Wednesday, 28 February 2018

MIRADI SITA YA MAENDELEO TANGANYIKA YATAJWA KUPITIA RUZUKU




TANGANYIKA

Baraza la Madiwani katika Halimshauri ya wilaya ya Mpanda wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi limeidhinisha jumla ya miradi sita ya maendeleo itakayo tekelezwa na Fedha za Mradi kutoka Ruzuku ya mtaji LGDG  kwa mwaka 2017/2018

Akiwasilisha hoja hiyo mbele ya kikao maalumu cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa idara ya maji kaimu afisa mipango wa halimashauri ya wilaya ya Mpanda bwana Philimoni Mlageli ameitaja baadhi ya miradi itakayo tekelezwa katika Mpango huo kuwa ni pamoja na ujenzi wa stendi katika kijiji cha ikola pamoja na miradi mingine


Kwa upande wake diwani wa kata ya Kalema Maiko Kapata amesema ametumia nafasi hiyo kuliomba Baraza kubadilisha matuminzi ya pesa yaliyotengwa kwa jaili ya ukarabati wa shule ya msingi kalema na badala yake pesa hiyo ielekezwe katika utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha itetemia

Naye kaimu afsa mipango Bwana Filemon Mlageli amebainisha kuwa mashart ya pesa hizo ni mpaka miradi ikamilike

Miradi hiyo kwa pamoja inatarajia kughalimu zaidi ya shilingi billion moja za kitanzani hadi kukamilika kwake.

Chanzo: Poul Mathias 

MAJAMBAZI YAUA NA KUJERUHI WANUNUZI WA MADINI KATAVI


Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamemuua Mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watatu usiku  wa kuamkia leo katika mgodi wa dhahabu wa Isulamilomo uliopo Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi.


Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Jaffari Gwiyama Kitambwa,amemtaja aliyefariki kuwa ni Kalister Kalyalya mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa machimboni aliyepigwa risasi mgongoni na kutokezea tumboni.

Kwa upande wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo  Joseph Panya na Mrisho Abdalla  ambao pia walikuwa wakinunua dhabau machimboni hapo ,wamesema tukio la kuvamiwa kwao limetokea jana usiku

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amesema polisi limeanza uchunguzi wa tukio hilo
Chanzo: Isack Gerald

Monday, 26 February 2018

JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI LINAMSAKA MKAZI WA AIRTEL YA KWAMKUMBO KWA TUHUMA ZA KUMJERUHI VIBAYA MWANAE KWA MOTO.


MPANDA
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linamsaka mkazi wa Airtel ya kwamkumbo kwa tuhuma za kumjeruhi vibaya kwa kumchoma moto mwanae aitwaye  Nohadia Michael kwa kumtuhumu kuiba kiasi cha shilingi mia tano.

Katibu wa dawati la jinsia mkoani katavi Koplo Judithi Mbukwa  Ameimbia Mpanda redio kuwa Tukio hilo limetokea  tarehe February 23 mwaka huu  katika manispaa ya mpanda ambapo mzazi huyo alimchoma viganja vya mkono kwa moto wa jiko la mkaa Mwanaye  na kumsababishia maumivu makali.
         
Aidha Coplo Mbukwa  ametoa wito kwa wananchi na kuacha kutumia hasira katik kufanya maamuzi mbalimbali
Kwa  upande wake afisa ustawi wa jamii Manipsaa ya Mpanda Bi,  Agnes  bulaganya ametoa wito,amesema wanaendelea kumtibu motto huyo mpaka atakapopona na kuitaka jamiii  kuacha vitendo hivyo vya ukatili wa dhidi ya watoto ikiwemo Kumjengea mazingira salama dhidi ya vitendo vya ukatili kwa na utetezi wa kutumia mifumo sahihi ya ulinzi mtoto.

Kwa mujibu wa  Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 ni waraka unaoshughulikia masuala ya kitaifa yanayohusu haki na ulinzi wa mtoto inaainisha kuwa Suala la ulinzi wa mtoto ni jukumu la jamii nzima, mlezi na mzazi mmoja mmoja kwa nafasi yake katika ngazi ya familia pamoja na serikali kwa ujumla.


Chanzo:Ezelina Yuda

WANANCHI WILAYANI MPANDA WAMELALAMIKIA UBOVU WA BAADHI YA BARABARA NI CHANZO KINACHOPELEKEA UKOSEFU WA HUDUMA ZA KIJAMII KWA WAKATI.


MPANDA
Wananchi wilayani mpanda mkoani katavi wamelalamikia ubovu wa baadhi ya barabara katika maeneo yao  chanzo kinachopelekea ukosefu wa  huduma za kijamii kwa wakati.
Wamesema hayo wakizungumza na mpanda redio huku wakibainisha adha wanayoipata kutokana na  changamoto ya barabara hizo.
Kwa mujibu wa kaimu  mratibu wa tarura mkoa mhandisi zuberi kirenza ametaja barabara zilizoko kwenye mpango wa kutengenezwa kwa mwaka huu.
Aidha barabara zitakozotengenezwa mpanda mjini zitagharimu kiasi cha shilingi milioni 360  huku barabara za mjini zikigharimu shilingi milioni165 na vijijini milioni 195.

Chanzo:Ester Baraka

WAKAZI WA KATA YA NSEMULWA WAMEASWA KUCHANGIA KWA WINGI KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA.

Picha ya kituo cha afya 

MPANDA
Wakazi wa Kata ya Nsemulwa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameaswa kuchangia kwa wingi asilimia ishirini kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.
Wito huo umetolewa na diwani wa kata hiyo Mh.Bakari Kapona wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu mikakati ya ujenzi wa kituo cha huduma ya afya ili kutatua kero ya wananchi kupata matibabu umbali mrefu.
Aidha Mh. Kapona amesema "Manispaa ya Mpanda imetenga shilingi milioni 35 kwa ajili ya kituo hicho na kinachosubiriwa kwa sasa ni wananchi kuchangia nguvu zao ambapo ujenzi wa unatarajiwa kuanza fikapo mwezi juni Mwaka huu".
Kata ya Nsemulwa yenye wakazi wapatao elfu kumi na moja ni miongoni mwa kata 15 za Manispaa ya Mpanda na wakazi wake kwa sasa wanapata huduma ya afya katika vituo vilivyo jirani au kulazimika kwenda Hospitali ya wilaya Mpanda.
Chanzo:Issack Gerald

MWENYEKITI WA CCM MKOANI KATAVI AMEWATAKA VIONGOZI WA NGAZI ZOTE ZA KATA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.




MLELE
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Katavi Beda Alfred amewataka viongozi wa ngazi zote katika kata kutekeleza majukumu yao.
Akiwa ziarani wilayani Mlele katika kata ya utende wakati akizungumza na Wajumbe hao amesema kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kutawasaidia kuwaweka karibu na wananchi wao.
Kwa upande wao wajumbe hao wamesema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana na ni pamoja na migogoro ya ardhi baiba ya wakulima na wafugaji na vitendea kazi.
Katika ziara hiyo wilayani mlele Mwenyekiti wa ccm mkoa ametembelea pia mradi wa umeme uliopo katika kijiji cha Uzega.

Chanzo:Furaha Kimondo

CHANGAMOTO YA MIUNDO MBINU KIKWAZO KWA WANANCHI NA WATALII KUSHINDWA KUTEMBEA HIFADHI ZA NDANI.


KATAVI
Imeelezwa kuwa changamoto ya Miundombinu ikiwemo Bara bara imekuwa ni kikwazo kwa wananchi na watalii kushindwa kutembea hifadhi za ndani ikiwemo ya hifadhi ya Katavi.
Katika mazungumzo maalum na Mpanda redio mmoja ya  watumishi katika hifadhi hiyo  Private Ezekiel eliufoo  amesema endapo maboresho yatafanywa katika Nyanja hizo yatasaidia  kukuza utalii wa ndani.
Aidha Katika hatua nyingine amebainisha pia ujangili ukiwemo wa tembo umepelekea changamoto katika hifadhi hiyo inayopoteza tembeo wengi.
Awali Daudi Godowin ambaye ni afsa utalii ndani ya hifadhi hiyo amewataka wananchi wakiwemo wa katavi kujiwekea taratibu za kutembelea hifadho kuweza kujifunza masuala mbalimbali.
Hifadhi ya Katavi ni hifadhi ya tatu kwa ukubwa kati ya hifadhi kumi na sita zilizopo nchini Tanzania na ambayo pia imekuwa ikifanya kazi ya kuhifadhi mazingira ,kuifadhi vyanzo vya maji na wanyama.

Chanzo:Furaha Kimondo 

Friday, 23 February 2018


Wanafunzi wa shule ya Msingi Kabungu iliyoko  kata ya kabungu Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wameiomba serikali kuwaboreshea madarasa ambayo yaliezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

Wameyasema hayo walipozungumza na mpanda radio shuleni hapo " kuezuliwa kwa  madarasa kumetuathiri kwani vipindi vingi vimepunguzwa hali inayopelekea baadhi ya vipindi kutofundishwa pia madaftari na vitabu vingi vimeharibika ",walisema wanafunzi hao.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amesema kuwa upepo huo umesababisha uharibifu wa vitabu na madaftari yaliyokuwepo katika maktaba na kuiomba halmashauri kuwasaidia kufanya marekebisho ya miundombinu ili kuboresha elimu.


Ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi inatakiwa miundominu iwe imara inayoweza kuwa rafiki kwa  mwanafunzi na mwalimu.

WATUMISHI MKOANI KATAVI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KUBAINI WAFANYAKAZI HEWA


 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael  Muhuga

Watumishi wa umma katika Mkoa wa Katavi wameombwa kutoa ushirikiano kwa kamati maalumu iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael  Muhuga ili kubaini wafanyakazi hewa katika ofisi za umma.
Watumishi wa umma katika Mkoa wa Katavi wakiwakatika ukumbini katika kamati maalumu ya kubaini wafanyakazi hewa katika ofisi za umma.

Wito huo umetolewa katika kikao cha mapendekezo ya sekretarieti ya bajeti ya  Mkoa wa Katavi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ambapo Mkuu wa mkoa  alikuwa akizungumza na wafanyakazi wa hao .

Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo kwa wafanyakazi katika halmashauri zote kuhamia katika vituo vyao vyote vya kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

 
Watumishi wa umma katika Mkoa wa Katavi wakiwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael  Muhuga
Katika kipindi cha mwaka 2018/2019 mkoa wa katavi umepanga kutumia shilingi bilioni mia moja kumi na tisa namilioni mia moja na mbili na laki sita sitini na tatu elfu na mia tatu na nne(119,102,663na 304) sawa na asilimia 35% kwaajili ya utekelezaji mbalimbali wa miradi ya maendeleo.

Chanzo:Paul Mathias

TAKUKURU YATAKIWA KULINDA FEDHA ZA MIRADI MKOANI KATAVI

Mbunge wa Mpanda vijini Mh. Suleiman Kakoso


Mbunge wa Mpanda vijini Suleiman Kakoso ameitaka  Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani hapa  kufuatilia ili kuondoa ubadhilifu wa fedha katika miradi mikubwa ya serikali .

Ameyazungumza hayo katika kikao cha 11 cha kamati ya ushauri mkoa wa Katavi na kusema kuwa fedha nyingi za miradi ya serikali  zimekuwa zikifanyiwa ubadhilifu na kuiomba taasisi hiyo kufuatilia kwa karibu ili kuweza kulinda fedha hizo.

Akijibu swali la mbunge huyo  Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi, "kutokana na changamoto za fedha na raslimali watu imekuwa ikisababisha kupunguza kasi ya kukamilika kwa uchunguzi wa matukio ya rushwa ambayo taasisi hiyo imekua ikifuatilia
"amesema John Minyenya

Aidha ametoa wito kwa wabunge na viongozi wa ngazi zote kutoa ushirikiano pindi waonapo dalili za ubadhilifu wa fedha katika miradi mbalimbali.

Miradi mingi ya maendeleo mkoani katavi imekuwa ikisua sua katika ukamilishwaji huku ikielezwa kuwa chanzo ni ubadhilifu wa fedha.

Chanzo:RESTUTA NYONDO

AHUKUMIWA KIFO KWA KOSA LA KUUA KWA KUKUSUDIA



pichani mtuhumiwa Malandu  Likwaja akisubiri hukumu ya kesi yake

Mahakama kuu kanda ya sumbawanga mkoani Katavi imemhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa  Malandu Likwaja mwenye umri wa  miaka 42 mkazi wa igalula Wilayani Mlele  kwa kosa la kuua kwa kukusudia.


Mwendesha mashtaka wa serikali Lugano mwasubila mbele ya Jaji Dr Adamu Mambi ameiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Tarehe 13 mwezi wa saba mwaka 2007 ambapo alimuua Ibrahimu Juma kwa kumkata kwa shoka sehemu za kichwani na shingoni
Mahakama ya hakimu mkazi ilikotolewa hukumu ya mshitakiwa malandu

Aidha Jaji Dr Adamu Mambi amemhukumu kunyongwa hadi kufa  kwa mujibu wa kifungu  cha 195 na 196 cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002  na kubainisha kuwa kilichomtia hatiani ni kifungu cha 26 kifungu kidogo cha kwanza.

Chanzo: Furaha Kimondo

Thursday, 22 February 2018

WALIMU WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA WAITAKA SERIKALI KUTEKELEZA AGIZO LA KULIPA MADENI YA WALIMU HAO

Pichani walimu wa mkoa wa katavi
Baadhi ya walimu katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamesema wanasubiri kuona serikali inatekeleza agizo lake la kulipa madeni ya walimu mwezi huu.
Wamesema miongoni mwa athari zitokanazo na kutolipwa mishahara na stahiki nyingine kwa wakati ni pamoja na kudhorotesha ufanisi katika kazi pamoja na kusababisha ugumu wa maisha kwao.
Mara kadhaa,chama cha Walimu Mkoani Katavi kimekuwa kikipaza sauti ya kuitaka serikali ilipe madeni na sahiki nyingine za walimu ili kuchochea utendaji kazi shuleni.
Mwezi uliopita,serikali ilisema katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu,italipa madeni ya walimu na watumishi wengine wanaoidai serikali.

Source Issack Gerlad

VIJANA MKOANI KATAVI WATAKIWA KUTUMIA FURSA ILI KUENDANA NA SERA YA TANZANIA YA VIWANDA



picha kiwanda cha kusindika maziwa katavii

Vijana mkoani katavi wametakiwa kutumia fursa ya mazingira ili kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda ili kukabiliana na tatizo la ajira nchini

Wito huo umetolewa leo na mkurugenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa cha Katavi Diary bwana Gabriel Lunguya wakati cha kilichopo mtaa wa kasimba wakati akizungumza na mpanda radio ofisini kwake

Amesema kila mzalishaji anayo nafasi ya kushinda soko la bidhaa zake endapo atajikita katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora


Akizungumzia fursa za ajira tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho zaidi ya miezi  Bwana Lunguya mamesema mpaka sasa kimeajiri vijana watatu kwenye ajira rasmi na wengine zaidi ya 100 kwenye ajira zisizo rasmi

Katika hatua nyingine amewataka vijana kujiamini na kuthubutu kuwekeza katika sekta mbalimbali ili kunyanyua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla

Source:Haruna Juma




UHABA WA SEKONDARI WASHUSHA VIWANGO VYA UFAULU TANGANYIKA

Mkuu wa wilaya ya tanganyika Salehe Muhando

Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari hali inayopelekea kushusha kiwango cha ufaulu mkoani katavi.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya hiyo salehe muhando wakati wa kipindi cha majadiliano  katika kikao cha 11 cha kamati ya ushauri  mkoa.
Aidha amesema uhaba wa shule za kata imekuwa chanzo cha kutengeneza mazingira ya utoro na kuiomba ofisi ya elimu mkoa kuonyesha ushirikiano ktk jitihada zinazotoka kwa wazazi na wilaya hiyo.
Wilaya ya Tanganyika iliyopo mkoani katavi ina kata 16 huku ikiwa na shule za kata sekondari 8 pekee.

Source Restuta Nyondo

TASAF YAWA CHACHU YA KUBORESHA MAISHA YA WAKAZI WA KABUNGU



Bi. Agnes akionyesha mafanikio yake baaada ya Tasaf kumsaidia

Wanufaika 
wa mradi wa tasaf kata ya kabungu iliyopo katika wilaya ya Tanganyika wameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi ambao umewasaidia kuboresha maisha yao.
 Wameyasema hayo walipozungumza na mpanda radio na kusema kuwa maisha waliyokuwa nayo zamani hayakuweza kukidhi mahitaji yao ukilinganisha na sasa walivyoingizwa katika mradi huo.

Mradi wa tasaf ulianzishwa mwaka 2014 ambao ulikuwa na lengo la kunusuru kaya masikini ambazo hazina uwezo wa kukidhi mahitaji muhimu  ya kijamiiambayo ni  elimu,maradhi na chakula.

Vijiji 170 vipo kwenye mpango wa mradi huo na vijiji 80 tu ndivyo vilivyonufaika na mradi huo mpaka sasa mkoani Katavi.
bwana maulid akiwa mbele ya nyumba aliyoboresha baada ya kupata manufaa kupitia tasaf
Source:Furaha Kimondo


Wednesday, 21 February 2018

Mkazi wa kata ya Inyonga Halmashauri ya Wilaya ya Mlele anayefahamika kwa jina la Amani Silveri Pendelesi amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na vibali maalumu.


MLELE

Mkazi wa kata ya Inyonga Halmashauri ya Wilaya ya Mlele anayefahamika kwa jina la Amani Silveri Pendelesi amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na vibali maalumu.

Tukio hilo limetokea tarehe 14 mwezi huu katika kata ya inyonga  mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 35 raia wa Burundi  amekamatwa wakati akijaribu kujipatia kitambulisho cha uraia wa Tanzania ambacho ni kinyume cha sheria za nchi hii..

Kesi hiyo imesikilizwa leo katika Mahakam ya hakimu mkazi mkoani katavi mbele ya hakimu Omari Hassani Kingwele na mwendesha mashtaka wa uhamiaji Joseph Bajagae na mshitakiwa kukiri kutenda kosa hilo.

Hata hivyo mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kutoa faini ya shilingi laki tano za kitanzania.

Kuingia  nchini bila kibali ni kinyume na kifungu cha 45 sehemu ya kwanza cha sheria ya uhamiaji na ukurasa wa saba sura ya 54 kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 2016 imehukumu kesi hiyo.

Chanzo:Furaha Kimondo      

MAABARA YAONGEZA UFAULU WA MASOMO YA SAYANSI RUNGWA SEKONDARI

wanafunzi rungwa sekondari

Wanafunzi wa shule ya sekondari  Rungwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,wamesema kuwepo kwa maabara shuleni hapo kumewasaidia kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.

Wanafunzi hao wakiwemo Nichoraus Ntagaye,Hagma Shabaani na Sekela Laurence wameiambia Mpanda Radio kuwa,masomo ya sayansi yamekuwa rahisi kwa sababu ya kujifunza kwa vitendo.

pichani ni maabara ya wanafunzi kujifunzia

Mwalimu Martin Songolo  wa Kemia na Baiolojia katika shule hiyo amesema pamoja na uhaba wa vifaa katika maabara ufundishaji umekuwa rahisi kuliko kufundisha kwa nadharia.

Deus Kazonde ambaye ni mwalimu mwandamizi  taaluma katika shule hiyo amesema ufaulu kwa  kidato cha nne  kwa mwaka 2017 ulikuwa asilimia tisini tofauti na miaka iliyopita.


Source: Issack gerald

UKOSEFU WA MABARAZA YA WATOTO MKOANI KATAVI WACHANGIA UNYANYASAJI WA WATOTO

Watoto wakipata elimu

Wananchi katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema kutokuwepo kwa mabaraza ya watoto katika ngazi ya kata kunachangia kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji kwa watoto katika jamiii.

Wamesema kuwa vitendo vya ukandamizaji dhidi ya watoto vimekuwa vikiongezeka kila mwaka kutokana na kunyimwa fursa kuelezea changamoto na maswaibu mbalimbali wanayokabiliana nayo.


 Katika hatua nyingine wananchi hao wamezitaka mamlaka zinazo husika kuaandaa semina elimishi kuhusu umuhimu wa kuyatambua mabaraza hayo na kufahamishwa juu ya utendaji wake .

Maafisa wa maendeleo ya jamii manispaa ya Mpanda hawakutoa ushirikiano  kuhusu kueleza uwepo wa mabaraza hayo ngazi ya kata .

Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya Mwaka 2008 imeanisha tamko la Sera kuhusu uanzishwaji mabaraza hayo katika ngazi mbalimbalina  ikizingatiwa  kuwa mabaraza hayo ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya Mtoto namba 21 ya Mwaka 2009.


Source: Paul mathias

MKUU WA MKOA WA KATAVI AWATAKA MAWAKALA WA BARABARA KUBORESHA BARABARA ZA MKOA WA KATAVI


Barabara zinazotengenezwa mkoani Katavi

Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amewataka mawakala wa barabara kushirikiana na halmashauri zote  kuweza kubuni na kuboresha barabara  mpya  zitakazo saidia  kukuza uchumi mkoan katavi.


Aliyasema hayo katika kikao cha 11 cha utekelezaji wa matengenezo ya barabara kwa mwaka 2017/2018 na mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019"halmashauri ndizo zinazotambua swhemu ambazo zinauhitaji zaidi"alisema Muhuga.
Mkuu wa Mkoa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Muhuga
Kaimu Meneja Tanroads Mkoa wa Katavi  Mhandisi MARTIN MWAKABENDE alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2018/19 wakala wa barabara mkoa wa katavi waliomba kutengewa jumla ya shilingi bilion 15.1 kwa ajili ya kulipa fidia,kufanya ukarabati wa barabara,kufanya usanifu wa kina na kujenga madaraja.

Ubovu wa miundombinu hususani barabara na madaraja mkoani katavi ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa wananchi'


Source: Restuta Nyondo

Tuesday, 20 February 2018

UKUAJI WA UCHUMI UMESABABISHA KUPANDA KWA BEI ZA TOZO KWA WAFANYABIASHARA MKOANI KATAVI



Wananchi wa mkoani katavi wakitoa maoni

Wananchi wa mkoa 
wa katavi manispaa ya mpanda wametoa maoni yao kuhusu ukuaji wa uchumi nchini  huku wakiilalamikia serikali kuwapandishia tozo za kodi kitu kinachopelekea kuua mtaji wa biashara.  

Walisema  kuwa uchumi wa nchi unakua ingawa bado wanapata shida katika ulipaji kodi kutokana na tozo hizo kupanda bei na biashara zao hazina mtaji mkubwa ‘serikali inatakiwa kuangalia swala hili katika jicho la tatu kwa kuwa wafanyabiashara wadogo tunashindwa kutumia mashine za EFD na huku mitaji ni michache’amesema Charles Ruben mmoja wa wafanyabiashara.

Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kila mwaka ambapo mpaka kufikia mwaka2016 kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumiumefikia asilimia6.9 ikiwa imeshikilia nafasi ya pili katika nchi za bara la afrika ikiongozwa na  nchi ya Cote D’ivore ikiwa na asilimia 8.5.

Chanzo:Ezelina Yuda


Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imepata fedha kwaajili ya uboreshaji wa vyumba vya madarasa na mahabara.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Bw. Michael Nzyungu

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imepata shilingi milioni 281 kwaajili ya kutatua  changamoto ya uhaba wa vyumba vya mdarasa na maabala katika shule mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Michael Nzyungu,wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu tatizo la wanafunzi wa shule ya sekondari Kasokola kusomea katika vyumba vya maabala vyenye kemikali hali inayo hatarisha usalama wa walimu na wanafunzi.

Aidha Nzyungu amekiri kuwa tatizo hilo limetokana na wingi wa wanafunzi katika shule hiyo hususani kidato cha kwanza walioripoti mwaka huu.

Shule ya sekondari Kasokola ina jumla ya wanafunzi 415 ambayo ni miongoni mwa shule za sekondari 16 za manispaa ya Mpanda,tangu ianzishwe mwaka 2008 inakabiliwa na uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi.

Chanzo:Issack Gerlad

Wafanyabiashara wa soko la mpanda hotel wameitaka serikali kuwatafutia maeneo rafiki kwaajili ya kufanyia biashara zao.


Maeneo ya mnada wa soko la Mpanda hotel


Wafanyabiashara wa soko la mpanda hotel wameitaka serikali kuwatafutia maeneo rafiki kwaajili ya kufanyia biashara zao.

Wameyasema hayo walipozungumza na mpanda radio  kufuatia tamko la serilikali kusitisha mnada ambao umekuwa ukifanyika kila jumapili katika soko hilo.
  
Mfanyabiashara wa soko la Mpanda hotel akihojiwa na mwandishi wetu Furaha Kimondo
Mstahiki  meya wa halmashauri  ya manispaa ya Mpanda William Mbogo  amesema kuwa zoezi hilo litafanyika kama ilivyofanyika mwaka 2014.

Uongozi wa manispaa ya mpanda umekuwa ukipiga marufuku eneo hilo kufanyia shughuli za mnada kwa madai kuwa ni eneo la kituo cha afya hali iliyopelekea mgogoro kati ya wafanyabiashara na uongozi huo.
Maeneo ya ndani ya soko la mpanda hotel


Chanzo :Furaha Kimondo

Mwenyekiti wa pikipiki za miguu mitatu maarufu kama bajaji wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Rashidi Juma amewataka madereva wa bajaji kuendelea kutoa tozo ili kuweza kupata usajili wa namba za maegesho.


Maegesho ya  bajaji city centre  


Mwenyekiti wa pikipiki za miguu mitatu  maarufu kama bajaji wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Rashidi Juma amewataka madereva wa bajaji kuendelea kutoa tozo ili kuweza kupata usajili wa namba za maegesho.
 
Ameyasema hayo alipozungumza na mpanda radio na kusema kufanya hivyo itawasaidia madereva kuepuka usumbufu wa kukosa maegesho huku akitolea ufafanuzi suala la bajaji kupewa mihuri na namba na nyingine kupewa mihuri bila namba.

Kwa upande wa madereva wamekuwa na maoni tofauti kuhusu kuwepo kwa tozo hizo.  
Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Katavi Amani Mwakalebela amesema kuwa kutowepo kwa namba katika bajaji hizo ni kutokana na baadhi ya madereva kutokutimiza masharti yanayotakiwa.

Zoezi la ugawaji wa namba za maegesho limefanyika kutokana na uwepo wa matukio ya uharifu na uporaji ambayo yanaendelea kutokea  mkoani hapa.

 Chanzo:Furaha Kimondo

Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi inatarajia kufanya maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani katika kata ya Itenka.


NSIMBO

Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi inatarajia kufanya maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani katika kata ya Itenka.
              
Taariiifa hiyo imetolewa na afisa habari wa halimashauri ya Nsimbo  John Mganga wakati akizungumza na mpanda radio kwa njia ya simu ambapo ameeleza kuwa nia ni kuihamasisha jamii kujua nafasi ya mwanamke katika  maendeleo ya uchumi nchini.

Aidha amesema kuwa maadhimisho hayo yatakuwa yakifanyika katika kata mbalimbali za halimashauri hiyo kila mwaka.

Maadhimisho ya mwanamke duniani hufanyika kila  mwaka tarehe 08 mwezi wa tatu ambapo mwaka huu yakiwa na kauli mbiu isemayo“kuelekea uchumi wa viwanda kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wanawake vijijini”.


Chanzo:Restuta Nyondo

Wananchi wametakiwa kuzingatia ujenzi wa majengo ya makazi yao kwa kufuata ushauri wa jeshi la zima moto na uokoaji ili kurahisiha huduma pindi majanga ya moto yanapojitokeza.


MPANDA
Wananchi wametakiwa kuzingatia ujenzi wa majengo ya makazi yao kwa kufuata ushauri wa jeshi la zima moto na uokoaji ili kurahisiha huduma pindi majanga ya moto yanapojitokeza.

Hayo yamesemwa na Afisa polisi kitengo cha ukaguzi  Wilfred Luhega wakati akizungumza na mpanda radio na kueleza kuwa tatizo la makazi yasiyokuwa na mpangilio pamoja na uchimbaji holela wa visima ni changamoto kubwa na wakati mwingine kusababisha vifo .

Aidha ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika ofisi zao  kwaajili ya kupata elimu  ya zimamoto na uokoaji ili kuweza kusaidia kupunguza majanga yasiyokua ya lazima.

Mara kadhaa  Maafisa wa Jeshi la zimamoto na uokoaji  nchini wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa vitendea kazi kama kikwazo cha kukwamisha utendaji kazi.

Chanzo:Restuta Nyondo

Monday, 19 February 2018

Mkazi wa kata majengo iliyopo halmashauri ya manispaa Mpanda Mkoani katavi anayefahamika kwa jina la Omari Ally amefikishwa mahakamani kwa kosa la ubakaji.


MPANDA
Mkazi wa kata majengo iliyopo  halmashauri ya manispaa Mpanda Mkoani katavi  anayefahamika kwa jina la Omari Ally amefikishwa mahakamani kwa kosa la ubakaji.

Tukio hilo limetokea tarehe 13 mwezi wa kwanza  katika kata ya majengo ambapo mshitakiwa huyo mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa mji wa zamani mpanda alimbaka (jina linahifadhiwa) msichana  mwenye umri wa miaka 17 na kumsababishia maumivu makali.

Kesi hiyo imesomwa  leo katika mahakama ya wilaya mbele ya hakimu Chiganga Tengwa  na mwendesha mashtaka wakili wa serikali bi Flaviana Shiyo na mshitakiwa hakutakiwa kuzungumza chochote.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 5 mwezi wa tatu mwaka huu na  mtuhumiwa amerudishwa rumande .

Chanzo:Furaha kimondo

Wakazi wa kijiji cha Kamakuka kilichopo kata ya Kakese wameitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya Mkandarasi aliye shindwa kukamilisha Ujenzi wa dalaja linaunganisha kijiji hicho na kijiji cha Kampuni .



MPANDA
Wakazi wa kijiji cha Kamakuka kilichopo kata ya Kakese  wameitaka serikali  kuchukua hatua dhidi ya Mkandarasi aliye shindwa kukamilisha Ujenzi wa dalaja  linaunganisha kijiji hicho na kijiji cha Kampuni .
Wameiambia Mpanda radio kuwa uongozi wa kijiji na Kata umeshindwa kutatua kero hiyo ambapo wananchi hulazimika kupita majini hali ambayo ni hatari.
Mmoja wa viongozi ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Ipwaga Bw Moses Taratibu amesema kunahujuma katika utekelezaji wa mradi huo ambapo hata hivyo ameshindwa kumtaja mkandarasi aliye husika.
Licha ya eneo hilo kuwa maarufu kwa uzalishaji wa Mpunga na mahindi suala la miundo mbinu ya barabara ni kikwazo kwa mstakabari wa maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.

Chanzo:Alinanuswe Edward

Wananchi katika manispaa ya Mpanda Mkoa wa katavi wameombwa kuwa wavumilivu wakati ujenzi wa uwanja wa michezo wa Mwenge ukiwa unaendelea kujengwa.


MPANDA

Wananchi katika manispaa ya Mpanda Mkoa wa katavi wameombwa kuwa wavumilivu wakati  ujenzi wa uwanja wa michezo   wa Mwenge ukiwa unaendelea kujengwa.

Wito huo umetolewa na Mhandisi  msaidizi wa manispaa yam panda  Mohamed ulanga wakati akizungumza na mpanda redio kuhusu zoezi la ujenzi wa uwanja huo amesema bado unaendelea kwani ujenzi  wa uwanja ni mradi mkubwa.

Aidha  Ulanga amesema ujenzi wa uwanja huo unategemea michango mbalimbali ya wananchi na taassisi kwa kushirikiana na uongozi wa mkuu wa mkoa Meja jeneral mstaafu Rafael Mhuga.

Kwa upande wake mratibu wa mwenge mkoa wa katavi Boko majinge  amesema waratibu wa mwenge mkoa wamekabidhi uwanja huo chini ya uangalizi wa manispaa ya Mpanda.


chanzo:Paul Mathias

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...