Friday, 29 September 2017

Mbunge wa Kilombero ameshikiliwa na kuhojiwa na polisi wilayani Malinyi kwa saa nne.

Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali 

MOROGORO
Mbunge wa Kilombero mkoani Morogoro, Peter Lijualikali ameshikiliwa na kuhojiwa na polisi wilayani Malinyi kwa saa nne.
Pamoja naye, viongozi wengine watatu wa Chadema walishikiliwa jana wakidaiwa kufanya mkusanyiko bila kuwa na kibali cha polisi.
Akizungumza leo baada ya kuachiwa mbunge huyo amesema aliamriwa na polisi  kusimama alipokuwa akitoka kwenye kikao cha ndani cha viongozi na baadhi ya wanachama wa Chadema katika Kijiji cha Makerere wilayani Malinyi.
Mbunge huyo amesemabaada ya kumpigia simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amejibiwa  yupo likizo.

Wengine waliokamatwa pamoja na mbunge huyo ni Mwenyekiti wa Chadema Malinyi, Emmanuel Lukindo; Katibu wake, Sadi Lyampawe na Katibu Mwenezi wa wilaya, Lucas Lyambalimu ambao wote wameachiwa kwa dhamana

Mapungufu ya UN katika mzozo wa Rohingya.

Mamia kwa maelfu ya wakimbizi wa Rohingya wakiwa kambini Baghladesh
Mamia kwa maelfu ya wakimbizi wa Rohingya wakiwa kambini Baghladesh
Haki miliki ya pichaImage captio
Uchunguzi wa bbc umeibua maswali mazito kuhusiana na Umoja wa mataifa ulivyoshughulikia hali ya machafuko ya Rohingya.
Nyaraka zilibainika na mahojiano yanaonyesha kuwa Umoja wa mataifa na serikali ya Myanmar waliwazuia maofisa waliokuwa wakiibua matatizo ya watu wa Rohingya dhidi ya serikali ya Burma.
Maofisa wa umoja wa mataifa kwa mujibu wa uchunguzi wa BBC waliwazuia wafanyakazi wa haki za binadamu kuingia katika maeneo muhimu ili kutoa misaada.
RohingyaHaki miliki ya picha
Image captionBaadhi ya maeneo ya Rohingya
Umoja wa mataifa wa Myanmar katika kuendelea kupinga uchunguzi wa BBC unasema kuwa umekuwa mstari wa mbele kusaidia raia, ambapo hata waliokimbia nchi walisaidiwa ulinzi na umoja wa mataifa na sasa wanaendelea kuhudumiwa katika katika kambi za wakimbizi.
Hata hivyo vyanzo kutoka ndani ya umoja wa mataifa nchini humo vimeiambia BBC miaka mine iliyopita kabla ya mzozo huu wa sasa, mkuu wa Umoja wa mataifa wa Myanmar raia wa Canada Renata Lok Dessallin alizuia makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu kufika katika maeneo ya Rohingya.
Pia alijaribu kuzuia uhamasishaji kuhusiana na vurugu za eneo hilo pamoja na kuwaondoa wafanyakazi waliojaribu kutuliza mzozo huo kwa kuendesha mikutano na makongamano.
Zaidi ya watu laki tano wa Rohingya wamekimbilia nchi jirani ya Bangladesh.
@habari na bbc swahili

Watu 22 wafariki katika mkanyagano kwenye reli Mumbai.


Barabara ya Elphinstone inaunganisha njia mbili za reli Mumbai
Haki miliki ya picha
Image captionBarabara ya Elphinstone inaunganisha njia mbili za reli Mumbai
Watu kumi na wawili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, kufuatia kisa cha mkanyagano baada ya daraja moja kuporomoka karibu na kituo cha treni, mjini Mumbai India.
Waliyoshuhudia wanasema, daraja hilo huenda liliporomoka kutokana mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati huo, hali ambayo iliwafanya watu kukimbilia mahala hapo kujikinga.
Mwandishi wa BBC mjini Mumbai, anasema mamlaka imekuwa ikilaumiwa kwa kutelekeza miundo mbinu katika mji huo licha ya kuwa mji huo unapokea watu wengi kila siku.
Nilibakwa nikiwa na miaka 10, lakini nimejifunza kuwasamehe watu
Watu waliojeruhiwa wamefikishwa katika hospitali iliyo karibu na maafisa wakuu wa reli wapo katika eneo la mkasa.
Msemaji wa shirika la reli Anil Saxena ameambia waandishi habari kuwa daraja hilo lililofunikwa lilikuwana shughuli nyingi kwasababu idadi kubwa ya wasafiri waliokuwa wanajikinga na mvua kubwa walijaribu kuondoka kwa wakatimmoja na abiria wengine.
Ameongeza kuwa mkasa huo utachunguzwa
@habari na bbc swahili

Serikali ya Tanzania yalifungia gazeti la Raia Mwema kwa siku 90

Gazeti la Raia Mwema ni gazeti la pili ndani ya miezi minne
Raia Mwema limefungiwa na Serikali ya Tanzania


Gazeti la Raia Mwema ambalo ni gazeti la kila wiki, limefungiwa na serikali ya Tanzania kwa siku 90 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo.
Idara hiyo imeeleza sababu za kusitisha uchapishaji na usambazaji wa gazeti hilo kuwa ni kutokana na kuchapishwa kwa toleo la tarehe 27 mwezi Septemba hadi 3 Oktoba 2017, lenye kichwa cha habari inayosomeka, "URAIS UTAMSHINDA JOHN MAGUFULI."
Idara hio imedai kuwa gazeti hilo limetoa nukuu zisizo za ukweli kuhusu Rais John Magufuli, japo imekubali kuwa ni haki ya gazeti hilo kutoa maoni. Kusitishwa kwa gazeti hilo ni pamoja na toleo ya mtandaoni.
Hili ni gazeti la tatu kufungiwa ndani ya miezi minne, ikiwemo gazeti la Mwana Halisi lilifungiwa takriban wiki mbili zilizopita kwa kile kilichodaiwa kuwa ni uchapishaji wa habari za uongo na kuchochea ambazo inadaiwa kuwa zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa hilo.
Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikimulikwa kwa karibu nchini Tanzania. Mapema mwaka huu Raisi Magufuli alionya vyombo vya habari 'visifikirie viko huru kwa kiwango hicho.'
@habari na bbc swahili

China yatoa msaada 29.4 bilioni.



Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi 29.4bilioni kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu, utalii wa kijiolojia na kuukarabati Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong.
Katibu huyo amesema 22.4bilioni  zitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera.
“Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” amesema   James

Ameeleza kwamba  kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho.
“Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu wake watakaochangia kukuza sekta ya uzalishaji na hatimaye kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini” amesema  James
Katibu Mkuu huyo amesema China, itatoa 6.7bilioni kwa ajili ya kuukarabati Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.

“Katika makubaliano yetu ya msaada wa kuendeleza Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000, China itatoa msaada wa kiufundi na vifaa vya kisasa vya michezo na utaalamu katika usimamizi na ukarabati wa uwanja” Amefafanua James

Amesema  kiasi kingine cha shilingi 300milioni zitatumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuanzishwa kwa aina mpya ya utalii ujulikanao kama utalii wa kijiolojia “Geopark Project” katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, mkoani Arusha.
Alisema lengo la utafiti huo ni kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika na maajabu mbalimbali ya kitalii yaliyopo nchini ambayo hayajatumika kikamilifu kuvutia watalii watakaoongeza pato la Taifa
“Tanzania ina kila sababu ya kujifunza kutoka katika Hifadhi ya Kimataifa ya Jiolojia ya Jiaozuo ya Yuntaishan ya China, iliyoanzishwa mwaka 2000 ambayo inaongeza asilimia 37.2 ya watalii kila mwaka na huchangia asilimia 12 ya pato la Taifa la nchi hiyo” 
Tangu miaka ya 1960 mpaka sasa nchi hiyo imeendelea kuisaidia  Serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo upanuzi wa Chuo cha Polisi Moshi, Ujenzi wa Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong, amesema ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Veta huko Ngara mkoani Kagera utaanza haraka kama ilivyopangwa.
Kuhusu masuala  ya utalii wa kijiolojia katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, amesema Tanzania ina bahati ya kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini haijavutia idadi kubwa ya watalii kutoka China kuja kuvitembelea.
“Zaidi ya watalii milioni moja kutoka China wanatembelea nchi mbalimbali dunia lakini kati ya hao, Tanzania inapokea watalii 20,000 tu kila mwaka kutoka China, lakini kwa kuanzisha mradi huu, watalii wengi kutoka China watavutiwa kuja nchini kufurahia utalii wa miamba, mandhari nzuri, urithi wa dunia, na kutembelea hifadhi za Taifa” ameongeza Haodong
Akizungumzia masuala ya uchumi, Balozi huyo amesema  hivi sasa China imekuwa mwekezaji mkubwa zaidi nchini Tanzania kwa kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani 1.77bilioni  na kukuza ajira nchini.
Ameitaja baadhi ya miradi mikubwa iliyowekezwa kuwa ni pamoja na mradi wa miundombinu ya mtandao (Tanzania ICT broadband backbone), Bomba la gesi la kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, mradi wa kuboresha miundombinu ya bandari ,barabara na madaraja.
@habari na mwananchi

(MCT) limesema litaanza kuwashtaki watakaovunja uhuru wa Habari ikiwamo kuwazuia waandishi wa Habari kupata taarifa, vipigo na matukio yote ya udhalilishaji dhidi yao.

Mneja Viwanja na Udhibiti wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bi. Pili Mtambalike,

DAR ES SALAAM
Baraza la Habari Tanzania  (MCT) limesema litaanza kuwashtaki watakaovunja uhuru wa Habari ikiwamo kuwazuia waandishi wa Habari kupata taarifa, vipigo na matukio yote ya udhalilishaji dhidi yao.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa MCT, Ofisa Miradi wa Baraza hilo Pili Mtambalike amesema matukio hayo yanaongeza hofu na kuwafanya waandishi  washindwe kutimiza wajibu wao kikamilifu.
Mtambalike amesema pamoja na hatua nyingine wataanza kuwachukulia hatua ikiwamo kuwashtaki wale watakaofanya hivyo huku akiwaasa wanahabari kutoa taarifa vinapotokea vitendo vinavyokiuka uhuru wa habari.
Hata hivyo amesema kwa mwaka huu zaidi ya matukio 11 yameripotiwa ikiwamo lile la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuvamia kituo cha  TV cha Clouds.

Rais wa MCT, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema baraza hilo lilianzisha Rejista ya  Matukio ya Uvunjaji Haki wa Habari  ili kuhakikisha kila tukio linaripotiwa na kuchukuliwa hatua.

WAKAZI wa kijiji cha Milala wameilalamikia serikali kutochukua hatua dhidi ya viboko waliopo bwawa la Milala vinavyoharibu mazao shambani na kutishia uhai wa binadamu.


MPANDA

WAKAZI wa kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo katika Manispaa ya Mpanda,wameilalamikia serikali kutochukua hatua dhidi ya viboko waliopo bwawa la Milala vinavyoharibu mazao shambani na kutishia uhai wa binadamu mara kwa mara.

Wakizungumza na Mpanda Radio wakiwemo pia wakazi wa mitaa ya Kigamboni,Misunkumilo  na Makanyagio wamesema, madhara mengine ambayo yametokana na viboko hao ni kuvunjika kwa ndoa zao kutokana na wanaume kuhamishia makazi yao shambani ili kudhibiti viboko wasiharibu mazao yao.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Misunkumilo Bw.Antipas Kalumbete ambaye pia ndiye anayekaimu nafasi hiyo katika kijiji cha Milala,amethibitisha viboko hao kuwa tishio wa wakazi wa maeneo hayo akisema kuwa maliasili waliandikiwa barua lakini mpaka sasa hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa dhidi ya wanayama hao.


Bwawa la milala ambalo ni miongoni mwa vyanzo vya maji yanayotumika kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda inasemekana kwa sasa lina viboko zaidi ya thelathini huku wakazi wa maeneo jirani na bwawa hilo wakilazimika kujifungia ndani majira ya jioni wakiogopa kushambuliwa.

Thursday, 28 September 2017

Tabora: Watu 57 kortini kwa kujaribu kuua


WENYEVITI wawili wa Serikali ya Kijiji cha Mwamabondo na Songambele, Charles Buligi na Machele Kalele na watu wengine 55 kutoka Kata ya Loya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, wamefi kishwa mahakamani wakikabiliwa na tuhuma nne za kujaribu kuua wanawake wanne.
Watuhumiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Tabora, Emmanuel Ngigwana jana. Wenyeviti waliofikishwa mahakamani hapo ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Songambele, Machele Kalele mwenzake wa Mwamabondo, Charles Buligi.
Upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Idd Mgeni uliiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo Septemba 17, mwaka huu. Mgeni alidai kwenye shitaka la kwanza kuwa siku hiyo majira ya mchana, watu hao katika Kijiji cha Mwamabondo wilayani Uyui, walijaribu kumuua Elizabeth Kashindye.
Ilidaiwa katika shitaka la pili, tatu na nne kuwa Septemba 17, mwaka huu majira ya mchana katika Kijiji cha Mwamabondo, watuhumiwa walijaribu kuwaua Manugwa Lutema, Rahel Mkomazwa na Maria Sahani wakiwatuhumu kuwa ni washirikina.
Watuhumiwa wengine waliosomewa mashitaka hayo ni Basu Mitalu, Gwala Mwita, Dettu Macha, Mwandu Samwel, Kapaya Sombi, Masanja Sadi, Yaledi Masegese, Soda Mateman, Masanja Ditu, Samson Kabizo, Jumanne Lugembe, Mayombya Nyanda, Mwandu Masanja, Makoye Madirisha, Juma Charles na Mbulu Chagijo.
Pia wamo Masanganya Sinzo, Shija Jileka, Bala Mangosa, Jitumbi Mboje, Jileke Numbua, Samudi Buchenja, Shaban Saguda, Kaseko Masinzagule, Masanja Magite, Jilala Salum, Shinje Malosa, Japhet Nicholaus, Boniphace Deo, John Yusuph, Chinumbo Jileke, Shija Mayunga, Fred Elia, Haji Kashinje, Haji Ramadhan, Shilinde Jileke na Mashana Matemba.
Wengine ni Masunga Barabara, Shinje Masanja, Mwandu Ndashimu, Sungu Anthony, Rambo Kihanda, Yohana Charles, Said Daud, Basu Mpamwa, Makoleo Kashiwa, Kuba Samwel, Nkuba Zengo, Shigela Ngelela, Sambo Cholamadama, Michael Kashinye, Hamis Makoleo na Mbiji Mwanamila.
Shauri hilo limeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu, na dhamana kwa watuhumiwa zitafikiriwa baada ya kujiridhisha juu ya afya za walalamikaji ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete kwa matibabu kufuatia majeraha waliyopata.
Septemba 16, mwaka huu, mkazi wa kijiji hicho cha Mwamabondo, Mafumbi Jilawise ambaye ni mume wa Manugwa Lutema, alifariki dunia na ndipo wananchi wakawashambulia akinamama hao wakiwatuhumu kwa ushirikina wakiwahusisha na kifo hicho.
Kutokana na shambulio hilo, Jeshi la Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia walilazimika kufika kijijini hapo na kuwaokoa akina mama hao ambao walikuwa tayari mikononi mwa wananchi hao wakihukumiwa kwa kuchapwa fimbo na kutaka kuchomwa moto.
@habari na habari leo

Mwigulu: Lissu atatusaidia kukamilisha upelelezi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba 
Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amezungumzia uchunguzi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akisema anaamini akipona atatoa mchango mkubwa katika upelelezi.
“Lissu tunamuombea akishapona atatupa mchango mkubwa wa kusaidia uchunguzi, mtu akiwa kwenye maumivu makali huwezi kumuuliza lolote,” amesema Mwigulu akizungumza leo Alhamisi katika kipindi cha Clouds 360.
Amesema kutokana na upya wa uhalifu wa aina iliyotokea kwa Lissu, kuna mambo wanaendelea kuyafuatilia ambayo hawezi kuyaeleza kwa sasa. 
“Suala la Lissu kutokana na upya wake, kuna vitu tunaendelea kuvifuatilia, hivyo kuna mambo hatuwezi kuyasemea,” amesema.
Amewataka Watanzania waendelee kuwa na subira kwa kuwa kazi inaendelea kufanyika.
Mwigulu amesema baada ya tukio la kushambuliwa Lissu Septemba 7, taarifa kadhaa zilichukuliwa eneo la tukio ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi ili kupata undani wake.
“Wahalifu hawajakamatwa wote, ukianza kusema itakuwa ni shida, kuna mambo yanaendelea kufanywa na hayana ukomo. Ukomo utafikiwa endapo wote waliohusika watakamatwa. Nikisema naweza kuvuruga kazi inayoendelea,” amesema.
Akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho kuwa watu wanahoji kwamba askari wanapouawa wahalifu wanakamatwa mapema Mwigulu amesema, “ Watu wakiwaza hivyo watakuwa wanakosea, hatuweki madaraja, ni mazingira ya tukio tu.”
Akizungumzia uchunguzi unaoendelea kuhusu kuvamiwa kwa Lissu amesema hawezi kueleza waliokamatwa bali tayari kuna magari zaidi ya 10 yanayofanana na lililohusika kwenye tukio yamekamatwa.
Mwigulu amesema alimuona Lissu siku ya tukio Septemba 7 akiwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na baadaye uwanja wa ndege aliposafirishwa kwa ajili ya matibabu jijini Nairobi nchini Kenya ambako yuko hivi sasa.
Amesema hajafika Nairobi kumjulia hali Lissu bali kwa Mkoa wa Singida, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amefika.
“Katika mazingira mengine tunaendelea kupata taarifa, kama Serikali tuna balozi,  kama waziri kwenda kumuona ni jambo jema katika utaratibu wa uchunguzi hata dereva tutazungumza naye,” amesema.
Amesema dereva hivi sasa anapata tiba ya kisaikolojia na anaamini atakapokuwa tayari atazungumza na wanaokusanya taarifa.
@habari na mwananchi

Waziri, wabunge 25 wasimamishwa kuhudhuria vikao Uganda.


Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Kadaga amewasimamisha waziri mmoja na wabunge 25 kuhudhuria vikao vya bunge kwa madai ya kushiriki katika vurugu ambayo ilimlazimisha kuahirisha kikao siku ya Jumatano.
Mmoja wa waliozuiliwa kuhudhuria vikao ni Waziri wa Maji, Ronald Kibuule kwa madai ya kwenda katika ukumbi wa bunge akiwa na silaha.
Wabunge wengine waliosimamishwa kuhudhuria kikao wengi wao ni wa upinzani wanaopinga kufutwa kwa kifungu 102(b) kutoka katika katiba ambayo inakataza watu ambao wanaumri zaidi ya miaka 75 kugombea nafasi ya urais, ambao wamekataa kutoka katika ukumbi wa bunge na kumlazimisha spika kuahirisha kikao.
Wale waliozuiwa kuhudhuria vikao vya bunge ni : Robert Kyagulanyi aka Bobi Wine (Kyaddondo Mashariki), MP Allan Ssewanyana (Makindye Magharibi),Monica Amoding (Wilaya ya Kumi ), Dr Sam Lyomoki (Wafanyakazi) Betty Nambooze (Manispaa ya Mukono) Ibrahim Kasozi (Makindye Mashariki) andMoses Kasibante (Rubaga Magharibi).
Baada ya mgogoro huo, maafisa wa ulinzi wakiwa katika vazi la suti walivamia Ukumbi huo na kuwalazimisha Kyagulanya na Ssewanyana kutoka nje.
Serikali ya Uganda inataka kuondoa ukomo wa umri kwa wagombea urais kitu kilicholeta vurugu Jumatano katika bunge la Uganda.
Hatua hivyo ya serikali itamwezesha Yoweri Museveni kuendelea na nafasi yake ya urais.
Sheria hizo zilikuwa tayari zimebadilishwa 2005 zikiondoa ukomo wa awamu mbili ambapo ilimwezesha Museveni ambaye sasa ana umri wa miaka 72 na awamu yake ya tano, kuendelea kuwepo katika madaraka.
Chini ya katiba iliyokuwepo Rais Museveni atakuwa amepitiliza umri unaoruhusiwa na katiba kugombea katika uchaguzi wa mwaka 2021.
@habari na voa swahili

Watoto Wa Africa Mashariki Wapo Hatarini Kukumbwa Na Njaa.


Mmoja wa watoto katika eneo la Afrika mashariki



Zaidi ya watoto 800,000 wako katika hatari ya kukumbwa na njaa huko Afrika mashariki na mashirika ya misaada yana wiki kadhaa tu kuwaokoa. Shirika la hisani la World Vision limesema Jumatano.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters mzozo nchini Sudan Kusini na ukame wa muda mrefu ambao umelikumba eneo hilo umewaacha zaidi ya watoto milioni 15 wakiwa na shida ya chakula, maji, huduma za afya, elimu au ulinzi imesema idara ya Umoja wa Mataifa ya kuhudumia watoto- UNICEF.
Nchi ya Ethiopia, Somalia na Kenya zimeshuhudia kupanda kwa viwango vya njaa miongoni mwa watoto katika wiki za karibuni huku maeneo kadhaa yakiripoti zaidi ya theluthi moja ya watoto wana matatizo ya afya ikiwa ni matokeo ya hali hiyo taarifa ya World Vision ilisema. “Bado tuko katika hali ya hatari zaidi ya watoto 800,000 wana utapiamlo uliokithiri na wako katika hatari ya kukumbwa na njaa ambayo itapelekea vifo alisema Christopher Hoffman mkurugenzi wa Afrika mashariki wa World Vision. Tuna wiki chache tu kusitisha hali hii kutokea”.
@habari na VOA swahili

Wednesday, 27 September 2017

Wanawake ruhsa kuendesha magari Saudia

Saudi
Image captionWanawake wa Saudi Arabia sasa kuruhusiwa kuendesha gari


Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametoa idhini ya wanawake kuendesha magari, hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa. Uamuzi huu umefikiwa kutokana na harakati za muda mrefu kwa makundi ya wanawake na haki za bindamu kushinikiza wanawake waruhusiwe kuendesha magari.
Kwa muda mrefu Saudi Arabia imekuwa nchi pekee Duniani kuwazuia wanawake kuendesha magari. Abdallah al-Mouallimi Mwakilishi wa umoja wa mataifa kutoka Saudia ametangaza habari hizi umoja wa huko umoja mataifa.
"Ndugu Mwenyekiti, Mabibi na mabwana. Najua mtapenda kujua jambo hili kwamba dakika chache zilizopita Mfalme amepitisha sharia inayowapa idhini,wanawake nchini Saudia kuendesha magari.Hii ni historia mpya leo kwa jamii ya Saudia,kwa wanaume na wanawake.Na kwa sasa tunaweza kusema kitu angalau.'' Abdallah al-Mouallimi.

Saudia
Image captionWanawake wa Saudia

Akizungumza na waandishi wa msemaji wa idara ya Marekani,Bi.Heather Nauert amelezea kupokea kwa furaha tangazo hilo.
"Tuna wanafuraha kusikia jambo hilo,kwamba wanawake wa Saudia sasa wanaruhusiwa kuendesha magari,kwa hapa Marekani tunafurahia jambo hilo,na kuona ni hatua kubwa na mwelekeo mzuri kwa taifa hilo'' Heather Nauert.
Mwanaharakati wa Saudi Arabia aliyewahi wekwa kizuizini kwa siku 73 kutokana na kupinga wanawake kuzuiwa kuendesha magari, ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akisema 'Thank you God', yaani asante Mungu.
Sheria hii inaanza kufanya kazi mwezi june mwaka ujao, na kwa sasa wizara itatakiwa kuandaa ripoti maalumu kuhusiana na jambo hilo.
@habari na bbc swahili

wakazi wa kata ya Litapunga Halmashauri ya Nsimbo wamelalamikia ubovu wa barabara inayotoka Mnyaki kuelekea kijiji cha Kaburonge A na B.


MPANDA.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Litapunga Halmashauri  ya Nsimbo Mkoani Katavi wamelalamikia ubovu wa barabara inayotoka Mnyaki kuelekea kijiji cha Kaburonge A na B.

Wananchi hao akiwemo Bi. Janeti Sadi wamesema kuwa ubovu wa barabara hiyo hasa daraja linalounganisha eneo la Mnyaki na Kaburonge inaweza kusababisha vifo kwa wagonjwa. 

Sadekia Ndikumana Mwenyekiti wa kijiji cha Kaburonge A amesema  ubovu wa barabara hasa daraja umekuwa ni wa kipindi kirefu  na wamekuwa wakimlilia diwani juu ya suala hilo  lakini hawaoni juhudi zozote za kutatua changamoto hiyo.

Diwani wa Kata ya Litapunga Juma Masoud Mnyongagule amesema wapo katika mchakato wa kutatua changamoto hiyo. 

Aidha diwani Mnyongagule amewaomba wananchi kuwa na subira kwa kusema anashirikiana na Wenyeviti wa vitongoji, Vijiji pamoja na watendaji wa kata ili kuletea taifa maendeleo.  


@habari na Mdaki Hussein.

IEBC kukutana na vyama vya Jubilee na NASA kabla ya uchaguzi.


Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imepanga kukutana na wawakilishi wa chama tawala Jubilee na wale wa upinzani NASA, kuelekea Uchaguzi wa urais mwezi ujao.
Licha ya kutoa mwaliko huo, haijafahamika vema iwapo mkutano huo utafanyika baada ya pande zote mbili katika siku zilizopita kuonekana kuwa na misimamo ya kutotaka kushauriana na tume hiyo.
Muungano wa upinzani NASA, ulioanza maandamano siku ya Jumanne wiki hii kushinikiza mabadiliko ndani ya tume hiyo, unasema uchaguzi huo hauwezi kufanyika iwapo masharti yao hayatashughulikiwa.
Naye rais Uhuru Kenyatta atakayepambana na Odinga katika uchaguzi huo mpya, amesema mpinzani wake hana mamlaka ya kushinikiza mabadiliko hayo.
Umoja wa Mataifa kupitia Shirika linalohusika na maswala ya mipango na maendeleo, UNDP, linsema liko tayari kusaidia katika maandalizi ya uchaguzi huo lakini pande mbili za kisiasa nchini humo hazitaki usaidizi huo.
@habari na rfi swahili

Usajili vyeti vya kuzaliwa sasa kwa njia ya simu za mkononi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akikabidhi cheti jana cha kuzaliwa kwa mmoja wa mzazi wa mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano aliyesajiliwa katika mpango maalumu wa utoaji vyeti vya kuzaliwa  bure katika mikoa ya Lindi na Mtwara. 



Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Tigo imezindua usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Ongezeko la mikoa hiyo unafanya jumla ya halmashauri zinazonufaika na mpango huo nchini kufika tisa. Katika mikoa saba ambako mfumo huo unatumika, zaidi ya watoto milioni 1.6 wamenufaika.
Akizindua mpango huo, Waziri wa Habari, Dk Harrison Mwakyembe alisema cheti cha kuzaliwa ni haki ya kila mtoto na ni muhimu katika kupanga maendeleo kwa kuwa takwimu sahihi zinahitajika kuifanikisha.
“Takwimu zinaiwezesha Serikali kujua mahitaji yaliyopo. Mpango huu utatuondoa katika ukisiaji kwa kuwa unawasiliana na kanzidata ya (Wakala wa Usajili wa Vizazi na Vifo) Rita,” alisema Dk Mwakyembe.
Kabla ya kuanza kutumika kwa mfumo huo mwaka 2012, takwimu zinaonyesha watoto waliokuwa wanapata vyeti vya kuzaliwa walikuwa asilimia kumi na moja, lakini mikoa inayonufaika mpaka sasa imeongeza hadi kufikia zaidi ya asilimia 90.
“Vyeti vinavyotolewa vimejazwa kwa mkono na haviwezi kughushiwa. Taasisi za umma na binafsi zivitambue kwa kuwa ni halali,” alisema Dk Mwakyembe.
Kufanikisha mpango huo, Tigo imetoa simu 1,000 za kisasa (smartphones) zenye thamani ya Sh95 milioni. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya mawasiliano, Simon Karikari alisema teknolojia ya simu za mkononi ni muhimu katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
“Serikali inaweza kufuatilia usajili wa vizazi kwa urahisi zaidi kuanzia vijijini na kujua muda, mahali, umri hata jinsia ya kila mtoto anayesajiliwa kutoka popote nchini, hivyo kurahisisha matumizi ya taarifa hizi. Haya yote yasingewezekana kama si kwa ushirikiano,” alisema Karikari.
Karikari alisema umuhimu wa vyeti hivyo ni pamoja na kuwezesha kupata nyaraka nyingine za umma kama vile kitambulisho cha taifa, mpigakura, hati za kusafiria au leseni ya udereva na hata leseni za kampuni za biashara.
“Leo hii huwezi kusajili laini ya simu bila kuwa na vitambulisho nilivyovitaja. Tigo itaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wote wanaozaliwa wanasajiliwa ifikapo mwaka 2021,” alisema.
Mwenyekiti wa bodi ya Rita, Profesa Hamis Dihenga alisema utafika wakati itakuwa ni lazima kila mwananchi kuwa na cheti cha kuzaliwa.
“Utafikia wakati hata kuanza shule cheti hiki kitahitajika ili watoto watambulike,” alisema Profesa Dihenga.
Aidha, alisema takwimu za usajili wa watoto katika mikoa ya Lindi na Mtwara zipo chini, akibainisha kwamba ni asilimia kumi na moja ya watoto wa Lindi ambao wamesajiliwa na asilimia 9.4 Mtwara.
Tayari mpango huo unaofadhiliwa na serikali ya Canada na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) unatekelezwa Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Songwe, Iringa, Geita na Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliitaka Serikali kuendelea kutenga bajeti ili mpango huo uwe endelevu.
“Tutautekeleza mpango huu kwa ufanisi na kuwa mfano kwa mikoa mingine,” alisema.
@habari na mwananchi

Uhamiaji yatoa tamko kuhusu wakimbizi.





Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala amewasili wilayani Ngara na kuagiza kambi za wakimbizi za muda zifungwe kwa wanaotoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Amesema wageni watakaoingia wasiitwe wakimbizi bali watakuwa ni wahamiaji haramu.
Dk Makakala amesema leo Jumatano kuwa, Mkoa wa Kagera unapakana na Uganda, Rwanda na Burundi, hivyo wananchi wasioe raia wa kigeni kinyume cha utaratibu. Amesema ni lazima hati ya ukaazi ilipiwe
Kamishna Jenerali Makakala ameahidi kuongeza watumishi wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera.
Pia, ameiomba Serikali kutoa vifaa vya usafiri.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Michael Mntenjele alisema kuna watu 223 wanaoomba hifadhi kutoka Burundi na DRC ambao wanapokewa katika kambi ya Rumasi wilayani hapa.
Amesema changamoto iliyopo ni maeneo ya mipaka kuwa wazi na kutokuwepo askari wa kutosha kudhibiti raia wa kigeni ambao huingia kufanya kazi kwa Watanzania na baadhi hupata makazi na wengine kuolewa.
Pia, amesema vigingi vya mipaka vilivyowekwa tangu wakati wa ukoloni na vingine vya mwaka 2014 vinaingia kwenye mashamba ya wananchi.
Mkuu wa wilaya amesema walioolewa au kuoa wanakabiliwa na changamoto ya kukosa Dola 50 za Marekani za kulipia hati ya ufuasi.
@habari na mwananchi

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...