni mara baada ya ukaguzi wa kituo hicho, aliendelea na ziara yake mkoani Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa aina hiyo mjini Chalinze na baadaye Msata na kuimalizia ziara yake Bagamoyo.
Habari toka Tanzania today

Seneta John McCain apatikana na saratani ya ubongo.

Seneta John McCain


Seneta wa chama cha Republican John McCain amepatikana na saratani ya ubongo na anatafuta matibabu kulingana na duru za offisi yake.
Matibabu hayo huenda yakashirikisha matumizi ya dawa ama mionzi kulingana na daktari wake. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 80 yuko katika hali nzuri akiendelea kupata afueni nyumbani. Uvumbe huo ulipatikana wakati wa upasuaji wa kuondoa damu ilioganda juu ya jicho lake la kushoto. McCain ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita nchini Vietnam pia alitumikia miaka mitano jela.
 Seneta huyo aliyehudumu kwa mihula sita na kuwa mgombea wa urais wa chama cha Republican 2008 alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Phoenix katika jimbo la Arizona siku ya Ijumaa.

 Uchunguzi wa tishu ulibaini kwamba uvimbe wa ubongo unaojulikana kama glioblastoma ulisababisha damu hiyo kuganda kulingana na taarifa ya kliniki hiyo ya Mayo. Madaktari wa Seneta huyo wanasema kuwa anaendelea kupona kutoka kwa upasuaji huo na afya yake iko shwari, iliongezea.

Matibabu yake yatashirikisha utumiaji wa dawa na mionzi. Glioblastoma ni uvimbe mbaya wa ubongo na huongezeka kutokana na umri wa mtu ukiwaathiri wanaume wengi zaidi ya wanawake. habari kutoka Bbc swahili

Magufuli avipatia vituo vya mafuta wiki mbili kufunga mashine za kielektroniki (EFDs)

Rais wa Tanzania  Mh. John Pombe Magufuli
Wamiliki wa vituo vyote vya mafuta nchini Tanzania wamepewa siku 14 kufunga na kuanza kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti la sivyo wafutiwe leseni.

 Rais Magufuli, ambaye ametoa agizo hilo jana, ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhakikisha vituo vyote vya mafuta nchini vinatumia mashine hizo ambazo kwa Kiingereza zinafahamika kama Electronic Fiscal Petrol Printer na kusisitiza kuwa wamiliki watakaokiuka agizo hilo vituo vyao vifungwe na kufutiwa leseni.

 "Na kwa hili natoa siku 14, wale wenye vituo vya mafuta wote, uwe upo Chato, uwe Biharamulo, uwe Kagera, uwe Dar es Salaam hakikisha una hiyo mashine, ndani ya siku 14," amesema Dkt Magufuli. Mwishoni mwa wiki Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ilivifungia vituo vya mafuta kutokana kutotimiza vigezo baada ya kutofunga mashine za kielektroniki kwenye pampu za mafuta.

 Kufikia Jumatatu, vituo vipatavyo 241 nchini humo vilikuwa vimefungwa na kusababisha tatizo la upatikanaji wa mafuta katika miji mingi Tanzania. Mamlaka ya mapato ilisema wamiliki wa vituo hivyo wamekuwa wakikwepa kulipa kodi kwa kutofunga mashine hizo. Wakati wa kuanza kutekelezwa kwa agizo hilo Jumapili, vituo 710 vilifungiwa nchi nzima lakini baadaye vituo 469 vikafunguliwa baada ya kulipia mashine hizo kwa mawakala watano walioidhinishwa kufunga mashine hizo kwa vituo vyote takribani 1800 kwa nchi nzima.

 Zoezi hilo la kufunga na kutumia mashine hizo lilistahili kuwa limekamilishwa na vituo vyote kufikia Septemba 30 2016 lakini kukawepo na malalamiko toka kwa TAPSOA (Umoja wa wauza mafuta ya petroli na diseli rejareja Tanzania) kuwa mashine hizo zilikua zikiuzwa ghali lakini pia zilikua na shida ya mtandao hivyo zingekwamisha mauzo.

 Kwa mujibu wa Tapsoa waliafikiana na TRA kuzitatua changamoto hizo kabla ya kuendelea na zoezi hilo hivyo kuwapa wafanya bishara hao wa mafuta nafasi ya kuendelea na biashara.
habari kutoka Bbc  swahili

Wednesday, 19 July 2017

MKUU WA MKOA AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA KIWANDA CHA MAZIWA MKOANI KATAVI.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha maziwa cha Kashaulili Livestock Keepers Saccos kinachojengwa katika kata ya Makakanyagio Halmashauli ya Manispaa Mpanda.

 Katika uzinduzizi huo,Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi kujitokeza kwa wingi kuwekeza viwanda ili kujenga Tanzania ya viwanda kama serikali ya awamu ya tano ilivyoagiza.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa kiwanda hicho chenye wanachama zaidi ya 50 Andrea Fumbi amesema,kiwanda hicho kitagharimu zaidi ya shilingi milioni 600 kwa udhamini wa Benki ya TIB,ambapo kinatarajia kuzalisha maziwa ifikapo September mwaka huu.




 Wakati huo huo Afisa mazingira Manispaa ya Mpanda Bw.Said Mandua pamoja na mambo mengine amewatoa hofu usalama wa mazingira katika makazi wakazi wa Manispaa ya Mpanda kutokana ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kipo nje kidogo ya mita 60 kutoka chanzo cha mto mpanda.





 Mpaka sasa Mkoa wa Katavi una viwanda viwili vya maziwa ambapo kimoja kilichopo kata ya Ilembo kilizinduliwa na na mwenge wa uhuru mwezi April mwaka huu.

POLISI AFYEKWA MKONO KWA KUGOMBEA MWANAMKE


Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, linawashikilia watu wawili wakazi wa Mtaa wa Nkende mjini Tarime wakidaiwa kumkata mkono Mkaguzi wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana-River cha nchini Kenya, James Mnuve (50), wakati wakimgombania mwanamke.

 Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kukatwa mkono Mkaguzi huyo wa Polisi wa nchini Kenya.

Mwaibambe alidai kuwa tukio hilo lilitokea Julai 13 mchana katika mtaa wa Nkende mjini Tarime ambapo vijana hao walitenda kosa hilo.

 Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Michael Omahe, anayedaiwa kumtorosha mwanamke huyo, Anne Njeri, kutoka Kenya na kumleta Tanzania kisha kuishi naye kinyumba huku akisaidiana na rafiki yake, Daniel Onchiri.

 “Mwanamke huyo (Njeri) anadaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi pia na askari James Mnuve na walikuwa wakiishi huko Tana River nchini Kenya, baada ya kuondoka, Julai 13 mchana askari huyo alimfuatilia kutoka Kenya hadi Mtaa wa Nkende, Tarime alipokuwa anaishi na kijana aliyemtorosha (Michael Omahe),” alisema Kamanda.

 Akaongeza, “Alipofika Mtaa wa Nkende alimkuta Michael, pamoja na rafiki yake huyo wakiwa na mwanamke huyo na hapo ndipo ugomvi ulipoanza kwani askari James alitaka kuondoka na mwanamke huyo na zikazuka vurugu kubwa na kusababisha Mnuve kukatwa kwa kutumia panga.”

 Aidha Kamanada huyo alisema kuwa, “Jeshi la Polisi tulifika kwenye eneo la tukio mapema na kuweza kuwakamata watuhumiwa wote watatu; Marandi, Ochiri na mwanamke huyo na kisha tukawahoji kabla ya kuwafikisha mahakamani huku majeruhi akiwa amepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa matibabu.” Gazeti hili lilipomhoji majeruhi James alidai kuwa yeye ni Inspekta wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana River nchini Kenya na mwanamke huyo, Njeri Wanjoi, ni mke wake.

AMUUA MKEWE WA KWA KTU CHENYE NCHAA KALI MKOANI MOROGORO

                                  Kamanda mkuu wa mkoa wa morogoro,Urich Matei
POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu tisa kwa tuhuma tofauti akiwemo mkazi wa Kijiji cha Chingholwe, Kata ta Chanjale wilayani Gairo, Bahati Malima kwa kumuua mkewe Janet Sajilo (35) kwa kuchoma na kitu chenye ncha kali sehemu ya kifuani na kufariki dunia papo hapo.

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei alisema jana kuwa mauaji hayo yalifanyika juzi saa sita eneo la Kijiji cha Chingholwe, Kata ya Chanjale, Tarafa ya Nongwe.

Kamanda Matei alisema chanzo cha tukio hilo ilidaiwa ni wivu wa mapenzi. Alisema baada ya mtuhumiwa kumchoma mkewe na kitu chenye ncha kali kifuani, alifariki dunia papo hapo baada ya kuvuja damu nyingi.

Hata hivyo, alisema chanzo halisi kilichosababisha mume huyo kuchukua uamuzi wa kumchoma mkewe na kitu chenye ncha kali kifuani, hakijafahamika na uchunguzi zaidi unaendelea na hatua za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zitafuatwa. Aidha, Haji Athuman (28) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Makambako,

 Mkoa wa Njombe anashikiliwa na Polisi akiwa na simu aina mbalimbali zipatazo 748. Simu hizo ni Tecno, Itel na Ditel pamoja na betri za simu 650 na chaja za simu 830.

Tuesday, 18 July 2017

VITUO VYA MAFUTA 710 VILIFUGWA NCHI NZIMA TANGU UKAGUZI WA MASHINE ZA KIELETRONIKI(EFDs).

JUMLA ya vituo 710 vya mafuta vilifungwa nchi nzima tangu ianze kazi ya kuvikagua vituo hivyo kuona kama vinatumia mashine za kieletroniki za malipo (EFDs).
 Vituo 469 kati ya hivyo vimefunguliwa baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa na Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) ambavyo ni kulipia gharama za ufungaji mashine hizo kwa mawakala walioidhinishwa na TRA kisha kuingia makubaliano ya muda maalumu wa kuhakikisha kuwa mashine hizo zimefungwa.
 Kigezo kingine ni kufunga mashine za EFPP kwa wale wote waliokwishanunua, lakini hawakufunga au waliofunga mashine hizo, lakini wakawa hawajaunganisha na pampu zao za mafuta.

Vituo vingine 241 havijafunguliwa kutokana na kushindwa kukidhi masharti ya TRA. Kwa mujibu wa Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Elijah Mwandumbya, makubaliano hayo ya muda maalumu yanamruhusu mmiliki wa kituo cha mafuta kuendelea kutumia mashine za kawaida mpaka hapo mashine za kisasa zitakapofungwa.

 Aidha, Kamishna Mwandumbya alisema wamiliki wa vituo vya mafuta ambao watashindwa kutekeleza agizo la kufunga mashine za malipo za kielektroniki za kutolea risiti kwa muda uliowekwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufungwa vitu vyao na kufikishwa mahakamani.

 Alisema muda waliopewa kufunga mashine hizo hautaongezwa na wamiliki wanapaswa kulizingatia hilo ili kuepuka adhabu, na kwamba baadhi ya wamiliki wa vituo hivyo wamekuwa siyo waaminifu kwa kuzificha mashine hizo ndani badala ya kuzifunga kwenye pampu na wengine wamezifunga, lakini hawakuziunganisha na pampu.

 Aliongeza kuwa wamiliki wa vituo vya mafuta wanatakiwa kuwasiliana na mawakala wa usambazaji wa mashine za kielektroniki na kueleza mahitaji yao ili wajulishwe gharama za mashine na gharama za kuzifunga.

 Alisema kuna jumla ya mawakala tisa waliopewa jukumu la kusambaza mashine hizo nchini na kuwataja baadhi yao kuwa ni Advatech Technologies Ltd, Pergamon Ltd na Web Technologies Ltd.

 Mwandumbya alisema asilimia 70 ya vituo vya mafuta nchini vinamilikiwa na kuendeshwa na wajasiriamali wadogo wanaojulikana kama DODO (Dealer Owned Dealer Operated). Alisema wafanyabiashara hao kupitia chama chao cha TAPSOA wanamiliki vituo vya mafuta kati ya 1,500 hadi 1,800 nchi nzima.

RAIS MAGUFULI KUZINDUA MIRADI 9.

Raisi John Pombe Magufuli
RAIS John Magufuli anatarajiwa kuzindua miradi tisa ya barabara na uwanja wa ndege ambayo itaunganisha mikoa ya Ukanda wa Kati na Magharibi nchini na nchi jirani kwa barabara za lami katika kuchochea harakati za maendeleo ya uchumi wa viwanda.

 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Ujenzi, Joseph Nyamhanga alisema jana kwa simu kwamba uzinduzi wa miradi hiyo utafanyika katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kuanzia kesho hadi 25, mwaka huu.

 Nyamhanga alisema ufunguzi wa barabara ya Kigoma – Biharamulo – Lusahunga yenye urefu wa kilometa 154 utafanyika Biharamulo Mjini mkoani Kagera kesho huku uzinduzi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Nyakanazi – Kibondo yenye urefu wa kilometa 50 utafanyikia Kakonko mkoani Kigoma, Julai 21.

 Alieleza kuwa uzinduzi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kidahwe –Kasulu yenye urefu wa kilometa 63 utafanyika Kasulu Mjini mkoani Kigoma, Julai 21 ambako pia ufunguzi wa barabara ya Kaliua – Kazilambwa yenye urefu wa kilometa 56 utafanyika Julai 23 Kaliua Mjini mkoani Tabora.

 Alisema ufunguzi wa barabara ya Urambo –Ndono – Tabora yenye urefu wa kilometa 91 utafanyika Julai 24, Tabora Mjini na ufunguzi wa barabara ya Tabora – Nyahua yenye kilometa 85 utafanyika siku hiyo hiyo.
 Aidha, Katibu Mkuu alieleza kuwa ufunguzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora utafanyika Julai 24 na ufunguzi wa mradi wa Manyoni – Itigi – Chanya wenye urefu wa kilometa 89.3 utafanyika Itigi mkoani Singida Julai 25, mwaka huu.

 Aidha, alisema ufunguzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha miundombinu ya viwanja vya ndege na usafiri wa anga nchini.Alifafanua kuwa miradi yote ya barabara imejengwa kwa fedha za ndani isipokuwa mradi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora.

 Aliongeza kuwa kuzinduliwa kwa miradi hiyo kutafungua fursa za kiuchumi ndani na nje ya nchi na kuwataka wananchi kuilinda ili waone matunda yake katika kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.



VIONGOZI WA NEMC WAFYEKWA.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba
SERIKALI imevunja Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC), sambamba na kufanya mabadiliko ya uongozi huku watumishi wanne wakisimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili. Akizungumza jana na waandishi wa habari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba alisema hatua hiyo imetokana na kukithiri kwa malalamiko ya wananchi na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

 “Tunapoelekea kuwa nchi ya uchumi wa viwanda, usimamizi wa mazingira lazima uwe imara na urahisishe na kuharakisha utekelezaji wa ujenzi wa viwanda, miradi mbalimbali na uwekezaji katika sekta zote ili kwenda kwa kasi na weledi unaotakiwa,” alieleza January.Aliongeza: “Utendaji wa NEMC umekuwa ukilegalega sana na umekuwa hauridhishi jambo ambalo limeibua malalamiko mengi kwa wawekezaji wa ndani na nje.”

Aliendelea kusema “Tumejitahidi kurekebisha hali hii na kumejitokeza nafuu, lakini bado hali haijafikia pale nilipotarajia. Nimefuatilia kwa karibu na kugundua kuwa matatizo mengi yanasababishwa hasa na usimamizi usio imara wa bodi na pia watendaji wakuu wa NEMC.
 Nimeamua kutengua uteuzi wa wajumbe wote saba wa Bodi ya NEMC ili baadaye niteue wajumbe wapya ambao wataenda na kasi na ari tunayoihitaji sasa katika kuelekea uchumi wa viwanda.” Alisema Mwenyekiti wa Bodi ambaye mamlaka yake ya uteuzi ni ya Rais, ataendelea kuwepo hadi hapo atakapoteuliwa mwingine.

 Alisema amemteua Dk Elikana Kalumanga, kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NEMC hadi hapo rais atakapofanya uteuzi kwa nafasi hiyo. Kalumunga ni Mhadhiri katika Taasisi ya Usimamizi na Tathmini ya Rasilimali Asili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alisema ili kuboresha utendaji wa NEMC, amefanya mabadiliko ya baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa kanda, kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa NEMC, Charles Wangwe kumrejesha Wizara ya Fedha na Mipango atakapopangiwa kazi kulingana na mahitaji ya serikali. Nafasi hiyo itakaimiwa na Adam Minja kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

Aliwataja wakuu wa kanda waliobadilishwa ni Jafari Chimgege aliyekuwa Kanda ya Mashariki anakwenda Kanda ya Kati- Dodoma, Goodlove Mwamsojo aliyekuwa Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu –Mbeya atakuwa Mkuu wa Kanda ya Mashariki- Dar es Salaam. Pia Dk Ruth Rugwisha aliyekuwa Mkuu wa Kurugenzi ya Ufuatiliaji na Uzingatiaji wa Sheria, sasa atakuwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa-Mwanza, Dk Vedastus Makota aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma atakuwa Mkuu wa Kanda ya Kusini- Mtwara na Joseph Kombe aliyekuwa Mkuu wa Kurugenzi ya Utafiti na Mipango wa NEMC anakwenda kuwa Mkuu wa Kanda ya Kaskazini- Arusha.
 Mabadiliko hapo pia yamemgusa Dk Menard Jangu aliyekuwa Arusha ambaye anapanda na anarudishwa Makao Makuu ya NEMC kuwa Kaimu Mkuu wa Kurugenzi ya Utafiti na Mipango huku Jamal Baruti aliyekuwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa anarudi Makao Makuu na Lewis Nzari aliyekuwa Mkuu wa Kanda ya Kusini -Mtwara, sasa anakuwa Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini- Mbeya. Pia Risper Koyi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ameteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria NEMC kuchukua nafasi ya Jandwa anayehamishiwa Kanda ya Kati-Dodoma.

 Pia Dk Yohana Mtoni ambaye ni Ofisa Mazingira Mkuu NEMC anakuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji na Uzingatiaji wa Sheria kumbadili Rugwisha ambaye anakwenda Kanda ya Ziwa- Mwanza, na Carlos Mbuta aliyekuwa Ofisa Mawasiliano Mkuu wa NEMC ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa NEMC. Aidha, January alisema wamewasimamisha kazi watumishi watumishi wanne ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma za utendaji wao; ambao ni mwanasheria Manchare Heche, Deus Katwale, Andrew Kalua na Benjamin Dotto. Alifafanua kuwa malalamiko yaliyokithiri NEMC ni ucheleweshaji na urasimu usiokuwa wa lazima katika mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA), tuhuma za rushwa katika mchakato wa ukaguzi na utengeneza vyeti ambavyo havijafuata mchakato.

 Alisema pia kumekuwapo na malalamiko ya kutokuwa na lugha nzuri kwa wateja na kuwatisha ili watoe chochote, kutumia kampuni binafsi ya watumishi wa NEMC kufanya kazi za ukaguzi kwa kisingizio cha kutokuwa na watumishi wa kutosha na kuwaelekeza wawekezaji kufanya kazi na kampuni inayomilikiwa au yenye ubia na watumishi hao.

 Katika hatua nyingine, January ameagiza ruksa ya ujenzi itolewe ndani ya siku tatu za kazi kwa miradi yote inayohusu ujenzi wa viwanda, baada ya mwekezaji kuwasilisha taarifa hitaji la ujenzi wa kiwanda kwa NEMC. Alisema kuanzia sasa miradi itakayopelekwa NEMC kuombewa cheti cha EIA ni ile ambayo tayari imefanyiwa kazi na washauri elekezi.
“Hapatakuwepo na haja ya kusajili mradi NEMC kwanza. NEMC itaweka maofisa katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na maeneo mengine muhimu ili kuhakikisha suala la kuwa na cheti cha mazingira linakuwa sehemu ya hatua za awali pale ambapo mwekezaji au mwenye mradi anapoanza kuomba vibali ingine.

 Pia ameagiza NEMC ndani ya wiki hii kufuta watu binafsi na kampuni zote za ushauri wa EIA ambayo hayana sifa au yameshindwa kutekeleza kazi zao vizuri, na ameagiza iweke bei elekezi na ukomo kwa washauri kwa kila aina ya miradi inayotakiwa kufanyiwa EIA.

Monday, 17 July 2017

WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA YA PETROL,DIZEL NA MAFUTA YA TAA MKOANI KATAVI WAMETII AGIZO LA SERIKALI KUNUNUA MASHINE ZA KIELEKTRONIKS.

WAMILIKI wa vituo vitano vya mafuta ya Petrol,Dizel na Mafuta ya taa Mkoani Katavi,wametii agizo la serikali linalowataka kununua mashine za kielektroniks(EFDs).

Hatua hiyo imethibitishwa leo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoani Katavi Bw.Michael Temu,wakati akizungumza na Mpanda Radio Ofisini Kwake.

 Wakati serikali ikitaka kila anayeuza na kununua risiti itolewe,bado kuna makundi ambayo pengine kutokana na uharaka kikazi au kutoelewa umuhimu wa kudai risti,kwao kudai risiti inaonekana ni kupoteza muda kama ambavyo baadhi leo wamebaisha wakati wakihojiana na Mpanda Radio.

 Katika hatua nyingine,Bw.Temu amesema,kwa mjibu wa kifungu cha sheria namba 38,muuzaji na mnunuzi wanatakiwa kulipa faini hadi shilingi milioni nne ikiwa itathibitika kuwa hakuna risiti iliyotolewa baada ya manunuzi.

 Wiki iliyopita,mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Katavi,ilivifungia vituo vyote vinavyouza mafuta ambapo kwa sasa biashara ya mafuta inaendelea baada ya wamiliki wa vituo hivyo kuafikiana na serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFDs.

MAPACHA WALIOUNGANA WAFAULU KIDATO CHA SITA .

Maria na Consolata waona ulemavu sio mwisho wa kutimiza ndoto zao
Pacha walioungana, Maria na Consolata wamejawa na furaha baada ya kufaulu mitihani yao ya mwisho ya kidato cha sita, katika shule ya Sekondari ya Udzungwa mjini Iringa, Kusini magharibi mwa Tanzania.

Maria na Consolata, walio na umri wa miaka 19, wamefaulu kwa kupata daraja la pili katika masomo yao ya kidato cha sita na kuwa na matumaini kuwa ndoto yao ya kuwa walimu hapo baadaye inaelekea kutimia. Maria na Consolata wameieleza BBC furaha yao:

"Tulipokea matokeo yetu tukiwa kwenye mazingira ya nyumbani tu, tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, tukaambiwa matokeo yametoka na tumefanya vizuri, tulikuwa tukiwaza kabla ya hapo, unajua kwenye mitihani ya mwisho huwezi kujiamini sana," ameeleza Consolata. Mabinti hawa wangependa kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu katika Chuo Kikuu Cha Ruaha mkoani humo. Wameeleza sababu za kuchagua chuo kwenye mkoa wanaoishi tofauti na vyuo vingine au kama ilivyo kwa wanafunzi wengine ambao wangependa kubadili mazingira.

"Kwanza tunapenda mazingira ya Iringa, hatukutaka kwenda Dar es Salaam kwa sababu ya kwanza tunapenda kuishi pamoja na walezi wetu Masista waliokuwa wanatulea tukiwa wadogo na pili mikoa mingine ni mbali na tunapoishi. Pia ni kwa sababu kwa hali yetu tulivyo hatumudu kuishi kwenye mazingira ya joto. Mji wa Iringa ni baridi, hali hii tumeizoea.

'' Maria na Consolata wanaona kuwa, hakuna linaloshindikana iwapo wazazi watawajibika ipasavyo kwa watoto wao wenye ulemavu " Wazazi washukuru Mungu kupata watoto wenye changamoto kama wao wasione kuwa na mtoto mlemavu ni laana.
 Pili wawaone kama watoto wengine na kuwapa mahitaji yao ya msingi, wawawezeshe, wawapatie nafasi ya kujiendeleza maana wakiwezeshwa wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri.''

Sunday, 16 July 2017

kipindi cha watoto kinachoenda hewani kila jumamosi.

Baadhi ya watoto waliokuja katika kipindi cha watoto kinachokuwa hewan kila siku ya jumamosi kuanzia mida ya saa 3 asubuhi mpaka mida ya saa 4 asubuhi kinachowapa fursa kubadilishana mawazo kwa kupigiana hadithi,vitendawili,nahau pia bila kusahau kuimbiana nyimbo nzuri.
jumamosi ya jana ya tarehe 15 julai 2017 kipindi chako cha watoto kilikuwa na baadhi ya watoto ambao walikuja kituoni kwetu  mpanda radio fm kilichopo kata ya mpanda hoteli.


  Walikukutana na shangazi Safina Joeli pamoja na mjomba Issack Gerald katika kipindi cha watoto pia kipindi hichi kinakutanisha watoto wa kila rika kutoka shule mbalimbali za za mkoa wa katavi.

Pia tunazinguka kila shule za halmashauri ya mpanda katika mkoa wa katavi.




Matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 yametoka Jumamosi hii, shule ya Wasichana ya Feza Girls ikiibuka na ushindi kwa watahiniwa wake 67.
Shule nyingine ni Marian Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza BOYS (Dar es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...