China imeiomba Marekani iachane na fikra ya 'Vita vya baridi' baada ya Washington kusema inapanga kupanua mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia kwa kuunda mabomu madogo.
"Nchi inayomiliki silaha kubwa za nyuklia duniani, inapaswa kuongoza mkondo badala ya kwenda kinyume ," Waziri wa ulinzni wa China alisema Jumapili.
Jeshi la Marekani linaamini silaha zake za nyuklia zinaonekana kuwa kubwa kustahili kutumika na sasa inataka kutengeneza mabomu madogo.
Urusi tayari imelaani mpango huo.
Ni nini hasaa sera hiyo ya Marekani?
Marekani ina wasiwasi silaha zake za nyuklia hazitoweza kutumika tena, na hazina tishio. Imeitaja Uchina, Urusi Korea kaskazini na Iran kama mataifa yanayoweza kuwa tishio kwake.
Nyaraka iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Marekani siku ya Ijumaa- inayojulikana kama Nuclear Posture Review (NPR), inadai kuwa kutengeneza silaha ndogoza nyuklia itasaidia kupambana na fikra kuwa Marekani sio tishio. Silaha hizo ndogo hazina nguvu sana lakini bado zinaweza kusababisha madhara.
Sera hiyo pia inapendekeza:
- Makombora ya masafa marefu, nyambizi zilizohamiwa kwa makombora na silaha zitakazoundwa katika vyombo vya angani - vyote vitakavyokarabatiwa na kufanywa vya kisasa, kama mpango ulivyoanzishwa chini ya utawala warais wa zamani Obama.
- Imependekezwa ukarabati kwa baadhiya nyambizi zilizo na makombora yanyuklia kuzifanya kutoa milipuko ya kiwango kidogo au yasio na nguvu kubwa.
- Imependekeza pia kurudishwa kwa meli zilizo na makomobora ya nyuklia.
Sababu kubwa ya kuidhinishwa mpango mpya wa ulizni wa Marekani mwezi jana, ni kukabiliana na "tishio linaloongezeka la mataifa yenye yenye nguvu", kama Uchina na Urusi.
China imesema nini?
China imesema inapinga "vikali" ukarabati huo wa sera ya Marekani ya nyuklia.
Wizara za ulinzi mjini Beijing na Washington zilichukuliwa wepesi tishio linalowezekana kutokana na tishio la nyuklia la Uchina, zikiongeza kuwa sera zake ni kwa minajili ya ulinzi.
"Tunatarajia kuwa Marekani itaachana na fikra yake ya Kivita vya baridi, na iwajibikie kikweli majukumuyake ya kusitisha matumizi ya silaha hizo , ielewe kisawa sawa nia za Uchina na itazame kwa busara idaraya ulinzi yaUchina na uimarishajiwa jeshi lake," taarifa yake ilisema.
Urusi imesema nini?
Wizaraya mambo ya nje ya Urusi imeishutumu Marekani kwa kusambaza vita , na imesema itachukua 'hatua zipasazo' kuhakikisha usalama wa Urusi.
"Tangu kuisoma kwa mara ya kwanza, kauli ya kivita na inayoonekana kuipinga Urusi inajitokeza katika nyaraka hii," ilisema katika taarifa yake Jumamosi.
Waziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov ameeleza "kusikitishwa pakubwa" na mpango huo.
Chanzo:Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment