Tuesday, 17 April 2018

TAHADHARI YA ZIMA MOTO

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuondoka katika maeneo hatarishi katika kipindi hiki cha mvua ili kujinusuru  na majanga yanayoweza kujitokeza.

Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa katavi Abdalha Maundu wakati akizungumza na Mpanda Redio na kusema kuwa wananchi waliopokatika maeneo ya bondeni au yanayoweza kukumbwa na mafuriko wanatakiwa kuondoka ili kujikinga na majanga  mbalimbali yanayoweza kutokea.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi ambao hawajui jinsi ya kutumia vifaa vya kuzimia moto na uokoaji wafike katika ofisi zao ili waweze kupewa elimu itakayowasaidia kutumia vifaa vya kujikinga na majanga.

Jeshi la zima moto na uokoaji  lina majukumu mbalimbali  ikiwemo kuzima moto na  kuokoa maisha na mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengineyo.

Chanzo:Rebecca 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...