Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli |
MARA
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa
halmashauri ya Butiama mkoani Mara Solomoni Ngiliule kuanzia leo kutokana na
ubadhirifu wa fedha za Umma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI,
Selemani Jafo ametangaza maamuzi hayo leo zikiwa zimepita siku tatu toka Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa alipotoa maagizo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara
Bw. Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu
katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.
Waziri Mkuu aliagiza kiongozi huyo
kuchunguzwa kutokana na matumizi yasiyoeleweka ya fedha za miradi ya maendeleo
zinazotolewa na Serikali zikiwemo sh. milioni 12 walizotumia kuandaa profile ya
Halmashauri hiyo huku fedha zingine ni pamoja na sh. milioni 70 za elimu
maalumu, sh. milioni 288 za mradi wa maji Butiama ambazo zote hazikujulikani
zimetumikaje.
Chanzo :mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment