Tuesday, 23 January 2018

Vijana wanaojishughulisha na utengenezaji wa thamani za ndani katika manispaa ya mpanda mkoa wa katavi, wanakabiliwa na ukosefu wa masoko ya bidaa wanazozalisha.

MPANDA

Vijana wanaojishughulisha na utengenezaji wa thamani za ndani katika manispaa ya mpanda mkoa wa katavi, wanakabiliwa na ukosefu wa masoko ya bidaa wanazozalisha.

Wakizungumza kwa nyakati  tofauti na mpanda radio fm wafanya biashara hao wamesema kuwa hakuna utaratibu wowote uliofanya na serikali katika kuwatafutia masoko ya bidhaa wanazozalisha.

Aidha wamebainisha changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo katika shughuli zao kuwa ni pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu  pamoja na uelewa mdogo wa wateja kuhusu malighafi zinazotumika katika kutengeneza bidhaa hizo.

Hata hivyo wameiomba serikali kusaidia katika upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa bidhaa wanazozalisha ili kukuza uchumi wa nchi.

Halmashauri zote nchini hauatakiwa kuatenga 10% kwa uwiano wa asilimia tano kwa vijana na asiliamia tano kwa makundi ya wanawake ambayo shabaha yake ni kuwainua kichumi.


 #Changia Damu okoa Taifa.


Chanzo:Ezelina Yuda                                                                         

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...