MPANDA
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi imetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa halmashauri hiyo
ili kuwabaini watu watakawatoza michango ya shule iliyopigwa marufuku na
serikali
Wito huo umetolewa na Afisa elimu
Taaluma Manispaa ya Mpanda Mwalimu Rashid Pili wakati akizungumza na Mpanda
Radio Ofisini kwake kuhusu namna ambavyo wamejipanga kusimamia na kutekeleza
sera ya serikali ya elimu bila malipo.
Aidha,Mwalimu Pili amesema muda
wowote wanatarjia kuendesha msako wa watoto ambao hawajapekwa shule ili wazazi
wachukuliwe hatua za kisheria kwa kumnyima mtoto haki ya kielimu.
Manispaa ya Mpanda ina jumla ya shule
34 za serikali ambazo zinatakiwa kusimamiwa ili kuhakikisha agizo la elimu bila
malipo lililotolewa na Rais Dkt.John Magufuli linatekelezeka.
Chanzo:Mpanda radio
#Changia Damu Okoa Taifa.
#Changia Damu Okoa Taifa.
No comments:
Post a Comment