Saturday, 31 March 2018

“ENDELEZENI MEMA YOTE KAMA MLIVYOKUWA MKIFANYA KIPINDI CHA KWARESMA"-ASKOFU


KATAVI
Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga, wa Jimbo Katoliki la Mpanda Mkoani Katavi

Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga, wa Jimbo Katoliki la Mpanda Mkoani Katavi  amewataka waumini wa kikristo kuendelea  kutenda mema kama walivyofanya katika kipindi cha mfungo wa Kwaresma.
Askofu Nyaisonga ametoa wito huo katika maadhimisho misa takatifu ya Ijumaa kuu ibada ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Bikira Maria Emakulata Jimbo la Mpanda.
Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo wamesema kipindi cha Kwaresma ni kipindi cha kutafakari wema ambao Mungu ameuonesha kwao na hivyo kutakiwa kutenda hivyo hivyo kwa wenye uhitaji.
Ijumaa Kuu  ambayo kitaifa imeadhimishwa mkoani Mbeya ni siku maalumu ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa ambapo inatanguliwa na Alhamisi Kuu.
Sikukuu ya pasaka Jumapili ya Aprili mosi mwaka huu,Watanzania wataungana na wakristo wengine duniani kote katika maadhimisho siku hiyo muhimu katika ukristo.
Chanzo: Restuta Nyondo

MATUKIO YA UKATILI KIJINSIA YAPUNGUA MPANDA


MPANDA

Matukio ya ukatili wa kinjisia yamepungua kwa asilimia kubwa katika  manispaa ya Mpanda Mkoni Katavi tofauti na kipindi cha mwaka jana.

Hayo yamesemwa na Coplo  Judith Mbukwa kutoka katika dawati la jinsia mkoani katavi wakati akizungumza na mpanda radio kwa njia ya simu  ambapo amesema kesi za  ukatili wa kinjisia zimepungua kutokana na wanaoriport kuwa wachache.

Pia amesema kuwa dawati la jinsia limeanza kutoa elimu kwa wananchi mkoani kote kwa lengo la kuelimishana,kushirikiana na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika semina zinazotolewa na dawati hilo ili wapate elimu husika juduithi ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi maswala ya ukatili yanapotokea katika mazingira yao .

Ukatili wa kijinsia ni kitendo anachofanyiwa mtu yeyote mwanamke au mwanaume kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia,. 

Hata hivyo tafiti nyingi zimeonyesha kwamba wanawake na watoto ndiyo wahanga wakuu wa ukatili wa kijinsia
CHANZO:Ezelina Yuda

VIJANA WA CCM MPANDA WAONYWA

MPANDA

Vijana wa Chama cha Mapinduzi ccm wilayani Mpanda wameonywa kutoingiza masuala ya udini na ukabila kwenye siasa.

Hayo yamesemwa na katibu wa umoja wa vijana wa chama cha cha mapinduzi UVCCM Bwana Deus Thomas katika mkutano na wananchi wa kata ya Kanoge

Bwana Thomas amewataka vijana kujikita katika kutekeleza sera za chama hicho kwani ndizo zinazowaunganisha

Aidha ameongeza kuwa chama hakitasita kuwachukulia hatua kali zikiwemo kuwafuta uanachama wale wote watakaobainika kwenda kinyume na matakwa ya chama
CHANZO:RESTUTA NYONDO

VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI VYADAIWA KUTESA RAIA


 MPANDA

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kasimba katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametaka vikundi vya polisi jamii na ulinzi shirikishi mtaani hapo kufuata maelekezo waliyopewa ili kudhibiti uharifu kuliko kupiga wananchi na kukamata pikipiki barabarani.

Malalamiko hayo yametolewa na wakazi hao kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na Mpanda Radio ambapo pia wengine wamesema uwepo wa vichaka vingi mtaani hapo kumechangia kuongezeka kwa uharifu.

Bw.Said  Rashid Mdemela na Rejius Damiano Mwanisawa ni miongoni mwa wananchi ambao wamezungumzia changamoto hiyo ya ulinzi.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba Bw.Laurent Machimu amekiri polisi jamii kukikuka taratibu za ulinzi ambapo amesema wamewaita na kuwaelekeza vizuri huku akisema viwanja vilivyopimwa na kutelekezwa vimechangia kuficha waharifu.

Mtaa wa Kasimba wenye watu wapatao 2000 ni miongoni mwa mitaa mitatu ya kata ya Ilembo na mtaa huo una vikundi viwili vya polisi jamii vyenye jumla ya vijana 43.
CHANZO:Ezalina Yuda

MALEZI YA MZAZI MMOJA HUWAATHIRI KISAIKOLOJIA WANAFUNZI-AFISA TAALUMA MPANDA


KATAVI


Jamii imetakiwa kuwa na ushirikiano katika malezi hususani ngazi ya familia ili kumjengea mtoto mazingira rafiki ya kitaaluma na nidhamu katika  maisha.

Mwalimu Philbert Nguvumali ni Afisa taaluma katika halmashauri ya wilaya ya mpanda mkoani katavi amesema kuwa watoto wengi wamekuwa wakiathirika kisaikolojia kutokana na tatizo la kutengana kwa wazazi au mtoto kupata malezi ya mzazi mmoja.

Nguvumali amesema kuwa watoto wanaopata malezi ya mzazi mmoja hujikuta wakishindwa kuwa na uwezo mkubwa wakufikiri na ni chanzo cha kuwa na tabia ya ubinafsi.

Imeelezwa kuwa katika nchi ya Tanzania na kenya kati ya  familia 10 kuna familia 7 za mzazi mmoja  hususani familia zinazoongozwa na mama pekee.

Chanzo :Restuta Nyondo

WATOTO WATOA MISAADA KWA WAGONJWA KUELEKEA SIKU KUU YA PASAKA


MPANDA

Watoto wa shirika la mtoto Yesu kutoka Jumuiya Mtakatifu Filomena Kigango cha Kawajense Majengo Mapya jimbo katoliki la Mpanda Mkoani Katavi,wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda.

Wakizungumza kwa niaba ya watoto wenzao Sesilia John Enock na Samweli wamesema wameamua kutoa msaada kwa wagonjwa wenye uhitaji ikiwa ni kuadhimisha Alhamisi kuu katika kuelekea sikukuu ya pasaka.

Kwa upande wake Katekista Joseph Paul Kansato ambaye pia ni mwalimu wa parokia ya kanisa kuu jimbo la Mpanda amesema watoto hao wametoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni, mafuta na sukari kama ishara ya upendo walionao kwa watu wenye shida mbalimbali.

Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa wakiwemo Mussa Paul na Magreth Peter Ndekeja wametoa shukrani zao kwa watoto hao waliotoa msaada huo huku wakiomba jamii kuiga mfano uliooneshwa na watoto hao.

Maadhimisho ya Ijumaa kuu kuelekea sikukuu ya Pasaka Jumapili ya Aprili mosi mwaka huadhimishwa na wakristo kote duniani kwa kutekeleza amri ya mapendo kama Yesu Kristo alivyosema.

CHANZO:ISACK GERALD 

WAJASIRIAMALI MPANDA WAIANGUKIA SERIKALI KUOMBA MTAJI

MPANDA

Wanawake wajasiliamali wa kikundi cha Tasilija Mpadeko katika kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda wameiomba serikali kuwasaidia kuwapatia mtaji katika kikundi chao kinacho jishughulisha na kazi ndogo ndogo za kujikwamua kiuchumi.

Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Mpanda Redio kuhusu namna ambavyo kikundi hicho kimewasaidia katika kujikwamua kiuchumi wamesema nivyema srikali ikawasaidi kuwaongezea mtaji utakao saidia kutunisha mfuko wa kikundi chao katika shughuli wanazo zifanya

Aidha wamebainisha baadhi ya changamoto wanazo kabiliana nazo katika kikundi chao kuwa ni baadhi ya wanakikundi kutorejesha pesa kwa wakati pamoja na hali mbaya ya biashara kwa baadhi ya misimu hususani wakati wa masika

Kikundi hicho cha Tasilija Mpadeko kina jumla ya wajasiliamali kumi na sita wanao jishughulisha na shuhguli mbali za kujikwamua kiuchumi kama vile kuchoma mandazi,kufanya bishara za kuuza mkaa na kuuza bidhaa mbali mbali sokoni.

CHANZO:Paul Mathius  

"VYOMBO VYA DOLA IMARISHENI ULINZI SIKU KUU YA PASAKA"-MCHUNGAJI


KATAVI


Vyombo vya dola Mkoani Katavi vimeombwa kuwa makini katika kipindi hiki cha sikukuu kuhakikisha hakuna uvunjifu wa Amani utakao sababishwa na  matukio ya kihalifu.

Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste Tanzania   Nsemulwa Gliady Eliazeri akizungumza na mpanda redio leo amesema kuna baadhi ya watu hutumia siku za Sikukuu kama Nyanja za kufanya uhalifu.

Kwa upande wa waumini wa dini ya kikirsto wamesema wanatarajia kuipokea sikukuu hiyo kwa Amani na utulivu ikiwa ni pamoja na kufika katika sehemu za ibaada ili kuadhimisha kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu.

Sikukuu ya Pasaka inatarajiwa kuadhimishwa tarehe mosi April mwaka huu kama kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
CHANZO:Ester Baraka 


Wednesday, 28 March 2018

MACHINGA SASA KUTAMBULIWA KWA VITAMBULISHO


MPANDA

 Wafanyabiashara wadogo wadogo  katika mkoa wa Katavi wameishukuru serikali kwa kuanzisha utaratibu wa kuwapatia vitambulisho tambuzi ambavyo vitawasaidia kufanya kazi zao.

Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Redio mpanda kwa nyakati tofauti ambapo wamesema vitambulisho hivyo vitawasaidia  kufanya shughuli zao pamoja na kuirahisishia serikali katika ukusanyaji mapato

Meneja wa mamlaka ya kukusanya mapato TRA Mkoa wa Katavi Enosi Mgimba amesema zoezi hilo limeshaanza kwa wafanyabiashara hao kupatiwa vitambulisho hivyo kama maagizo yalivyotolewa na ofisi  ya  kamishina mkuu wa TRA makao makuu

Utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo unatokana na marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 yaliyofanywa na Bunge la Bajeti la Mwaka wa Fedha 2017/2018 ambapo moja ya marekebisho hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho maalum wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi


Chanzo:PAUL MATHIAS

AJALI YA KIPANYA YAKATISHA MAISHA YA MWALIMU


MPANDA
Aliyekuwa Mwalimu wa shule ya sekondari ya St.Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Hipoliti Julius Milambo amefariki dunia papo hapo baada ya kogongwa na gari aina ya Hiace.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo,marehemu aligongwa jana majira ya jioni na gari linalotajwa kuwa lilikuwa likitoka kata ya Kakese ambapo aligongwa na gari hilo wakati akivuka barabara.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Theopister Elisha akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake amesema hajapata ripoti ya kifo cha mwalimu huyo.
Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alipotafutwa kuelezea tukio hilo amedai kuwa yupo msibani.

Waendeshaji wa vyombo vya moto wameshauri kuwekwe matuta katika barabara Mpanda - Kigoma ili kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea.

Chanzo:Isack Gerald

MBUNGE AAHIDI HOSPITALI, KUPITIA BILION 1.5 ZA SERIKALI


NSIMBO


Serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 kwa kila halmashauri nchini ili kujenga hospitali za wilaya

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo (CCM) Richard mbogo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kanoge kilichopo halmashauri ya nsimbo mkoani katavi

Mbogo amesema eneo la kujenga hospitali hiyo ya wilaya bado halijatengwa rasmi lakini kuna uwezekano wa kujengwa yalipo makao makuu ya Halmashauri ya Nsimbo

Wiki iliyopita mbunge huyo alikabidhi gari la kubebea wagonjwa katika zahanati ya Kata ya Kanoge kama mojawapo ya ahadi zake kwa wananchi wa kata hiyo

WATATU MATATANI KWA KUENDESHA SHUGHULI ZA KILIMO KATIKA VYANZO VYA MAJI


MPANDA
Wakazi wa kitongoji cha Itogolo kata ya misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameilalamikia serikali kuwakamata, kuwatoza faini na kuwalazimisha kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa.

Malalamiko hayo wameyatoa katika mkutano wa hadhara ambao umeitishwa na mwenyekiti wa kijiji cha Kampuni Bw.James Simoni ili kusikiliza kero za wananchi wa kitongoji hicho wanaosema wanakamatwa ovyo wakati elimu haijatolewa ya kutambua mita sitini kutoka chanzo cha maji ya mto Mpanda.

Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya watumia maji bonde la mto Mpanda Mahela Mahanda na Daudi Sumuni wamekanusha kuwaamrisha wananchi kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa lakini wamekubali kuwakamata na kuwatoza faini kabla ya kutoa elimu kwa wananchi hao.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kampuni Bw.James Simoni amesema mpaka sasa watu watatu wamekamatwa na kutozwa faini katika kitongoji hicho chenye kaya zipatazo 71 zinazotegemea mto Mpanda kuendesha maisha yao.

CHANZO: Issack Gerlad


SHEREHEKEEN PASAKA KWA KUTENDA YALIYOMEMA -MCHUNGAJI


KATAVI



Waumini wa dini ya kikrsto mkoani Katavi wameaswa kusherekea sikukuu ya pasaka kwa kumcha mwenyezi Mungu na si kwa kufanya matukio ya kuvunja amani ya nchi.

Mchungaji wa kanisa la Pentecoste Tanzania Dotto Gliady Eliazeri amezungumza na mpanda redio kuelekea maadhimisho ya sikukuu hiyo na kusema kuwa ipo kwajili ya kumbukumbu ya kifo cha Yesu Kristo.

Mchungaji dotto amesema dunia ikiwa na watu wenye hofu ya mungu matukio ya kiharifu yatapungua hivyo watumie kipindi hiki kuliombea amani taifa

Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ya kufanya ukumbusho wa kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulubiwa, kufa na kuzikwa kwake. 
Chanzo:Ester Baraka

Tuesday, 27 March 2018

MIKOPO YA SERIKALI YAWANUFAISHA WAJASIRIAMALI KATAVI


MPANDA

                     Picha ya wajasiriamali wakiwa darasani(Picha na Maktaba)
Wananchi wa Manispaa ya Mpanda ambao wanajihusisha na usajiriamali katika vikundi mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu mchango wa serikali katika vikundi  hivyo.
Agustina Kunikwiza ni mwenyekiti wa kikundi cha mwembeni ambacho kinahudumiwa na serikali, amesema serikali imewapatia kiwango cha fedha ambacho kikundi hicho wanatumia katika shughuli za  kilimo na ufugaji.
Aidha ametaja changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo  mtaji kutokana na wanakikundi kuongezeka hali inayopelekea  fedha hizo kutokutosheleza na kuiomba serikali kuweza kuwaongezea fedha ili kuweza kuendeleza miradi yao.
Kila halmashauri hutenga asilimia 10 ya mapato yake kwaajili ya kuwawezesha wanawake na vijana  ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Chanzo:Ezelina Yuda

Monday, 26 March 2018

KUTOSOMA MAPATO NA MATUMINZI KWAWATOKEA PUANI VIONGOZI SIJONGA


TANGANYIKA

Wananchi wa Kitongoji cha Sijonga kata ya Kabungu wilayami Tanganyika Mkoani Katavi wameulalamikia uongozi wa kijiji kwa kutokuwa na utaratibu wa kutoa taarifa ya mapato na matumizi katika kijiji hicho.
Wakizungumza na Mpanda Radio kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema katika kijiji hicho wamekuwa wakichangia michango mbalimbali kama ya maji lakini wanashangazwa na kitendo cha kutosomewa mapato ma matumizi yaliyopo.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Kata ya kabungu na ambaye  ana kaimu  nafasi mtendaji kijiji cha kabungu  Othumani Kasamia ameshanganzwa na malalamiko hayo na kusema kuwa wao kama viongozi taarifa za mapato na matumizi wanasoma kila baada ya miezi mitatu na baada ya hapo wanabandika katika mbao za matangazo ili kila mmoja aweze kujisomea.
Ni haki ya kila mwananchi kupewa taarifa za maendeleo katika eneo analoishi hususani kujua mapato na matumizi.
Chanzo:Rebecca Kija

IDADI YA VIFO WALIOKULA UYOGA IMEONGEZEKA YAFIKIA WATATU


MPANDA
Idadi ya walio fariki kutokana na kula uyoga unaosadikiwa kuwa na sumu katika kijiji cha Stalike wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imeongezeka na kufikia watu  tatu.
Christopher  Anjero ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho amezungumza na Mpanda radio kwa njia ya simu akieleza kuhusu kifo cha Mariana Jerad Saanane ambaye ni Mama wa marehemu wawili walio fariki siku ya jana.
Kisa hicho  ambacho kimeiacha jamii ya eneo hilo katika simanzi kinatajwa kuwa cha mara ya kwanza tangu miongo kadhaa iliyopita.
Frenki Mayaga  amefariki akipatiwa huduma ya kwanza katika kijiji cha Stalike huku  Erizabeth Joji ambaye alikimbizwa hospitali ya Manispaa ya Mpanda akiaga dunia mlangoni kwa daktari.
Mpanda radio imemtafuta Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambaye amekana kueleza zaidi kuhusu suala hilo kwa madai ya kutokuwa msemaji kwa sasa.
Chanzo:Alinanuswe Edward

UJENZI WA ZAHANATI KIJIJI CHA KAJEJE KUTATUA CHANGAMOTO ZA AFYA KWA WANANCHI


 NSIMBO


Ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Kajeje kata ya Kanoge  Halmashauli ya Nsimbo unaoendelea  utasaidia kutatua changamoto ya huduma za afya katika kata hiyo.
Diwani wa kata ya Kanoge Salehe Mrisho akizungumza na Mpanda Radio amesema huduma za afya zinaendelea kuboreshwa katika maeneo mabalimbali.
Amesema uboreshwaji  huo umeambatana na serikali kutoa gari la wagonjwa litakalohudumia wagonjwa kuwafikisha Hosptali kwa wakati hasa akinamama wajawazito ambao wamekuwa wakipoteza maisha kwa kuchelewa kufika hosptali.
Ujenzi wa Zahanati hiyo ya kijiji cha Kajeje umeingizwa kwenye  bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019  ambapo  unatarajia kugharimu kiasi cha shilingi milioni 25.
Chanzo:Ester Baraka

WAWILI WAPOTEZA MAISHA,WATATU MAHUTUTI KWA KULA UYOGA WILAYANI MPANDA


MPANDA
 
Video Mwenyekiti wa Kijiji cha Stalike Christopher  Anjero akizungumza na Mwandishi wetu Haruna Juma eneo la Tukio 

Watu wawili wa familia moja katika kijiji cha Stalike Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi  wamefariki dunia kutokana na kula uyoga unaodhaniwa kuwa na Sumu na watatu wakiwa mahututi.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher  Anjero ameelezea kisa hicho kuwa cha mara ya kwanza tangu miongo kadhaa iliyopita ambapo amewataja marehemu hao kuwa ni  Frenki Mayaga na Erizabeth Joji.
Ndugu wa marehemu  ambao  wanamuuguza mama wa familia hiyo wameelezea kusikitishwa na tukio hilo na kulitaja  kuwa maajabu.
Mpanda radio imemtafuta Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda ili kujua taratibu za kitabibu zinazo endelea bila mafanikio kutokana na kuto kuwepo katika eneo la kazi.
Chanzo:Alinanuswe Edward


Sunday, 25 March 2018

HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA YAWAFIKIA WANANCHI KWA ASILIMIA 45 NSIMBO


NSIMBO

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo mkoani Katavi Richard  Mbogo amesema katika kipindi cha miaka miwili iliyopita zaidi ya visima arobaini vimechimbwa katika jimbo hilo kwa ajili ya kusaidia wananchi kupata maji safi na salama.
Richard Mbogo ameeleza baadhi ya mikakati ya ukamilishaji wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2017/ 2018 akiitaja kuwa suluhu ya tatizo la maji katika Vijiji vya kata ya Stalike na Itenka B, .
Katika hatua nyingine amesema katika mwaka wa fedha 2018/2019 maeneo ya vijiji vipya yatafikishiwa miradi ya visima vya maji ili kuboresha huduma za kijamii katika maeneo hayo.
Inaelezwa kuwa katika kipindi hicho cha miaka miwili upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama imepanda kutoka 34% mpaka 45%.
Chanzo :Alinnuswe

MBOGO AKABIDHI GARI LA WAGONJWA KANOGE


NSIMBO
                           Gari la kubebea wagonjwa 
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoani KataviKupitia Chama  Cha Mapinduzi (CCM) Richard Mbogo  amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya cha Kanoge
Akingumza na wananchi wa kijiji wa Kanoge wakati wa makabidhiano hayo Mbogo amewataka wananachi hao kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea kutatua kero mbalimbali zinzawakabili
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo Dk Sospeter Boyo amewataka wananchi kulitunza gari hilo ili lidumu na kuendelea kuwasaidia
Kituo cha afya ni Kanoge kinahudumia wakazi wa vijiji kadhaa ikiwemo Kanoge, Katumba, Kambuzi na Mnyaki
Chanzo:Haruna Juma 

Friday, 23 March 2018

UHABA WA MABWENI WAWAATHIRI WANAFUNZI SEKONDARI KABUNGU


KATAVI

Uhaba  wa mabweni katika shule za Sekondari Mkoani Katavi umetajwa kuchangia kushusha taaluma ya wanafunzi hasa wa kike

Mpanda radio imetembelea shule ya Sekondari Kabungu iliyopo wilaya ya Tanganyika, moja ya shule za sekondari mkoani Katavi inayokumbana na changamoto hiyo

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kukosenakana kwa mabweni katika shule za sekondari kunasababisha wasome katika mazingira magumu na hata wengine kulazimika kuishi kinyumba na wanaume

Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Patrick Kapita amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 627 wa kidato cha  kwanza mpaka cha sita na kati ya hao ni wanafunzi 52 pekee wa kidato cha kwanza hadi cha nne ndio wanaokaa hosteli na wengine 128 wa kidato cha tano na sita

Kufuatia hali hiyo uongozi wa shule ya sekondari Kabungu umepanga kukutana na wadau wa elimu siku za usoni kujadili changamoto hiyo na kupanga ni namna gani ya kutatua changamoto za kieleimu kwa wanafunzi
Chanzo: Haruna

UKATA WA MITAJI WA WAYUMBISHA WAUZAJI WA MAHINDI MPANDA


MPANDA

Wafanya biashara wa Zao la mahindi katika Soko la Mpanda Hotel katika Halimashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wanakabiliwa na ukata wa mitaji yao kutokana na mahindi mapya kuanza kuanza kuingia sokoni.

Wakizungumza na Mpanda Radio wamesema wateja wengi wanapendelea kununua mahindi mapya ambayo yanauzwa kwa shilingi elf 36kwa gunia tofauti na mahindi ya zamani yanayo uzwa shilingi elfu 42 kwa gunia.

Aidha wamebainisha changamoto wanazo kumbana nazo katika kazi yao kuwa ni pamoja na baadhi ya wakulima kuwawadanganyifu wakati wa kununua mazao hayo hususani suala la vipimo

Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Mikoa inayo tajwa kuzalisha kwa  wingi  mazao ya chakula hapa nchini ikiwemo Mahindi
Chanzo:Paul Mathius

TUDUMISHE ULINZI SHIRIKISHI TUKOMESHE MATUKIO -WANANCHI


MPANDA


Wananchi wa Kata cha Magamba katika Halmashauri ya  ya Manispaa ya Mpanda wameiomba serikali kuunda vikosi vya kudumu vya ulinzi shirikishi ili kuweza kuzuia matukio ya kiharifu katika kijiji hicho.

Hayo yamesemwa wakati wakizungumza na mpanda radio na kusema kuwa wamekuwa wakiunda vikosi vya ulinzi shirikishi baada ya kutokea kwa matukio ya uharifu

Anna Thomas Mapazi ni mwenyekiti wa kijiji cha magamba ametaja aina ya matukio ya kiharifu ambayo yamekuwa yakijitokeza katika eneo hilo kuwa ni pamoja na wizi wa mifugo na sola.

 Polisi Jamii au Ulinzi Shirikishi(community policing) ni mkakati wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi, Lengo la mkakati ni kuweka mazingira ya ushirikiano wa dhati baina ya wananchi na Polisi ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Chanzo: Restuta Nyondo

Thursday, 22 March 2018

PONGEZI KWA SERIKALI KUTATUA KERO YA MAJI -WANANCHI TANGANYIKA


TANGANYIKA

Wakazi wa kitongoji cha Sijonga kata ya Kabungu wilaya ya Tanganyika  mkoani Katavi wameipongeza serikali kwa kutatua kero ya maji katika maeneo yao.
Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti na wnananchi hao wamesema kuwa katika maeneo yao suala la maji siyo tatizo hali inayowapa fursa ya kufanya shughuli zingine za kimaendeleo badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.
Kitongoji cha Sijonga kimekuwa na utofauti mkubwa ukilinganisha na maeneo mengine ambayo mkoani Katavi wakazi wake wanalalamika kuwepo kwa kero ya maji.
Wiki ya maji Duniani imebeba kauli mbiu Hifadhi maji na mfumo wa kiikolojia kwa maendeleo ya jamii na kwa mkoa wa Katavi imefanyika katika kijiji cha Dilifu.
Chanzo Rebecca

WAWILI MBARONI KWA KUHAMASISHA MAANDAMANO KATAVI


KATAVI

KAMANDA WA POLISI MKOANI KATAVI ACP DAMAS NYANDA 
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kwa njia ya Mtandaoni.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu namna ambavyo jeshi hilo limejipanga kudhibiti maandamano hayo.
Aidha Kamanda Nyanda ametoa onyo kali kwa watu watakaohamasisha au kuandamana ambapo amesema watakaoandamana watakabiliwa na hatua kali za kisheria.
Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi ambao wamezungumza na Mpanda Radio wakiwemo Said Rashid,Juma Bairon,Jonathan Midende na Wenseslaus Obed wamesema maandamano hayo hayana tija na hawatashiriki kwa sababu ya madhara yanayoweza kujitokeza.
Maandamano hayo yanayodaiwa kupangwa kufanyika  Aprili 26 mwaka huu
Chanzo: Issack Gerlad

TUNAOMBA ELIMU YA MATUMINZI YA CHOO BORA -WANANCHI


MPANDA
                                            PICHA YA   CHOO BORA 
Wananchi wa kijiji cha magamba Halimashauri ya Manspaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya vyoo bora ili  kuzuia  magonjwa ya mlipuko.
Wakizungumza na mpanda radio kwa nyakati tofauti wamesema hali ya matumizi ya vyoo bora katika kijiji hicho bado hairidhishi huku wakieleza sababu ni ukosefu wa elimu na uhaba wa maji katika eneo hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Magamba Anna Thomas Mapazi amekiri kuwa baadhi ya wananchi  hawana uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya vyoo bora na kutoa wito kwa wananchi kujenga vyoo bora ili kulinda afya zao dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
Asilimia 60 ya  kaya nchini  hazina vyoo bora  na  Kaya zenye vifaa maalum kama sabuni na  maji  ya  kunawa mikono ni 34% pekee.
Chanzo:Restuta Nyondo

"MAJI YA UHAKIKA TANGANYIKA 2020" -SABUNI

 TANGANYIKA


                    Wananchi wilayani Tanganyika wakipata huduma ya maji 

Halmashauri ya Mpanda mkoa wa Katavi inakadilia kuwa ifikapo mwaka 2020 vijiji vingi vitafikiwa na maji safi na salama Wilayani Tanganyika kwa asilimia 80.
Mhandisi wa maji Alkam Omary Sabuni amebainisha hayo mapema leo kupitia Mpanda radio na kuitaja shabaha ya serikali kuwa nikuhakikisha sera ya upatikanaji wa maji vijijini umbali wa mita 400 inatekelezeka kwa vitendo.
Katika hatua nyingine ameitaja baadhi ya miradi ya maji ambayo inatumika na wananchi kama sehemu ya mikakati ya halmashauri hiyo kuwa ni mradi wa maji Majalila, Igagala, Ikola na Mishamo.
 Wiki hii benki ya dunia imekubali kuisaidia Tanzania kiasi cha dola milioni  300  kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji safi  mijini na vijijini.
Chanzo: Allinanuswe

Wednesday, 21 March 2018

WALIOTAPELIWA MASHINE ZA EFD'S KATAVI WAREJESHEWA FEDHA ZAO


KATAVI

Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania mkoani Katavi imethibitisha kurejeshwa kwa fedha za wafanyabiashara waliokuwa wakidai kutapeliwa na baadhi ya makampuni yanayouza mashine za kielektronic (EFDs) hapa nchini

Hatu hiyo imethibitishwa na Katibu wa jumuiya hiyo Bw.Robison Thompson Bumela wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu hatima ya malalamiko ya wafanyabiasahara waliokuwa wakidai kutapeliwa fedha bila kupata mashine hizo.

Aidha katibu huyo amesema wafanyabiashara ambao bado hawajarudishiwa fedha zao ni waliokuwa wamelipa bila kupewa risiti kutoka kwa wakala aliyekuwa akilalamikiwa.

Kwa nyakati tofauti,Mkuu wa Mkoa wa Katavi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda walikuwa wakiiagiza mamlaka ya ya Mpato Tanzania TRA kuhakikisha wafanyabiashara wanapata fedha au mashine zao

Kwa mjibu wa Bw.Bumela jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2014 ina wafanyabisahara wanachama zaidi ya 150 na wafanyabiasahara waliokuwa wametapeliwa ni zaidi ya kumi.

Chanzo:Isack Gerald

"WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO WAPENI MADEREVA WENU VITAMBULISHO VYA KAZI"-SHIGELA


MPANDA

Wamiliki wa magari Mkoani Katavi  wameaswa kutunza kumbukumbu za madereva wanaowakabidhi magari wanayomiliki kwa mujibu wa kanuni ya 79 ya sheria ya usalama barabarani.
Askari wa Jeshi la polisi  kitengo cha usalama Barabarani Wilayani Mpanda PC Samwel Shigela amesema ni  kosa kwa mmliki kushindwa  kutunza kumbukumbu hizo .
PC Shigela amesema  ni wajibu wa wamiliki kuwatambua vizuri madereva wao ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitambulisho vya kazi 
Kwa mujibu sheria ya  usalama barabarani  sura ya 168 iliyofanyiwa maerekebisho mwaka 2002 kifungu cha 95 kimeainisha  tozo kwa makosa ya  papo kwa hapo kwa magari na pikipiki kuwa ni Tsh 30000 kwa kila kosa 
 Chanzo :Ester Baraka

Tuesday, 20 March 2018

ULINZI SHIRIKISHI WAPUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU NSIMBO


NSIMBO


Wananchi katika Kijiji cha Sitalike Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi kwa kushirikiana na Viongozi wao wamesema wamefanikiwa kukomesha matukio mbalimbali ya kihalifu

Hatua hiyo imethibitishwa na mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw.Christopher Angelo Mrisho wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu mikakati waliyonayo katika kupambana na uharifu kijijini hapo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Ilangasika kata ya Sitalike Bw.Michael Augustino Hamis pamoja na mambo mengine ameishauri serikali kutafuta fursa za ajira kwa vijana kwani uharifu unaotokea kwa kiasi kikubwa unahusisha vijana wasiokuwa na kazi maalumu za kufanya.

Kijiji cha Sitalike kipo kata ya Sitalike Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo ambapo halmashauri hiyo hivi karibuni imekumbwa na matukio ya watu wake kuvamiwa,kujeruhiwa,kuuwawa na uporaji wa mali.

Matukio ya hivi karibuni ni pamoja na tukio la uvamizi kata ya Ugalla na Mgodi wa Isulamilomo ambapo katika matukio hayo watu wawili waliuawawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Chanzo:Isack Gerald 


BEI ELEKEZI YA MAFUTA KAA LA MOTO KWA WASAFIRISHAJI MPANDA


MPANDA

Watumiaji wa vyombo vya moto katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani  Katavi wamelalamikia bei elekezi ya mafuta ya dizeli, mafuta ya taa na petrol iliyotolewa na mamlaka ya uthibiti  wa maji na   nishati Ewura.
Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio  kwa nyakati tofauti  wamesema bei ya shilingi elfu 2400 kwa lita imekuwa ngumu kuendesha shughuli kutokana na wateja wao kutoelewa mabadiliko ya bei hizo.
Aidha wameziomba mamlaka zinazo husika ziwasaidie kuliangalia suala hilo kwakina ilikurahisisha kazi zao kwani imekuwa vigumu kufanya kazi hiyo kutokana na bei hiyo ambayo haiwapatii masilahi
Mapema mwezi huu mamlaka ya udhibiti wa maji na nishati eura imetoa bei elekezi ya mafuta ya disel petrol na mafuta ya taa bei ambayo ilionekana kuwa ya kiwango cha juu
Chanzo:Paul Mathius

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...