Mtu mmoja amelazwa katika hospital ya manispaa ya Mpanda baada ya kujeruhiwa na simba katika kata ya mtapenda mkoani katavi .
Akithibitisha k mganga mkuu wa hospital ya manispaa ya Mpanda Dr Theopister Elisa amesema amempokea majeruhi huyo mwenye umri wa miaka kumi na tano na anaendelea kupatiwa matibabu zaidi.
Kwa upande wa diwani wa kata ya mtapendwa Fyula Samwel amesema kuwa simba wapo watatu ambao wanazunguka katika maeneo ya kata hiyo na yameshaua mbuzi 8 na ng’ombe 7 na kumjeruhi mtu mmoja.
Hata hivyo Bwana Fyula amewataka wananchi wasiende maeneo ya porini mtu mmoja na kuacha kutembea wakati wa usiku mpaka hali itakapo kuwa nzuri.
Mbunge wa jimbo la Nsimbo mkoani katavi Mh. Richard Mbogo amewataka wananchi walioondolewa katika kata ya starike mkoani katavi kuwa wavumili wakati taratibu zinafanyika ili waweze kurudishwa katika maeneo yao .
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Mpanda redio kasema kuwa wananchi wa mgorokani wameondolewa kimakosa katika maeneo yao na hivyo taratibu zinafanyika ili waweze kurejeshwa kwani walikuwa kisheria.
Hata hivyo amesema taratibu zitakapomalizika watarudishwa na kuendelea na shughuli zao walizokuwa wanazifanya kabla ya kuondolewa kama vile kilimo.
Hivi karibuni operesheni ya kuwaondoa wananchi katika maeneo yanayosemekana kuwa ni miliki ya hifadhi mkoani katavi imekumba maeneo mengi ikiwemo Mgolokani ,makutanio na Litapunga na Luhafwe.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hakuna bomoabomoa itakayoendelea katika mkoa wake zaidi ya inayoendelea katika Barabara ya Morogoro na inayofanywa kwa ajili ya reli ya kisasa na kwamba, yeyote anayetaka kufanya ubomoaji lazima atoe taarifa kwa mujibu wa sheria.
Alisema hayo jana alipotembelea eneo la Masaki-Toangoma wilayani Temeke na eneo la Kigogo katika Manispaa ya Kinondon alipozungumza na wananchi wa maeneo hayo waliotarajiwa kukumbwa na bomoabomoa. Hivi karibuni, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilitangaza kubomoa nyumba zaidi ya 17,000 zilizojengwa katika hifadhi ya Bonde la Mto Msimbazi kuanzia Pugu hadi Daraja la Selander katika Manispaa ya Kinondoni.
Mbali na NEMC, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pia ilizipiga alama ya X nyumba zaidi ya 300 katika eneo la Masaki-Toangoma na kuitaka Manispaa ya Temeke kuanza kuzibomoa. Aidha, Makonda amewataka watu wote waliovamia maeneo ya masoko, shule, viwanja vya mpira na maeneo ya wazi wajisalimishe katika manispaa zao. Aliagiza viongozi wa serikali za mitaa na wananchi waliowadhulumu watu viwanja wakamatwe.
Akizungumzia bomoabomoa ya nyumba 17,000, Makonda alisema watu wanaotaka kufanya bomoabomoa hiyo hawakufuata utaratibu ikiwemo kuwasiliana na ofisi yake kuhusu utekelezaji wake. Makonda alisema mbali na viongozi hao hata Rais John Magufuli amesikitishwa na suala hilo na kumtaka kufuatilia ili kujua taratibu zilizotumika katika utekelezaji huo.
“Baada ya taarifa hizi kuandikwa katika vyombo vya habari rais alinipigia simu kama nina taarifa kuhusu ubomoaji huo nikamwambia sina taarifa na yeye akasema hajapata taarifa, alichokisema yeye hakuchaguliwa kwa ajili ya kubomoa nyumba za watu, bali kuleta maendeleo kwa wananchi,”alisema Makonda.
Akizungumzia suala la alama zilizowekwa na Wizara ya Ardhi Masaki, Makonda alisema baada ya kufuatilia alibaini kuwa viongozi wa serikali za mtaa walichangia kuuza viwanja hivyo ilhali wakijua kuwa maeneo hayo ni ya wazi na mengine ni ya bondeni yasiyopaswa kuwa makazi ya watu.
“Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa siyo muuzaji au mpimaji wa viwanja ukitaka kununua viwanja usiende huko wananchi wengi wamelizwa na watu hawa fuateni taratibu za ununuzi wa viwanja ili kupunguza migogoro hii ambayo imekuwa kero,” alisema. Makonda amewataka wananchi hao kujiepusha na ununuzi wa maeneo hatarishi, wafuate taratibu za ujenzi ili kujiepusha kujenga kiholela
Vikosi vya usalama mbele ya mitambo ya ukaguzi, Makka tarehe 29 Agosti 2017.REUTERS/Suhaib Salem
Miji mitakatifu ya Kiislamu ya Makka na Madina inawapokea Waislamu zaidi ya milioni mbili ikiwa Jumatano hii ni siku ya kwanza ya ibada hiyo.
Katika ibada hii Wairani ambao walikua walipigwa marufuku kuingia katika nchi hiyo ya Kiislamu kutoka madhehebu ya Sunni, hatimaye wameruhusiwa kufanya ibada hiyo katika mji mitakatifu ya Kiislamu ya Makka na Madina.
Mwaka jana Wairan hawakuweza kwenda Makka kufuatia mivutano ya kisiasa kati ya Tehran na Riyadh. Usalama wa mahujaji ni moja ya changamoto ya ibada hii.
Mamlaka nchini Saudi Arabia inasema imetenga kikosi cha polisi 100,000 mwaka huu, lakini pia wafanyakazi 17,000 wa ulinzi wa raia na magari ya wagonjwa zaidi ya mia moja. Nchi hiyo ya kifalme imeahidi kutoa ulinzi wa kutosha kwa mahujaji kutoka nchi 80.
Saudi Arabia inataka kuepuka ajali yoyote hasa tukio jipya la mkanyagano. Matukio mabayayalitokea mara kadhaa katika miongo ya hivi karibuni katika mji wa Makka ambapo watu 2,300 walipoteza maisha muaka miili iliyopita kulingana na takwimu za serikali.
Matukio mengine ya hatari huenda yakashuhudiwa katika ibada hii ya Hija: shambulio la kigaidi au magonjwa ya kuambulia. Mnamo mwaka 2009, virusi vya mafua ya ndege A vilizua hali ya sintofahamu nchini Saudi. Mwaka huu, janga la kipindupindu nchini Yemen linatia wasiwasi kwa huduma za afya.
Madereva wa bodaboda katika Halmashauri ya manispaa ya mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kujisajili katika vituo vya magesho kama agizo la Sumatra ili kupunguza matukio ya uhalifu.
Hayo yameelezwa na askari usalama barabarani mkoa wa kativi John Shindika wakati wakizungumza na Mpanda Redio na kusema kuwa matukio mengi yanatokea pale ambapo waendesha bodaboda wanakuwa hawafahamiani wao kwa wao.
Shindika amesema madhara wanayoyapata madereva bodaboda kutoka na uhalifu unaofanywa na watu wasiojulikana ni pamoja na kupoteza maisha kujeruhiwa na wakati mwingine kunyweshwa madawa ya kulevya na kutupwa maeneo hatarisha wakiwa hawajitambui.
hata hivyo ametoa wito kwa madereva wote kuzingatia kanuni za kazi zao ikiwemo kuvaa kofia ngumu kutoongea na simu pamoja na kuacha kuendesha kwa mwendo kasi hali ambayo itapunguza ajali za barabarani.
WABUNGE wa Bunge la Canada
wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa
jinsi anavyofanya kazi zake za kuwapambania Watanzania wa chini ili wawe juu
kwa kuwapatia maendeleo yaliyo na tija.
Wamesema Rais Magufuli ni miongoni
mwa marais wachache duniani, wenye kuthamini wananchi wake kwa kuwapambania
kupata mahitaji muhimu, ambayo nchi inastahili kupata kwa kubana mianya ya
wakwepaji wa kulipa kodi, ambayo ndio ingechangia kwa upatikanaji wa maendeleo
kwa kuwa Pato la Taifa limeongezeka kidogo.
Maneno hayo yamesemwa na Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge la Jumuiya ya Madola kutoka Canada, Yasmin Rentasi katika
kikao cha kamati hizo mbili za Canada na Tanzania kwenye Ukumbi Mdogo wa Bunge
jijini Dar es Salaam, huku Kamati ya Bunge la Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti
wake, Dk Raphael Chegeni.
Rentasi alisema Serikali ya Canada
ipo tayari kutoa misaada mbalimbali ya kibunge ili kuhakikisha Bunge la
Tanzania, linakuwa ni Bunge bora katika usimamizi mzuri wa kisheria na
kuishauri serikali juu ya masuala ya msingi yenye kuleta tija katika nchi hiyo.
“Tunaipongeza serikali ya Rais
Magufuli kwa juhudi zake za kupambana na kuinua uchumi wa nchi ya Tanzania kwa
kubana matumizi, kupambana na mafisadi, kudhibiti rushwa hivyo hali hii
inaonesha jinsi Tanzania itakavyofanikiwa kukuza uchumi wake kutoka chini na
kuongezeka, pia kutapelekea kupungua kwa kiwango cha umaskini pamoja na
kuboresha huduma za kijamii kwa muda mfupi,” alieleza Rentasi na kuongeza:
“Mimi nilizaliwa hapa Tanzania (Dar
es Salaam) wakati huo baba yangu alikuwa akifanya kazi hapa enzi za Mwalimu
Nyerere, niliondoka hapa nikiwa mdogo sana, lakini nafarijika leo kurudi hapa
na kuona Tanzania inasonga mbele.”
Aidha, aliwataka Watanzania
kumwombea Rais Magufuli ili apambane na mchwa ambao wana lengo la kutaka
kumkwamisha katika kutekeleza ahadi yake aliyoipanga kuwafanyia Watanzania.
Kwa upande wake, Dk Chegeni
aliwapongeza wabunge hao wa Canada, kwa kuona juhudi zinazofanywa na Rais
Magufuli kupambana na kuinua uchumi. Alisema Tanzania ni nchi yenye utulivu na
siasa safi hivyo aliwaomba wabunge hao kuwekeza zaidi ili wananchi wa Tanzania
wanufaike kupitia serikali yao ya Canada.
Alisema Tanzania na Canada
zitaendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya
kuwahakikishia wananchi wake upatikanaji wa huduma bora za kijamii.
UBINAFSISHAJI wa Kampuni ya
Maendeleo ya Viwanja vya Ndege (KADCO), umehojiwa kutokana na kile
kilichoelezwa kuwa umegubikwa na utata, hali ambayo baadhi ya wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wametaka wapewe maelezo ya serikali,
vinginevyo suala hilo litahamishiwa bungeni lijadiliwe.
Hayo yalibainika jana katika kikao
kati ya wajumbe wa PAC na Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA). Miongoni mwa mambo ambayo wajumbe walisema yana utata, ni pamoja na CAG
kubaini kuwa licha ya serikali kuwa na hisa asilimia 100 katika Kadco, kampuni
hiyo imeendelea kuachiwa kuendesha Kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro (KIA).
Utata mwingine ni hatua ya KIA
kuendeshwa tofauti na viwanja vingine, kwa maana ya kuwa chini ya kampuni hiyo
wakati viwanja vya ndege vingine vyote viko chini ya TAA. "Kwa nini hiki
kiendeshwe tofauti na viwanja vingine?
Na TAA wanaendesha viwanja vingine
na siyo KIA... Tutamuita waziri atueleze kuna nini," alisema mwenyekiti wa
kamati, Naghenjwa Kaboyoka ambaye ni Mbunge wa Same Mashariki (Chadema).
Kwa upande wake, Mbunge wa Sikonge,
Joseph Kakunda (CCM) alisema: "Tuwe wazi kuwa huko serikalini kuna watu
wanaendesha Kadco wanamaintain status quo kwa sababu wanapata fedha.
Kama Baraza la Mawaziri halitakuwa
wazi katika hili, tutawasha moto bungeni.” “Kwa nini hawa TAA wawe na
share(hisa) na Kadco wakati hawana mamlaka?” alisema mbunge huyo akirejea
maelezo ya Mkurugenzi wa TAA katika kikao hicho aliyesema kuwa suala la Kadco
haliwahusu ingawa wana hisa.
Awali, Mwenyekitiwa Bodi ya TAA,
Profesa Ninatubu Lema alipoulizwa na wajumbe wa kamati kuhusu masuala kadhaa ya
Kadco, alisema kampuni hiyo iko nje ya mamlaka ya TAA kwa kuwa inaripoti moja
kwa moja kwa serikali.
Miongoni mwa maswali kuhusu Kadco
yaliyoulizwa na Kakunda na kufanya wajumbe wengi kuchangia, ni uhusiano wa TAA
na kampuni hiyo kama kama wana mkataba wowote. Pia alitaka kufahamu kama
kampuni hiyo, imerithiwa na serikali au imeanzishwa upya.
Kutopewa mikopa katika vikundi vya
wajasiliamali katika halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani katavi imekuwa
moja ya matatizo yanayorudisha nyuma maendeleo yao.
Wakizungumza na mpanda redio wamesema kuwa
vikundi vingi hushindwa kuendelea au kuvunjika kutokana na kukosa mikopo na uongozi kuwa mbovu ambao
hupelekea kudidimiza malengo ya kikundi.
Aidha kwa upande wa mwenyekiti wa kikundi cha
mapadeko mtoni group amesema ili kikundi kiendelee kukua vizuri ni lazima
kuhakikisha wanakikundi wanarejesha pesa mapema kwenye kikundi ili kukiimarisha
kikundi na kuepuka kuvunjika kwa
kikundi.
Vikundi vingi vya kijasiliamali hushindwa
kukua kutokana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kutosajiliwa;kukosa
mikopo na kuwepo kwa uongozi mbovu.
Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017.
Mahakama ya juu nchini Kenya imetoa uamuzi kuruhusu mawakili wanaomwakilisha kiongozi wa Upinzani Raila Odinga, kumulika mitambo za kompyuta zinazohifadhi hati za uchaguzi wa urais ambazo zimewekwa na tume ya uchaguzi.
Siku ya Jumatatu asubuhi Majaji saba wa mahakama ya juu nchini Kenya walianza kusikiliza kesi ambayo kiongozi wa upinzani Raila Odinga anapinga kuchaguliwa tena kwa rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8, 2017.
Kesi hiyo ilianza siku ya Jumamosi kwa maelezo ya mwanzo ambayo kila upande ulitoa ili kuhakikisha nafasi kwa kusikilizwa rasmi.
Katika kikao cha kwanza ambacho kilichukua muda wa masaa matano, na kumalizika saa tano usiku, mawakili wa pande zote walitoa maombi yao na matakwa yao ya kisheria.
Ombi kuu alilotoa James Orengo, mmoja wa mawakili wa Raila Odinga lilikuwa mahakama kumruhusu kumulikwa kwa mitambo ya kompyuta ambayo imehifadhi hati rasmi za uchgaguzi uliofanywa mapema mwezi huu.
Hata hivyo ombi la Orengo lilipingwa vikali na mawakili wanaomwakilisha rais Uhuru Kenyatta na pia tume inayosimamia uchaguzi Kenya.
Siku ya Jumapili kuamkia Jumatatu Mahakama ya Juu pia ilikubali kuingizwa kwa ushahidi kwenye kesi ya kupinga matokeo ya urais, hatua ambayo sasa imetenga uwanja wa makabiliano ya hoja kati ya mawakili wa rais Uhuru Kenyatta na wale wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
Tofauti na ilivyokuwa mwaka 2013, majaji saba wa mahakama hiyo walitupilia mbali mapingamizi yaliyotolewa na mawakili wa pande zote mbili waliotaka kila mmoja ushahidi wake utupwe kwa sababu uliwasilishwa nje ya muda. @habari na rfi swahili
Mzozo unaohusisha Korea Kaskazini ni mzozo ambao unaweza hata kusababisha vita vya vinyuklia, vita ambavyo huenda pengine haviwezi vikawa na mshindi. Lakini ni mzozo wenye mambo mengi tata. Hebu tuchanganue kiasi.
Ni kwa nini Korea Kaskazini inataka silaha za nyuklia?
Rais ya Korea iligawanyika na kuwa mataifa mawili baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na kukawa na Korea Kaskazini na Kusini. Korea Kaskazini iliegemea siasa za Kikomunisti na iliongozwa na serikali ya kiimla, uongozi sawa na wa Stalin katika Muungano wa Usovieti. Marafiki wake wakuu ni Urusi na Uchina.
Nchi hiyo ilijitenga pakubwa na nchi nyingine, isipokuwa nchi kadha marafiki wake. Viongozi wa nchi hiyo wanasema silaha za nyuklia ndiyo njia pekee ya kujikinga dhidi ya maadui kutoka nje ambao wanataka kuliangamiza taifa hilo.
Wamekaribia kiasi gani?
Majaribio yake ya karibuni zaidi ya makombora yanaachilia kwamba nchi hiyo inakaribia sana kuwa na makombora ya kuruka kutoka bara moja hadi jingine yanayofahamika kama (ICBM) ambayo yana uwezo wa kufika Marekani bara.
Wamefanyia majaribio silaha za nyuklia mara tano. Taarifa za kijasusi zinadokeza kwamba nchi hiyo inakaribia sana, au tayari imeweza, kuunda kichwa kidogo cha silaha za nyuklia kinachoweza kuwekwa kwenye makombora.
Nchi hiyo inaichukulia Marekani kuwa audi wake mkuu na pia ina maroketi ambayo yameelekezwa kwa Korea Kusini na Japan, nchi ambazo zina wanajeshi wengi sana wa Marekani.
Nini kimefanywa kuwazuia?
Juhudi za kutumia mashauriano kutatua mzozo huo zimeshindwa kupata suluhu.
Umoja wa Mataifa umeiwekea nchi hiyo vikwazo vingi - lakini bila mafanikio.
Uchina, mshirika wake wa dhati, pia imeiwekea shinikizo za kiuchumi na kidiplomasia.
Marekani sasa imetishia kutumia nguvu za kijeshi na Rais Donald Trump ameitahadharisha kwamba itakabiliwa kwa "moto na ghadhabu".
Marekani inaweza kuishambulia Korea Kaskazini?
Mzozo huo umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi, lakini hali kwamba Korea Kaskazini inakaribia kuwa na/ au tayari ina uwezo wa kuunda kichwa kidogo cha nyuklia kinachoweza kuwekwa kwenye makombora, na kwamba ina makombora yanayoweza kufikia Marekani bara, yanabadilisha mambo sana.
Miezi kadha iliyopita, kumekuwa na hatua za 'uchokozi' mara kadha za Korea Kaskazini pamoja na majibizano kati yake na Marekani ambazo zimezidisha mzozo huo.
Korea Kaskazini ilitishia kurusha mabomu karibu na kisiwa cha Guam ambacho kinamilikiwa na Marekani katika Bahari ya Pacific.
Na leo Jumanne, nchi hiyo imerusha kombora kupitia anga ya Japan.
Lakini huku majibizano yakiendelea, bado ni vigumu kubashiri ni nini kitafuata.
Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mjini Vwawa.
Mwakajoka amekamatwa leo Agosti 29 baada ya kufika mahakamani hapo kufuatilia kesi inayomkabili mbunge mwenzake wa Mbozi, Pascal Haonga.
Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbozi, James Mbasha amesema mbunge huyo amekamatwa lakini hajui kosa linalomkabili.
Mbasha amesema alipata taarifa leo asubuhi kwamba mbunge huyo anatafutwa na polisi.
Katika kesi mahakamani hapo, Haonga na wenzake wawili Wilfred Mwalusanya na Mashaka Mwampashi wanakabiliwa na mashtaka mawili, kufanya vurugu na kuwazuia askari kufanya kazi yao kinyume cha sheria.
Mwendesha mashitaka wa polisi, Samwel Saro anadai jana Agosti 28 saa saba mchana, washtakiwa walimzuia askari kutimiza majukumu yake ya kumkamata Mwampashi aliyedaiwa kwamba si mjumbe halali katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo.
Washtakiwa pia wanadaiwa kumfanyia vurugu msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbozi, Lauteri Kanoni.
Washitakiwa walikana mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Asha Waziri ambaye alisema dhamana iko wazi kwa kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka kwa watendaji wa maeneo yao watakaoweka bondi ya Sh2 milioni kila mmoja.
Washtakiwa walitimiza masharti na kuachiwa huru kwa dhamana. Kesi itatajwa Septemba 25 na washtakiwa watasomewa maelezo ya awali.
Watu takriban 2,000
wameokolewa kutoka kwa mafuriko katika mji wa Houston na viunga vyake, huku
kimbunga Harvey kikiendelea kusababisha mvua kubwa sana maeneo ya jimbo la
Texas.
Kumekuwa na
ripoti za kutokea kwa vifo pamoja na magari kadha kuzidiwa na nguvu za maji.
Hata hivyo,
uchunguzi bado unaendelea, afisi ya liwali mkuu wa wilaya ya Harris, Darryl
Coleman amesema.
Gavana wa Texas
Greg Abbott ameambia wanahabari kwamba hawezi kuthibitisha vifo vinavyodaiwa
kutokana na mafuriko hayo.
Idara ya Taifa ya Hali ya Hewa (NWS) imesema hali
ambayo inashuhudiwa katika eneo hilo haijawahi kushuhudiwa awali.
Idara hiyo
imesema kulitokea mafuriko ya ghafla eneo la katikati mwa mji wa Houston, na
uchukuzi umetatizika.
Vyumba vingi vya
kutoa hifadhi wakati wa majanga vimefunguliwa, ukiwemo ukumbi mmoja wa
mikutano.
Gavana Abbot
amesema barabara karibu 250 zimefungwa Texas na kwamba ameiomba serikali kuu
itangaze janga katika wilaya 19, ombi ambalo limeidhinishwa na Rais Donald
Trump.
NWS awali walisema walikuwa wamepokea taarifa za vifo
vitano, lakini wamesema wameweza kuthibitisha kifo cha mtu mmoja pekee eneo la
Houston.
Kufikia sasa,
watu wawili wamethibitishwa kufariki tangu kimbunga hicho kilichofika maeneo ya
bara, katika wilaya ya Aransas, ambapo Rockport ndio mji mkuu, mtu mmoja
alifariki baada ya nyumba yake kushika moto Ijumaa usiku.
Na eneo la
Houston, mwanamke mmoja alifariki akiendesha gari katika barabara zilizokuwa
zimefurika maji Jumamosi.
Meya wa Houston
Sylvester Turner amewashauri wakazi kutopigia simu maafisa wa huduma za dharura
ila tu iwapo maisha yao yanatishiwa na wanahitaji kuokolewa kwa dharura.
"Msiingie
barabarani. Msifikirie kwamba kimbunga kimepita," amesema.
Mjini
Washington, ikulu ya White House imesema Rais Trump atazuru Texas Jumanne
kutathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga hicho. Rais Trump alikuwa
amesema awali kwamba angezuru eneo hilo haraka iwezekanavyo lakini kwa
kuhakikisha kwamba hatatatiza juhudi za uokoaji.
Idara ya Umoja wa mataifa
ya mpango wa chakula duniani -WFP inasema inapunguza mgao wa chakula kwa
wakimbizi 320,000 wanaoishi kaskazini-magharibi mwa Tanzania kutokana na
upungufu wa msaada wa ufadhili. WFP ilisema katika taarifa ya Jumapili kwamba
inahitaji haraka msaada wa dola milioni 23.6 ili kukidhi mahitaji ya chakula na
lishe kwa wakimbizi hadi mwezi Disemba.
Kwa
mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP wakimbizi walioathirika
wengi wanatoka nchini Burundi na Congo. Michael Dunford, mwakilishi wa WHO
nchini Tanzania alisema “kuna umuhimu wa kupunguza mgao zaidi wa chakula” kama
wafadhili hawatajibu haraka.
WFP inasema ugawaji wa chakula ulipunguzwa kwa mwezi
Agosti kufikia asilimia 62 pekee inayotakiwa kwa mgao wa kila siku wa kaloris
2,100. Umoja wa Mataifa pia unaisihi jumuiya ya kimataifa kuchangia fedha ili
kuwasaidia zaidi ya wakimbizi milioni mbili wa Sudan Kusini wanaopewa hifadhi
katika nchi za jirani huko Afrika mashariki.
Mkuu wa Mkoa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga
Mkoa wa katavi kwa sasa upo katika
Mpango wa kuangalia Zao lingine la biashara ili kuleta maendeleo katika mkoa
huo.
Hayo yamsemwa na Mkuu wa Mkoa wa
katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ijumaa hii katika kikao maalum cha baraza la Madiwani wa
halmashauri ya manispaa ya Mpanda cha kujadili hoja za utekelezaji wa ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/16.
Amesema tayari amefanya mawasiliano
na Mkurugenzi wa bodi ya korosho kutoka mtwara ambao wanajiandaa kuja mkoani
katavi kwa ajili ya kuangalia maeneo kuona kama zao la korosho linaweza kuwa
moja ya Mazao hapa Mkoani.
Aidha
amesema kuwa hatua hiyo ni baada ya
kuona zao la tumbaku ambayo ilikua inaleta asilimia 60 ya mapato katika
halmashauri za Mkoani katavi kuonekana halina uhakika.