Tuesday, 31 October 2017

Vifaranga 6,400 kuchomwa moto, mmiliki aomba kuvirejesha Kenya.





Picha ya mtandao

Arusha.
Vifaranga vya kuku 6,400 vinatarajiwa kuchomwa moto baada ya kunaswa vikiingizwa nchini kupitia Longido mkoani Arusha.
Vifaranga hivyo vilikamatwa juzi vikitokea nchini Kenya.
Taarifa zinasema thamani ya vifaranga hivyo ni Sh12.5 milioni na ni mali ya mfanyabiashara Mary Matia (23) mkazi wa Mianzini jijini Arusha anayeshikiliwa na polisi.
Akizungumza na Mwananchi katika mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Namanga, ofisa mfawidhi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo Kanda ya Kaskazini, Obedi Nyasembwa alisema tangu mwaka 2007 Serikali ilipiga marufuku kuingiza mayai na vifaranga kutoka nje ya nchi.
Alisema uamuzi huo wa Serikali ulichukuliwa ili kudhibiti magonjwa ya mifugo ukiwamo wa mafua ya ndege.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Magonjwa ya Wanyama ya mwaka 2003, vifaranga hivi tutaviteketeza kwa kuwa vinaweza kuwa na magonjwa,” alisema.
Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpaka wa Namanga, Edwin Iwato alisema kwa mujibu wa sheria vifaranga hivyo havikupaswa kuingizwa nchini, hivyo licha ya kuviteketeza, gari lililotumika kuvisafirisha litatozwa faini.
Akizungumza akiwa chini ya ulinzi wa polisi, mfanyabiashara Matia alikiri kuingiza nchini vifaranga hivyo akisema hakuwa akijua kama uingizaji umepigwa marufuku.
“Naomba wasivichome moto vifaranga, ni bora waniruhusu nivirudishe Kenya kwa kuwa ninadaiwa Sh12.5 milioni nilikovinunua,” alisema.
Hata hivyo, ofisa mfawidhi mkaguzi wa Mifugo, Medard Tarimo alisema kwa muda mrefu yamekuwapo malalamiko ya kuingizwa nchini vifaranga na mayai lakini wamekuwa wakishindwa kuwakamata wahusika.
“Wamekuwa wakipita njia za panya usiku na kuingiza nchini jambo ambalo ni la hatari kwa afya za binadamu kwa kuwa nchi jirani tu ya Uganda kuna ugonjwa wa mafua ya ndege,” alisema.
@habari toka mwananchi

TPA Wametekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufungua ofisi zake nchini Rwanda kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara wa nchi hiyo.

DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), umetekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufungua ofisi zake nchini Rwanda kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara wa nchi hiyo.

Haya yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko hivi karibuni alipokutana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura aliyeitembelea mamlaka hiyo.

TPA imeshakamilisha taratibu zote na tayari ina ofisi na mtumishi wake nchini humo, hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni ufunguzi rasmi wa ofisi hiyo jijini Kigali.

Hatua hiyo imepongezwa na Balozi Kayihura, akisema anaushukuru uongozi wa TPA na Serikali ya Tanzania kwa kuwajali watu wa Rwanda.

 Balozi Kayihura ameeleza  kuwa biashara kati ya Tanzania na Rwanda imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni baada ya TPA kuimarisha huduma zake.

Source TBC 1

Editor REBECCA KIJA

Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda ameagiza kuajiriwa kwa baadhi ya maafisa kata wa muda katika baadhi ya Kata.


Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu


MPANDA.

Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu ameagiza kuajiriwa kwa baadhi ya maafisa kata wa muda katika baadhi ya Kata.

Amesema hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda alipokuwa akijibu baadhi ya maswali yaliyo ulizwa na Waheshimiwa madiwani kuhusu tatizo hilo.

Katika hatua nyingine amezitaja baadhi ya sababu zilizopelekea upungufu wa watendaji hao kuwa ni baadhi yao kukumbwa na sakata la watumishi wenye vyeti feki.

Baraza la Madiwani linaendelea leo ambapo Madiwani watawasilisha mapendekezo mbali mbali ya utekelezwaji wa bajeti katika kata zao.



HABARI NA ALINANUSWE EDWARD

Wamiliki na madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinafanyiwa ukaguzi.


KATAVI.

Wamiliki na madereva wa vyombo vya moto Mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinafanyiwa ukaguzi.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama Barabarani Mkoani Katavi Nassoro Alphi wakati akizungumza na Mpanda Redio kwa njia ya simu na kusema kuwa zoezi hilo linafanyika nchi nzima na litadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Amesema kuwa kwa mkoa wa katavi wameanza na magari ya abiria pamoja na Malori na ofisi ya Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani imetoa wiki tatu ya ukaguzi wa hiari nje ya hapo zoezi la kukamata litaanza.

TEMBO MZEE Amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuhakikisha magari yote yanakuwa katika hali ya ubora na ambaye gari lake halitakaguliwa hata patiwa stika.



HABARI NA  MDAKI HUSEIN

Kiongozi wa Catalonia aliyefutwa "aenda Ubelgiji"



portrait of Carles Puigdemont seen through a window of the Palau de la Generalitat, 30 October 2017Haki miliki ya pich
Image captionBw Puigdemont aliondoka Catalonia lakini bado picha yake iko kwenye majengo ya serikali
Rais wa Catalonia aliyefutwa Carles Puigdemont ameenda nchini Ubelgiji, wakili wake aliye chini humo anasema.
Wakili huyo Paul Bekaert, hakuzungumzia ripoti kuwa Bw. Puigdemont anajiandaa kuomba kupewa hifadhi.
Mwendesha mashtaka nchini Uhispania ametaka mashataka ya uasi kufunguliwa dhidi yake na viongozi wengine ya kura ya maoni iliyopogwa marufuku.
Serikali ya Uhispania ilichukua udhibiti kamili wa Catalonia siku ya Jumatatu, kuchukua mahala pa viongozi waliofutwa.
Ilifuta utawala wa eneo hilo na kuitisha uchaguguzi mpya baada ya Bw Puigdemont na serikali yake kujitangazia uhuru wiki iliyopita.
Wakili huyo wa Ubelgiji Paul Bekaert alisema kuwa Bw. Puigdemont kwa sasa yuko mji mkuu wa Ubelgiji Brussels.

Mbona Puigdemont akaenda Ubelgiji?

Uhispania ilikuwa imekumbwa na mzozo wa kikatiba tangu kura ya maoni iliyopangwa na serikali ya Bw. Puigdemont, ilipoandaliwa tarehe mosi Oktoba kinyume na amri ya mahakama iliyoamua kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na katiba.
Serikali ya Ctalonia ilisema kuwa asilimia 43 ya wapiga kura walishiriki huku asilimia 90 ya wapiga kura hao wakiunga mkono uhuru
Siku ya Ijumaa bunge la Catalonia likatangaza uhuru.
Kisha waziri mku wa Uhispania akatangaza kuvunjwa kwa bunge la eneo hilo na kuondole kwa Bw. Puigdemont kama kiongozi wa Catalonia.
@habari toka bbc swahil

Uhuru Kenyatta ndiye rais mpya wa Kenya.

Kenias Staatschef Kenyatta gewinnt Präsidentschaftswahl (Picture-Alliance/dpa/AP/S. A. Azim)

Uhuru Kenyatta ndiye rais mteule wa taifa la Kenya baada ya kuzoa kura milioni 7.4 ya kura zote zilizopigwa kwenye  uchaguzi mpya  wa urais.
Tume ya Kusimamia uchaguzi na mipaka imesema kuwa wapiga kura milioni 7.6 walijitokeza kupiga kura wakiwakilisha asilimia 42.3 Tume hiyo imesema kuwa matokeo kwenye majimbo manne ambayo hayakujumuishwa kwenye mchakato wa uchaguzi kufuatia machafuko hayana athari kubwa kwenye matokeo ya kura zilizopigwa.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema kuwa uchaguzi huo uliendeshwa kwa njia huru, haki na ya kuaminika. Kenyatta ataapishwa baada ya majuma mawili iwapo hakuna kesi itakayowasilishwa kwenye mahakama ya Juu kupinga uteuzi wake. Shisia Wasilwa anaripoti kutoka nairobi.
"Kabla ya uchaguzi kupigwa nilikuwa nimeridhika kuwa tulikuwa tumefanya kila kitu kilichohitajika kufanya, wakati huu hakukuwa na vitisho ama muingilio kutoka kwa mtu yeyote," alisema Chebukati.
Uhuru Kenyatta aliwashinda wagombea wengine sita kwenye uchaguzi ambao alitarajiwa kushinda kwa urahisi baada ya kushindana na wagombea ambao hawana umaarufu nchini Kenya.
Chebukati anasema amezingatia sheria katika kuendesha uchaguzi
Idadi ndogo ya wapiga ikijitokeza kutekeleza haki yao ya kidemokrasia huku ngome za upande wa upinzani zikisusia uchaguzi wenyewe. Kenya imefanya chaguzi mbili katika miezi miwili, suala ambalo mwenyekiti wa tume ya Kusimamia uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati amesema limekuwa changamoto.
Kenia Wahlwiederholung | Chef der Unabhängigen Wahlkommission (IEBC) Wafula Chebukati (picture-alliance/AP Photo/S. Abdul Azim)
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati
Hata hivyo Chebukati anashikilia kuwa amezingatia sheria na maadili kwenye mchakato mzima wa marudio ya uchaguzi huu ambao baadhi ya waangalizi wametaja kuwa ulikuwa huru na wa haki hivyo kuwataka wakenya kutangamana na kujenga taifa, licha ya kunukuliwa awali akisema kuwa hana uhakika na mazigira ya uchaguzi huru na wa haki.
Septemba mosi, mahakama ya Juu ilibatilisha uchaguzi wa urais ambao ulifanywa tarehe nane mwezi Agosti na kuagiza uchaguzi mpya ufanywe.
Mahakama hiyo iliamua kuwa uchaguzi huo ulikiuka sheria na katiba. Kwa mujibu wa matokeo yaliotangazwa na Tume wakati huo. Rais Uhuru Kenyatta alikuwa amemshinda kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kura milioni 1.4.
Hata hivyo Odinga alijiondoa baada ya masharti yake kutozingatiwa na Tume hiyo. Tume hiyo imefanya uamuzi huo licha ya majimbo manne ya Nyanza kutoshiriki kwenye uchaguzi huo. Matokeo ya leo yametoka kwenye vituo 266 vya kupigia kura kati ya vituo 290.
Tume ilifanya mageuzi kabla uchaguzi
Naibu wa mwenyekiti wa Tume ya Kusimamia Uchaguzi  Consolata Nkatha alielezea kuridhika kwao, "Kama inavyaogizwa kufanyika kwa marudio ya uchaguzi, tumeridhika kuwa katika maeneo ambayo uchaguzi uliahirishwa, matokeo ya uchaguzi hayatakuwa na athari kubwa kwa matokeo ya urais." alisema Nkatha.
Kenia Ezra Chiloba Leiter der Wahlkommission (Getty Images/AFP/T. Karumba)
Afisa Mkuu wa IEBC Ezra Chiloba alitakiwa na upinzani kujiuzulu
Mageuzi ambayo tume ilifanya kabla ya uchaguzi ni pamoja na kuongeza mitambo ya kutuma matokeo ya uchaguzi, kuhusisha mawakala wa vyama mbali mbali kwenye mchakato mzima wa uchaguzi, huku maafisa wake wakipewa mafunzo ya kutosha.
Hata hivyo rais Uhuru Kenyatta alisusia mkutano ambao alitarajiwa kukutana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati kulainisha masuala tata kabla ya uchaguzi kurudiwa.
Upinzani ulitaka baadhi ya maafisa wa Tume hiyo watimuliwe afisini hali ambayo baada ya vuta nikuvute  ya muda mrefu, afisa mkuu mtendaji wa Tume hiyo Ezra Chiloba alitangaza anachukua likizo ya wiki tatu.
Upande wa upinzani ulitisha kutangaza Odinga mshindi, iwapo Chebukati angemtangaza Kenyatta mshindi. Hilo linasubiriwa kwa sasa. Huku macho yote ya jumuiya ya Afrika Mashariki yakilenga demokrasia ya taifa Kenya, wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa masuala tata kama vile ya ukabila yanastahili kujadiliwa na kila mmoja mkenya ahusishwe kwenye serikali ili ahisi ni sehemu ya taifa.
@habari toka Dw swahili

Miili 9 iliyokatwakatwa yapatikana kwenye nyumba Tokyo Japan.



Members of the media gather in front of an apartment building where media reported nine bodies were found in Zama, Kanagawa Prefecture, Japan in this photo taken by Kyodo on October 31, 2017Haki miliki ya picha
Image captionMiili 9 iliyokatwakatwa yapatikana kwenye myumba Tokyo Japan
Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamume mmoja baada ya kupata viungo vya miili tisa katika nyumba yake iliyo Zama huko Tokyo.
Polisi walipata vichwa viwili kwenye jokovu nje ya nyumba ya mshukiwa kwa jina Takahiro shiraishi, wakati wakichunguza kutoweka kwa mwanamke mmoja.
Pia walipata viungo vya watu saba kwenye majokovu yaliyo ndani ya nyumba yake.
Mtu huyo wa umri wa miaka 27 anashtakiwa kuwa ndiye alitupa miili hiyo.
Polisi walikuwa wamepata miili ya wanawake 8 na mwanamume mmoja, mingine tayari ikiwa imeanza kuoza.
"Niliwaua na nikaifanyia kazi miili yao ili kuficha ushahidi," shirika la habari la NHK lilimnukuu akisema.
Jirani wake alisema kuwa alikuwa ameanza kuhisi harufu mbaya kutoka kwa nyumba yake tangu Bw. Shiraishi ahamie nyumba hiyo mwezi Agosti.
Polisi walifanya ugunduzi huo walipokuwa wakimtafuta mwanamke wa umri wa miaka 23 ambaye amekuwa hajulikani aliko tangu tare 21 mwezi Oktoba.
Wachunguzi waligundua kuwa Bw. Shiraishi amekuwa akiwasiliana na mwanamke huyo baada ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikuwa anataka kujiua.
@habari na bbc swahil

Monday, 30 October 2017

Nyalandu aachia ubunge, ajivua uanchama CCM.












 Dar es Salaam. 
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amejivua uanachama wa CCM na nyadhifa zake zote, akisema haridhishwi na mwenendo wa siasa nchini.
Nyalandu, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne, aliiambia Mwananchi  Jumatatu mchana kuwa ameamua kujiondoa CCM na ameiomba “Chadema wafungue malango yao” ili aweze kuungana nao.
"Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017," alisema Nyalandu ambaye video ya uamuzi huo imesambaa mitandaoni.
"Hali kadhalika, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

"Aisha, nimechukua uamuzi huu kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya Watanzania."
Kwa uamuzi huo, Nyalandu, ambaye aliomba ridhaa ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi uliopita, amejivua ubunge na nafasi nyingine zote alizokuwa akishikilia ndani ya CCM, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa Halmashauri Kuu.
@habari  toka mwananchi

Yanayojiri kwenye mvutano wa kisiasa wa nchini Uhispania.


Wafanyakazi wa serikali leo hii Jumatatu wameanza wiki ya kazi tangu serikali kuu ya Uhispania ilipobatilisha tamko la uhuru wa jimbo la Catalonia kwa kumvua madaraka kiongozi wa jimbo la hilo Carles Puigdemont.
Spanien - Demonstrationen fĂĽr die Einheit von Spanien und Katalonien in Barcelona (Reuters/Y. Herman)
Wafanyakazi wa serikali walipofika mahala pao pa kazi leo hii wamekuta bendera zote mbili za Uhispania na jimbo la Catalonia zikipepea juu ya majengo ya serikali. Bila shaka kinachosubiriwa kwa shauku ni iwapo hali ya utulivu itaendelea kuzingatiwa wakati serikali kuu ya Uhispania inapotekeleza hatua ya kuchukua mamlaka ya jimbo hilo? hata ingawa hali hiyo inadhaniwa kuwa inaweza ikazusha mvutano zaidi katika nchi ambayo imekumbwa na mgogoro wa kisiasa kwa muda wa mwezi mmoja sasa. Wakati huo maelfu ya watu wanaounga mkono Catalonia kubakia katika Uhispania moja walifanya maandamano makubwa katika mji wa Barcelona.
Spanien Katalonien Rede Carles Puigdemont (picture-alliance/AP Photo/Presidency Press Service)
Kiongozi wa jimbo la Catalonia aliyevuliwa mamlaka Carles Puigdemont
Hakuna ishara yoyote iwapo baraza la mawaziri wa jimbo la Catalonia lililoondolewa madarakani  litajaribu kurejea kwenye ofisi zao siku ya Jumatatu baada ya baraza hilo kushiriki katika kura ya siri juu ya jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania mnamo siku ya Ijumaa.  Kiongozi wa Catalonia Carel Puigdemont amesema ataendeleza upinzani kwa kutumia njia za kidemokrasia dhidi ya hatua zilizochukuliwa na serikali kuu za kuyatwaa mamlaka ya jimbo lake kwa kuahinisha ibara ya 155 ya katiba ya Uhispania. Hata hivyo tamko hilo la Puigdemont halikufafanua kama linamaanisha ndio amekubali uchaguzi wa mapema ufanyike kama hatua mojawapo ya kupunguza mvutano baina ya jimbo lake na serikali kuu ya mjini Madrid. Kiongozi huyo wa Catalonia anaweza kuingia kwenye lawama nzito leo hii za uhaini na kuvuruga uchumi. Waziri wa mambo ya nje wa Uhispania Alfonso Dastis amesema ana imani kuwa serikali kuu itarejesha hali ya utulivu na sheria katika jimbo la Catalonia. Dasdis amesema serikali kuu ina imani kuwa mpaka sasa ukweli umedhihirika na kwamba busara itarudi kwenye mawazo ya Wacatalonia ili kjuweza kutambua kwamba kiongozi wa zamani wa jimbo la Catalonia alitoa ahadi za uongo.
Kiongozi wa Catalonia aliyenyang‘anywa mamlaka Carles Puigdemont amechapisha ujumbe ulioandamana na picha kwenye mtandao wa kijamii, picha hiyo inamwonyesha akiwa amekaa kwenye ua wa bunge katika jimbo la Barcelona. Picha hiyo imeambatanishwa na ujumbe wa maandishi yasemayo ''Habari za Asubuhi'' pamoja  na kikaragosi kinachotabasamu. Picha hiyo imezua maswali mengi iwapo Puigdemont yuko ndani ya majengo ya bunge?
Serikali kuu ya Uhispania inayoongozwa na Waziri Mkuu Mariano Rajoy moja kwa moja itasimamia mamlaka ya jimbo la Catalonia. Serikali kuu ya Uhispania tayari imeshatwaa udhibiti wa jeshi la polisi katika jimbo hilo, imelivunja bunge na imeitisha uchaguzi wa mapema utakaofanyika tarehe 21 mwezi Desemba.
@habari toka Dw swahil

Watu 60 watengwa kutokana na homa ya tumbili Nigeria




Watu 60 watengwa kutokana na homa ya tumbili NigeriaHaki miliki ya picha
Image captionWatu 60 watengwa kutokana na homa ya tumbili Nigeria

Watu 60 wametengwa katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kano, baada ya kukaribiana na watu wanakosiwa kuugua homa ya tumbili au monkeypox.
Kamishia wa afya katika jimbo la Kano, Kabul Gesto, alisema kwau moja ya dalili za ugonjwa huo iligunduliwa kwenye mgongwa lakini akasema kuwa ugonjwa huo huenda ukawa homa ya ndege.
"Hadi pale matokeo ya sampuni za damu yaliyotumwa kwenda mji mkuu Abuja yatakaporudishwa, hiki kitakuwa kisa cha kushukiwa," alisema wakati wa mahajIano na BBC.
Dr Getso anasema kuwa wagonjwa 11 katika majimbo 36 nchini Nigeria wameathirika na homa ya tumbuli.
Mamlaka za afya nchini Nigeria zimekuwa zikionya dhdi ya ulaji wa tumbili na nyama ya msituni wiki chache zilizopita.
Waziri wa afya Isaac Adewole anasema katika taarifa ya hivi punde kuwa licha ya tiba ya ugonjw ahuo kutujulikana hakuma wasi wasi kwa sababu homa hiyo siyo hatari.
Hata hivyo amewashauri watu kuchukua tahadhari ikiwemo kujiepusha na maeneo yenye misongamano.
@habari toka bbc swahil

Makandarasi wazalendo walamba dume reli ya kisasa.


 Kampuni inayojenga reli ya kisasa ya standard gauge (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, Yapi Merkhezi Construction imepanga kuzitumia kampuni za makandarasi wazalendo kujenga baadhi ya madaraja na mifereji kwenye mradi huo.
Akizungumza na wanachama wa Chama cha Makandarasi Wazalendo Tanzania (ACCT) waliotembelea ujenzi wa reli eneo la Soga, mhandisi mkuu wa kampuni hiyo, Mert Oz alisema uamuzi wa kuwatumia makandarasi wazalendo kujenga mifereji na makaravati unalenga kuwawezesha kupata uzoefu na kujifunza teknolojia mpya. “Ninaposema tutawapa makandarasi wazalendo kazi za kujenga baadhi ya mifereji na makaravati yawezekana baadhi ya watu wakadhani ni kazi za kiwango cha chini, hiyo sio kweli,” alisema.
Alisema unapojenga makaravati au mifereji kwenye mradi wa reli ya SGR ujenzi wake unakuwa kwenye kiwango cha kimataifa na viwango vyake viko wazi.
Licha ya kutoa kazi kwa makandarasi wazalendo, aliwataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa viwango vya juu ili kupata uaminifu na sifa za kutekeleza miradi mikubwa. Pia, aliongeza kuwa reli hiyo itakuwa ya kimataifa na ni moja ya reli za kisasa duniani.
“Reli hii tunayojenga ni ya teknolojia ya kisasa kama zile zinazotumika Uturuki, Ujerumani na hata Marekani na nchi nyingine zilizoendelea,” alisema.
“Ubabaishaji hata chembe hautakiwi hapa na kama utafanya hivyo utaingia katika orodha ya kampuni duni zisizostahili kupata kandarasi za kimataifa.”
Kwa upande wake, mwenyekiti wa ACCT, mhandisi Milton Nyerere alisema ushiriki wao katika ujenzi wa baadhi ya miundombinu ya reli hiyo utatoa nafasi kwa makandarasi hao kujifunza ubora na viwango vya kimataifa vinavyopaswa kutekelezwa katika miradi mikubwa. Mkadiriaji gharama za ujenzi wa kampuni ya ukandarasi ya Nordic, Magdalena Richard alisema jambo kubwa alilojifunza ni namna Yapi Merkhezi Construction inavyosisitiza kumaliza kazi katika muda uliopangwa. Mradi wa ujenzi wa reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ulioanza Mei unatarajia kukamilika mwaka 2019.
@habari na mwananchi

Baadhi ya watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne katika shule mbalimbali manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameeleza matumaini ya kufaulu mtihani wao ulionza leo nchi nzima.


MPANDA.
Baadhi ya watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne katika shule mbalimbali manispaa ya Mpanda Mkoani hapa wameeleza matumaini ya kufaulu mtihani wao ulionza leo nchi nzima.

Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti wanafunzi hao wakiwemo wa shule ya sekondari mwangaza na kashaulili wamesema maandalizi yao katika mtihani huo yako vizuri huku wakiwaomba wenzao kuondoa hofu ya mtihani.

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Mwangaza Mwl. Simoni Lubange amewataka wanafunzi wake kujiamini na kumtanguliza mungu katika ujibuji wa mitihani yao kwa alichokisema hakuna kitu kigeni watakachokutana nacho.

Jumla ya watahiniwa 385, 938 wa kidato cha nne nchini wameanza mtihani leo huku baraza la mitihani likitoa onyo kwa na tahadhari kwa wamiliki wa shule watakaofanya udanganyifu.


Friday, 27 October 2017

IDARA ya uvuvi Mkoani Katavi imezindua mafunzo ya siku kumi ya uvuvi,uchakataji na usindikaji wa mazao ya samaki.


MPANDA. 
IDARA ya uvuvi Mkoani Katavi imezindua mafunzo ya siku kumi ya uvuvi,uchakataji na usindikaji wa mazao ya samaki.
Afisa  Uvuvi Mkoani Katavi Kayumba Torokoko amesema lengo la kuendesha semina hiyo inayofanyika Tarafa ya Karema Wilayani Tanganyika inalenga kuelimisha wachakataji wengi kujua  namna ya kuhifadhi samaki kwa njia ya kisasa zaidi.
Amesema mafunzo hayo yatakayodumu kwa siku kumi yatapelekea vikundi vingi vya kuchakata samaki kuwa katika ubora mzuri ili kupata soko zuri.

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Tarafa ya Karema Mary Patric Kawogo amesema mafunzo hayo yataongeza uwezo wa wachakataji wa samaki ili ili kuendesha shghuli yenye tija.
Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema kupitia mafunzo hayo watajua namna  ya kuinua kipato na kuimarika kiuchumi.
@habari na  Rehema Msigwa

RC Katavi ameagiza ujenzi wa wadi ya wazazi katika zahanati ya kata ya Kakese kukamilika kabla ya Desemba Mosi mwaka huu.


MPANDA
MKUU wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya muhuga,ameagiza ujenzi wa wadi ya wazazi katika zahanati ya kata ya Kakese kukamilika kabla ya Desemba Mosi mwaka huu.
Muhuga ametoa agizo hilo leo wakati akifanya ukaguzi wa maendeleo ya zahanati hiyo
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bi.Mary Lihulu amesema tayari wameshapokea shilingi milioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo na Shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya ukarabati wa wa jingo la zahanati.
Zahanati ya Kakese inahudumia vijiji vya Mbugani na mkwajuni vijiji ambavyo vinaaminika kuwa na wakazi wengi kutokana na kuwa na watu wengi wanaojishghulisha na kilimo cha mazao kama mpunga na mahindi.
@habari na Issack Gerald.

Rasimu ya marekebisho ya Katiba yapitishwa Burundi


mediaRais wa Burundi Pierre Nkurunziza anaongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu wenye utata.
 Burundi,
 Baraza la Mawaziri lilipitisha siku ya Jumanne, Oktoba 24, wakati wa mkutano maalum, mapendekezo ya marekebisho ya katiba ambayo yatabadili kwa kina nakala hii muhimu na kuruhusu Rais Pierre Nkurunziza, ikiwa itapitishwa kwa kura ya maoni, kuwania muhula wa nne mwaka 2020.




Kwa hili halishangazi wengi nchini humo, ingawa uamuzi huu haujawekwa wazi, kutokana na muda ambao haujapatikana. Muswada huu ulikuwa tayari umeandaliwa tangu zaidi ya miezi sita iliyopita na mazungumzo ya mwisho kati ya Warundi yaliyofanyika bila kuwepo kwa upinzani wenye itikadi kali na vyama vya kiraia. Viongozi wa upinzani kutoka muungano wa CNARED na wanaharakati kutoka vyama vikuu vya kiraia wako uhamishoni tangu kuzuka kwa machafuko nchini Burundi mwaka 2015.
Ibara ya 96 ya Katiba, ambayo inaweka kikomo cha mihula miwili ya miaka 10 kwa rais itaondolewa. Toleo jipya la Katiba ya Burundi inaeleza kuwa rais atachaguliwa kwa miaka saba kama muhula mmoja na kuendelea kama atachaguliwa na wananchi, hata kama hawezi "kuongoza zaidi ya mihula miwili mfululizo."
Hakuna kitu kinachoweza kuzuia Rais Pierre Nkurunziza kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 na kuendelea kusalia mamlakani hadi mwaka 2034, afisa mwandamizi nchini Burundi amesema. Marejeleo yoyote ya makubaliano ya amani ya Arusha yamendolewa kwa ufanisi, kwani ni katazo kwa rais kuongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 10. Kwa mujibu wa afisa huyo mwandamizi, Pierre Nkurunziza anaweza kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2041.
Utawala umejizuia kubadili ibara zinazozungumzia usawa wa kikabila zilizomo katika Katiba ya sasa: 60% ya Wahutu na 40% ya Watutsi katika serikali na bunge, na usawa uliopo katika jeshi na polisi.
Lakini muundo wa serikali utabadilishwa upya: hakuna mfumo wa makamu wawili wa rais. Nafasi zote hizo zitachukuliwa na waziri mkuu kutoka chama kiliopata wabunge wengi na makamu wa rais kutoka upinzani, lakini atakua hana mamlaka.
Kura ya maoni kupigwa mnamo mwezi Februari
Hatimaye sheria rahisi zitapitishwa kwa idadi kubwa inayohitajika bungeni, wakati ambapo hadi sasa ilikua inahitajika theluthi mbili tu. Mpango ambao ulitakiwa kulazimisha chama chenye wabunge wengi kujadiliana na wapinzani wake.
Hakuna tarehe iliyowekwa hadi sasa kwa kura ya maoni ya kikatiba, lakini serikali ya Bujumbura inataka kura hiyo ipigwe haraka. Serikali ya Bujumbura inataka kura ya maoni iwe imepigwa hadi katikati ya mwezi Februari mwaka 2018.
@habari na Rfi swahil

Zoezi la kuhesabu kura laendelea Kenya.

Ulinzi umeimarishwa wakati huu zoezi la kuhesabu kura likiendelea nchini Kenya


.
Siku moja baada ya Wakenya kupiga kura kumchagurais wao mpya, zoezi la kuhesabu kura linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini Kenya.

Hatua hii inakuja baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa saa 11 jioni siku ya Alhamisi Oktoba 26. Kumekuwa na idadi ndogo ya wapiga kura iliyojitokeza kupiga kura, katika maeneo mengi nchini humo kinyume na ilivyotarajiwa mwezi Agosti.

Pamoja na hilo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati alisema kuwa, zoezi hilo lilikwenda vizuri katika maeneo mengi nchini humo.

Bw. Chebukati amesema ni asilimia 48 ya wapiga kura ndio waliojitokeza.

Wabunge wa upinzani wamekuwa wakizungumza jioni hii na kusema Uchaguzi huo hautafanyika katika kaunti hiyo.

Aidha, wamesema kuwa kwa tathmini yao asilimia 65 ya wapiga kura hawakujitokeza kupiga kura kote nchini.

Hata hivyo uchaguzi huo haukufanyika katika baadhi ya maeneo kutokana na usalama mdogo.

Uchaguzi mpya wa urais wa siku ya Alhamisi Oktoba 26 uligubikwa na makabiliano kati ya waandamanaji wa upinzani n apolisi.

Watu watatu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na polisi katika ngome za upinzani, katika makabiliano na maafisa wa polisi.

Taarifa kutoka nchini Kenya zinasema mtu mmoja aluawa katika mtaa wa Mathare jijini Nairobi wakati wafuasi wa upinzani walijaribu kuzuia zoezi la upigaji kura.

Awali vyanzo vya polisi na hospitali Mjini Kisumu vilisema kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 ameuawa huku kijana mwingine akiuawa katika kaunti ya Homa Bay.

Mkurugenzi wa Amnesty International nchini Kenya, Justus Nyangaya ameonya kuwa kuna hatari ya kutokea kwa machafuko zaidi ikiwa hali haitadhibitiwa.

Uchaguzi haukufanyika katika ngome nyingi za upinzani hasa katika Kaunti za Kisumu, Siaya, Homabay na Migori na Uchaguzi huo umeahirishwa hadi siku ya Jumamosi.

Uchaguzi nchini Kenya unafanyika baada ya mahakama ya Juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi wa awali uliofanyika Agosti 8.
@habari toka rfi swahil

Barrick yaweka masharti kulipa Dola 300 milioni.


Rais John Magufuli akimweleza jambo Mwenyekiti
Rais John Magufuli akimweleza jambo Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada, Profesa John Thornton walipokutana Ikulu.Picha na maktaba.
Dar es Salaam. 
Licha ya kupata hasara kwenye robo ya tatu ya mwaka, kampuni ya Barrick imetenga dola 300 milioni za Marekani (zaidi ya Sh660 bilioni) kuilipa Serikali, lakini imeweka sharti; inataka iruhusiwe kusafirisha makinikia.
Acacia, kampuni tanzu ya Barrick na inayomiliki migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, imezuiwa tangu mwezi Machi kusafirisha mchanga huo wa madini kwenda kuuyeyusha nje ya nchi kwa ajili ya kupata mabaki ya dhahabu, shaba, fedha na madini mengine yaliyoshindikana kuchenjuliwa migodini.
Baada ya majadiliano baina ya Serikali na Barrick, kampuni hiyo ya Canada ilikubali kulipa dola 300 milioni “kuonyesha uaminifu”.
Taarifa ya miezi mitatu ya Barrick (Julai-Septemba) iliyotolewa juzi, inaonyesha kuwa ilipata hasara ya dola 11 milioni (zaidi ya Sh24 bilioni) tofauti na faida ya dola 175 milioni (zaidi ya Sh385 bilioni) iliyopata katika kipindi kama hicho mwaka jana (dola moja ya Kimarekani ni sawa na takriban Sh2,200 za Tanzania).
“Kupungua kwa mapato kunatokana na kushuka kwa uzalishaji na bei ya dhahabu pamoja na zuio la kusafirisha makinikia ambalo Serikali ya Tanzania iliiwekea Acacia,” inasema ripoti hiyo.
Vilevile, Barrick inasema kupungua kwa mapato yake kumechangiwa na ongezeko la makadirio ya kodi yanayofika dola 172 milioni (zaidi ya Sh378 bilioni) zilizopendekezwa kwenye majadiliano ya mustakabali wa operesheni za Acacia nchini.
Wakati Barrick ikitenga kiasi hicho cha kodi, Acacia ina dola 128 milioni (zaidi ya Sh282 bilioni) na kufanya jumla ya dola 300 milioni zilizokubaliwa kwenye mazungumzo yaliyofanyika kwa miezi mitatu iliyopita.
Masharti hayo si ya kwanza, itakumbukwa kwamba siku chache baada ya mkutano wa kukabidhi ripoti ya majadiliano hayo, kampuni ya Acacia ilisema haiwezi kulipa Dola 300 milioni kwa mkupuo na kwamba Barrick inajua hilo.
Ofisa fedha mkuu wa Acacia, Andrew Wray alinukuliwa na vyombo vya habari akisema: “Hatuna huo uwezo kuilipa Tanzania ili tumalizane kwenye mgogoro wa kodi uliopo.”
Wray alisema hayo Oktoba 20 wakati Acacia ilipokuwa ikiwasilisha ripoti yake ya fedha kwa robo ya tatu ya mwaka iliyoishia Septemba, ikionyesha kushuka kwa mapato na faida ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Barrick imeiunga mkono Acacia kwenye msimamo wake kuhusu malipo hayo ya dola 300 milioni ikisema: “Kutokana na hali ya Acacia kifedha, malipo haya yanapaswa kufanywa kwa awamu yakitegemea mauzo ya dhahabu na usafirishaji wa makinikia.”
Katika robo hiyo ya tatu, faida ya Acacia imeshuka kwa asilimia 70 kutoka dola 52.878 milioni (zaidi ya Sh116.331 bilioni) mpaka dola 16.038 (zaidi ya Sh35.283 bilioni).
Wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Ikulu, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ambaye alikuwa mwenyekiti wa wawakilishi wa Serikali alisema Barrick wamekubali kutekeleza masharti yote ya sheria mpya ya madini.
Lakini kwenye taarifa yake, kampuni hiyo inasema itaendelea kuzungumza na Serikali ili kuondoa zuio la kusafirisha makinikia na kwamba mazungumzo hayo yataenda sambamba na kutafuta suluhu ya deni la kodi la kiasi cha dola 190 bilioni (zaidi ya Sh424 trilioni) ambazo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeitoza Acacia ikiwa ni malimbikizo ya kodi, faini na riba.
“Tunatarajia mazungumzo haya yatakamilika ndani ya nusu ya kwanza ya mwaka ujao,” inasema Barrick.
Pamoja na hasara hiyo ya robo ya tatu, kwa miezi yote tisa, Barrick imepata faida ya dola 1.752 bilioni (zaidi ya Sh3.854 trilioni) ambayo ni zaidi ya mara saba ikilinganishwa na iliyopata kwa muda kama huo mwaka jana. Mwaka uliopita, ilitangaza faida ya dola 230 milioni (zaidi ya Sh506 bilioni).
Mbali na taarifa hiyo ya fedha, Barrick imefafanua kwa wadau wake kuhusu makubaliano yaliyoafikiwa kwenye majadiliano ya miezi mitatu baina yake na Serikali.
Makubaliano
Kwenye ripoti hiyo, Barrick inasema imekubaliana na Serikali kuhusu mfumo mpya wa uendeshaji ambao, endapo utaridhiwa, utatoa mwelekeo mpya wa shughuli za Acacia nchini. Barrack imefanya mazungumzo hayo kwa niaba ya Acacia kwa kuwa ndiye mmiliki mkuu wa hisa, ikimiliki asilimia 63.9.
Lakini, pamoja na ukweli huo, inasema chochote kitakachoafikiwa kitapaswa kutathminiwa na kuthibitishwa na Acacia kabla ya utekelezaji, ingawa Barrick inaamini makubaliano yaliyofikiwa yataleta suluhu ya mgogoro uliopo kwenye uchimbaji wa dhahabu nchini.
Mgogoro kati ya kampuni ya Acacia, mchimbaji na msafirishaji mkubwa wa dhahabu ya Tanzania, na Serikali ulishika kasi Machi baada ya kampuni hiyo kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini.
Baadaye Rais John Magufuli aliunda kamati mbili kuchunguza kiwango cha madini kilichokuwa katika makontena 270 yaliyokuwa Bandari ya Dar es Salaam, athari za kuusafirisha kwenda nje, sheria na mikataba.
Kamati hizo zilisema zimebaini kiwango cha dhahabu ni mara kumi ya kile kilichotangazwa na Acacia, kukwepa kodi na kukiuka sheria, huku mikataba ikionekana kunufaisha wawekezaji.
Ripoti hizo zilisababisha mawaziri kuwajibishwa na baadaye Serikali na Barrick kukubaliana kuunda timu za majadiliano, ambayo yalijikita katika muundo na mfumo mpya wa uendeshaji wa kampuni tanzu za Barrick, kubadilisha uendeshaji wa biashara ya madini na kuwanufaisha zaidi wananchi wanaoizunguka migodi.
Mengine ni kubadilisha mikataba ya madini (MDA) ili iendane na sheria mpya kwa lengo la kuongeza ushiriki na mapato ya Serikali, pamoja na kuainisha fidia ya makosa ya Acacia. Makubaliano manne yalipata muafaka na la mwisho bado linajadiliwa.
“Kwa makubaliano haya tunaamini tutapata suluhu ya kudumu na operesheni za Acacia nchini Tanzania zitaendelea kama kawaida,” inasema taarifa hiyo.
Mgawanyo wa mapato
Alipokuwa akiwasilisha ripoti ya majadiliano hayo kwa Rais Magufuli, Profesa Kabudi alisema Barrick wamekubali kutekeleza masharti yote ya sheria mpya za madini.
Alisema kuanzia sasa mapato au faida itagawanywa sawa kati ya Acacia na Serikali.
Siku ya pili alitoa ufafanuzi zaidi ikisema: “Mgawanyo wa asilimia 50 kwa 50 wa faida ni baada ya tozo na kodi nyingine zote kulipwa. Kwa ujumla, Tanzania itapata asilimia 70 na Barrick asilimia 30. Kwingineko wanagawana asilimia 50 kwa 50 zikiwamo kodi, sisi tulikataa hilo.”
Lakini Barrick ikasema: “Mgao wa asilimia 50 za Serikali utahusisha mrabaha, kodi na asilimia 16 ya hisa itakazopewa kukidhi matakwa ya sheria mpya za madini.
@habari toka mwananchi

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...