Monday, 30 April 2018

MBOGO AWAKUMBUSHA WAUMINI KUFANYA USAFI KATIKA MAKABURI



Wito umetolewa kwa Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini  kuwahimiza  waumini kufanya usafi katika maeneo ya makaburi.

Hayo yamebainishwa na mstahiki meya wa manispa ya Mpanda Willium Mbogo ambapo amewataka wauminini wote kukumbuka kufanya usafi na kuweka mazingira mazuri katika maeneo ambayo wanatumia kuzika .

Aidha amesema makaburi mengi kwa sasa yamezungukwa na majani ambazo zimeleta vichaka hali ambayo inashusha vigezo vya usafi kitaifa hivyo kila mtu aone umuhimu wa kujali maeneo hayo.

Tatizo la usafi katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi bado ni changamoto kutokana na mwamko mdogo wa wananchi katika usafi wa  mazingira.

Source:Rebacca kija

Sunday, 29 April 2018

HII NAYO KALI ... VYANDARUA VYA KUJIKINGA NA MALARIA VYATUMIKA KUVULIA SAMAKI MPANDA


Wakati serikali ikihimiza matumizi ya vyandarua ili kujikinga na ugonjwa wa Maralia  baadhi ya Vijana wa Manispaa ya Mpanda  mkoani Katavi wanavua samaki kwa kutumia vyandarua Katika mto Mpanda.

Katika Mahojiano vijana hao ambao hawakuwa tayari kujitambulisha wamedai kutumia vyandarua hivyo ili kurahisisha upatikanaji wa kitoweo cha Samaki.
Mto huo ambao unadaiwa kuwa chanzo cha jina Mpanda umezongwa na shughuli lukuki za kibinadamu ambazo huhatarisha, mazingira hata kuwepo kwa kitisho cha magonjwa ya mlipuko.

Diwani wa Kata ya Misunkumilo Matondo Alfred amesema anafanya kila liwezekanalo ili kuchukua hatua dhidi ya vijana hao.Katika nchi za Afrika Mashariki inakadiriwa kuwa na wagonjwa milioni 60 na watu milioni moja huripotiwa kufa duniani kila mwaka.

Source:Alinanuswe Edward

WAJASIRIAMALI KATAVI WALIA NA PRIDE KUTOWALIPA GAWIO LAO LA ZAIDI YA MILIONI 1



Baadhi ya Wajasiriamali halimashauri ya manispaa ya mpanda wamelilalamikia shirika la pride Tanzania mkoani Katavi linalojihusisha na utoaji wa mikopo kushindwa kuwalipa gawio la fedha kwa muda wa miezi  minne sasa.

Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti wamesema madai yao ni zaidi ya shilingi milioni moja tangu mwezi wa kumi mwaka jana lakini mpaka sasa hawajalipwa fedha hizo licha ya kufuata masharti ya marejesho ya mikopo kwa wakati kwenye shirika hilo.

Aidha wamesema malalamiko yao yamefikishwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kupata ufumbuzi jambo ambalo mpaka sasa halijatatuliwa.

Kwa upande wa Meneja wa Pride Mkoa wa Katavi Ambele Chamba amesema anafuatilia ili kujua ukweli wa madai hayo yafanyiwe kazi.

Chanzo:Paul mathias

WAZAZI WALEZI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONO


Wazazi na walezi Mkoa wa Katavi  wametakiwa kushirikiana seriakali kutokomeza  tatizo la mimba za utotoni.

Hayo yamesemwa na  Mwalimu Victa Lutajumlo wa Idara ya elimu msingi katika kongamano la mafunzo kwa wanafunzi wa msingi na sekondari lililolenga kutoa elimu ya kujikinga na mimba za utotoni.
Mmoja kati ya wa wanafuzi walio hudhuria kongamano hilo amesema mafunzo hayo yatawabadisha kifikra na kujiepusha na vitendo hatarishi vinavyo pelekea kuongezaka kwa tatizo hilo mkoani Katavi.

Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Mkoa wa katavi unaongoza kwa mimba za utotoni kwa kiwango cha asilimia 45

Chanzo:Furaha Kimondo

Tuesday, 24 April 2018

MARUFUKU KULIMA KWENYE VYANZO VYA MAJI"MKUU WA WILAYA YA MPANDA"



Mkuu wa wilaya ya Mpanda Liliani Matinga amewataka wananchi kuacha tabia ya kulima katika vyanzo vya maji ili kuepusha uharibifu wa mazingira.

Ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha kuwasilisha mpango kabambe wa maendeleo katika Manispaa ya Mpanda kilichofanyika leo amesema kumekuwepo na baadhi ya wananchi wanaolima bila kuzingatia umbali wa mita sitini kama sharia inavyoelekeza.

Aidha amebainisha kuwa wale wote watakaokiuka agizo hilo hatua kali azitachukuliwa dhidi yao pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria .

Halmashauri ya manispaa ya Mpanda imezindua mpango wa mpango miji wa mwaka 2018-2038 ambapo mradi huo utaainisha maeneo mbalimbali ya kiutawala ,kilimo,vyanzo vya uchumi pamoja na maeneo ya utalii ndani ya manispaa na mkoa  kwa ujumla.

Mpango huo wa miji unasimamiwa na kampuni ya city plan iliyoshinda tenda ya kupanga mji wa Mpanda kuonekana wa kisasa kwa kuzingatia mazingira na nyakati za kukua kwa kasi maeneo mbalimbali hapa nchini

Source:Paulo Mathius  


WANANCHI WA MTAA WA TAMBUKA RELI HATARILI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU



Wananchi wa Mtaa wa Tambuka Reli  kata ya Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda  wapo hatarini kukumbwa na Magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafu uliolundikana katika eneo lao kwa takilibani miezi sita.

Wakizungumza na Mpanda Redio wananchi hao wamesema licha ya kuchangia mchango kwa kila kaya kwaajili ya uzoaji wa taka hizo bado taka hizo hazija zolewa hali ambayo huleta harufu mbaya hususani wakati huu wa masika
                  
Aidha wanachi hao wamesema kwa mara kadhaa wamekuwa wakikamatwa na askari mgambo kwaajili ya pesa ya tozo ya kuzolea uchafu lakini hadi sasa bado taka hizo zinaendelea kuwepo.

Katika hatua nyingine Mpanda Redio fm ilifika katika ofisi za mtendaji wa kata hiyo nakuambiwa afisa huyo yupo kwenye kikao hivi karibuni manispaa ya mpanda ilinunua gari kwaajili ya kusaidia ubebaji wa taka ndani ya manispaa.
Source:Paul Mathias

MIUNDO MBINU MIBOVU IMEKUWA KERO SOKO LA MISUFINI KWA WAFANYABIASHARA



Baadhi ya Wafanyabiashara  wa Soko la Misufini mtaa wa Rungwa kata ya kazima mkoani Katavi wamebainisha changamoto wanazokabiliana nazo baada ya kufanya biashara katika soko hilo kwa takribani miezi miwili sasa.

Wakizungumza na Mpanda Radio wafanyabiashara hao wamesema kumekuwa na changomoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchafu,miundombinu na baadhi ya wafanyabiashara waliokaidi kuhamia sehemu elekezi.

Mwenyekiti wa soko hilo Bi Neema Rashid amesema changanoto hizo wameshazifikiisha kwa wahusika wanacho subiri ni utekelezaji na kuwaomba wafanyabiashara kufanya kazi kwa ushirikiano ili kudumisha biashara zao.

Soko la misufini linajumuisha wafanyabiashara wadogowadogo wanaouza nyanya,mahindi, viazi, ndizi,mchele, na bidhaa nyinginezo.
CHANZO:Ester Baraka

Monday, 23 April 2018

WASAFIRI KUTOKA MPANDA KWENDA TABORA KUTUMIA NJIA MBADALA



Mwenyekiti wa Kamati  ya miundombinu Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa  jimbo la Mpanda vijijini Sulemani Kakoso amewataka wasafiri wanaosafiri kutoka Mpanda kwenda Tabora kutumia njia ya Treni mpaka barabara itakapotengenezwa.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Mpanda Radio leo kupitia kipindi cha Kumekucha Tanzania na kusema kuwa tayari wameshazungumza na meneja wa shirika la Reli ili waweze kuongeza behewa litakaloweza kupunguza adha ya usafiri.
Insert.kakoso

Aidha Kakoso amesema serikali imejipanga kufanya matengenezo ya dharura katika barabara zote nchini ambazo zimeharibiwa na mvua inayoendelea kunyesha .

Tarehe 14 mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Raphael Mhuga aliagiza barabara ya Mpanda –Tabora kufungwa kutokana na mvua iliyoharibu barabara hiyo
chanzo:Rebecca kija

BIASHARA HATARINI SOKO LA BUZOGWE



Wafanyabiashara wa soko la Buzogwe katika Halmashauri ya Manipaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba  Halmashauri kuweka huduma ya maji na umeme katika soko hilo ili kunusuru biashara zao.

Akizungumza na Mpanda Radio mwenyekiti wa soko hilo  Ramadhani Athumani amesema kitendo cha kutokuwa na umeme katika soko hilo kinafanya biashara ziwe hatarini kwani wezi wanaweza wakaiba kwa urahisi kutokana na usalama kuwa mdogo

Aidha ameiomba Halmashauri kuliangalia swala hilo kwa haraka kwani walinzi wanatumia tochi kulinda wakati wa usiku hali ambayo huatarisha mali za wafanyabiashara katika soko hilo.

Katika hatua nyingine ameishukuru halimashauri kwa kujenga choo lakini ameiomba kuboresha huduma ya maji ili madhara ya magonjwa ya mlipuko yasiweze kutokea soko hapo.
chanzo:rebecca

MPANDA REDIO IMECHOCHEA MAENDELEO KATAVI




Wakazi wa kata ya Kapalala Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wamesema,kituo cha Matangazo cha Mpanda Radio kimechochea maendeleo kwa kiasi kikubwa kutokana na kutangaza habari na vipindi vinavyoigusa jamii.
Wakizungumza na Mpanda Radio kwa Nyakati tofauti wakazi hao wamesema,jamii imekuwa na uelewa wa mambo mengi yanayolenga katika sekta ya afya,kilimo,elimu,usafiri pamoja  na miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara.

Kwa upande wake Daud Peter Nyasio ambaye ni mwenyekiti wa kijiji katika kata hiyo ameishukuru Mpanda Radio kwa jinsi inavyofikisha ujumbe kwa wananchi huku akisema usikivu mzuri umesaidia wananchi kuelimika kwa kiasi kikubwa.

Kituo cha kijamii cha Mpanda Radio kinachopatikana eneo la Mtaa wa Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,kilianza kurusha matangazo yake mwaka 2013.
Chanzo:Isaack

Friday, 20 April 2018

ADHA YA MAJI YAWASUGU



Wakazi wa kijiji cha Mtakuja kilichopo Kata ya Kapalala wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,wameitaka serikali kushughulikia miundombinu ya huduma ya maji kijijini hapo ili waondokane na adha ya ukosefu wa maji safi na salama.

Wengi wanazishutumu mamlaka kushindwa kuwajika kwa kuchukua hatua za haraka badala yake zimekuwa zikitolewa ahadi zisizo tekelezeka.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Daud Peter Nyasio amekiri kuwepo kwa kero  ya maji katika kijiji hicho na kueleza kuwa visima viwili vilivyopo haviwezi kutosheleza idadi ya wananchi ambao idadi yao ni zaidi ya elfu tatu.

Hata hivyo Reward Sichone ambaye Diwani wa Kata ya Kapalala inayojumuisha vijiji vya Mtakuja,Songambele na Kapalala amesema  kuwa hana jambo lolote la kuzungumza kuhusu suala la maji katika kata ya Kapalala kwani kila wanapoomba pesa serikalini hazitolewi kama inavyotakiwa.

Chanzo Issack Gerald

ACT WAZALENDO KATAVI WATOA MSIMAMO



Chama cha ACT-Wazalendo mkoani Katavi kimefanya maazimio ili kuishinikiza serikali kuchukua hatua stahiki juu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi inayo wakabili  wananchi katika maeneo mbali mbali mkoani Katavi.

Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Katavi Joseph Mona amewaambina wanahabari kuwa shabaha ya kikao hicho ilikuwa ni kufanya tahimini ya namna ambavyo serikali ya mkoa inavyo shughurikia kero hizo.

Mara kadhaa Chama hicho kimetaja waziwazi kuwa kero hizo zimetokana na kutwaliwa na serikali kwa baadhi ya maeneo yaliyokuwa makazi ya wananchi kwa kile kinacho daiwa kuwa ni maeneo yaliyo katika hifadhi za misitu.

Katika hatua nyingine Mona ameyataja baadhi ya mapendekezo yatakayo wezesha kufikia hatima ya migogoro hiyo kuwa ni pamoja na Serikali kutumia njia shirikishi kabla ya kufanya maamuzi sanjari na utekelezaji wake utakao kwenda sambamba na  kuheshimu misingi ya kisheria.

Mwaka 2017 mwezi agost mamia ya wananchi katika vijiji vya Mgorokani, kata ya Stalike,  na Kijiji cha Nsambwe Kata ya Kanoge waliondolewa kinguvu katika makazi yao kwa madai ya kukaidi maagizo ya serikali yaliyokuwa yakiwataka kuhama katika vijiji hivyo kwa madai ya kuwa ni hifadhi za misitu.
Chanzo: Alinanuswe Edward

Wednesday, 18 April 2018

UHAKIKI WA TIN NAMBA KATAVI




Mamlaka ya kukusanya Mapato TRA katika Mkoa wa Katavi imeanza zoezi la kuhakiki namba za utambuzi wa kwa wafanyabiashara zinazojulikana kama Tini Namba

Akizungumza na Mpanda redio ofisini kwake Meneja wa TRA mkoa Enos Mgimba amesema zaidi ya wafanyabiashara Elfu nne wanatarajia kufanyiwa uhakiki huo katika mkoa na kwa sasa zoezi hili limeanza hapa Manispaa na baadae litahamia katika maeneo mengine ya mkoa

Aidha Mgimba amebainisha kuwa faida ya utambuzi wa tini namba kwa wafanyabiashara huwasaidia wao kama mamlaka kuwa na taarifa sahihi za wafanyabiashara hali ambayo huwasaidia katika kukusanya mapato pamoja na kuwasaidia wateja wao panapotokea shida mbalimbali za kibiashara

Ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kufika katika ofisi hizo kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki wa Tini namba za biashara zoezi hilo limeanza leo 18/4/2018 na linatalajia kukamilika tarehe 27/4/2018

Chanzo:Paul Mathius

Tuesday, 17 April 2018

USHAURI KWA KULIMA


Wakulima mkoani Katavi wameshauriwa kulima kilimo kinazichozingatia utalaamu wa kilimo hali itakayo saidia  kuhifadhi ardhi yenye rutuba.

Ushauri huo umetolewa na mtaalamu wa kilimo Ramadhani Athumani wakati akizungumza na mpanda redio kwa njia ya simu kuhusu namna bora ya kutunza ardhi kwajili nya kilimo.

Kwa upande wa baadhi ya wakulima mkoani Katavi wamesema wengi hushindwa kuzingatia kilimo bora kutokana na ukosefu wa elimu kutoka kwa watalaamu hao na kuwaomba kutoa elimu Zaidi kwajili kuendelea kuhifadhi ardhi  inayotegemewa na watanzania wengi.

Kwa takriban miaka 1960 nchi imekuwa ikijinasibu na uchumi unaotegemea kilimo ambapo  zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wanajihusisha na kilimo au biashara inayotokana na kilimo.
 Source:Ester Baraka

TAHADHARI YA ZIMA MOTO

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuondoka katika maeneo hatarishi katika kipindi hiki cha mvua ili kujinusuru  na majanga yanayoweza kujitokeza.

Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa katavi Abdalha Maundu wakati akizungumza na Mpanda Redio na kusema kuwa wananchi waliopokatika maeneo ya bondeni au yanayoweza kukumbwa na mafuriko wanatakiwa kuondoka ili kujikinga na majanga  mbalimbali yanayoweza kutokea.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi ambao hawajui jinsi ya kutumia vifaa vya kuzimia moto na uokoaji wafike katika ofisi zao ili waweze kupewa elimu itakayowasaidia kutumia vifaa vya kujikinga na majanga.

Jeshi la zima moto na uokoaji  lina majukumu mbalimbali  ikiwemo kuzima moto na  kuokoa maisha na mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengineyo.

Chanzo:Rebecca 

Monday, 16 April 2018

KIBOKO AWATISHIO KWA WANANCHI


Wakazi na  wakulima wa eneo la Mpanda Hoteli  Kata ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameiomba mamalaka ya maliasili kuondoa viboko walio jirani na makaz yao kutokana na kutishia maisha
Wakizungumza na Mpanda radio wananchi hao wamesema kuwa wanahofia zaidi  maisha yao baada ya viboko hao kuvamia eneo la mto Mpanda
Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda maiko znyungu ameahidi kulishulikia suala hilo kwa kuwasiliana na mamalaka ya maliasili
Kuzagaa kwa wanyama hao hali imetajwa kuwa ni kuendelea kunyesha kwa mvua za masika  huku wanyama hao wengine wakitajwa kusombwa na maji
 CHANZO:Ezelina Yuda

SAKATA LA WATUMISHI HEWA LAACHA MAPENGO MAPANDA



Wito umetolewa kwa watumishi katika sekta mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kujituma katika kazi zao ili wananchi waweze kupata huduma.

Ameyasema hayo mkurugenzi wa manispa ya Mpanda Michael Nzyungu wakati akizungumza na Mpanda Redio kwa njia ya simu kuhusu mapungufu ya watumishi katika halmashauri baada ya sakata la watumishi hewa ambalo limeathiri sekta mbalimbali za kiutendaji hapa nchini zikiwepo Afya ,elimu,utawala.

Aidha amesema kuwa swala la watumishi hewa halijaathiri Halmashauri japo kuwa kuna mapungufu ya kudumu kwa watumishi katika sekta mbalimbali.

Serikali kupitia kwa wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika April 9 mwaka huu Bungeni imeagiza kurudishwa kazini kwa watumishi wote wa Umma waliofukuzwa kimakosa ikiwemo wale walioishia darasa la saba.
CHANZO:Rebecca Kija

MVUA ZAKWAMISHA WASAFIRI



Baadhi ya wafanyabiashara wa usafirishaji abiria mjini Mpanda wamelazimika  kusitisha huduma kutokana na ubovu wa miundombinu.

Mpanda Radio imefika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani mjini Mpanda na kuzungumza na baadhi ya wahudumu wa kampuni za usafirishaji ambazo zinatumia barabara ya mpanda-tabora.

Kwa sasa magari yaliyokuwa yakitumia barabara hiyo yameamriwa kutumia barabara ya Mpanda-Kigoma ambapo wafanyabiashara hao wamesema kuwa wanalazimika kuongeza nauli kwa shilingi elfu kumi hadi elfu kumi na tano kwa kila safari kwa kuwa umbali wa safari umeongezeka

Hata hivyo wamesema kuwa barabara mbadala ya kupitia uvinza nayo haipo kwenye hali nzuri kitendo kinachosababisha ugumu wa safari.

Mwishoni mwa wiki iliyopita mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Muhuga alitangaza kufungwa kwa barabara ya Mpanda-Tabora baada ya barabara hiyo kujaa maji

Chanzo:Haruna juma

MVUA YAZIDI KUHARIBU MIUNDOMBINU MPANDA


Wananchi wa mtaa wa  Airtel katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wameiomba Serikali kuwasaidia kuboresha daraja ambalo limekuwa likijaa maji katika kipindi cha mvua

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio na kusema kuwa daraja hilo limesombwa na kujaa maji na kusababisha wananchi kushindwa kuvuka na wengine kusombwa na maji hayo.

Hivi  karibuni wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA mkoani Katavi  imesema kuwa upo mpango wa kukarabati barabara na madaraja yote ya mijini na vijijini ili kupunguza ubovu wa miundombinu.

Tatizo la miundombinu maeneo mengi mkoani Katavi kipindi cha masika limekuwa kikwazo  kwa wananchi kushindwa kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Chanzo:Restuta Nyondo

Sunday, 15 April 2018

DIWANI KATA YA MWAMKULU AOMBA TARURA KUNUSURU MIUNDOMBINU ILIYOZINGIRWA NA MAJI


Diwani wa Kata ya Mwamkulu Kalipi  Katani amesema kata yake ipo katika hatari kubwa ya kimundombinu kutokana na barabara inayounganisha kata hiyo na maeneo mengine kuzongwa na mafuriko.
Akizungumza na Mpanda Radio Katani amesema adha hiyo imetokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kwamba sasa wananchi wanaendelea kuathirika na hali hiyo.
Katika hatua nyingine amesema baadhi ya makazi yameharibiwa na watu wawili wamepata majeraha baada ya kuangukiwa na nyumba.
Hata hivyo ameiomba mamlaka ya wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA Kuchukua Hatu za matengenezo ya barabara hiyo.
Kata Ya Mwamkulu ni miongoni mwa kata zinzoongoza kwa uzalishaji wa mpunga mkoani Katavi


MATUKIO KATIKA PICHA MKUU WA MKOA WA KATAVI AKISIKILIZA KERO ZA WANANCHI WAKE

Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga Akisikiliza kero za wananchi waliojitokea katika Viwanja Vya Azimio Manispaa Ya Mpanda Mkoani Kata
 Mwananchi akimimina Kero zake za kudhurumiwa na kuteelekezwa na mumewe Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi 
 Mama Mwenye ulemavu akiomba eneo la hifadhi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ambapo ameahidiwa kupewa Kiwanja 
Umati wa wananchi waliojitokeza kuwasilisha Kero zao kwa Mkuu wa Mkoa ambapo asilimia kubwa ili kuwa ni kero za Ardhi

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZAFUNGA BARA BARA YA TABORA-KATAVI


Eneo la mto Koga Lilivyo kufuatia mvua za masika zinazoendela kunyesha hali iliyosababisha  bara bara ya Tabora Katavi kufungwa 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amesema barabara ya Mpanda–Tabora imefungwa kwa muda usiojulikana kuanzia  Aprili 14,2018.

Muhuga ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara unaofanyika katika uwanja wa Azimio mjini Mpanda kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi ambapo hata hivyo mkutano huo umeahirishwa baada ya mvua kunyesha na kupangwa kuitishwa baadaye ili kujibu malalamiko ya wananchi.

Muhuga amesema barabara hiyo imefungwa baada ya maji kujaa barabarani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na hivyo kuhatarisha maisha ya wasafiri.

Kwa upande wake mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi Amani Mwakalebela amesem kutokana na barabara kuharibika kwa kiasi kikubwa,wenye mabasi watalazimika kusafirisha abiria kupitia mkoani Kigoma au Mbeya.

Mwaka 2016 barabara ya Mpanda – Tabora ilifungwa baada ya kukatika kwa daraja la mto Koga ambapo karibu watu kumi walipoteza maisha baada ya gari kusombwa na maji.

Chanzo:Issack Gerald

Friday, 13 April 2018

KINACHOKWAMISHA KUMAMILIKA KWA MIUNDOMBINU NI ULIPWAJI WA MADENI-MRATIBU TARURA KATAVI


                   Mratibu wa Tarura Mkoa Katavi Zuberi Kilenza

Wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA mkoani Katavi imesema kinachokwamisha baadhi ya barabara  za maeneo mbalimbali kukamilika ni kutokana na kutumia fedha za bajeti kulipa madeni.

Akizungumza na Mpanda Radio  mratibu wa Tarura Mkoa Zuberi Kilenza amesema baada ya kulipa mdeni hayo zimebaki shilingi Bilioni mbili na milioni mia tatu kwa ajili ya matengenezo  ya kawaida ya muda maalumu ,madaraja ,makaravati na mifereji.

Kilenza amesema kuna mikataba kumi na moja  kwenye halmashauri tano za mkoa wa Katavi ambapo wakandarasi wanaendelea na utengenezaji wa barabara hizo.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa hivi karibuni unaonyesha kila mwaka  ni wastani wa asilimia 30 pekee za barabara za Mjini na vijijini  ndizo hukamilika
Chanzo:Ester Baraka



 

EKARI 2000 TUMEWATENGEA WAFUGAJI WILAYAN TANGANYIKA-DC MUHANDO


Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi imetanga zaidi ya ekari elfu mbili kwa ajili ya wafugaji waliopo katika eneo la Luhafwe katika kata ya Tongwe.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Salehe Mbwana  Muhando wakati akizungumza na wafugaji wa eneo hilo amesema serikali kwa kushirikiana na uongozi wa Halmashauri imetenga eneo la malisho ili kuepusha usumbufu kwa wafugaji kuhamahama kwa ajili ya kutafuta malisho ya mifugo yao

Aidha Mhando amewaagiza maafisa kilimo na ufugaji wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa  eneo la luhafwe  kufanya sensa ya utambuzi wa mifugo katika eneo hilo ili kuwa na idadi kamili ya mifugo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wafugaji wilaya ya Tanganyika Mussa Kabushi amewaomba wafugaji kuanzisha umoja utakao sajiliwa kisheria ili kurahisisha utatuzi wa changamoto kwa wafugaji.

Chanzo:Paul Mathius 

VIONGOZI IGENI MFANO WA SOKOINE-WANANCHI KATAVI


Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi wamewashauri viongozi wa serikali wa serikali ya awamu ya tano kuenzi kifo cha Wazairi Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine kwa kupeleka huduma muhimu za kijamii kwa wananchi ikiwemo maji.

Wakazi hao wametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na Mpanda Radio kuhusu kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo cha waziri mkuu hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki Apriki 12,1984.

Aidha wamesema ni kiongozi aliyechukia uhujumu uchumi,rushwa,ufisadi huku akishiriki vema kuandaa majeshi wakatio wa vita vya Kagera baina ya Tanzania na Uganda mwaka 1978.

Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili Februaei 13 mwaka 1977 hadi Novemba 7 mwaka 1980 na  Februari 24 mwaka 1983 hadi kifo chake kwa ajali ya gari Mkoani Morogoro akitokea Bungeni Dodoma kuelekea Jijini Dar es salaam.
Chanzo:Isack Gerald

WANAKATAVI MSIOGOPE KUIBUA KERO ZINAZOWAHUSU APRILI 14 MBELE YA MKUU WA MKOA -MUYA



Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kutoogopa kutoa kero zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa lengo la kuleta maendeleo ya mkoa kwa ujumla.

Afisa Tawala mkoa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya malalamiko mkoa David Muya ametoa ufafanuzi wakati akizungumza na mpanda redio kuhusu utaratibu wa kupokea kero mbalimbali  zinazowakabili wananchi

Muya  amewatoa wasiwasi wananchi kua kila atakeyifika atasikilizwa na kero zake kutatuliwa kwa wakati kutokana na madawati maalumu ya wasimamizi  kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga anatarajia kusikiliza kero za wananchi april 14 mwaka 2018  siku ya Jumamosi  katika viwanja vya Azimio.

Chanzo:Allynanuswe Edward

KATA YA KAKESE YAANZA UTEKELEZAJI WA ASILIMIA 10 KWA MAKUNDI MAALUM


Kata ya Kakese iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imetekeleza mpango wa ugawaji wa asilimia kumi kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Akizungumza na Mpanda Fm kwa njia ya simu afisa Mtendaji kata ya Kakese Lauben Kasomo amesema mapaka sasa shilingi milioni mbili zimetolewa kwa vikundi viwili vya wanawake .

Katika hatua nyingine amebainisha uwepo wa hamasa kubwa miongoni mwa wananchi katika kuunda vikundi kama inavyo takiwa na serikali kwamba ili kurahisisha utoaji huduma kwa jamii kwa njia ya vikundi.

Aidha ameongezea kuwa swala la ugawaji mikopo katika vikundi hivyo limekumbwa na changamoto nyingi ikiwemo bajeti kutokidhi mahitaji hasa kutokana na ongezeko la watu.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Mkaguzi mkuu wa wa hesabau za serikali Prof Juma Assad amezionya halmashauri kuacha kususua katika kutekeleza utoaji wa asilimia kumi kwa makundi ya vijana na wanawake.

Chanzo:Ezelina Yuda

Wednesday, 11 April 2018

FURSA YA KUWAHOJI VIONGOZI KUMETUSAIDI KUPATA MAENDELEO -WANANCHI KATISUNGA


Wakazi  wa kijiji cha Katsunga Machimboni Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wamesema wanapata fursa ya kuwahoji viongozi wao juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo katika kijiji hicho.

Mpanda Redio imefika kijijini hapo ambapo wakazi hao wamebainisha kufika kwa viongozi wao mara kadhaa na kuwauliza kuhusu upatikanaji wa maji,zahanati  na umeme.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Lukas Kumpamba amesema wanapokea maoni ya wananchi kupitia sanduku la maoni na mikutano mbalimbali ya hadhara ambapo kwa sasa wako katika ufumbuzi wa changamoto ya zahanati.

Kijiji cha Katisunga Machimboni kina jumla ya wakazi 6000 kwa mujibu wa sensa iliyofanyika hivi karibuni kijijini hapo.

Chanzo:Ester Baraka

Tuesday, 10 April 2018

HUBA MIAKA 20 JELA KWA KUMILIKI RISASI ZA BUNDUKI YA KIVITA


Hatimaye Mahakama ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu kwenda jela miaka 20 Bw.Kigalu Huba Mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa kijiji cha Kambuzi wilayani Mpanda Mkoani Katavi kosa la kukutwa na risasi 12 za silaha AK-47 ya kivita.

Hakimu mkazi wa mahakama  hiyo Mh.Chiganga Tengwa amesema ametoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Awali upande wa Jamhuri ambayo ni serikali wamesema Machi 19,2018 mtuhumiwa alikutwa na risasi 12 kinyume na kifungu cha sheria namba 7 ya mwaka 2015 kinachohusu umiliki wa silaha ambapo waliiomba itolewwe adhabu kali kwa mtuhumiwa ili kuwa funzo kwa wengine kwa kuwa amekuwa tishio kwa wananchi.
Kwa upande wake Bw.Huba katika utetezi wake ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa madai kuwa anategewa na mke na watoto watatu na asipopunguziwa adhabau familia yake itaathirika.

Kufuatia utetezi huo baad aya mahakama kujirisha bila shaka kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo hakimu Mh.Tengwa kwa kuzingatia kifungu cha 235(1) ya mwenendo ya makosa jinai sheria namba 20 ya mwaka 20102 amemhukumu kwenda jela miaka 20 kuanzia Aprili 10,2018.

Hata hivyo mtuhumiwa anaruhusiwa kukata rufaa ikiwapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa dhidi yake
Chanzo:Isack Gerald

MABEHEWA MANNE YA TRENI YA MIZIGO YAANGUKA ENEO LA SHANKALA MKOANI KATAVI


Mabehewa manne ya Treni ya mizigo iliyokuwa inatoka Katavi kuelekea Tabora yameacha njia na kuanguka katika eneo la Shankala mkoani Katavi.

Afisa Uhusiano Shirika la Reli Mohamed Mapondela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo nakusema hakuna mtu aliyejeruhiwa wala uharibifu wa mali na kinachoendelea sasa ni kutoa mizigo na kuweka sawa njia ya treni ili safari iendelee.

Hata hivyo Bwana Mapondela hakueleza sababu haswa zilizosababisha ajali hiyo lakini hii inaweza ikawa imechangiwa na uchakavu wa njia hiyo ya treni

Reli hiyo inayotajwa kuwa ni miongoni mwa reli kongwe zilizojengwa nchini miongo kadhaa iliyopita

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...