MPANDA
Wakazi wa kitongoji cha Itogolo
kata ya misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameilalamikia serikali
kuwakamata, kuwatoza faini na kuwalazimisha kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa.
Malalamiko hayo wameyatoa
katika mkutano wa hadhara ambao umeitishwa na mwenyekiti wa kijiji cha Kampuni
Bw.James Simoni ili kusikiliza kero za wananchi wa kitongoji hicho wanaosema
wanakamatwa ovyo wakati elimu haijatolewa ya kutambua mita sitini kutoka chanzo
cha maji ya mto Mpanda.
Kwa upande wao wajumbe wa
kamati ya watumia maji bonde la mto Mpanda Mahela Mahanda na Daudi Sumuni
wamekanusha kuwaamrisha wananchi kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa lakini
wamekubali kuwakamata na kuwatoza faini kabla ya kutoa elimu kwa wananchi hao.
Mwenyekiti wa kijiji cha
Kampuni Bw.James Simoni amesema mpaka sasa watu watatu wamekamatwa na kutozwa
faini katika kitongoji hicho chenye kaya zipatazo 71 zinazotegemea mto Mpanda
kuendesha maisha yao.
CHANZO:
Issack Gerlad
No comments:
Post a Comment