Thursday, 6 July 2017

Ndoto za watanzania kufika fainali za kombe la cosafa zilifikia wisho Jana

Timu ya taifa Tanzania
Taifa Stars sasa inalazimika kuwania nafasi ya tatu katika michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini, baada ya leo kupoteza mchezo wake wa nusu fainali dhidi yay a Zambia. Katika mchezo wa leo, Taifa Stars imepokea ‘kipigo kitakatifu’ cha mabao 4-2 kutoka kwa Chipolopolo licha ya kucheza soka safi na la kujiamini.
Stars ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 14 kupitia kwa Eraso Nyoni aliyefunga kwa ‘free kick’ iliyomshinda kipa wa Chipolopolo na kujaa wavuni. Zambia waliamka dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza na kutumia vizuri uzembe wa mabeki wa Taifa Stars na hatimaye kufunga mabao mawili chap-chap ndani ya dakika 4 kabla ya mapumziko zikiwemo 2 za nyongeza kupitia kwa Justine Mwila na Brian Shonga. Kipindi cha pili kimeanza kwa Stars kuonesha uhai tena, lakini walikuwa ni Zambia waliopata bao la 3 kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Stars, Gadiel Michael kunawa mpira katika eneo la hatari.
 Zambia waliendelea kulisakama lango la Stars na hatimaye kupata ‘free kick’ kama ile iliyowapatia bao Taifa Stars, na wao hawakufanya ajizi kupitia kwa Chirwa, wakapachika bao la nne. Saimon Msuva aliifungia Stars bao la pili dakika ya 85, na kisha kufanya mashambulizi kadhaa ambayo hata hivyo hayakuwa na manufaa yoyote.
 Stars itakutana na timu Lesotho kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano ya cosafa yatakayochezwa siku ya ijumaa tarehe 07 mwezi huu. pia bila kusahau fainali ya cosafa itakuwa siku ya jumapili tarehe 09-07-2017.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...