KATAVI
Jeshi la zimamoto mkoani Katavi limetoa wito kwa wananchi kupata vibali vya ujenzi wa nyumba zao ili kupunguza ujenzi holela.
Hayo yamebainishwa na kamishina msaidizi jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa katavi Kuhindi wakati akizungumza na Mpanda redio na kusema kuwa majanga mengi yanatokea kwa kutofuata taratibu za namna bora ya ujenzi wa makazi.
Amesema kuwa wananchi wanaojenga bila kufuata taratibu na kupata kibali wanasababisha ugumu wa uokoaji katika maeneo hayo pindi majanga mbalimbali yanapotokea.
Hata hivyo amesema kupungua kwa gharama kutoka kiasi cha shilingi laki moja na nusu mpaka kufikia elfu hamsini kumetokana na tathimini ya muda mrefu ambayo ililenga kuondoa vikwazo kwa kundi kubwa la wananchi ambao wasingeweza kumuda gharama hizo.
Source Rebeca Kija
No comments:
Post a Comment