Wednesday, 31 May 2017

IGP Sirro atoa Milioni 10 kudhibiti uhalifu Pwani

Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema kuwa jeshi hilo halitachukua muda kuwatia nguvuni  kikundi cha uhalifu wa mauaji ya baadhi ya askari, raia na viongozi wa wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji katika Mkoa wa Pwani.
IGP Sirro akiongea na waandishi wa habari
IGP Sirro ametoa onyo hilo leo Mei 31, 2017, wakati akizungumzia mikatati yake ya kutokomeza mauaji hayo, ambapo ametangaza dau la shilingi milioni 10 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi zitakazosaidia jeshi hilo kukamata wahalifu hao.
Ameeleza kuwa, Jeshi hilo linapanga kukutana na wananchi wa maeneo hayo hivi karibuni ili kuzungumza nao juu ya matukio yaliyotokea kwa lengo la kupata ushirikiano wao, na kuwatoa hofu.
Ameongeza kuwa nguvu inayotumiwa na jeshi hilo sasa ni za mpito katika kuhakikisha linarudisha amani, na kuwataka raia wema kutokimbia makazi yao.

Pia IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi huku akisisitiza utii wa sheria bila shuruti.

Mwenyekiti CHADEMA Kilimanjaro Afariki Dunia

Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini na mwenyekiti wa (Chadema)mkoa wa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo amefariki dunia ghafla leo, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.
Ndesamburo enzi za uhai wake
Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa mwili wa marehemu unafanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake cha ghafla.

Lema amesema Ndesamburo alifika ofisini kwake asubuhi  kama ilivyo kawaida yake  lakini aliugua ghafla mnamo saa nne asubuhi ndipo alichukuliwa na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC na wakati madaktari wanakifanya jitahada za kumpa matibabu alifariki dunia.

Kenya wazindua Treni ya Kisasa

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo amezindua treni ya kwanza ya abiria katika reli mpya ya kisasa {SGR} iliyojengwa kutoka Mombasa hadi Nairobi.

Reli hiyo ina urefu wa kilomita 472 ambapo treni zitakuwa zikisafiri kwa kasi ya wastani ya kilomita 120 kwa saa na kutumia muda wa saa nne na nusu kutoka Mombasa hadi kufika Jiji la Nairobi, ikiwa ni safari ambayo ilikuwa ikitumia takriban saa 8 kwa njia ya basi.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia uzinduzi huo wamesema treni hiyo itakuwa mkombozi kwao kwa madai kuwa hapo awali walikuwa wanapata shida kubwa katika kusafiri kutoka Mombasa hadi Nairobi.
Rais Kenyata wakati akipokea mfano wa treni ya mizigo itakayosafiri katika reli ya kisasa

Tuesday, 30 May 2017

Akamatwa kwa kutapeli na Sare za Jeshi

Mkazi mmoja wa Kitangili mkoani Shinyanga Francis Martin Kilalo (31) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kufuatia kukutwa na sare na vifaa vingine vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambavyo anatuhumiwa kuvitumia kupateli nakuwadanganya kwa kuchukua fedha kutoka kwa vijana wanaotafuta nafasi yakujiunga na Jeshi hilo.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mtafungwa alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi kwake juu ya hatua mbalimbali walizochukua katika kupambana na uhalifu mkoani humo.
Alisema kuwa Polisi walifanikiwakumukamata mtuhumiwa huyo katika Hoteli ya JM iliyopo Wilayani Igunga akiwa na sare mbalimbali za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) zikiwa na cheo cha Koplo ambavyo ni pamoja na kofia tatu, begi, sweta, buti jozi moja, magwanda na mikanda mitatu.
Mali nyingine zilikamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni pamoja na fomu za likizo cha likizo, fomu za kujaza vijanawanaotaka kujiunga na Jeshi hilo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria na hiari na mihuli zenye nembo inayofanana na Jeshi hilo. 
Kamanda Mtafungwa alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia nyaraka na sare za Jeshi hilo kuchukua fedha kwa kuwadanganya na kuwatapeli wananchi mbalimbali kwa kudai atawatafutia ajira katika majeshi ya Kujenga Taifa na la Wananchi.
Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo pia alikutwa barua kutoka Serikali za mitaa zaDar es salaam na gari aina ya Toyota Starlet yenye namba za Usajili T633 ARF ambalo wanaendelea kuchunguza uhalali wa umiliki wake na ambalo mtuhumiwa alikuwa akilitumia na kuwafanya baadhi ya wananchi wamuamini kuwa atawasaidia kupata nafasi katika majeshi.
Aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo piaalikuwa na barua za maombi ya watu yakuomba kujiunga na Jeshi, Fomu za Matibabu za Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kalaya Vyeti vya kumaliza elimu ya Sekondari vya baadhi ya watu.
Kufuatia tukio hilo alitoa witokwa waananchi waliowahi kutapeli ndani na nje ya Mkoa wa Tabora kujitokeza katika vituo vya Polisi ili waweze kutoa ushahidi utakasaidia kuonyesha ni jinsi gani walivyumizwa na mtuhumiwa huyo .
Kamanda Mtafungwa alisema kuwa Polisi inaendelea kushirikiana na JWTZ ili iweze kubaini sare na vifaa hivyo alivipata wapi , kwa lengo lipi na ni nani aliyompatia ili wahusika wote waweze kufikishwa katika vyombo vyaSheria kwa hatua zaidi.
Aidha, Kamanda huyo aliwaasa wananchi kuwa makini na matapeli wanaowadai fedha na kuwadanganya kuwa watawatafutia kazi katika Majeshi kwani vyombo hivyo vinaotaratibu wake ambao ndio unaotumika kuwapata vijana wanaojiunga kwa mujibu wa sheria na wale wahiari na sio kwa kuchangishwa fedha.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kukamata watuhimiwa 17 kwa kukutwa na lita 205.25 za gongo wakati wa msako wa kukamata wa watumiaji na wauzaji wa bidhaa hizo haramu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Mtafungwa alisema kuwa watuhimiwa watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao wakati wowote. Aidha, alisema kuwa katika zoezi hilo pia Polisi ilifanikiwa kuteketeza ekari tano na nusu za mashamba ya zikiwana uzito wa kilogramu 220 yalikuwa yamelimwa katika Msitu wa Hifadhi wa Igombe wilayani Uyui.
Alisema kuwa jitihada za kuwasaka watuhumiwa wa mashamba hayo zinaendelea na kuwaomba wananchi wenye taarifa yawalipo wahusika walisaidie Jeshi la Polisi ili wahusika waweze kufikishwa Mahakama kujibu tuhuma zao.

Mzee anayedaiwa kuchora nembo ya taifa afariki Muhimbili

Na Mwandishi Wetu
Msanii anayedaiwa kuchora nembo ya Adam na Hawa, inayotumika kitaifa, Francis Maige (Ngosha) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Mzee Ngosha  enzi za uhai wake, pembeni Nembo ya Taifa.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Cha Hospitali ya Muhimbili Aminiel Buberwa imesema kuwa madaktari wamejitahidi kuokoa maisha yake bila mafanikio.
Ngosha aliyepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita   kwa ajili ya matibabu zaidi akitokea Hospitali ya Amana, amefariki dunia saa 2 usiku Mei 29 2017.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa hali ya Ngosha ilibadilika ghafla akiwa hospitali hapo kabla ya kupoteza maisha na Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti hapa Muhimbili.

Monday, 29 May 2017

WANAWAKE Wawili wauwawa Tabora

Na Mwandishi Wetu
Wanawake wawili wilayani Igunga mkoani Tabora wameuwawa kikatili kwa kukatwa na mapanga na watu wasiojulikana huku mmoja akikatwa kiganja cha Mkono.
Mtendaji wa kata ya Tambalale Salum Kitindi amesema kuwa aliyeuwa ni Elizabeth Charles mkulima wa kijiji cha tambalale Tarafa ya Nsimbo, ambaye watu hao walimvamia usiku na kumshambulia kwa mapanga hadi kupoteza uhai wake kasha kukata kiganja cha mkono na kuondoka nacho.
Katika tukio linguine, Mtendaji wa Kata ya Mwisi Issa Omary amemtaja aliyeuawa kuwa ni Suzana Alex, mkazi wa kijij cha Busomeke, aliyeshambuliwa na mapanga huku mume wake John Matheo akijeruhiwa na amelazwa Katika Hospitali ya Misheniya Ndala, Nzenga.
Mkuu wa wilaya ya Igunga John Mwaipopo ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalam wa wilaya amethibitisha Kutokea kwa matukio hayo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi Igunga Linaendelea na msako kuwabaini waliohusika.

Mkuu hyo wa wilaya ametoa onyo kwa wanaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria na Amani kuacha mara Moja.

Waziri Ummy hawatoa hofu Watanzania Kuhusu Ebola

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kufuatia kupatikana kwa taarifa ya ugonjwa wa Ebola huko DRC Congo hakuna mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na virusi vya Ebola hapa nchini hadi wakati huu.
ummymwalimu
waziri Ummy Mwalimu
Akizungumza na vyombo vya habari leo, Mwalimu alisema nchi yetu inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hata hivyo kuna uwezekano wa ugonjwa huo kuingia hapa nchini kutokana na mwingiliano  wa watu, hasa wasafiri wanaotoka na kuingia.
Alisema kutokana na hali hiyo wizara inaendelea kuchukua tahadhari ili kuzuia ugonjwa huu usiingie hapa nchini.
"Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu, waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu.  Aidha Wizara inaendelea kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huu hapa nchini," alisema Ummy.

Vilevile alisema wizara inaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali katika kuimarisha ufuatiliaji na kutekeleza mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo ili usiingie hapa nchini.

IGP Sirro Aapa Kula Sahani Moja na Wahalifu

Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro baada ya kuapishwa leo na Rais Magufuli amefunguka na kusema kazi yake ya kwanza kufanya ni kuhakikisha uhalifu unakwisha ili Watanzania waishi kwa amani nchini mwao.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la polisi nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam
Simon Sirro amedai uhalifu nchini unaweza kupungua kama kutakuwa na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na jeshi la polisi nchini sababu wahalifu hao wanaishi katika jamii zetu hizi hizi. 
"Kipaumbele kikubwa ni uhalifu hivyo kazi yangu ni kuhakikisha uhalifu unapungua kwa kiasi kikubwa ili Watanzania waishi kwa amani lakini uhalifu huu utapungua tukipata ushirikiano mzuri na jamii, sababu hao wahalifu wanaishi kwenye jamii kwa hiyo ombi langu kwa Watanzania ili waishi kwa amani na utulivu ni vizuri sana watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi. Naamini kabisa tutaweza sababu hawa wahalifu ni wachache kuliko sisi kwa hiyo umoja wetu ule lazima tutashinda" alisema Sirro 
IGP Simon Sirro
Mbali na hilo IGP Sirro ametoa onyo kwa wahalifu wote nchini akiwataka waache mara moja kwani mwisho wa siku watapoteza tu maisha yao na kuacha familia zao zikipata shida.
"Lakini niwape onyo wahalifu kuwa uhalifu haulipi, kung'ang'ania uhalifu mwisho wa siku utaacha familia yako hivyo ni afadhali ufanye kazi ya halali itakusaidia kulea familia yako lakini ukijiingiza kwenye uhalifu wa ujanja ujanja haitakusaidia kitu, mwisho utaacha familia yako" alisisitiza IGP Sirro 

Sunday, 28 May 2017

Sirro Kamanda Mpya Jeshi la Polisi

Na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  John Pombe Magufuli leo Mei 28 2017 amemteua Kamishina wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)

Kabla ya Uteuzi huo IGP Simon Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

IGP Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa IGP Simon Sirro ataapishwa Jumatatu Mei 29, 2017 saa 3:30 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli atembelea Wagonja Muhimbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe wamewatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuwashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazofanya kunusuru maisha ya watu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anaongea na Mzee Ngosha


Miongoni mwa wagonjwa waliojuliwa hali ni Mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) aliyelazwa katika chumba namba 310 na Mtoto Shukuru Musa Kisonga aliyelazwa katika chumba namba 312 ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuugua ugonjwa usiofahamika uliosababisha aishi kwa kunywa mafuta ya kula, sukari na Maziwa.

Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli wamefanya matembezi hayo leo majira saa moja ya asubuhi wakiwa wanatokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro liliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ambako walihudhuria ibada ya Jumapili.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali itaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo pamoja na zile zinazowakabili madaktari na wauguzi hao.

“Jamani, Madaktari tunawashukuru sana, mnafanya kazi nzuri, Madaktari wote nchini pokeeni pongezi zangu, sisi serikali tutaendelea kuzikabili changamoto hizo na siku moja zitakwisha. Kikubwa ni kumtanguliza Mungu mnapofanya kazi ya kuokoa maisha ya watu kwa juhudi kubwa, mnafanya kazi ya Mungu”alisema Rais Magufuli.

                                     Rais Magufuli na Mkewe wakiwa wanaongea na Mtoto Shukuru

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ameweza kumshukuru Rais Mgufuli kwa kuwatembelea huku akisisitiza kuwa tayari madaktari wamegundua magonjwa yanayomkabili Ngosha pamoja na Mtoto Shukuru.

Aidha, Prof. Museru amesema hospitali hiyo imepiga hatua kubwa ya kujenga uwezo wa kutibu magonjwa ambayo wagonjwa walilazimika kwenda kutibiwa nje ya nchi na hivyo kuokoa fedha nyingi za serikali.

“Mhe. Rais hospitali yetu sasa imeanza kufanya upasuaji na kutoa tiba ya magonjwa ambayo yalilazimu wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, mfano hivi sasa tunatoa huduma ya kusafisha figo kwa wagonjwa takribani 250, na kuanzia mwezi Julai mwaka huu tutaanza kupandikiza figo.Huduma hii hugharimu kati ya Shilingi Milioni 60 na Shilingi Milioni 70 kwa mgonjwa mmoja anayekwenda kutibiwa nje ya nchi, lakini hapa nchini gharama zinashuka hadi Shilingi Milioni 21” alisema Prof. Museru.

Kwa upande mwingine Prof. Museru amesema kuwa hospitali ya Muhimbili imejipanga kuanza kutoa huduma ya matibabu kwa watoto wenye matatizo ya usikivu ambao wapo hatarini kuwa viziwi ili kuweza kuokoa fedha nyingi zinazokazo kwenda kuwatibu nje ya nchi, kutoka Shilingi Mil 90 hadi Mil 30.

Saturday, 27 May 2017

RAIS MAGUFULI Awaapisha Wateule Wake

Na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Mei, 2017 amemuapisha Bw. Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - anayeshughulikia Elimu.




Viongozi wengine walioapishwa na Mhe.Rais Dkt. Magufuli ni Bwa. Rajab Omar Luhwavi ambaye anakuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji,Bw. Bernard Mtandi Makali ameapishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa na Bw. Clifford Katondo Tandari, kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro.
Pia Rais Magufuli amemuapisha Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Rais Magufuli akimuapisha Ndugu Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  Ikulu jijini Dar es salaam Mei 27,2017
Viongozi wote walioapishwa wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Hafla ya kuapishwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na viongozi mbalimbali wa Serikali.

CHADEMA Wamkataa ODINGA Wampa shavu UHURU

Na Mwandishi Wetu,
DODOMA, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kumuunga mkono Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Kenya utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Msimamo huo umetolewa leo katika mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho unaofanyaki mjini Dodoma, ikiwa ni maamuzi ya Baraza hilo, na kutangazwa rasmi na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
Akizungumzia uamuzi huo, Mbowe amesema sababu kuu ya uamuzi huo ni kugeukwa na mgombea wa muungano wa ODM Raila Odinga, ambaye chama hicho kilikuwa kikimuunga mkono mara zote.
Mbowe amesema "Kwa muda mrefu chama chetu kimekuwa kikimuunga mkono Raila Odinga achukue nafasi ya kuliongoza Taifa la Kenya. Mwaka 2015 ilipofika zamu yetu rafiki yetu Raila Odinga alitugeuka na kumuunga mkono adui yetu. Sisi kama Chama, safari hii tunamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na Umoja wa vyama vinavyounda JUBILEE".
Chama hicho kinaendelea na Baraza Kuu mjini Dodoma, baada ya hapo jana kumaliza kikao cha Kamati Kuu yake, na kimedhamiria kutoka na maamuzi mazito kuhusu mustakabali wa taifa.

Friday, 26 May 2017

Kunchela Apasua Jipu la Machimbo Katavi

Serikali imemtaka Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Katavi Rhoda Kunchela kuwasaidia kujua mwekezaji anayemiliki mgodi wa Isulamilomo.

Akijibu swali bungeni leo Naibu waziri wa Nishati na Madini Medadi Karemani amesema kuwa serikali itafuatilia taarifa hiyo baada ya anayehusika katika mgodi huo.

Naibu waziri Karemani ameongeza kuwa serikali itachukua maeneo yote yaliokaliwa na wawekezaji bila kuyaendeleza na kuwagawia wananchi wa maeneo huska.

Awali Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Katavi Rhoda Kunchela ametaka kujua mmiliki halali wa machimbo ya Isulamilomo kwa kuwa wananchi na wachimbaji wadogo wamekuwa wakinyanyaswa na mwekezaji anayefanya shughuli katika eneo hilo.

Katavi Wachukua Tahadhali Kuzuka kwa Ebola Kongo

Wananchi mkoani katavi hususani wilaya ya Tanganyika wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhali ikiwa na kutoa taarifa sehemu husika wanapohisi kuwa na dalili moja wapo za ugonjwa wa ebola ili huduma sahihi itolewe.
kirusi cha ugonjwa wa Ebola
Tahadhali hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Selemani Mtenjela ambapo pia amewatoa hofu wananchi kwa kuwa ugonjwa huo bado haujaingia nchini.

"Tumeanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wananchi kuhusu ugonjwa huu, lakini pia kuwaondoa hofu ili waendelee na shughuli zao huku wakichukua tahadhali," tunachukua tahadhali kwa kuwa mkoa wetu hasa wilaya ya Tanganyika imepakana na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambako shirika la Afya duniani wamethibitisha kutokea kwa visa vya watu kukutwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo,"amesema Mtenjela.


Amesema kuwa ni vyema wananchi wakaendelea na shughuli zao  huku wakizingatia maelezo ya wataalamu kwani ugonjwa wa ebola madhara yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha.

Amezitaja dalili za ugonjwa huu kuwa ni mgonjwa kulalamika kichwa kukosa nguvu ini kudhofika na kutokwa na damu sehemu za mwili zilizo wazi na kuwa ujitokeza baada ya siku tano hadi 21 tangu kuambukizwa.


Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo mwezi April 22 mwaka huu lili tangaza kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo mwaka 2014, mripuko wa ugonjwa huo ulidhibitiwa kwa haraka ingawa watu 49 walifariki nchini humo.

Serikari Katavi Wajipanga kudhibiti Ramli Chonganishi

Na Rehema Msigwa

WAGANGA wa kienyeji wa tiba asilia wametakiwa kujisajili ili kufuata taratibu za uendeshaji wa huduma hiyo kwa kufuata sheria.
Agizo hilo limetolewa leo na Katibu tawala wa mkoa Paul Chagonja alipokuwa waganga wakienyeji na tiba asilia kufuatia kuwepo kwa lamri chonganishi.

Umeuambia umati wa waganga hao kuwa wakati umefika wa kukubali kuwa tiba asilia pamoja a madawa ya kienyeji, ni urithi ulio haribiwa na tamaduni za kigeni, na kwamba kazi kubwa iliyobakia ni kutengeneza njia sahihi za kihuduma ambazo zitawalinda watoa huduma pamoja na kutoa msaada kwa wapokea huduma.
Baadhi ya waganga wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Katibu tawala Mkoa wa Katavi Paul Chagonja (hayupo pichani)

kwa upande wa waganga wa kienyeji na tiba asilia wamewataka waganga ambao hawatambuliki na serikali waanze kufanya taratibu za kufanya usajili  ili kujilinda na matatizo ya kihuduma ikiwemo mtego wa ramli chonganishi.

Maria Komba ni mmoja wa waganga wa Kienyeji amesema ipo haja ya badhi ya waganga wa kienyeji kuaacha kuwashauri vibaya wagonjwa hasa kutokana na baadhi ya magonjwa kuhitaji uchunguzi zaidi wa kitabibu ambao unapatikana hospitalini.

ALAAT Mkoa Wa Katavi Wakagua Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Tanganyika



matanki ya mradi wa maji katika kijiji cha majalila wilaya ya Tanganyika


ZAIDI ya watu 3000 katika kata ya Majalila iliyopo wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wameanza kunufaika na mradi wa maji uliogharimu kiasi cha shilingi 703,501,240.00.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuia ya serikali za mitaa ALAAT tawila la mkoa wa Katavi Bw Wilium Mbogo ambaye pia ni Msitahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wakati wa ukaguzi wa miradi mbali mbali inayo tekelezwa mkoani Katavi ambapo amewaambia wajumbe wa katai tendaji kuwa mradi huo pekee unaondeshwa kwa nishati ya mionzi ya jua ni mwarobaini wa adha ya maji kwa wakazi wa eneo hilo.

Ameongeza kusema kuwa jitihada za serikali kwa kushirikiana na Benki kuu ya dunia kwa pamoja na nguvu za wananchi zimefanikisha kukamilika kwa mradi huo, na kwamba kazi kubwa iliyopo ni mamlaka za kamati za maji kuhakikisha mradi huo unadumu.

umeme wa nishati ya jua unaotumika kwa ajili ya kuendeshea mradi wa maji.

Miradi mingine iliyo ridhiwa na kamati hiyo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa sita na chumba kimoja cha utawala katika kata ya Kasekese iliyopo wilayani humo ambao ambapo mradi huo umeanza kutekelezwa 2016 /2017 na kukamilika mwezi machi 217.
baadhi ya wanafunzi wakiwa nje ya vyumba vya madarasa ambayo vimekamilika


Mradi huo kwa mara ya kwanza ulibuniwa na wananchi baada ya kuona adha ya wanafunzi walio kuwa wakilazimika kusomea nje , hali iliyokuwa ikipelea utoro katika kipindi caha mvua za masika ambazo hunyesha mara kwa mara.
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda Hamad Mapengo akihojiana na baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Kasekese.


Nguvu za wananchi na wadau wamaendeleo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mpanda na kutumia kiasi cha shilingi62,033,000.00.



Mradi wa ujenzi wa zahanati Katika kijiji caha Itetemya kata ya Kalema umetekelezwa kwa ufadhili wa serikali kuu kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF 111Kwa kushirikiana na wananchi pamoja na halmashauri ya wilaya ya Mpanda.

KAIMU mkurugenzi mtendaji wa Halimashauri ya wilaya ya Mpanda Bw Roumuli John ameelezea shabaha ya mradi huo kuwa ni kupunguza msongamano wa huduma ya afya katika kituo cha afya cha Kalema kwa wananchi wa kiji cha Kalema na vijiji vya jirani na kwezesha walengwa kutimiza masharti ya afya kwa urahisi zaidi hivyo kuendelea kupataruzuku kutoka TASAF111 na kutimiza dhana ya mpango wa kunusuru Kaya masikini.
wajumbe wa ALAAT mkoa wa Katavi wakiendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo na hapa ni katika zahanati ya Itetemya.

Mradi wa ujenzi wa zahanati ya Itetemya umegaharimu kiasi cha 76,391,800.00.
Wilaya ya Tanganyika ni ya tatu katika mkoa wa Katavi imeanzishwa mwezi july 2016 ambapo makao yake makuu yaliidhinishwa na baraza la madiwani mwaka huo huo kuwa ni Kata ya Majalila.


Saturday, 20 May 2017

Matumizi hafifu ya vipaji barani Africa ni chanzo cha umasikini kwa Vijana Tanzania

 Imeandikwa na. Prosper Kwigize, Kasulu, Kigoma
Sisi vijana wenye vipaji tupo wengi sana vijijini, elimu yetu ni ya darasa la saba lakini vipaji vyetu ni zaidi ya aliyesoma hadi chuo kikuu, tunachangia pato la Taifa kupitia kazi za mikon.
Bahati mbaya thamani yetu kwa jamii ni ndogo, wanaothaminiwa ni walioajiriwa serikalini ambao wengine hata hatuoni tija ya usomi wao.
Mwaka 2014 serikali ya Tanzania ilitangaza rasmi sera mpya ya elimu nchini humo, ambayo ilitambua elimu ya vipaji maalumu vya kisayansi kama njia muhimu ya kukuza uchumi katika dunia ya utandawazi

Ni kwa sababu ya masomo ya teknolojia ya habari na mawasiliano maarufu kama TEHAMA pamoja na stadi za kazi yalihimizwa kufundishwa katika ngazi za elimu ya msingi, sekondari na vyuo ili kuwaandaa vijana kuwa na uwezo wa kuingia katika ushindani wa soko la ajira duniani.

Mwandishi Prosper Kwigize, Kigoma, Tanzania Katika mahojiano ya DW na Waziri wa Elimu nchini Tanzania Profesa Joyce Ndalichako katika kipindi cha Kinaga ubaga cha mwezi Octoba 2014, katika moja ya majibu yake juu ya kuibua vipaji alisema serikali imeandaa utaratibu wa kupita nchi nzima kuwatambua vijana na watoto wenye vipaji mbalimbali.

Hata hivyo kwa kijana Salumu Rashid kijana mtanzania mwenye umri wa miaka 20 haoni kama serikali ya Tanzania inadhamira thabiti ya kuwasaidia vijana wenye vipaji nje ya mfumo rasmi wa elimu.

Salum amevumbua matumizi ya mabaki ya magurudumu ya magari kwa ajili ya utengenezaji wa majiko ya kutumia nishati ya mkaa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Utengenezaji wa majiko haya umemsaidia Bw. Salum pamoja na vijana wengine waliojitokeza kujifunza kwake kupata kipato huru kinachowawezesha kuepuka kutegemea familia Amefanikiwa kupata soko katika mkoa wa Kigoma na anakusudia kupanua wigo hadi nchi jirani ya Rwanda, Malawi, Zambia, DRC, Uganda, Kenya na Msumbiji.
Mtaalamu wa Majiko ya Waya Bw. Salum Rashid akionesha majiko yaliyokamilika tayari kwa kwenda sokoni

Kiwanda chake kidogo kina wafanyakazi sita, ambao hufanya kazi ya kukusanya matairi kutoka katika majalala mbali mbali katika miji ya Kibondo, Kasulu, Kigoma na katika nchi jirani ya Burundi na kisha kuyachoma ili kutoa waya ambazo ndhizo hutumika kutengeneza majiko hayo

Jumla ya majiko 10 hadi 40 hutengenezwa kila siku na vijana hawa, ambapo huyauza kwa bei kati ya shilingi 10,000 hadi 20,000 kwa jiko moja, kutokana na idadi inayozalishwa kila siku Bw. Salum hukusanya kiasi cha shilingi 50,000 hadi 120,000.

Kiwanda chake sasa kilichoko katika mazingira duni ya mjini Kasulu, kinafanya kazi kama kituo cha mafunzo kwa vijana kadhaa ambao baada ya kuona tija ya maisha ya mwenzao, nao wamejitokeza kupata mafunzo hayo ya aina yake.

Majiko yanayotumia mkaa kwa kupikia ambayo yametengenezwa kwa kutumia waya za magurudumu ya magari yaliyokwisha muda wake
Bi. Neema Segeza licha ya kuwa mwanamke katika mazingira yenye mfumo dume ni mmoja wa wanafunzi waliofaulu mafunzo ya utengenezaji wa waya za mataili ya magari, awali alikuwa mkulima anayefanya vibarua kulima mashamba ya watu wengine na kujipatia ujira mdogo.
Bi. Neema Segeza mwanamke aliyepata mafunzo ya utengenezaji wa majiko
Anaeleza kuwa kazi ya ufundi sanifu wa majiko hayo sasa amejiajiri na hana haja tenda ya kuwa kibarua katika mashamba ya watu, amemudu maisha na analipa ada ya watoto.

Wote wawili kwa pamoja wana matarajio ya kununua viwanja na kujenga nyumba kwa ajili ya makazi yao na kutafuta eneo maalumu kwa ajili ya kiwanda cha majiko hayo Hata hivyo chngamoto ya ukosefu wa mitaji na serikali kutotenga ardhi kwa ajili ya viwanda vya ubunifu na usanifu wa kazi za mikono ni kikwazo kwa vijana wengi wenye vipaji nchini Tanzania.

Bw. Salum Rashid na Bi. Neema Segeza wakiwa katika shughuli za utengenezaji wa majiko ya waya mjini Kasulu

Sera ya Elimu na Mafunzo ufundi Tanzania Kwa mujibu wa sera ya elimu nchini Tanzania ya mwaka 2014, utoaji wa elimu nchini humo unatekekelezwa kama sekta mtambuka ambapo wizara zaidi ya moja huhusika jambo linalotajwa kuwa sababu ya kudhorota kwa usimamizi.

Uchambuzi wa tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, umeonyesha kuwa matamko 59 kati ya matamko 149 ya Sera hayakutekelezwa.

Kati ya hayo, matamko 25 yalihusu elimu ya msingi na sekondari, 18 yalihusu elimu ya ufundi na 16 yalihusu elimu ya juu.

Tathmini iliyofanywa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ilibaini pia kuwa mpango mkakati wa kuelekeza utekelezaji wa sera hizo haukuandaliwa mpaka mwaka 1997 ulipoanzishwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu, na mwaka 2001 ulipoandaliwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM).

Tathmini ilibaini pia kuwa usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo katika ngazi ya mkoa na wilaya unafanywa na mamlaka mbalimbali zinazoongozwa na kanuni na taratibu tofauti pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu jambo linaloibua mkanganyiko wa nani anapaswa kusimamia haswa utoaji wa elimu yenye tija hasa kulingana na soko la ajira.

Friday, 19 May 2017

WAFANYAKAZI WA MPANDA RADIO FM WAPATIWA MAFUNZO YA UBUNIFU NA USIMAMIZI WA MIRADI

Bi. Silesi Malli Mwnyekiti wa UNA Tanzania
Mwenyekiti wa shirika la umoja wa mataifa la UNA Tanzania Bi. Silesi Malli ametoa wito kwa waandishi wa habari kujifunza namna ya kuandika na kutekeleza miradi ili uandaaji wa vipindi utokane na mahitaji ya jamii. 

Wito huo ameutoa jana mjini Mpanda ambapo waandaaji wa vipindi na viongozi wa Mpanda Radio wameshiriki mafunzo ya siku nne ya uandaaji wa miradi na usimamizi wa vipindi. 

Bi. Malli amebainisha kuwa waandaaji wa vipindi wengi hawana weledi wa kutambua, kuandika na kutaathimini miradi jambo linalopelekea uandaaji mbovu wa vipindi vya radio na runinga. 

Watumishi walioshiriki mafunzo ya Uandishi wa Miradi na usimamizi wa fedha yaliyofadhiliwa na Mpanda Radio walioko nyuma ni Ndg. Prosper Kwigize (mwenyekiti wa mtandao wa Radio jamii Tanzania) na Bw. Amini Mitha mkurugenzi wa Mpanda Radio
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Bw. Tizibazomo Bernard na Salome ramadhan wamekiri kunufaika na mafunzo hayo ambayo yamedhaminiwa na Mpanda Radio na kuahidi kufanya mageuzi katika uandaaji wa vipindi. 

Imeandaliwa na: Safina Joel
Mhariri: Alinanuswe Edward


Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...