Thursday, 6 July 2017

wadau wa maendeleo Mkoani Katavi,wamesema bajeti iliyopitishwa na serikali inatakiwa kufikishwa mahali ilipopangiwa

Raman ya mkoa wa katavi
Baadhi ya wadau wa maendeleo Mkoani Katavi,wamesema bajeti iliyopitishwa na serikali inatakiwa kufikishwa mahali ilipopangiwa itatatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa wakati.

Hayo yamebainishwa leo na wadau hao wakati wakizungumza na Mpanda Radio kuhusu bajeti iliyotengwa kwa ajili ya miradi ya mbalimbali ya maendeleo Mkoani Katavi.

Diwani wa Kata ya Katumba Mh.Seneta Baraka na Mh.Halawa Charles wa kata ya Ugalla waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ni miongoni mwa wadau wa maendeleo ambao wamezungumzia bajeti hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Wilayani Tanganyika Mh. Moshi Kakoso anayetoka Halmshauri mpya ya Mpanda, mwakilishi wa wananchi bungeni amezungumza kuhusu bajeti iliyoidhinishwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa Ofisi za serikali na nyumba za watumishi katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018.

 Zaidi ya shilingi bilioni 412 zimetengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo zaidi ya shilingi bilioni Tatu ujenzi wa miundombinu ya Ofisi na Nyumba za Watumishi Mkoani Katavi.

 Maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi yakiwemo Katumba na Itenka bado yanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji safi na salama,vituo vya huduma za afya,shule za Sekondari kwa baadhi ya kata na vyumba vya madarasa katika baadhi ya shule.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...