KAGERA
Serikali ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, imesema
wanafunzi 11 ambao ni majeruhi wa bomu waliolazwa katika Hospitali ya Rulenge
wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari bingwa kutoka Hospitali ya
Rufaa ya Bugando ya Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael
Mtenjele amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake na kuongeza kuwa hali za majeruhi hao zinaonesha matumaini kiafya
kutokana na juhudi za wataalamu za kuwapatia tiba.
Luteni Mtenjele amesema majeruhi watano baada ya
kufanyiwa uchunguzi wameonekana kuwa na vipande vya bomu sehemu za mishipa na
kwamba jitihada zinafanyika kuondoa vipande hivyo.
Aidha ameongza kuwa majeruhi wengine sita
wanaendelea kuhudumiwa majeraha yao baada ya kufanyiwa upasuaji na hofu kubwa
ilikuwa ni upungufu wa damu lakini wananchi wengi wamejitokeza kutoa damu.
Majeruhi 11 ni kati ya 42 ambao ni wanafunzi wa
Shule ya Msingi Kihinga waliolipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono, Novemba 8.
Source: mwananchi
No comments:
Post a Comment