Thursday, 30 November 2017

Wakazi wa vijiji vya Ndui Stesheni,Mnyaki A na Mnyaki B wanashindwa kufanya kazi za maeneleo kwa uhuru kutokana na uharifu unaofanywa na watu wasiojulikana.


MPANDA
Wakazi wa vijiji vya Ndui Stesheni,Mnyaki A na Mnyaki B wanashindwa kufanya kazi za maeneleo kwa uhuru kutokana na uharifu unaofanywa na watu wasiojulikana.

Hali hiyo imebainishwa na wakazi wa vijiji hivyo wakati wakizungumza na Mpanda Radio kwa Nyakati tofauti katika vijiji hivyo kutokana na matukio ya watu kuvamiwa nyumbani nyakati za usiku,kutekwa njiani na kuporwa mali.

Mmoja wa viongozi katika maeneo hayo Bw.Hussein Nasri ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ndui Stesheni,amekiri kuwepo kwa matukio ya kiuharifu hasa unyang’anyi wa pikipiki matukio ambayo hivi karibuni yameripotiwa na wenyeviti wa vijiji vya Mnyaki A na Mnyaki B.

Hivi karibuni,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda,akihojiwa na Mpanda Radio,alitoa kauli kuwa hajapokea za taarifa za kiuharifu za hivi karibuni hali ambayo imeibu maswali mengi miongoni mwa raia kuhusu mawasiliano kati ya kituo cha polisi Katumba na Makao makuu ya Polisi Mkoa.
Source: Issack Gerald

Viongozi wakubaliana Wahamiaji kuondolewa kwa dharura Libya.


Elfenbeinküste EU-Afrika-Gipfel in Abidjan (Reuters/P. Wojazer)
Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya na wa nchi za Umoja wa Afrika wanaokutana katika mkutano wa kilele nchini Ivory Coast wamekubaliana kuhusu mpango wa kuondoa nchini Libya wahamiaji wanaokabiliwa na mateso.
Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara katika mkutano wa tano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya na wa nchi za Umoja wa Afrika kutoa wito wa hatua za dharura kuchukuliwa kukomesha biashara ya utumwa na mateso mengine dhidi ya wahamiaji yanayoendela Libya. Rais Ouattara amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya kila liwezekanalo kukomesha madhila wanayopitia wahamiaji.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyeongoza kikao cha dharura pembezoni mwa mkutano huo kujadili suala hilo la biashara ya utumwa Libya, amesema viongozi wa Libya, Ujerumani, Chad, Niger, Ufaransa pamoja na nchi nyingine nne na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika wameamua kuanzisha operesheni ya dharura kuwaondoa wahamiaji hao kutoka Libya.
Libya yakubali wahamiaji kuondolewa
Waziri mkuu wa Libya Fayez Sarraj amekubali kuruhusu shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia wakimbizi UNHCR na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kuingia katika kambi za wakimbizi nchini mwake katika juhudi za kusaidia kuwarejesha makwao wakimbizi hao.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wafanya mazungumzo na Rais wa Ivory Coast Alassane Outtara katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Afrika mjini Abidjan
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ivory Coast Alassane Outtara
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa wito kwa Umoja wa Afrika kuyashirikisha makundi yote nchini Libya kwani waziri mkuu Serraj hana mamlaka katika maeneo yote ya nchi hiyo.
Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk na mwenyekiti kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahmati wametaka hatua za pamoja kuchukuliwa kulishughulikia tatizo hilo. Tusk amesema huu sio wakati wa kulaumiana bali wa kushirikiana ili kuyaokoa maisha.
Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa umetangaza kuanzishwa kwa kikosi cha pamoja cha kuwaokoa na kuwalinda wahamiaji hasa ndani ya Libya na kwa ushirikiano na maafisa wa Libya, kikosi hicho kinalenga kuharakisha kurejeshwa kwa hiari wahamiaji katika nchi zao, kupewa hifadhi kwingineko kwa wanaohitaji ulinzi wa kimataifa, kuyavunja makundi ya wafanyabiashara ya kusafirisha watu kimagendo na magenge ya wahalifu.
Mateso, ubakaji na utumwa Libya
Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari ameapa kuwarejesha nyumbani Wanigeria wote waliokwama Libya na kwingineko duniani.
Wanawake wawili wakimbizi kutoka Nigeria wakikumbatiana na kulia katika kambi ya kuwazuia wakimbizi ya Surman nchini Libya mnamo tarehe 178 mwezi agosti, 2017
Wakimbizi kutoka Nigeria wakilia katika kambi ya wakimbizi Libya
Mapema mwezi huu, kituo cha televisheni cha CNN kilionesha video inayoaangazia ukiukaji wa haki za binadamu Libya ambako wahamiaji wa Kiafrika waliuzwa mnadamani kama watumwa kwa kiasi cha hadi dola 400.
Kulingana na ripoti za mashirika ya kutetea haki za binadamu, wahamiaji wanaozuiwa Libya pia wanateswa, kubakwa na kuuawa.
Suala hilo limeghubika mkutano huo wa Abdijan ulioanza jana na kutarajiwa kukamilika leo. Ajenda kuu za mkutano huo wa Abidjan ni maendeleo kwa kuwekeza kwa vijana, uhamiaji na usalama.
Mkutano huo unalenga kuimarisha viwango vya elimu na fursa za kiuchumi kwa idadi ya watu inayokua kwa kasi barani Afrika ambapo inakadiriwa itaongezeka maradufu hadi watu bilioni 2.4 ifikapo mwaka 2050.
Umoja wa Ulaya unatumai kwa kulisaidia bara la Afrika kujiinua kiuchumi, kutapunguza idadi ya watu wanaotaka kuhamia Ulaya.
Chanzo:Dw swahili

Praljak: Mhalifu wa kivita afariki baada ya kunywa sumu mahakamani



Slobodan Praljak in court at The Hague, 29 NovemberHaki miliki ya picha
The Hague.
Kikao cha kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na washtakiwa wa uhalifu wa kivita mjini The Hague, Uholanzi kimesitishwa ghafla baada ya mmoja wa washtakiwa kusema amekunywa sumu baada ya kusikiliza hukumu.
Slobodan Praljak, 72, alikuwa mmoja wa viongozi sita wa zamani wa kisiasa na wa kijeshi wa Bosnia wa asili ya Croatia ambao walikuwa wamefika mahakamani.
Amefariki akitibiwa hospitalini na Umoja wa Mataifa umesema sasa mahakama hiyo ni "eneo la uhalifu".
Alikuwa amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 mnamo 2013 kwa makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa katika mji wa Mostar.
Baada ya kusikiliza hukumu kwamba majaji walikuwa wamedumisha kifungo hicho, alimwambia jaji, "Nimekunywa sumu".
Sita hao walikuwa wanasikiliza uamuzi wa mwisho wa rufaa uliokuwa unatolewa na mahakama maalum ya kimataifa ya UN iliyokuwa inashughulikiwa makosa yaliyotekelezwa Yugoslavia (ICTY).
Ingawa walikuwa washirika dhidi ya Waserbia wa Bosnia wakati wa vita hivyo vya 1992-95, Wacroatia wa Bosnia na Waislamu walipigana wenyewe kwa wenyewe kwa miezi 11.
Mji wa Mostar ulishuhudia mapigano makali zaidi.
'Usiondoe gilasi'
Praljak alisimama na akainua mkono wake hadi kwenye kinywa chake, kisha anainamisha kichwa chake nyuma na kuonekana kunywa kitu kutoka kwenye gilasi ndogo.
Jaji mwandamizi Carmel Agius mara moja alisitisha shughuli na gari la kuwabeba wagonjwa likaitwa.
"Sawa," jaji alisema. "Tunaahirisha ki...Tunaahirisha...Tafadhari, pazia. Usiondoe gilasi ambayo ameitumia alipokunywa kitu."
Kabla ya pazia kurejeshwa, ukumbi wa mahakama umeonekana kujawa na mkanganyiko, anasema mwandishi wa BBC Anna Holligan kutoka The Hague.
Gari la kuwabeba wagonjwa lilionekana baadaye likifika nje ya ukumbi wa mahakama huku helikopta ikipaa juu angani.
Wafanyakazi kadha wa uokoaji wameingia ukumbini na vifaa vyao.

Uhalifu dhidi ya Waislamu

Praljak, kamanda wa zamani wa wahudumu wakuu wa Jeshi la Walinzi wa Wacroatia wa Bosnia (HVO), alifungwa kwa makosa ya jinai dhidi ya binadamu.
Baada ya kufahamishwa kwamba wanajeshi walikuwa wanawakamata Waislamu Prozor majira ya joto 1993, alikosa kuchukua hatua zozote za maana kuzuia hilo, mahakama hiyo ya UN ilisema.
People take pictures in front of Mostar's Old BridgeHaki miliki ya picha
Image captionDaraja la kale la Mostar baada ya kukarabatiwa
Aidha alikosa kuchukua hatua hata baada ya kupashwa habari kwamba mauaji yalikuwa yamepangwa, pamoja na mashambulio dhidi ya wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa na kuharibiwa wka daraja la kale la mji wa Mostar na misikiti.
Mahakama ya ICTY ambayo iliundwa 1993 itamaliza kati yake mwisho wa mwaka huu.
Chanzo:Bbc swahil

Marekani yataka mataifa yote kukatiza uhusiano na Korea Kaskazini.



Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un na mwenzake wa Marekani Donald Trump
Image captionKiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un na mwenzake wa Marekani Donald Trump
Marekani imeyataka mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la masafa marefu.
Akizungumza katika baraza la usalama la umoja wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley amesema kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta kwa Pyongyang.
Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka.
Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili.
Korea Kaskazini imesema kuwa kombora hilo lililorushwa siku ya Jumatano ambalo inasema liliruka kimo cha kilomita 4,475, ikiwa ni mara kumi zaidi ya kimo cha kituo cha angani.
Madai hayo hayakuthibitishwa na wataalam wametiliashaka uwezo wa taifa hilo kuwa na teknolojia kama hiyo.
Hatahivyo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uzinduzi wa kombora hilo ulikuwa wa kufana.
Jaribio hilo likiwa mojawapo ya majaribio yaliofanywa na taifa hilo limeshutumiwa na jamii ya kimataifa na tayari baraza la usalama la umoja wa kimataifa limeitisha kikao cha dharura.
Bi Haley alionya kuwa kuendelea kwa uchokozi kunalenga kuliyumbisha eneo hilo.
''Tunahitaji China kuchukua hatua zaidi'', alisema.
Rais Trump alimpigia simu rais Xi Jinping mapema siku ya Jumatano , Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa rais Trump alizungumza na Xi Jinping kwa simu akimtaka kuchukua hatua zozote kuishawishi Korea Kaskazini kusitisha uchokozi na kusitisha mpango wake wa kinyuklia.
Chanzo:Bbc swahil

Waliotumia jina la Majaliwa kwa utapeli wakiona.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa 


DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro kuwakamata,Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw.Samwel kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya semi tela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Majaliwa ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuutapeli uongozi wa TPA kutaka kutoa magari hayo yaliyoingizwa nchini mwaka 2015 kutoka nchini Uturuki.

Aidha,Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu Serikalini.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bw.Bahman wa kampuni ya NAS kutaka kupata msamaha wa  kodi kwa kuidanganya TPA kwa madai kuwa wamewasiliana na Waziri Mkuu na wasipotekeleza jambo hilo watapata matatizo.
Source:EATV

HOFU imezuka katika kijiji cha Katani kata ya Nkandasi wilayani Nkasi mkoani Rukwa na kupelekea waombolezaji kutimua mbio na kuacha jeneza lenye mwili wa marehemu baada ya mvua kubwa kuanza kunyesha na kubomoa nyumba za wakazi


RUKWA
HOFU imezuka katika kijiji cha Katani kata ya Nkandasi wilayani Nkasi mkoani Rukwa na kupelekea waombolezaji kutimua mbio na kuacha jeneza lenye mwili wa marehemu baada ya mvua kubwa kuanza kunyesha na kubomoa nyumba za wakazi wa kijiji hicho.

Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kaungo,Robert Kanoni amesema tukio hilo limetokea wakati wakielekea kufanya maziko ya marehemu Dismas Kanoni aliyefari Juzi kwa kuugua.

Amesema ghafla mvua kubwa ilianza kunyesha ikiambatana na radi na upepo mkali hali iliyosababisha baadhi ya waombolezaji kukimbia na kurejea majumbani kwao kutokana na hofu iliyoibuka kufuatia tukio hilo.

Nyumba zipatazo 10 zimeharibiwa sana zinatakiwa kujengwa upya huku nyumba nyingine Saba zikiwa zimeezuliwa paa na wahanga kwa sasa wanategemea msaada wa majirani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya hiyo Said Mtanda ambaye pia ni mkuu wa wilaya  ya Nkasi,amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kujenga makazi bora kwani miongoni mwa nyumba  hizo zipo ambazo zimeezekwa kwa nyasi.
Source:Gurian

Wednesday, 29 November 2017

Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Leo kinafanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa nafasi za jumuiya mbalimbali Watakaoongoza jumuiya hizo kwa miaka mitano ijayo.


KATAVI.

Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Leo kinafanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa nafasi za jumuiya mbalimbali Watakaoongoza jumuiya hizo kwa miaka mitano ijayo.

Akizungumza na Mpanda Redio jana Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Katavi Bw. Kajoro Vyohoroka amewataka wagombea wa nafasi zote za jumuiya za chama kufuata kanuni za uchaguzi.

Amesema mgombea yeyote atakae bainika kushinda kwa kutumia rushwa  atafutiwa matokeo yake.

Katika hatua nyingine Katibu huyo amesema baada ya uchaguzi huo wa jumuiya za vyama leo wanatarajia kufanya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya mkoa kufanyika tarehe 5 mwezi wa 12 mwaka huu.

CHANZO: MDAKI HUSSEIN.

Uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari ndio chanzo kinachochangia wanafunzi kulazimika kupangiwa shule zilizopo mbali na maeneo yao.


MPANDA
Uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari ndio chanzo kinachochangia wanafunzi kulazimika kupangiwa shule zilizopo mbali na maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Afisa elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa Katavi Bi Helia Lukunguru wakati akizungumza na Mpanda Redio amesema shule za sekondari zilizopo hazitoshi kukidhi mahitaji yaliyopo kwa sasa.


Aidha ameeleza kuwa inawalazimu kuwapangia wanafunzi shule za mbali na maeneo yao kwa sababu shule za sekondari katika maeneo husika kushindwa kumudu idadi ya wanafunzi wanaofaulu.

Kauli hii inakuja siku chache baada ya wananchi kulalamika kuingia gharama zaidi.

CHANZO: REBEKA KIJA.

Korea Kaskazini: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani



Kombora hilo lililorushwa nyakati za giza alfajiri siku ya Jumatano lina uwezo mkubwa kushinda kombora lolote lile a taifa hiloHaki miliki ya picha
Image captionKombora hilo lililorushwa nyakati za giza alfajiri siku ya Jumatano lina uwezo mkubwa kushinda kombora lolote lile a taifa hilo
Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu ambalo linaweza kufika eneo lolote la Marekani.
Runinga ya kitaifa nchini humo imesema kuwa Pyongyang sasa imefanikiwa kuafikia azimio lake la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia.
Kombora hilo kwa jina Hwasong-15 ambalo imesema ndio kombora lenye uwezo mkubwa lilirushwa katika giza mapema siku ya Jumatano.
Lilianguka katika maji ya Japan lakini liliweza kuruka juu zaidi ya kombora jingine lolote la taifa hilo .
Kitengo cha habari cha taifa hilo KCNA kilisema kuwa kombora hilo liliruka katika kimo cha kilomita 4,475 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 950 katika dakika 53.
Kombora hilo lililofyatuliwa kwa mwinuko halikupitia katika anga ya Japan kama makombora mengine hapo awali na lilianguka kilomita 250 karibu na pwani yake ya kaskazini , kulingana na maafisa wa Japan.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alishuhudia kurushwa kwa kombora hilo
Image captionKiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alishuhudia kurushwa kwa kombora hilo
KCNA imeongezea kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ambaye alishuhudia kufyatuliwa kwa kombora hilo alitangaza 'kwa majivuno' kwamba sasa tumekamilisha lengo letu la miaka mingi la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia.
Ripoti hiyo imesema kuwa kama taifa lenye nguvu za kinyuklia na linalopenda amani, Korea Kaskazini itafanya kila iwezalo kutekeleza lengo lake la kuleta amani na udhabiti duniani.
Imesema kuwa, silaha zake za ulinzi dhidi ya sera ya kibepari ya Marekani, hazitatishia taifa lolote duniani iwapo maslahi ya Korea Kaskazini hayatakiukwa.''Hilo ndio tangazo letu''
chanzo:Bbc swahili

Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya NASA, Raila Odinga amesema anatarajia kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo Desemba 12, mwaka huu ambayo itakuwa siku ya uhuru wa Kenya.

kiongozi wa upinzani nchini kenya  Raila Odinga
NAIROBI.
Kiongozi wa Upinzani nchini  Kenya NASA, Raila Odinga amesema anatarajia kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo Desemba 12, mwaka huu ambayo itakuwa  siku ya uhuru wa Kenya.

Odinga ametoa kauli hiyo ikiwa katika uwanja wa Jacaranda saa chache baada ya Rais Kenyatta kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo katika uwanja wa Kasarani.

Hata hivyo, wakati Odinga akisema hayo, Rais Kenyatta mara baada ya kuapa amewaambia wananchi wa Kenya kuwa hakutakuwa na shughuli zingine za uchaguzi na yeye ndiye Rais mteule wa Kenya.

Hata hivyo, Polisi nchini Kenya walivamia uwanja uliopangwa kufanyika mkutano na maombolezo ya wananchi waliofariki wakati wa vurugu za uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, mwaka huu.

Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa jana  kuwa Rais wa Kenya ili kuwatumikia wakenya katika muhula wa pili wa uongozi.

CHANZO: EATV.

Kesi za udhalilishaji wanawake na watoto katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja zimepungua kuanzia Januari hadi Septemba 2017 ukilinganisha na mwaka jana


ZANZIBAR.
Kesi za udhalilishaji wanawake na watoto katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja zimepungua kuanzia Januari hadi Septemba 2017 ukilinganisha na mwaka jana.
Kesi hizo zilizokuwa zimeshika kasi kisiwani Zanzibar zimepungua kutoka 633 kipindi kama hicho mwaka jana hadi kufikia 404 mwaka huu.
Mratibu Msaidizi Dawati la Jinsia Wanawake na Watoto mkoani humo, Kassim Fadhil amesema hayo jana katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia yaliyofanyika Madema mjini Unguja.
Amesema kasi ya kupungua vitendo hivyo imekuja baada ya ushirikiano kati ya wananchi, taasisi za kiraia na Jeshi la Polisi ambalo ni wahusika wakuu wa kupinga matendo hayo dhidi ya raia.
Mkurugenzi Msaidizi Dawati la Jinsia Wanawake na Watoto Mjini Magharibi Unguja, Zahor Khamis amesema kwamba wanadhamira kuweka vitengo maalumu vya usuluhisho na utoaji wa elimu ya kutosha kwa baadhi ya wanandoa watakaobainika kuwa na matatizo ya udhalilishaji.

CHANZO: MWANANCHI.

IGP Simon Sirro amewataka wazazi na walimu wilayani Kibiti na Rufiji, kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola juu ya kutoweka kwa wanafunzi zaidi ya 1,300 wakati wa matukio ya kiuhalifu yaliyotokea katika wilaya hizo.

Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Simon Sirro

PWANI.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Simon Sirro amewataka wazazi na walimu wilayani Kibiti na Rufiji, kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola juu ya kutoweka kwa wanafunzi zaidi ya 1,300 wakati wa matukio ya kiuhalifu yaliyotokea katika wilaya hizo.
Katika ziara yake ya kikazi wilayani Kibaha, mkoani Pwani IGP amezungumza na wazazi, walimu pamoja na viongozi wa mashirika ya umma,wazee maarufu, wastaafu mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo.

IGP Sirro amewataka wazazi husika na walimu wa shule za msingi na sekondari ambazo wanafunzi walikuwa ni watoro ama hawajaripoti shule kwa miezi kadhaa kutoa taarifa kwani wapo baadhi ya watoto wanaotumika kufundishwa uhalifu hata wakutumia silaha na watu wasiowema.

Kamanda Sirro ameeleza kuwa taarifa ya wanafunzi zaidi ya 1,300 mkoani hapo kuwa ni watoro na hawajulikani walipo hivyo wazazi washirikiane kusaidia jeshi la polisi kujua walipo.

Mkuu huyo wa jeshi la polisi amewahakikishia wananchi mkoani Pwani kuwa silaha zote zilizochukuliwa na wahalifu wa huko Kibiti na Mkuranga zimerudi zote mkononi mwa dola na kusambaratisha mtandao wa kiuhalifu na wanaendelea kushirikiana na Msumbiji kutokomeza uhalifu.

CHANZO: EATV.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jana amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.


NAIROBI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jana  amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Makamu wa Raisi  amemfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake.

Kwa upande wake Mbunge Tundu Lissu amemshukuru Rais Magufuli na makamu wa Raisi  kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao.


CHANZO: MPEKUZI.

Tuesday, 28 November 2017

Rais Uhuru Kenyata Kenya ameapishwa leo kuhudumu muhula wake wa pili kama rais wa nchi hiyo.




Rais Uhuru Kenyata Kenya ameapishwa leo kuhudumu muhula wake wa pili kama rais wa nchi hiyo Maelfu ya watu wamekusanyika katika mji mkuu wa Kenya- Nairobi, kuhudhuria sherehe hiyo.

Takriban viongozi wakuu wa nchi 13 za Afrika wakiwemo marais wamehudhuria sherehe hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Kasarani.

Sherehe hiyo imefanyika huku usalama ukiimarishwa katika sehemu kadhaa za mji huo kufuatia wito wa upinzani kuandaa mkutano mbadala wa kuomboleza wafuasi wao waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga ushindi wa Kenyatta.

Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa Kenyatta waliotaka kuingia katika uwanja wa Kasarani.

Vilevile polisi wameshika doria na kuuzingira uwanja wa Jacaranda ambao muungano wa upinzani NASA ulipania kuutumia kuandaa mkutano wao wa maombolezi

CHANZO: BBC.

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...