Sunday, 4 February 2018

Shinikizo zaidi lamkabili rais Zuma ajiuzulu.



Jacob ZumaHaki miliki ya picha
Image captionRais Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa na jitihada za wapinzani na baadhi ya wafuasi wa ANC, wanaotaka kumtimua madarakani.
Shinikizo linaongezeka dhidi ya rais Jacob Zuma Afrika kusini kujiuzulu, huku maafisa wakuu kutoka chama tawala ANC wakitarajiwa kukutana naye Jumapili kujadili mustakabali wake.
Rais Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa na jitihada za wapinzani na baadhi ya wafuasi wa ANC wanaotaka kumtimua madarakani.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, maafisa wa ngazi ya juu wa ANC wana 'jadiliana tu' na rais Zuma kuhusu "ugavi wa uongozi" ndani ya chama.
Lakini nyuma ya kauli hiyo nyepesi - vita vikali vya uongozi vinajitokeza katika nchi hiyo.
Rais Zuma bado yupo madarakani, lakini tangu Desemba mwaka jana, yeye sio mkuu tena wa ANC.
Cyril RamaphosaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKiongozi mpya wa chama cha ANC - Ramaphosa, ameshutumu wazi rushwa katika kiwango cha juu, ndani ya chama na pia serikali
Waendesha mashtaka wakakamavu sasa wanaonekana kushika kasi katika uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa zinazomkabili bwana Zuma na baadhi ya marafaiki zake wa karibu.
Wengi ndani ya ANC wanamtaka rais huyo ajiuzulu hara iwezekanavyo, ili waweze kulenga kujenga upya sifa ya chama hicho kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu nchini mwakani.
Lakini kuna taarifa kwamba Zuma anajikita kisawasawa.
Anatarajiwa kulihotubia bunge wiki ijayo, lakini wafuasi wa upinzani wanataka kumzuia pia, wakieleza kuwa hastahili kusalia kama rais.
Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa, ameshutumu wazi rushwa katika kiwango cha juu ndani ya chama na serikali, lakini anasisitiza kuwa rais Zuma hastahili kuazirishwa.
Chanzo:Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...