Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amewashukuru wananchi wa Zimbabwe na jeshi kwa uungaji mkono wao.
Katika hotuba yake ya kwanza kwa wafuasi wake baada ya kuwasili Zimbabwe akitokea nje ya nchi alikokimbilia, Bw. Mnangagwa amesema ameguswa sana na wananchi wa Zimbabwe kumunga mkono baada ya kufukuzwa na rais wa zamani Robert Mugabe wiki mbili zilizopita.
Pia amesema, Zimbabwe inahitaji amani, inahitaji ajira kwa watu wake, na kwamba Wazimbabwe wanapaswa kushikamana na kukuza uchumi wa nchi yao.
SOURCES:CRI KISWAHILI.
No comments:
Post a Comment