DODOMA
Wabunge wameitahadharisha Serikali kuhusu
ulipaji wa fidia maeneo ambayo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima
nchini Uganda kwenda Tanga litakapopita, huku wapinzani wakisema mkataba wa
mradi huo unakinzana na sheria za nchi.
Wameyasema hayo bungeni
wakati wakichangia azimio la kuridhia mkataba baina ya Serikali na Uganda,
kuhusu mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki.
Mbunge wa Tanga Mjini (CUF),
Mussa Mbarouk ameomba viongozi wanaotoka maeneo yatakayopitiwa na mradi huo,
kuwashirikisha wananchi na Serikali ifanye maandalizi kuepusha migogoro.
Naye Mbunge wa Muleba Kusini
(CCM), Profesa Anne Tibaijuka ametahadharisha kuwa katika dhana ya ulinzi
wasiibue migogoro ya ardhi maeneo ambayo bomba hilo linapita.
Katika maoni yake, Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Deogratius Ngalawa ameshauri Serikali
kuhakikisha kuwa inatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kulipia fidia ya ardhi.
No comments:
Post a Comment