Ufaransa imelaani visa vya utumwa vinavyoendelea nchini Libya
na kuomba mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametaja visa vya kuwauza wahamiaji kutoka Afrika kama watumwa Libya kuwa ni uhalifu dhidi ya binadamu.
Wiki jana, kituo cha televisheni cha CNN kilifichua kuwepo kwa soko la watumwa karibu na mji wa Tripoli, hali ambayo ilishtumiwa katika Afrika na Ulaya.
Kwa mujibu wa rais Macron, kilichofichuliwa na CNN ni wazi kwamba ni biashara ya binadamu na Ni uhalifu dhidi ya binadamu.
SOURCES:RFI KISWAHILI.
No comments:
Post a Comment