DAR ES SALAAM
Mtoto wa miaka saba aliyelelewa kama mtoto wa kike kutokana na maumbile yake kutoeleweka vema baada ya vipimo vyote katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ameonekana kuwa ni mwanamume.
Kufuatia hatua hiyo,amefanyiwa upasuaji wa kwanza wa kushusha mbegu za kiume kwenda kwenye korodani ili kumrejesha katika hali ya kawaida.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto MNH Zaitun Bokhary amebainisha hali hiyo akizungmzia kuhusu kambi ya wiki moja iliyowekwa kwa ajili ya kufanya upasuaji ambao ni mgumu, wakishirikiana na wataalamu watano kutoka Chuo Kikuu cha Oxford nchini Marekani.
Dk Bokhary amesema upasuaji huo ni hatua ya kwanza katika kumrejesha mtoto huyo katika hali ya kawaida huku akisema hatua nyingine za upasuaji zitafuata kwani atafanyiwa upasuaji kwa hatua tatu.
Source: Eatv,
No comments:
Post a Comment