Tuesday, 12 December 2017

JESHI la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, linamshikilia kijana wa miaka 30 kwa tuhuma za kuwabaka watoto wanne.




JESHI la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, linamshikilia kijana wa miaka 30 kwa tuhuma za kuwabaka watoto wanne, wawili wa familia moja.

Tukio hilo limeripotiwa Desemba 8, mwaka huu, Muyuni A, Mkoa wa kusini Unguja na mtuhumiwa huyo anadiwa kuwabaka na kuwalawiti watoto hao ambao ni chini ya umri wa miaka 18.

Kamanda wa Polisi mkoa huo, Makarani Khamis, amesema hapo awali mtuhumiwa  huyo alidaiwa kuwabaka watoto saba, lakini baada ya uchunguzi wa daktari ulibainika kuwa ni watoto wanne ndio walioharibiwa na watatu wakiwa salama.

Amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni fundi seremala amedaiwa kuwafanyia matukio hayo watoto hao kwa siku na nyakati tofauti.

Amesema mtuhumiwa yupo ndani kwa hatua za kiupelelezi na zitapokamilika atafikishwa katika vyombo vingine vya kisheria kwa hatua zaidi.

SOURCE MUUGWANA BLOG.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...