Tuesday, 6 February 2018

Wafanyabiashara katika masoko ya halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kulipa kodi kabla ya tar 15 mwezi huu.



 

MPANDA

Wafanyabiashara  katika masoko ya  halmashauri  ya manispaa ya Mpanda  mkoani Katavi wametakiwa kulipa kodi kabla ya tar 15 mwezi huu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Mpanda Deodatus Kangu wakati akizungumza na Mpanda Redio na amebainisha kuwa kila mfanyabiashara lazima alipe kodi kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya maendeleo ya manispaa.

Kwa upande wa Afisa biashara  halmashauri ya manispaa yam panda Nkana Noel amewataka wafanyabiashara kuachana na mivutano ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya uchumi.

Katika hatua nyingine kaimu mkurugenzi amesema lori la taka lenye tani 16 linaingia leo ambalo litatumiaka katika kubebea takataka ili kuweka mazingira katika hali ya usafi.

CHANZO:REBECCA KIJA

#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...