Wednesday, 30 May 2018

HATIMAYE BARABARA YA MPANDA ---TABORA YAFUNGULIWA



Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ametangaza kufunguliwa rasimi kwa barabara kuu ya Mpanda kwenda Tabora kuanzia leo.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya udhibiti wa nchi kavu na majini SUMATRA Bw Aman  Mwakalebela ambaye amefafanua kuwa hali ya barabara hiyo kwa sasa ni shwari na kwamba inaruhusu magari kupita.

Katika hatua nyingine ametoa rai kwa abiria  walio toa nauli ya mzunguko wa barabara kudai kurejeshewa kiasi cha  nauri itakayo endana na barabara ya Mpanda Tabora.

Mnamo 14/04 /2018 Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerari Mstaafu Rapahael Muhuga aliifunga barabara hiyo kutokana na kujaa maji katika dalaja la mto koga.

Chanzo:Alinanuswe Edward

WAKULIMA WA TUMBAKU WATAKIWA KUZINGATIA SERA YA KATA MTI PANDA



Wakulima wa zao la tumbaku Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wametakiwa kuzingatia sera ya kata mti panda mti ili waweze kuepukana na tatizo la uharibifu wa mazingira.

Akizungumza na mpanda radio kaimu meneja wa chama cha wakulima wa tumbaku mpanda kati Marietha John amesema kila mwaka wakulima  kabla ya kulima zao hilo lazima aonyeshe miti aliopanda.
        
Mwenyekiti wa chama hicho Sospita Silivatory ameiomba selikali kutenga eneo kwaajili ya  wafugaji ili kuepusha mifugo hiyo kuharibu  miti walio panda wakulima hao.
          
Kuelekea wiki ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo hufanyika kila mwaka jun 5 na kaulimbiu ya mwaka huu ikiwa ni mkaa gharama tumia nishati mbadala
Chanzo: Neema Husein

TASAF YALETA MAENDELEO KWA WANUFAIKA



Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando amewapongeza wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini Tasaf  kwa kuanzisha miradi mbali mbali ya maendeleo katika kata ya kabungu kwani itasaidia kukua kiuchumi.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua miradi hiyo ambayo inatekelezwa na wanufaika wa Tasaf iliyopo katika kata hiyo ikiwemo shamba la miti  aina ya mitiki na visima vitatu.
       
Kwa upande wao wanufaika wa miradi hiyo wamesema kuwa fedha ambazo wamekuwa wakipata zimewasaidia kuendesha maisha yao na kuendelea kiuchumi.

Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya alitembelea na kukagua miradi ya Tasaf katika kijiji cha kabungu,mchaka mchaka,vikonge na Igalula.

Mpango wa kunusuru kaya maskini ni mmoja ya mipango ya kitaifa unaotekelezawa nchini ukiwa na lengo la kuziwezesha kaya maskini ili kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu ya kibinaadamu kama vile chakula, afya na elimu.
Chanzo: Restuta

WAKULIMA WALIA NA BEI YA MAZAO



Wakulima katika kata ya kakese halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamelalamikia kudolora kwa bei ya mazao ya chakula hali ambayo haiwasaidii kujikwamua kutoka Kwenye dimbwi  la umaskini.

Wakizungumza na mpanda Redio wamesema inawalazimu kuuza kiasi kikubwa cha mazao ilikujikimu kuendesha maisha yao na kupelekea kushidwa kujenga nyumba bora kutokana na bei ghari ya bidhaa za ujenzi zinavyo uzwa madukani kutokana na bei ndogo ya mazao.

Kwa upande wake diwani wa kata ya kakese Maganga Salaganda  amesema changamoto hiyo ipo na kuiomba serikali kuandaa utaratibu wa masoko na kuruhusu mazao kuuzwa nje ya nchi ilikuwa kuwakomboa wakulima.

Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Mikoa hapa nchini inayo tajwa kwa kuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa mazao ya chakula kama vile Mpunga mahindi na karanga. 
Chanzo: Paul Mathius


UCHUNGUZI KUFANYIKA UJENZI MAABARA SHULE ZA SEKONDARI MPANDA



Baraza maalumu la madiwani katika halmashauri ya wilaya yam panda mkoani katavi wameazimia kuundwa kwa timu ya uchunguzi ili kuchunguza ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.

Maazimo hayo yamekuja baada baraza hilo kubaini kuwepo kwa kasoro katika ujenzi wa maabara hizo na kuwepo kwa ongezeko la gharama tofauti na zilizokuwepo kwenye mikataba ya awali.

Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando ameitaka timu hiyo kufanya utekelezaji wa haraka ili ujenzi huo uweze kukamilika na ameiagiza mamlaka ya Takukuru na vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi na ikibainika kuna ubadhilifu wa fedha hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika.

Shule ambazo timu hiyo itapita kukagua na kujiridhisha na ujenzi majengo ya maabara ni sekondari ya kalema,ikola,kabungu,mwese,katuma na mpanda ndogo.
CHANZO:Rebecca Kija

UJENZI HOSPITALI YA RUFAA KATAVI



Serikali ya Mkoa wa Katavi na Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa SUMA JKT wamesaini mkataba kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ghorofa moja la hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Katavi.

Kaimu katibu tawala Bw.Wilbrod Malandu akizungumza wakati wa kutiliana saini hiyo ofisini kwake,amesema Bodi ya Zabuni imemtunuku zabuni SUMA JKT kutekeleza ujenzi wa ghorofa hilo kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 9 na milioni 798.76 ambapo ghorofa hilo litakuwa na vitanda 76 kwa safu ya chini na 71 kwa safu ya juu.

Aidha Malandu amesema eneo la ujenzi wa Hospitali hiyo lenye ukubwa wa ekari 243 linapatikana Kata ya Kazima ambapo zaidi ya shilingi milioni 468 zimetumika kuwalipa fidia watu 108 ili kupisha ujenzi .

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa SUMA JKT Kanali Andrew Mkinga pamoja na kuipongeza serikali ya mkoa wa Katavi kwa kumpatia zabuni hiyo,ameahidi kujenga kwa weledi na kukamilisha kazi kwa wakati uliopangwa.

Mkoa wa Katavi ulianza Mpango wa ujenzi wa hospitali ya Rufaa tangu mwaka 2014 ambapo katika eneo la ujenzi kunatarajia kuwemo vitengo mbalimbali vikiwemo Chuo cha sayansi na tiba,chuo cha uuguzi na utafiti pamoja na shule,maduka,hotel, stendi ya mabasi na viwanja vya michezo.
CHANZO:Issack Gerald

WAKULIMA WA TUMBAKU KUACHA UDANGANYIFU



Wakulima zao la Tumbaku katika mkoa wa Katavi wameaswa kuacha Tabia ya kuchanganya Tumbaku chafu maalufu kama Ngulai kwenye msimu huu wa masoko ya zao hilo unaoendelea sehemu mbali za mkoa kwa wakulima wa zao hilo.

Wito huo umetolewa na mwakilishi wa Kampuni ya Premiumu Tanzania katika mkoa wa katavi bwana Iddy Ramadhani wakati akizungumza na mpanda redio kuhusu mwenendo wa masoko yanayo endelea katika maeneo ya mkoa.

Aidha Ramadhani amesema katika msimu huu wa kilimo 2017/2018 kampuni hiyo inatalajia kununua zaidi ya kilo millioni sita za tumbaku kutoka katika vyama vya msingi vya wakulima wa Tumbaku vilivyopo katika mko wa katavi

Katika siku za hivi karibuni zao la tumbaku limekuwa likipigwa vita kutokana na changamoto ya uhalibifu wa mazingira katika kuzalishwa kwake na sasa kunampango maalumu unaotekelezwa na serikali kwa kuanzisha kilimo cha mazao mengine kama vile pamba, kolosho na alizeti.

CHANZO:Paul Mathius

Wednesday, 23 May 2018

WANANCHI WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA ILI KUBAINI WASIO WATANZANIA KATAVI



Afisa uhamiaji wa Mkoa wa Katavi  Vicent Haule amewataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo katika kuwafichua wananchi ambao sio watanzania maarufu kama wahamiaji haramu .

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Mpanda Radio ofisini kwake nakusema kuwa njia ambazo wanazitumia katika kuwabaini wahamiaji zimesaidia kupunguza ongezeko la wahamiaji hao .

Aidha Haule ameongeza kwa kutaja kazi za jeshi hilo na malengo yake ikiwa ni pamoja na kuimarisha mipaka ili kudhibiti wahamiaji haramu.

Pia amesema kuwa ulinzi na usalama ni jukumu la kila mwananchi hivyo wanapaswa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kupata msaada wa haraka.
CHANZO:Furaha Kimondo

BARABARA ZA KWAMISHA SHUGHULI ZA MAENDELEO



Wakazi wa kijiji cha Ilebula  wilayani Tanganyika mkoani Katavi wanakwama kufanya shughuli za maendeleo kutokana na ubovu wa miundombinu.

Wamebainisha hayo wakati  Wakizungumza na Mpanda Redio na kusema   wamekuwa wakiahidiwa na viongozi mbalimabli juu ya uboreshaji wa miundombinu ambapo mpaka sasa adha hiyo inaendelea.

Mbunge wa Mapanda Vijijini Suleiman Kakoso amesema serikali inaendelea na jitihada za kuboreshsa miundombinu ambapo kuna matengenezo ya barabara yanafanyika kutoka Kalilankulunkulu kwenda Kampanga na barabara hiyo itapita katika kijiji cha Ilebula.

Ubovu wa miundombinu mkoani katavi ni moja kati chamgamoto zinazosababisha kuzorota kwa uchumi

Itakumbukwa kuwa April 14 mwaka huu mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Msataafu Raphael Muhuga alitangaza kufungwa kwa barabara ya Mpanda-Tabora kutokana na barabara kujaa maji

CHANZO:Ester Baraka

Monday, 21 May 2018

ULINZI SHIRIKISHI WAANZA KWA KISHINDO KATA YA MISUNGHUMILO


Vikundi vya polisi jamii na ulinzi shirikishi katika kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi vimeanza kushiriki katika ulinzi na usalama baada ya kusitisha kwa muda mrefu.

Hatua hiyo imethibitishwa na Afisa mtendaji wa kata ya Misunkumilo Bw.Januari Kayungilo katika Mazungumzo maalumu na Mpanda Radio kuhusu namna wanavyoendesha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Awali Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alikuwa ameiambia Mpanda Radio kuwa hana taarifa za polisi kutoshiriki ulinzi na usalama katika kata ya misunkumilo nyakati za usiku ambapo amelazimika kuingilia kati na hatimaye kuitishwa mkutano ambao umerejesha ushirikiano kati ya Polisi,wananchi na viongozi.

Kata ya Misunkumilo yenye mitaa ya Misunkumilo,Mtemi Beda,Kampuni na kijiji cha Milala ina wakazi zaidi ya Elfu kumi.

RUZUKU KWA SHULE ZA MSINGI ZATAJWA KUNUA KIWANGO CHA ELIMU


Mpango wa Serikali kusaidia Shule za Msingi kutoa Ruzuku zimekuwa zikisaidia kuendelea kutoa mchango mkubwa katika elimu.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya Walimu wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kuwa serikali imekuwa ikisaidia elimu ya shule za msingi kutoa ruzuku kwa wakati.

Aidha wamesema  changamoto  ya madarasa pamoja na upungufu wa walimu imekuwa inawapa ugumu   kujifunza kwa wanafunzi  na kuomba wazazi washikilikishwe katika suala la kuchangia michango ya ujenzi.

Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inasema  kuwa serikali itahakikisha Elimu ya msingi inakuwa ya lazima na ya bure kwenye shule za umma kwa kuzipatia ruzuku za kuziwezesha ili kutoa elimu bora.

CHANZO:Johar Secky     

TANESCO KATAVI YAJIDHATITI KUSAMBAZA UMEME VIJIJI 117


Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoani katavi limesema liko katika mipango ya mwisho katika ukamilishaji wa usambazaji wa umeme wa Rea awamu ya tatu
Katika mpango huo ambao umetajwa kuvifikia vijiji 117 unatarajiwa kuanza mara moja tu baada ya mkandarasi kupatikana
Akizungumza na Mpanda radio kwa njia ya simu Meneja Uhusiano na wateja Amon Maiko amebainisha kuwa kukamilika kwa mpango huo kutapunguza kero ya upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo mkoani hapa.
Hivi karibuni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaagiza Watendaji wa TANESCO Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Wizara ya Nishati, na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kabla ya Juni mwaka 2021 kuhakikisha kuwa zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wawe wameunganishwa na huduma ya umeme kufikia mwaka huo.
Chanzo:Ezelina Yuda 

KOFIA NGUMU ZAZUA KIZAA ZAA KWA ABIRIA MKOANI KATAVI



Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wameiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi juu ya uvaaji wa kofia ngumu pindi wanapotumia usafiri huo ili kujikinga na ajali za barabarani.

Wakizungumza na Mpanda redio kwa nyakati tofauti ambapo ni takribani wiki moja kupita baada ya agizo la kila dereva wa pikipiki kuwa na kofia mbili ili aweze kufanya kazi hiyo bila kufuatiliwa na askari wa usalama barabarani

Aidha wamesema abiria wanawakwamisha kwa kukataa kuvaa kofi hizo kwa kisingizo cha kuogopa kuambukizwa magonjwa kutokana na kutumiwa na watu wengi.

Hivi karibuni  jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Katavi lilitoa siku saba kwa kila dereva boda boda kuwa na kofia ngumu mbili.
Chanzo:Rebacca kija

WANANCHI MKOAN KATAVI WATAHADHARISHWA JUU YA UGONJWA WA EBOLA


Mganga Mkuu mkoani Katavi Dr Omary Sukari 

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa ebola  

Mganga mkuu wa mkoa wa katavi DK Omary Sukari ameimbia Mpanda radio kuwa kuna mikakati kadhaa ambayo wameiweka baada ya kupata taarifa za tishio la kuwepo kwa ugonjwa wa ebola katika nchi ya Kongo.

Dk Sukari amesema tayari wameshatoa elimu kwa njia ya vipeperushi katika eneo la Karema linalopakana na nchi ya Congo ambayo ni chimbuko la ugonjwa huo

Ugonjwa wa ebola uligundulika mwaka 1976 ambapo hadi kufikia mwaka 2014 takribani watu 1740 walipata maambukizi katika nchi za Afrika magharibi ikiwemo Liberia, Sierra Lione na Nigeria

Chanzo: Ester Baraka 

Friday, 18 May 2018

MADEREVA BODA BODA MPANDA WAWAJIA JUU TRAFIKI


Baadhi ya waendesha Bodaboda Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamekuwa wakiwalalamikia askali wa usalama barabarani kukamata pikipiki zao bila makosa.

Wakizungumza na Mpanda Radio wamebainasha  kwa mara kadhaa piki piki huchukuliwa kinguvu wakati mwingine zikiwa zimeegeshwa bila taarifa kwa mhusika.

Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Katavi  Wille Joasi Mwamasika amekanusha taarifa hizo akidai kuwa  kufanya hivyo ni kinyume cha sheria katika utendaji kazi wa kitengo cha usalama barabarani.

Idadi ya vijana wanao jiajiri kupitia udereva piki piki maarufu kama boda boda imekuwa ikiongezeka kila mwaka lakini ikikabiliwa na vikwazo lukuki kutoka taasisi mbali mbali za Serikali.

VUMBI LA VIWANDA VYA KARANGA LATAJWA KUWAAATHIRI WAKAZI MPADEKO


Wakazi wa Mtaa wa Mpadeko kata ya Mpanda hoteli iliyopo halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wamelalamikia uchafuzi wa mazingira unaotokana na viwanda vya karanga.

Wameyasema hayokwa nyakati tofauti  walipozungumza na Mpanda radio wameitaka serikali kubadili eneo la uendeshwaji wa viwanda ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza kiafya kufuatia vumbi kali wakati viwanda hivyo vikifanya kazi .

Kwa upande wake mmoja wa wamiliki wa viwanda hivyo amesema wanasubiri serikali kuwaonyesha maeneo mbadala yatakayo kuwa nje ya makazi ya watu.

Uwekezaji unaohimizwa sasa kwa kasi lazima uzingatie mahitaji ya sheria mbalimbali zilizopo kama Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, na Sheria ya Mipango miji ya mwaka 2007.


WANANCHI KATA YA MAKANYAGIO WAIJIA JUU TARURA


Wananchi wa Mtaa wa Makanyagio katika  Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameilalamikia mamlaka inayoshughulikia utengenezaji wa barabara za mjini na vijijini TARURA  kwa kushindwa kujenga karavati katika maeneo yao.

Wakizungumza  na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti tofauti kua ni mda mrefu sasa tangu watoe kivukio cha zamani lakini mamlaka iyo haikutoa mrejesho wowote kwa wakazi wa mtaa huo.

Aidha kwa upande wake maneja wa TARURA Manispaa ya Mpanda  Albart Kyando amekili kuwa katika mtaa huo hawakuweka kivukio kutokana sababu mbali mbali za kimikataba na Mkandarasi kwa kushindwa kuelewana.

Hata hivyo  meneja huyo amesema kuwa baada ya siku 14 tatizo la ukosefu wa kivuko hicho litakuwa limeshughulikiwa kwa kuwa wamesha tafuta mkandarasi mwingine wa kushughulikia tatazo hilo.

SHEKHE MKUU WA MKOA WA KATAVI AWAPA NENO WAISLAMU KATIKA KIPINDI HIKI CHA MWEZI WA RAMADHAN


Waislamu mkoani Katavi wameaswa kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kupata rehema ,msamaha na kujiepusha na moto.

Sheikh wa Mkoa  wa Katavi  Sheikh Ally  Husein  akizungumza na Mpanda Radio amesema waislamu hasa vijana wamekuwa wakikaidi kufunga kwa sababu mbalimbali.

Sheikh Husein amesema si jambo jema kwa muislamu kuacha kufunga mwezi mtukufu bila udhuru kwani  kufunga ni amri ya Mwenyezi Mungu.

Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni nguzo ya nne kati ya nguzo tano za dini ya kiislamu.

Thursday, 17 May 2018

WAKULIMA KAKESE MBUGANI WAIANGUKIA SERIKALI KUTOA ELIMU YA UHIFADHI MAZAO



Wakulima wa kata ya Kakese Mbugani Halmashauri ya manspaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu juu ya uhifadhi wa mazao ya nafaka.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio na kusema kuwa wengi wao hawana elimu hiyo hali inayosababiisha  kuendelea kuhifadhi mazao hayo kienyeji na kusababisa hasara.

Kwa upande wake mtendaji wa kata hiyo Felix Kalonga amesema kuwa elimu hutolewa katika mikutano ya hadhara lakini wananchi wengi wamekuwa hawahudhurii mikutano hiyo.

Kuhifadhi mazao ya nafaka  kupitia elimu itolewayo na wataalamu wa kilimo huwasaidia wakulima wengi kuepuka na uharibifu wa mazao hasa yanayokaa kwa muda mrefu.

KUSAJILI WAGENI KATIKA MAENEO MENGI KWATAJWA KUMALIZA MATUKIO YA KIHALIFU NDANI YA JAMII


Baadhi wananchi wa Mtaa wa Mpanda Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema Daftari la uandikishaji wa majina kwa wageni limeweza kupunguza uharifu katika mtaa huo.

Wakizungumza na Mpanda Redio Kwa nyakati tofauti tofauti wamesema  mpango wa serikali wa kuanzisha daftari la majina kwa wageni wanao hamia kutoka sehemu nyingine imekua ni silaha tosha kwa jamii nzima ya mtaa huo kwani wanapata nafasi ya kumjua kila mgeni anayehamia katika maeneo hayo.

Kwa upande wa Mwenyekiti  wa mtaa huo  Afredy Mtaita amesema kuwa kuanzishwa kwa daftari hilo kumesababisha  takwimu ya uharifu kupungua kwa kiasi kikubwa tofauti na mwaka jana.

Aidha   mwenyekiti huyo amesema kwamba  tayari wameshaunda  kamati ya ulinzi shirikishi kwa jamii itakayoweza kutokomeza uhalifu katika mtaa huo pia amewaomba wananchi wa mtaa huo kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake katika jamii.


JESHI LA POLISI TUPO TAYARI KUMALIZA MATUKIO YA KIHALIFU-KAMANDA NYANDA


Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema,hana taarifa za jeshi la polisi kutoshirikiana na serikali za mitaa katika kata ya Misunkumilo hasa nyakati za usiku kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama.

Kamanda Nyanda ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano na Mpanda Radio kufuatia taarifa za hivi karibuni kuwa kwa sasa ulinzi shirikishi haufanyiki katika kata ya Misunkumilo kutokana na ukosefu wa ushirikiano kati ya polisi,wananchi na viongozi.


Aidha Kamanda Nyanda ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu ili kuudhibiti kabla ya kusababisha madhara.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Misunkumilo Bw.Januari Kayungilo amekiri kuwepo ulinzi hafifu katika kata hiyo lakini amesema mikakati inapangwa ili kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika ulinzi ikiwemo kufanya mikutano ya hadhara ili kuwaelimisha wananchi.


Hivi karibuni,Mwenyekiti wa Mtaa wa Misunkumilo Bw.Katabi Jonas alikiri kutokuwepo kwa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi huku jeshi la polisi nalo likiwa limejiweka kando kwa sasa.

Vijana katika Manispaa ya Mpanda wafundwa


Vijana wametakiwa kuacha aibu na kuogopa kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara pale zinapojitokeza

Wakizungumza na Mpanda Radio baadhi ya vijana wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo mjini Mpanda wamesema hofu,kutojiamini na uoga ni baadhi ya sababu zinazowafanya vijana kujiweka nyuma

Kwa upande wake Bi Maimuna Omari ambaye ni msimamizi wa saluni ya kike mjini Mpanda amesema vijana wanatakiwa kujitengezea mazingira ya kuaminika katika jamii hivyo kuwa rahisi wao kukopesheka hata kwenye taasisi mbalimbali za kifedha

Vijana wanafikia zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini hivyo kama wataamua kuwekeza katika biashara mbalimbali kutainua pato la taifa na mtu mmoja mmoja

Wednesday, 16 May 2018

MAZOEA YATAJWA CHANZO CHA KUVUNJA NDOA NYINGI


Wananchi  wa Manispaa ya Mpanda  Mkoani Katavi wamesema hali ya kuzoeana katika ndoa ndio chanzo cha kuibuka kwa migogoro katika familia zao.

Wakizungumza na Mpanda Radio kwa nyakati tofauti wamesema kumekuwa  na matatizo  mbalimbali katika ndoa   hali inayosababisha migogoro katika familia ambayo inarudisha nyuma maendeleo kwa jumla

Aidha wamesema migogoro hiyo inaleta  maumivu  pande zote     kwani hakuna anaye msikiliza mwezi wake hali sababisha familia kutengana.

Katika jamii nyingi za kitanzania zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya migogoro ya kifamilia kutokana na sababau mbali mbali katika jamii.

MADAWATI YA JINSIA YAMESAIDIA KUPUNGUZA UKATILI NDANI YA JAMII-WANANCHI


Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameipongeza serikali kwa kuanzisha kitengo cha  Dawati la jinsia linalosaidia kutatua changamoto katika jamii husani maswala ya unyanyasaji.

Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti tofauti wamesema kumekuwepo na msaada mkubwa kwa  jamii na kuweza kutatua migogoro mbali mbali hasa ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili katiak familia.

Kwa upande wake Afisa wa kitengo cha dawati la jinsi katika jeshi la polisi  katika  Halmashauri ya manispaa ya  Mpanda Hawa amesema kuwa wanazidi kutoa elimu kwa jamii kuhusu maana ya Dawati la jinsia ili kupunguza vitendo vya kiukatili katika jamii.

Afisa huyo amesema Takwimu ya mwaka 2017 ya ukatili katika jamii kwa watoto ulikua mkubwa ukilinganishwa mwaka 2018 ambapo umeweza kupungua kwa kiasi kikubwa.


URASIMU WA AJIRA ZA BARA BARA WAWACHOSHA WAZAWA IKONDAMOYO

Wakazi  wa kijiji cha Ikondamoyo katika halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi wamelalamikia uwepo wa urasimu wa utoaji  ajira katika mradi wa ujenzi wa barabara unaoendelea katika eneo hilo.

Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti wamesema tangu tarehe moja mwezi huu kutangazwa kwa ajira mbali mbali ,  kumekuwa na utata kutokana na wageni kutoka sehemu nyingine kuhodhi ajira za wazawa.

 Mwenyekiti wa Kijiji  cha Ikondamoyo Bernad Yusuph  amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuahidi kulifuatilia suala hilo kwa wakati ili kulipatia ufumbuzi wa kina.

Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza miradi yoyote ya maendeleo inayo fanywa maeneo mbali mbali inchini kuhakikisha inawanufaisha wazawa wa eneo husika ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.

CHANZO:PAUL MATHIUS

WAFANYABIASHARA WA MCHELE MPANDA WATOBOA SIRI MCHELE KUSHUKA BEI


Baadhi ya wafanyabisahara wa Mchele katika Halmashauri ya Mnispaa ya Mpanda wamesema kubadilika haraka kwa bei ya mchele kunatokana na sababu mbalimbali ikiwemo mwingiliano wa wafanyabiashara kutoka nje ya mkoa wa Katavi.

Wafanyabiashara hao wamebainisha hali hiyo wakati wakizungumza na Mpanda Radio kuhusu hali ya biashara ya mchele.

Hata hivyo wamesema,wakati mwingine wafanyabiashara kutoka Kenya na Uganda hulazimika kuchukua mchele kutoka Mpanda kutokana na ubora asili wa mchele unaopatikana.

Kwa sasa bei ya mchele inatajwa kuwa kati ya shilingi 1000 mpaka 1400 kwa kilo.

SMG YAMTUPA JELA MIAKA 20, KIJANA MWENYE MIAKA 38



Mkazi wa kata ya Starike  Tarafa ya Nsimbo mkoani Katavi aliyefahamika kwa jina la Francis Aliseni Chapaulinge amehukumiwa miaka ishirini jela kwa kosa la kupatikana na silaha kinyume cha sheria.

Tukio hilo lilitokea tarehe 24 mwezi machi mwaka huu majira ya saa sita usiku ambapo mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 38 alikamatwa na bunduki moja aina ya SMG yenye namba 151614E na magazine moja isiyokuwa na risasi maeneo ya shambani kwake kijiji cha Matandalani.

Hukumu hiyo imetolewa tarehe 14 mwezi huu katika  Mahakama ya wilaya ya Mpanda mbele ya hakimu Chiganga Tengwa na Wakili wa serikali Hongera Malifimbo na mtuhumiwa kukiri kutenda  kosa hilo.

Kumiliki silaha  kinyume cha sheria ni kinyume  na kifungu 20(b)na cha 2 cha sheria za umiliki wa silaha za moto namba 2 ya mwaka 2015 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2006.

Chanzo:Furaha kimondo

Tuesday, 15 May 2018

MVUA YAKWAMISHA ZOEZI LA UANDIKISHWAJ VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WAKATI WILAYANI TANGANYIKA


Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Swalehe Mbwana Muhando  amesema zoezi la uandikishaji wa  Vitambulisho vya Taifa katika Wilaya yake linaendelea vizuri  japo kuna baadhi ya changamoto ziliweza kujitokeza.

Akizungumza na Waandishi wa Habari amesema zoezi hilo limekumbwa na  changamoto ya hali ya mvua kwa baadhi ya maeneo hasa katika meneo ambayo miundombinu ni mibovu hali iliyopelekea Maafisa wa Nida kushindwa kufanikisha zoezi hilo.
   
Aidha  amewataka wananchi ambao bado hawajaandikishwa  kuendelea kusubiri utaratibu ambao upo chini ya NIDA.

Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa linaendelea katika maeneo mbalimbali Mkoa wa Katavi hivyo wananchi wametakiwa kujitokeza katika zoezi hilo.

Monday, 14 May 2018

Lulu atarudi tena gerezani – Mkuu wa Magereza

Mkuu wa Magereza ya Mkoa wa Dar es salaam, ACP Augustino Mboje amesema muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anaweza kurudi gerezani endapo ataonesha mwenendo usioridhisha wakati ambao atakua chini uangalizi

ACP Mboje amesema hayo leo Mei 14, 2018 alipokuwa anaongea na vyombo vya habari kuelezea sababu za msanii huyo kutoka kabla ya muda kifungo kuisha ambapo amedai kuwa Lulu amenufaika na msamaha wa Rais Magufuli aliotangaza katika sherehe za sikukuu ya Muungano Aprili 26, 2018 mjini Dodoma
“Kama atakiuka masharti ya kuchelewa, kuonesha tabia mbaya, mara siku moja moja haji, akawa haoneshi mwenendo mzuri, community worker atawasiliana na sisi (Lulu) atarudi gerezani kwa kupitia mahakamni kwasababu aliletwa na mahakama” amesema ACP Mboje
Awali ACP Mbonje aliongeza kuwa msanii huyo asingeweza kutoka 26 April 2018 hata baada ya kupewa msamaha na Rais Magufuli kwasababu alikua hajatumikia robo ya kifungo chake ambacho kilikua kinaisha Novenba 12, 2018 baada ya msamaha huo.
Sambamba na hilo ACP Mbonje amedai kwasasa msanii Lulu bado ni mfungwa ila atatumikia kifungo chake nje ya gereza mpaka novemba 12, 2018 kwa kufanya huduma za kijamii.
Kwa mujibu wa sheria ya Mahakama kifungu na. 3 (2) (a) ya huduma ya jamii ya mwaka 2002 inatoa nafasi kwa mfungwa ambae kifungo chake hakijazidi miaka mitatu kutumikia kifungo chake nje ya gereza kwa kufanya kazi zisizo na malipo kwa manufaa ya jamii.
Novemba 13, 2017 Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam ilimtia hatiani msanii Elizabeth Michael (Lulu) na kumhukumu kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba April 7, 2012 nyumbani kwa marehemu Sinza Jijini Dar es Salaam

MVUA KUBWA KWA SIKU TANO YAJA-TMA


Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa kwa siku tano kuanzia jana, ambazo zinaweza kuleta mafuriko katika maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Katika taarifa ya TMA iliyotolewa Mei 13, mvua hizo zilizoanza kunyesha  zitaendelea mpaka Mei 17 mwaka huu.

TMA imesema athari zinazinaweza kutokea ikiwemo mafuriko ambayo yanaweza kusababisha kuvurugika kwa usafiri, barabara kubwa kutopitika na maisha ya watu kuwa hatarini  kutokana na maji kujaa au kupita kwa kasi.

Aidha imetoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.


Elimu ya hedhi itolewe kuanzia ngazi ya shule za msingi nchini-WAALIMU


Tatizo la uelewa kwa watoto wa kike hususani ambao wapo katika ngazi ya elimu ya msingi juu ya namna ya kujistiri pindi wanapokuwa wamefikia umri wa kupevuka imekuwa changamoto kubwa na kusababisha kushindwa kuhudhuria masomo.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mpanda  Yusta Sanga iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amesema watoto wa kike wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo kutokana na kupata maumivu makali au kukosa vifaa vya kujistiri kama vile taulo.      

Aidha ameiomba Serikali isaidie kutoa vifaa vya huduma ya kwanza kwani  vilivyopo havitoshelezi  hasa kwa shule za msingi.

Watoto wengi  wa kike wamekuwa wakikosa vipindi shuleni pindi wanapokuwa katika siku za hedhi kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa taulo na kupata maumivu makali ya tumbo.
CHANZO:Johari Secky

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...