NA, Rehema, Tizibazomo
JAMII imetakiwa kutambua haki za mtoto, ikiwa ni pamoja na malezi bora, haki ya ulinzi na haki ya mtoto kupata mahitaji muhimu yakiwemo ya elimu na Afya.
JAMII imetakiwa kutambua haki za mtoto, ikiwa ni pamoja na malezi bora, haki ya ulinzi na haki ya mtoto kupata mahitaji muhimu yakiwemo ya elimu na Afya.
Wito huo
umetolewa na watetezi wa haki za watoto wa Mkombozi Paralegal Association na
Afisa Ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda Agness Bulaganya, ikiwa ni siku ya Mtoto wa Afrika.
"jamii inapaswa itambue haki za watoto ili inapoona mtoto ananyanyaswa au anakuwa hatimiziwi haki zake basi wawe wa kwanza kumsaidia, na wakumbuke huyu mtoto hajajileta yeye mwenyewe duniani, hivyo anapaswa kutimiziwa mahitaji," walisema watetezi wa Haki za Mtoto.
Agness
ameongeza kuwa iwapo jamii itakuwa na usawa kati ya mtoto wa kike na kiume basi
maendeleo endelevu ikiwemo kulinda haki za mtoto zitatekelezwa kwa vitendo.
"kauli mbiu inataka usawa kwa mtoto ifikapo mwaka 2030, hivyo jamii inapaswa kuhakikisha usawa huu unakuwepo miongoni mwa watoto wa kike na kiume. sisi kama ustawi wa jamii sheria inatuagiza kulinda haki za mtoto, lakini haki hizi zinapaswa kulidwa kuanzia kwenye familia ambako ndio chimbuko la watoto" alisema Agness.
Baadhi ya
wazazi na walezi waliohojiwa kuhusu siku hiyo wamesema kuwa, siku imekuwa
ikiwakumbusha wajibu wao kwa watoto.
"hii ni siku nzuri ambayo wazazi wamekuwa wakikumbushwa wajibu wao na utekelezaji wa majukumu katika kulinda hai za watoto,
"serikali iwachukulie hatua wale wote ambao wanahusika na vitendo vya unyanyasaji kwa watoto,na wazazi waache kuwatumikisha watoto kazi ambazo haziendani na umri wao."
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila tarehe 16 ya mwezi
Juni ambapo Kitaifa yanafanyika Mkoani Dodoma, huku kauli mbiu ya
maadhimisho hayo ni maendeleo endelevu 2030 imarisha ulinzi na fursa sawa kwa
watoto.
No comments:
Post a Comment