Monday, 3 July 2017
Bavicha mkoani Kilimanjaro limetangaza nia ya kufanya maandamano
KILIMANJARO
Baraza la Vijana la Chadema(Bavicha), mkoani Kilimanjaro limetangaza nia ya kufanya maandamano ya amani yenye lengo la kuipongeza kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Akizungumza katika mahafali ya Umoja wa Wanachama wa Chadema Vyuo Vikuu (CHASO), Mkoa wa Kilimanjaro, Katibu Mwenezi wa Bavicha, Edward Simbeyi amesema kuwa watafanya maandamano mapema mwa mwezi huu ili kuipongeza kambi hiyo.
Amefafanua kuwa wanakusudia kufanya hivyo kama chama cha CCM kilivyofanya maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kuzuia mchanga wa madini (Makinikia).
Ameeleza kuwa wabunge wa upinzani wamekuwa wakipambana kwa kujenga hoja bungeni kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao wenyewe badala ya watu wachache kunufaika nazo.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amesema kuwa maandamano yalishapigwa marufuku na hayaruhusiwi kufanyika mahali popote pale.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
Mahindi MAHINDI yanaendelea kuwadodea wakulima mkoani Rukwa baada ya wafanyabiashara na watu binafsi kuchangamkia mahindi kut...
No comments:
Post a Comment