KAGERA
Serikali imepeleka madaktari bingwa katika
Hospitali ya Misheni ya Rulenge wilayani Ngara watakaoshiriki kuwatibu majeruhi
43 wa mlipuko wa bomu ulitokea katika Shule ya Msingi Kihinga.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngara,
Dk Revocatus Ndyekobora akizungumza na waandishi wa habari hospitalini amesema
timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera imewasili
Ngara kusaidiana na wenzao kuwafanyia uchunguzi na kuwatibu majeruhi hao.
Amesema majeruhi hao pia
wanahitaji uniti 50 za damu ili kuokoa maisha yao na kwamba, baadhi wamebainika
kuwa na vipande vya vyuma vilivyotokana na mlipuko wa bomu.
Mbali ya damu, majeruhi pia
wanahitaji mashuka na mablanketi zaidi ya 50 kutokana na yaliyopo kutotosheleza
mahitaji. Alisema baadhi wamelazimika kulala sakafuni kutokana na vitanda
kujaa.
Wakati huohuo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Aidan Bahama amepiga marufuku
biashara ya vyuma chakavu katika maeneo ya shule akionya kuchukua hatua dhidi
ya mwalimu mkuu na wakuu wa shule watakaobainika kuruhusu biashara hiyo
Chanzo: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment