DAR
ES SALAAM
Utafiti uliofanywa na wanayasansi wa Taasisi ya
Afya ya Ifakara (IHI) umebaini kuwa katika kila mwaka, madereva wa usafiri wa
umma jijini Dar es Salaam wako katika hatari kuambukizwa kifua kikuu (TB).
Kwa mujibu wa utafiti huo uliochapishwa katika
jarida la afya na maambukizi (Infection Journal), madereva wa usafiri wa umma
wako katika hatari kwa asilimia 20.3, wakati abiria wao wako katika hatari kwa
asilimia asilimia 2.4.
Hata hivyo, hatari kubwa zaidi imebainishwa
miongoni mwa wafungwa, ambao ni asilimia 41.6, ambao ni miongoni mwa makundi
yaliyofuatiliwa, ikiwemo majumba ya starehe, makanisa, sehemu za biashara na
kumbi za kijamii
Majibu ya utafiti huu, hasa kuhusu madereva na
abiria wao yanakuja wakati ambapo watu wengi hudhani kwamba kifua kikuu
husambaa zaidi miongoni mwa watu walio katika msongamano, hususani magari ya
umma.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment