Wednesday, 31 January 2018

TASAF katika Kata ya Kabungu wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameishukuru Serikali kwa kuanzisha mpango wa kuwapatia fedha za kujikimu katika kaya zao.


TANGANYIKA

Wanufaika wa mfuko wa kunusulu kaya Masikini Tasaf katika Kata ya Kabungu wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameishukuru Serikali kwa kuanzisha mpango wa kuwapatia fedha za kujikimu katika kaya zao.
Miongoni mwa wanufaika wameuelezea mradi huo  kuwasaidia kuleta mageuzi katika kaya ikiwemo Ufugaji pamoja na ujenzi.
Pamoja na hayo wanaitaka serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza kiasi cha fedha kwaajiri ya mgao wa kila kaya husika ili kuendana na maisha ya sasa.
Mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii manispaa ya Mpanda bwana Kasala  Bulemo amesema lengo la mradi huo ni kusaidia kaya masikini  kielimu, afya ikiwemo uibuaji wa miradi midogo midogo katika kaya zao.
Zaidi ya wanufaika 145 wamepokea fedha kutoka mfuko wa kunusulu kaya masikini Tassaf katika kata ya Kabungu wilayani Tanganyika.

Source Paul Matius 

Tanesco mkoa wa Katavi litaachana na uzalishaji wa nishati ya umeme kwa Jenereta na kujiunga na gridi ya Taifa.


KATAVI

Miaka miwili ijayo shirika la umeme Tanesco mkoa wa Katavi litaachana na uzalishaji wa nishati ya  umeme kwa Jenereta na kujiunga na gridi ya Taifa.

Waziri wa nishati Dr Merdard Kareman  ameeleza hayo wakati akikagua mradi wa mashine za kuzalisha umeme katika kata ya Inyonga  wilaya ya Mlele  mkoani katavi huku akishukuru kazi nzuri inayofanywa na Tanesco.

Katika hatua nyingine amesema miezi kufikia mwaka 2019 vijiji vingi mkoani Katavi vitafikiwa na umeme ili kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia msukumo wa vyawanda ambavyo hutegea uwepo wa nishati ya umeme. 

Mkoa wa Katavi unawilaya Tatu ambazo ni Wilaya ya Mpanda, Tanginyika na Mlele lakini Mpaka sasa shirika la Tanesco hutumia Jenereta kama chanzo cha nishati ya Umeme.


Chanzo:Mpanda Radio

#Changia Damu Okoa Taifa 


DAR ES SALAAM
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli  amesema  uzinduzi wa hati ya kusafiria ya kierektroniki utamaliza changamoto za usafiri nnje ya nchi ikiwemo biashara haramu za madawa ya kulevya.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wageni wengine ambao ni Makamu wa rais wa Tanzania  Mama Samiah Suluh, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali.

Aidha ameelezea kuwa uwajibikaji wa serikali awamu ya tano ni chachu ya maendeleo hayo yaliyofikiwa katika kuimarisha uchumi wa Tanzania kwa kuangazia utatuzi wa vikwazo vya kibiashara nnje ya Tanzania.

Katika hatua nyingine ameitaka idara ya Uhamiaji kujitathimini katika utendaji wake akitolea mfano wa ukamatwaji wa mamia ya wahamiaji haramu nchini katika mikoa ya Mbeya na Iringa .


Hati ya kusafiria ya kierektoniki itapatikana kwa kiasi cha shiringi laki moja na nusu.

Chanzo:Tbc
#Changia Damu Okoa Taifa

UNHCR limeshtushwa na mapigano yanayoendelea Mashariki mwa Demokrasia ya Congo, hivyo kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi kutoka nchini humo wanaoingia katika nchi jirani kama vile Burundi, Tanzania na Uganda.


KINSHASA

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na mapigano yanayoendelea Mashariki mwa Demokrasia ya Congo, hivyo kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi kutoka nchini humo wanaoingia katika nchi jirani kama vile Burundi, Tanzania na Uganda.

Maelfu ya watoto, wanawake na wanaume wameacha makazi yao huku mapigano dhidi ya makundi yenye silaha ya Mai Mai yakiendelea Kusini mwa Jimbo la Kivu.

Kwa mujibu wa Shirika la UNHCR, mpaka sasa, wakimbizi wapatao 1200 wameingia nchini Tanzania.

Wakati huo huo, inaamika kwamba, kuna wimbi kubwa zaidi za wakimbizi ambao wapo Kivu Kusini wakiwa katika hali mbaya ya kukosa chakula na makazi.

Bi Joan amesema, wakimbizi hao wamekuwa wakiingia nchini Tanzania kwa kutumia Ziwa Tanganyika, huku wakiwa wamechoka na baadhi wakiwa katika hali mbaya ya kiafya.



Chanzo: Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa

Watuhumiwa 24 kati ya 61 wanaokabiliwa na kesi za ugaidi jijini Arusha wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kuvua nguo na kisha kugoma kuingia ndani ya chumba cha Mahakama kusikiliza kesi zinazowakabili.



ARUSHA


Watuhumiwa 24 kati ya 61 wanaokabiliwa na kesi za ugaidi jijini Arusha wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kuvua nguo na kisha kugoma kuingia ndani ya chumba cha Mahakama kusikiliza kesi zinazowakabili.

Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Nestory Baro, ambapo amesema, watu hao wamehukumiwa kwa mujibu wa kifungu namba 114 (a) cha mwongozo wa mashtaka ya jinai.

Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo baadhi ya watuhumiwa walivua nguo zao na kubakisha nguo zao za ndani wakati wakipandishwa kwenye karandinga kurejeshwa katika gereza kuu la mkoa wa Arusha.

Awali kabla ya kusoma hukumu hiyo mwendesha mashtaka wa Serikali ,Augustino Kombe aliiomba Mahakama hiyo iwachukulie hatua kali na kutoa adhabu kwa watuhumiwa wa kesi hizo wanaogoma Mahakamani.



Chanzo:Eatv
#Changia Damu Okoa Taifa

Raila Odinga aapishwa bila naibu wake Jana na kuongeza idadi yaViongozi wengine waliowahi kuapishwa na kujitangaza kuwa marais kama Odinga barani Afrika.


Haki miliki ya pich
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga 

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Jumanne aliapishwa kuwa 'rais wa wananchi' nchini humo baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini humo Oktoba mwaka jana.
Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper hakujitokeza kwa sherehe hiyo ya kuapishwa, ingawa alikuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuapishwa.
Bw Odinga alisema Bw Musyoka, ataapishwa "baadaye".
Waziri mkuu huyo wa zamani hayuko peke yake katika kujaribu kujitangaza marais, kukiwa bado kuna rais mwingine madarakani.

Wengine ni akina nani?

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Etienne Tshisekedi, Nigeria Moshod Abiola, Uganda Kiza Besigye na Jean Ping wa Gabon ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wa Afrika ambao wamejaribu kujitangaza kuwa marais, na sasa Raila Odinga amejiunga na orodha hii.

Etienne Tshisekedi

Etienne Tshisekedi
Image captionEtienne Tshisekedi
Etienne Tshisekedi alikuwa kiongozi mkuu wa upinzani, wakati wa utawala wa Rais Mobutu Sese Seko Zaire, na baadaye Laurent Kabila Joseph Kabila wa DRC
Kufanana kati ya Tshisekedi na Odinga ni kwamba wote wawili walikuwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka, wote walihudumu kama mawaziri wakuu na wote waligomea uchaguzi wa urais; Tshisekedi mwaka 2006, Odinga katika 2017.
Mwezi Novemba 2011, Tshisekedi alijitosa kwenye kinyang'anyiro dhidi ya mtoto wa Laurent Kabila, kisha aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka baada ya jaribio la kujiapisha katika uwanja wa Wahanga, Kinshasa kutibuka. Baadaye, aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani.

Moshood Abiola

Moshood AbiolaHaki miliki ya picha
Nigeria, Moshood Abiola alijitangaza mwenyewe kuwa rais kipindi ambacho Rais Sani Abacha alipokuwa madarakani.
Hii ni baada ya kutembelea nchi nyingi za Magharibi, kutafuta msaada ili kumkabili Abacha katika utawala wake.
Alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela kwa miaka minne hadi ilipofika mwaka 1995, Siku aliyoachiwa kutoka gerezani, alikutana na ujumbe wa Marekani na kuhuduria mkutano.
Baada ya kupewa chai akiwa mkutanoni alianguka na kuzimia na hatimaye kufariki dunia.

Jean Ping

Jean PingHaki miliki ya picha
Mwaka 2016 Gabon, kiongozi wa upinzani Jean Ping alijitangaza mwenyewe kuwa rais na kutoa wito kura kurudiwa kuhesabiwa kwa kura ambazo zilithibitisha kwamba Ali Bongo ameshinda.
Hata hivyo dunia nzima alijua kwamba Ping ndiye alikuwa rais wa nchi hiyo

Kizza Besigye

Kizza BesigyeHaki miliki ya picha
Nchini Uganda Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, kupitia kanda ya video alionekana akifanya sherehe za kula kiapo kuwa Rais wa Uganda baada yake kushindwa uchaguzini mwaka 2016 na Bw Museveni.
Alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.
Kizza Besigye azungumza kuhusu uchaguzi Uganda
Bw Besigye amekuwa akikamatwa na kushtakiwa mara kwa mara nchini humo.
Chanzo: Bbc swahili
#Changia Damu okoa Taifa

Tuesday, 30 January 2018

Shule ya msingi Misunkumilo iliyopo Manispaa ya Mpanda inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha elimu.


KATAVI

Shule ya msingi Misunkumilo iliyopo Manispaa ya Mpanda  mkoani Katavi inakabiliwa  na uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati  hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha elimu  na ufaulu kwa ujumla

Geofrey Kisaye ni mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo amekili kuwepo kwa tatizo hilo huku akilitaja kuwa kikwazo katika mstakabali wa maendeleo ya taaluma.

Wanafunzi wa shule hiyo hawakusita kuiomba serikali kuongeza vyumba vya madarasa pamoja na madawati ili kuepukana  na msongamano wa wanafunzi darasani.

Naye afisa elimu taaluma  wa shule za msingi Manispaa ya Mpanda Rashid pili amesema serikali inaendelea na mkakati wa uimarishaji wa miundo mbinu katika shule mbali mbali.

Tangu kuanzishwa kwa sera ya elimu bure nchini na kutekelezwa mwaka 2016 kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi.


Chanzo:Isack Gerald

#Changia Damu Okoa Taifa

Vituo vya habari vyafungiwa matangazo Kenya.


Kenya

Baadhi ya vituo vya redio na televisheni vya Royal Media Services (RMS), vikiwemo runinga ya Citizen TV, vimefungiwa matangazo pamoja na kituo cha televisheni cha NTV kinachomilikiwa na kampuni ya Nation Media Group (NMG) katika baadhi ya maeneo.
Vituo hivyo vimekuwa vikipeperusha matangazo kuhusu sherehe iliyopangiwa kufanyika leo ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga.
Serikali ilikuwa imetahadharisha vituo vya habari Kenya dhidi ya kupeperusha moja kwa moja hafla hiyo.
Mmoja wa wahariri wakuu wa Citizen Peter Opondo ameambia BBC kwamba maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) kwamba polisi wakiandamana na polisi walivamia vituo vya kupeperushia matangazo na kuzima matangazo.
Citizen TV ndicho kituo cha runinga kinachoongoza Kenya. Matangazo ya kituo cha NTV yanapatikana pekee kupitia ving'amuzi vya kulipia.
Chanzo: Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa

Mkutano wa 10 wa Bunge umeanza leo Januari 30 mwaka 2018 mjini Dodoma kwa wabunge wapya watatu wala kiapo.


DODOMA.

Mkutano wa 10 wa Bunge umeanza leo Januari 30 mwaka 2018 mjini Dodoma kwa wabunge wapya watatu wa CCM kula kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Wakati wabunge hao wakila kiapo, takribani wabunge 50 wa upinzani walikuwa nje ya ukumbi wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Walioapishwa ni Dk Damas Ndumbaro (Songea Mjini), Justin Monko (Singida Kaskazini)  na Dk Stephen Kisurwa wa Longido.

Pia, Dk Tulia ameomba wabunge kusimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama ambaye alifariki dunia Novemba mwaka jana.


Chanzo:Mwananchi

#Changia Damu Okoa Taifa

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kampuni za simu za mikononi zinaruhusiwa kusajili upya laini kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki.


DAR ES SALAAM
 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema kampuni za simu za mikononi zinaruhusiwa kusajili upya laini kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za vidole.

Kaimu meneja mawasiliano kwa umma wa mamlaka hiyo, Semu Mwakyanjala amesema walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa.

Akizungumzia mfumo huo, meneja uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando amesema kampuni hiyo itaanza kusajili kwa majaribio.

Amesema baadaye wataendelea kwa wateja wengine hata ambao walishasajili laini kupitia mfumo wa zamani Lengo ni kuboresha zaidi mfumo huu.     

Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu  Okoa Taifa

NECTA WANATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017.


 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA)  Dk Charles Msonde
Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 30, 2018, limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7.22 ikilinganisha na mwaka 2016.

Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,  Dk Charles Msonde ameeleza kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 7.22 huku watahiniwa 265 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu wakiwemo wanafunzi 136 waliofanya mtihani wa kujitegemea (Private Candidate) na 129 waliofanya mtihani wa shule (School Candidate).
“Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09%  kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7.22,” alisema Msonde.
Amemtaja mwanafunzi aliyeongoza kitaifa kuwa ni Ferson Mdee kutoka Shule ya Sekondari Marian Boys.

MSIKIE MSONDE AKITANGAZA MATOKEO HAYO

CHanzo:Global publishers
#Changia Damu okoa Taifa

Monday, 29 January 2018


DAR ES SALAAM.

 Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limesema mitihani ya kuhitimu kidato cha sita itaanza Mei 7 hadi 24, 2018.

Akizungumza Msemaji wa Necta, John Nchimbi amesema “lengo la kutoa ratiba ni kuwafanya wanafunzi na walimu wao kujiandaa kwa ajili ya mitihani yao.”


Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Necta inaonyesha somo la kwanza litakuwa ni masomo ya jumla ‘General Studies’ na somo la mwisho litakalofanyika Mei 24 litakuwa ni Baiolojia 3C (kwa vitendo).



Chanzo:mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amesema ameagiza Halamshauri zote tano za mkoa wa Katavi kuhakikisha kila moja inaanzisha viwanda 20 katika kipindi cha mwaka mmoja.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga 

KATAVI
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amesema ameagiza Halamshauri zote tano za mkoa wa Katavi kuhakikisha kila moja inaanzisha viwanda 20 katika kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza katika kipindi cha kumekucha Tanzania cha Mpanda radio,amesema ifikapo Machi 30 mwaka huu  anatarajia kupokea ripoti ya mikakati ya halmashauri zote za mkoa ili kujua mipango iliyopangwa kwa ajili ya utekelezaaji.


Aidha Muhuga amesema changamoto ya ukosefu wa umeme wa uhakika pamoja na miundombinu ya usafirishaji kama barabara na reli ni miongoni mwa changamoto ambazo bado ni kikwacho cha ukuaji wa uchumi wa haraka.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amesema kuanzia mwezi ujao,kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa inatarajia kutembelea halamshauri zote za Mkoa ili kukagua hatua zilizofikiwa katika kuendesha mazao ya kilimo cha biashara yaliyoagizwa kulimwa kama mbadala wa zao la tumbaku.



Chanzo:Isack Gerald
#Changia damu Okoa Taifa

Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limewauwa watu wawili kati ya watano waliokuwa na silaha tatu za kivita aina ya SMG ambapo watu hao wameuawa wakati wa majibizano kati yao na Jeshi la Polisi.


KATAVI
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limewauwa watu wawili kati ya watano waliokuwa na silaha tatu za kivita aina ya SMG ambapo watu hao wameuawa wakati wa majibizano kati yao na Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amesema tukio hilo limetokea Januari 25 mwaka huu katika kijiji cha Kapalamsenga Wilayani Tanganyika ambapo watu hao wamekutwa wakiwa na risasi 16 na Magazini 5.

Aidha Kamanda Nyanda amesema watu hao wamekutwa na meno ya Tembo yenye uzito wa kilo 6.6 yakiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi milioni thelathini na nne  pamoja na nyama ya pofu kilo ishirini yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tatu.

Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Katavi Zumbe Msindai amesema kukamatwa kwa watu hao kumetokana na ushirikiano kati yao na jeshi Polisi Mkoani Katavi ikiwa ni baada ya kupata taarifa za siri juu ya uwepo wa watu hao.

Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika

Chanzo:Issack Gerald
#Changia Damu Okoa Taifa
kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda

NSIMBO
Mtu mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Hassan Damsoni mkazi wa kijiji cha Katambike kata ya Ugalla Mkoani Katavi ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.

Kwa mjibu wa diwani wa kata hiyo Mh.Halawa Malembeja amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa January 27 majira ya saa tano usiku ambapo mbali na kuuwawa kwa mkazi huyo watu hao wamepora zaidi ya shilingi milioni mbili kutoka nyumba tano na kujeruhi wengine.

Kwa mjibu wa Diwani Malembeja mazishi ya marehemu yamekwishafanyika katika kijiji hicho huku akieleza kuwa wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kuliomba jeshi la polisi kupeleka kituo cha polisi katika kata hiyo kwa ajili ya usalama.

Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amekiri kutokea kwa tukio hilo na amesema wamemkamata mtu mmoja akiwa na silaha aina ya gobole na simu tano ambazo zilikuwa zimeondolewa.



Hata hiyo Jeshi la polisi limetoa wito kwa watu kuacha kujihusisha na uharifu kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria ambapo msako unaendelea ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.
Chanzo:Issack Gerald
#Changia Damu Okoa Maisha

Basi lawaka moto Tanga.





Handeni. 
Basi kampuni ya Tahmeed  lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Mombasa, Kenya limeteketea kwa moto leo Januari 29, mwaka 2018  katika kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni mkoani Tanga.  
Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Handeni, William Nyero amesema polisi wapo eneo la tukio na hakuna madhara yoyote kwa abiria waliokuwa kwenye basi hilo. 
Amesema dereva wa basi hilo baada ya kubaini kasoro aliliegesha pembeni na abiria kuteremka, kushusha mizigo yao.
"Abiria wote waliokuwa wakisafiri na basi hilo wapo salama. Baada ya abiria kushuka na kushusha mizigo yao basi liliwaka moto,” amesema.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa

Viongozi wa AU wajadili mizozo, tatizo la uhamiaji na miradi ya maendeleo,



Äthiopien Addis Abeba Afrikanische Union Gipfel Guterres (Palestinian Presidency)
Marais wa nchi za Umoja wa Afrika wamejadili kuhusu kufadhili miradi ya maendeleo ya umoja huo, tatizo la uhamiaji na ufumbuzi wa migogoro kwenye nchi kadhaa na kwamba bila mshikamano maendeleo ni ndoto barani Afrika.
Marais wa nchi za Umoja wa Afrika wamejadili kuhusu kufadhili miradi ya maendeleo ya umoja huo, tatizo la uhamiaji na ufumbuzi wa migogoro kwenye nchi kadhaa. Mwenyeketi mpya wa Umoja wa Afrika, Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema bila ya kuwepo mshikamano maendeleo ni ndoto barani Afrika.
Hayo yamezungumzwa wakati wa mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia. Aidha, mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Rais Alpha Conde wa Guinea, amesema kuwa matatizo ya Afrika lazima yatatuliwe na Waafrika wenyewe.
Conde amekosoa vikali uwajibikaji wa vikosi vya Umoja wa Mataifa barani Afrika na kupendekeza kuweko vikosi vya kikanda vya Waafrika wenyewe chini ya Umoja wa Mataifa
''Tumeona kwamba wanajeshi wa Umoja wa Mataifa hawakuwajibika ipasavyo. Kuna wanajeshi zaidi ya 20,000 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa miaka kadhaa sasa, lakini hakuna matokeo mazuri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat ametoa mwito kwa ajili ya ufumbuzi wa mizozo barani Afrika huku akiitolea mfano wa Sudan Kusini ambako ameomba pawepo na vikwazo dhidi ya viongozi wanaokwamisha mchakato wa amani.Kwa nini tunataka wanajeshi kutoka Bangladesh na Indonesia waje kufa barani Afrika ambako sio kwao? Ili kufa barani Afrika inapaswa awepo mzalendo anayeipenda nchi yake. Leo ni Waafrika wenyewe wanaotakiwa kupigana kwa ajili ya usalama na amani yao wenyewe,'' alisema Rais Conde.
Vikwazo kwa wanaokiuka mchakato wa amani
''Nchini Sudan Kusini, kwa nini tusihoji kinachoendelea licha ya pande zote kukiuka mkataba wa amani, huku wakiwaacha raia wanaendelea kutaabika? Wakati umefika tuwawekee vikwazo wale wanaokiuka juhudi za amani. Nchini Burundi, pande zote zinatakiwa kuyapa kipaumbele mazungumzo kwa ajili ya suluhisho la kudumu,'' alisema Faki.
Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika Rais Paul Kagame amesema kwamba maguezi ya mfumo wa Umoja wa Afrika yatafanikiwa kwa kupitia mshikamano wa nchi zote za umoja huo.
Mada nyingine itakayojadiliwa leo katika mkutano huo ni pamoja na uhamiaji haramu na vipi Umoja wa Afrika utajifadhili wenyewe.''Hakuna nchi ama kanda inayoweza kujiendeleza yenyewe, tunatakiwa kufanya kazi kwa pamoja. Mageuzi ya kifedha na taasisi za Umoja wa Afrika yatatokana na ukweli kama huo wa mshikamano,'' alisema Rais Kagame.
Wakati huo huo, Rais wa Misri, Abdel Fatah Al-Sissi ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa mwaka ujao wa 2019.
Chanzo:Dw swahili
#Changia Damu Okoa Taifa

Watu wanne wafariki katika mkasa wa moto mtaa wa Kijiji, Nairobi



Moto LangataHaki miliki ya pich
Mamia ya watu wamekesha nje usiku wa kuamkia leo Jumatatu, bila ya kuwa na mahali pa kulala, nchini Kenya, baada ya moto mkubwa kuteketeza nyumba zao katika mtaa wa Kijiji eneo la Langata, Nairobi.
Watu wanne wamethibitishwa kufariki.
Maafisa wa serikali wanasema nyumba 6,000 ambazo ni makao ya watu takriban 14,000 ziliharibiwa na moto huo.
Moto huo ambao chanzo chake bado hakijabainika ulizuka mwendo wa saa mbili jioni na kuenea kwa haraka.
Magari manne ya wazima moto yalifika eneo hilo kujaribu kuuzima moto huo lakini hazikuweza kuufikia kutokana na njia nyembamba mtaani humo.
Magari hayo yalijaribu kuuzima moto huo kutoka mbali lakini baadaye yakaishiwa na maji.
Moto huo uliharibu nyumba za familia takriban 6,000
Image captionMoto huo uliharibu nyumba za familia takriban 6,000
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Taifa ya Kukabiliana na Majanga anayeangazia mawasiliano Bw Pius Masai aliambia gazeti la kibinafsi la Nation kwamba walilazimika kuomba usaidizi zaidi.
Magari ya kuzima moto ya baraza la jiji yalifika baadaye, lakini wakazi waliwalaumu maafisa hao wa serikali kwa kuchelewa kufika eneo la mkasa.
Uharibifu
Moto huo baadaye ulizimwa, ingawa moshi bado ulikuwa unafuka katika baadhi ya maeneo asubuhi.
Uharibifu
Wakazi waliambia vyombo vya habari kwamba walipoteza mali ya mamilioni ya pesa, badhi wakipoteza biashara zao na wengine makazi.
Chanzo:Bbc swahili
#Changia Damu Okoa Taifa

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...