Tuesday, 6 February 2018

Idara ya uhamiaji mkoani Katavi imewarudisha wahamiaji haramu 38 waliotokea nchini Burundi na kuingia mkoani katavi bila kufuata utaratibu maalumu.



 

KATAVI

Idara ya uhamiaji mkoani Katavi imewarudisha wahamiaji haramu 38 waliotokea nchini Burundi na kuingia mkoani katavi bila kufuata utaratibu maalumu.

Mkuu uhamiaji mkoa Kamishina msaidizi Shabani Omar Khatibu amesema mkoa unakabiliwa na changamoto ya wahamiaji haramu ambao waingia mkoani hapa kupitia walowezi,wakimbizi ambao wamepewa uraia.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa idara ya uhamiaji pindi waonapo wageni ambao hawana taarifa za utambulisho wao.

Tanzania ni Nchi inayosifika kuwa na amani hivyo wajibu wa kila Mtanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani iliyopo.

Chanzo:RESTUTA NYONDO

#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...